Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 9,656
- 15,990
Naendelea na kilio changu cha ulanguzi wa biashara ya mafuta. Hivi sasa ukipita vituo vingi vya mafuta unaambiwa yameisha. Huu umekua kama mchezo sasa kuwa kila ikikaribia jumatano ya mwanzo wa mwezi ambapo ndio bei mpya za mafuta hutangazwa basi wenye vituo vya mafuta wanazuia kutoa huduma kusubiri bei mpya.
Sasa mimi nauliza huko EWURA ni nani anaetoa siri za bei ya mafuta kila mwezi kwa Wafanyabiashara hawa ambao nao kwa kutaka kwao maslahi mazuri wanaficha bidhaa hiyo muhimu wananchi tuendelee kupata tabu?
Nauliza tena Waziri Januari Makamba hivi umeshindwa kabisa kuwadhibiti wauzaji wa mafuta na kwamba sasa wajichukulie tu sheria mkononi?
Mwisho kabisa naendelea kumshauri Mh. Rais Samia mama chukua hatua kwenye sekta hii ya mafuta kama EWURA wameshindwa kuisimamia ni bora uivunje wapewe serikalini huko labda itasaidia .
Ni hayo tu kwa leo.