CCM: Kamati Kuu Kulikoni Tena?

Na leo hii wamasai wa LOLIONDO walienda Ikulu ndiyo wakakutana na hao watu wa CCM wanaenda kwenye hicho kikao chao Ikulu. Hivi Ikulu ni sehemu ya kufanya mikutano ya CCM? Hii imekaa aje wadau? I stand to be corrected....
 
It is all about saving CCM face and nothing about Tanzania!

Wameridhika na kukongwa nyoyo kutokana na kauli za Rais ambaye ni Mwenyekiti wao. Lakini mbona kauli hizi Kikwete amekuwa akizitoa tangu aingie madarakani na vitendo ni haba?

Vita vya Ufisadi si kumkomboa Mtanzania kutoka Umasikini, Unyonge, Ujinga au Maradhi au hata kuleta mfumo wa Uongozi Bora wenye Siasa Safi, bali ni kufukuzana ndani ya Chama kwa manufaa ya Chama na si Tanzania!

1. CCM inahitaji vipi face saving, wakati inashinda uchaguzi anyways? CCM ina makundi ndani yake kama Chadema, kundi la siasa za Wangwe limeshindwa na lile la Mtei, kwenye uchaguzi wa US, kundi la Liberal la Obama liliwashinda kundi la Establishment la Clinton na sasa wote they work together na sometimes wanakwaruzana, ndio maana Blue Dogs Democrats hawataki Health Care Plan ya Obama lakini haina maana kwamba wageuke kuwa maadui na kukataa kila kitu cha Obama,

2. Mchungaji mbona unaanza ku-preach siasa za divisions? Wananchi wanawaelewa na kuwaamini wapiganaji ndani ya CCM, nayo ni hasa kwa kuelewa mazingara magumu wanayofanyia kazi wapiganaji, sio kwa sababu Zitto amekataliwa na kundi jingine ndani ya chama basi ajitoe chama ama sivyo basi na yeye haamini in demokrasia, it does not work that way mkuu katika siasa, labda kwenye dini lakini sio siasa za vyama mkuu.

3. Maana ya vita vya ufisadi ziko nyingi sana sio moja tu, na hii yako it could be one of them, lakini sio final authority ya maana ya vita vya ufisadi in general, binafsi ninawapa support na kuwaheshimu sana wapiganaji kwa sababu ninayaelewa sana matatizo wanayoyapitia kila siku na maisha yao kutoka kwa mafisadi, na ni hivi majuzi tu wote tumejionea wazi jinsi walivyoshambuliwa ili wafukuzwe NEC na mafisadi, sasa inachekesha sana kwamba mafisadi wanapigania kuondolewa kwa mafisadi wenzao, it just does not make any sense!

Respect.

FMEs!
 
- Mkuu Mchungaji, again ndani ya chama chochote cha siasa duniani lazima kuwe na makundi yenye itikadi tofauti, Zitto aliposimamishwa ubunge, kuna wabunge wapiganaji waliokataa kushiriki kumuhukumu Zitto na kukemewa sana na Waziri Mkuu, lakini waligoma kata kata sasa unasema kwamba wapiganaji walifanya vile kwa manufaa ya nani?

- Sasa wapiganaji wanaoandamwa na mafisadi kila siku ya Mungu, mpaka kutaka kufukuzwa NEC unasema wanapigania mafisadi, halafu mafisadi hao hao wanataka kuwafukuza kina Sitta kwenye CCM, labda kuna sehemu sikuelewi maana it does not make a sense kwa any Great listener, acha tu a Great Thinker!

Mkuu punguza hasira na jazba na wapiganaji, unless una ushahidi wa ufisadi wao kwa taifa uweke hapa tuuchambue! Otherwise, mafisadi hawawezi kulala macho kumtoa Sitta fisadi mwenzao, as of your claim!

Respect.

FMEs!

FMES,

Sijawahi kusema kuwa Wapiganaji ni Mafisadi. Nimehoji matendo yao, mtu kama Sitta, kuacha nyumba ya Serikali na kukimbilia nyumba binafsi na kulipia Shilingi Milioni Nane kwa mwezi. Mtu kama Mwakyembe kuanzisha kampuni ya kufua Umeme ilhali yeye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nishati.

Hiyo ni mifano miwili tosha inayofanana na Rostam kuwa na Dowans au Karamagi kuwa na TICTS!

Labda tunalotofautiana zaidi na dnio maana unaona kama nina jazba ni kuwa mimi naulilia Utanzania na Tanzania kama Taifa, huku wewe mwenzangu unaangalia UCCM pekee!

Vita vyangu ni kudai maendeleo ya kweli kwa manufaa ya nchi bila kujali Itikadi, Kabila, Dini, Jinsia, Umri au lolote la Kibaguzi kisa manufaa ya Chama!

Nilikuuliza, wengine tunapoimba "Tanzania Mbele, Chama Nyuma" wewe unaimba "CCM Mbele, Tanzania Nyuma" kama Wakristo wanavyoimba "Msalaba Mbele, Dunia Nyuma"?
 
1. Mchungaji, huenda uko misinformed tu, kwa sababu Sitta kama Speaker hawezi kuamua mahali pa kuishi, ila huwa anaamuliwa na Usalama Wa Taifa.

2. Halafu kumbuka kwamba Azimio la Arusha halipo tena, kwa hiyo kwa viongozi wetu wa sasa kumiliki biashara sio ishu tena ya kimaadili, ila ni hizo biashara wanazipataje, kwa mfano Mpiganaji Mheshimiwa Mama Kilango, ana biashara zake nzito sana hata kabla hajawa kiongozi, sasa leo utasema ni tatizo yeye kuendelea nazo maana atakuwa kama Rostam na Dowans?

- Mbona Freeman na Ndesamburo wana biashara zao kama Karamagi

3. Wewe toka majuzi unawashambulia sana wapiganaji kwamba wao 11 ndio chanzo cha ufisadi dhidi ya wananchi Millioni 40 wa Tanzania, na kukwama kwa maendeleo yetu kitaifa, mimi ninasema hapana wao wanajitahidi tu kufanya the impossible,

- Kwamba eti ninatetea CCM kuliko taifa hapana sijawahi hata siku moja nafikiri record yangu JF iko wazi na very clear na hilo la masilahi ya taifa, tatizo moja tu ni kwamba sipendi kuburuzwa na mawazo ya wengine, hasa wenzetu wa huko Chadema, ambao wengi wao wameamua kwamba hii ni forum yao, ninatetea wapiganaji mkuu sio mafisadi ndani ya CCM,

- Na ninaikataa kwa nguvu moja hoja yako ya msingi kwamba wapiganaji 11 ndio mwanzo wa our national misery, ninasema hapana! na ninakuomba tu upunguze jazba na wapiganaji, maana wakibadili mawazo tutakwisha mkuu.

Respect.

FMEs!
 
3. Maana ya vita vya ufisadi ziko nyingi sana sio moja tu, na hii yako it could be one of them, lakini sio final authority ya maana ya vita vya ufisadi in general, binafsi ninawapa support na kuwaheshimu sana wapiganaji kwa sababu ninayaelewa sana matatizo wanayoyapitia kila siku na maisha yao kutoka kwa mafisadi, na ni hivi majuzi tu wote tumejionea wazi jinsi walivyoshambuliwa ili wafukuzwe NEC na mafisadi, sasa inachekesha sana kwamba mafisadi wanapigania kuondolewa kwa mafisadi wenzao, it just does not make any sense!

Respect.

FMEs!

My dear Friend FMES,

Kwa heshima na taadhima kubwa, naomba utuambie hawa "Wapiganaji" unaowatetea kuwa wanapigana dhidi ya vita vya Ufisadi, ni Ufisadi wa namna gani?

Umesema vita vya Ufisadi viko vingi, naomba utupe mnyumbulisho wa hivyo vita, ni vita gani "wapiganaji" wanapigana na ni kwa faida ya nani?

Je Ufisadi ni nini? Ni Kiwira, Richmond na EPA na hata ongeza Rada, IPTL, ATCL, TRL, TICTS na Buzwagi pekee?

Je uzembe, hujuma na ufujaji katika Serikali Kuu, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Serikali za Mikoa, Wilaya na vyombo vingine kama Ripoti ya Mdhibiti Mkuu viko sehemu gani ya vita hivi unavyodai vya Wapiganaji?

Ripoti ya Benki ya Dunia inasema Tanzania imeshindwa kujijenga na kuwa fanisi kwa kutosha ili ipewe misaada na mikopo ya bei nafuu na riba ndogo, na hivyo kupoteza sifa hiyo na upendeleo huo maalum kwa miaka mitatu ijao, je Wapiganaji wako tayari kuamka na kutaka Uwajibikaji?

Deni la Taifa limeongezeka marudufu na tunaambiwa tusiwe na hofu, lakini deni hili ni Asilimia 33 ya pato la Taifa ikiwa na maana kuwa katika kila Shilingi 100 tunayopata, shilingi 33 ni deni, kabla ya kuondoa gharama nyingine za uzalishaji na matumizi ili tupate salio la Akiba.

Je deni hili linaloongezeka kila siku, Wapiganaji wana mpango gani kulisitisha na kulipunguza?

Tofauti kati yangu na wewe ni mtazamo wa lipi ni la muhimu na manufaa kwa Taifa la Tanzania.

Kama Wabunge wanashindwa kufanya kazi zao na kuwajibika ipaswavyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na si ya katiba ya Chama kiwe CCM, CHADEMA, CUF au TLP, hao kwangu, hawafai kutuongoza Watanzania. Wanatuhujumu Watanzania kwa kuweka maslahi ya Chama chao kwanza na si maslahi ya Taifa. Maslahi ya Taifa yanafanywa kuwa ni kisingizio.

Umezungumzia hapo juu kuhusu vyama vya Siasa Marekani na Obama. Heri wao wanajulikana msimamo wao na wanafanya kazi kwa juhudi kwa manufaa ya nchi kwanza na chama kupokea hongera kutokana na ufanisi wa Serikali na si Chama.

Hivyo mategemeo yangu ambayo yalikuwa ni kuwaona "wapiganaji" wakipigana pande zote za vita dhidi ya Umasikini na Unyonge, bado hayajatimizwa na nionavyo ni kuwa vita ya kuondoa Unyonge wa Maendeleo ya kweli kwa Taifa letu, imegeuzwa kuwa ni vita ya Watu wasioelewana ndani ya Chama.

Ukweli ni kuwa ukisoma kinachofanywa na Mafisadi na Wapiganaji, utaona kinachogombewa si kwa manufaa ya Tanzania, la hasha! Ni kwa manufaa yao na Chama chao ya kutaka kujua ni nani ayashike madaraka ya nchi na hili chimbuko lake ni Ugombea Urais 2005 na matokeo yake!
 
1. Mchungaji, huenda uko misinformed tu, kwa sababu Sitta kama Speaker hawezi kuamua mahali pa kuishi, ila huwa anaamuliwa na Usalama Wa Taifa.

2. Halafu kumbuka kwamba Azimio la Arusha halipo tena, kwa hiyo kwa viongozi wetu wa sasa kumiliki biashara sio ishu tena ya kimaadili, ila ni hizo biashara wanazipataje, kwa mfano Mpiganaji Mheshimiwa Mama Kilango, ana biashara zake nzito sana hata kabla hajawa kiongozi, sasa leo utasema ni tatizo yeye kuendelea nazo maana atakuwa kama Rostam na Dowans?

- Mbona Freeman na Ndesamburo wana biashara zao kama Karamagi

3. Wewe toka majuzi unawashambulia sana wapiganaji kwamba wao 11 ndio chanzo cha ufisadi dhidi ya wananchi Millioni 40 wa Tanzania, na kukwama kwa maendeleo yetu kitaifa, mimi ninasema hapana wao wanajitahidi tu kufanya the impossible,

- Kwamba eti ninatetea CCM kuliko taifa hapana sijawahi hata siku moja nafikiri record yangu JF iko wazi na very clear na hilo la masilahi ya taifa, tatizo moja tu ni kwamba sipendi kuburuzwa na mawazo ya wengine, hasa wenzetu wa huko Chadema, ambao wengi wao wameamua kwamba hii ni forum yao, ninatetea wapiganaji mkuu sio mafisadi ndani ya CCM,

- Na ninaikataa kwa nguvu moja hoja yako ya msingi kwamba wapiganaji 11 ndio mwanzo wa our national misery, ninasema hapana! na ninakuomba tu upunguze jazba na wapiganaji, maana wakibadili mawazo tutakwisha mkuu.

Respect.

FMEs!

Ina maana walipoandika Magazetini kwua Spika anakaa kwenye nyumba binafsi ni Uzushi? Je walipodai kuwa ana stakabadhi za malipo ya matibabu zisizoeleweka nazo ni uzushi? kama ni uzushi, mbona hajatoa taarifa au tamko kukanusha?

Tena unakosea sana kuleta Usalama wa Taifa kwenye hili, maana ni hao hao Usalama wa Taifa ambao wameshindwa kazi na kutufikisha hapa tulipo leo hii kuhusiana na Ufisadi.

Kama leo wao UWT ni wepesi kumtafuta Male Lusinde kisa ni picha za uchi, lakini walishikwa kigugumizi kung'amua kuwa Richmond ni kampuni ya mfukoni na ya kiubabaishaji, huoni kuwa hata la Sitta kuamua kukaa nyumba binafsi hata kama lina baraka ya UWT, linawezekana kuwa lina walakini?

Kuvunjwa kwa miiko na maadili ya Viongozi, ndio chimbuko la Ufisadi na hivi vita ndani ya CCM kwa maana kila mtu anagombea ajipatie. Kuna wanaoendelea na biashara zao kwa uadilifu bila kutumia nyadhifa zao na mamlaka kujinufaisha na kuna wanao hujumu nafasi hii.

Sijasema kuwa Mama Kilango ni fisadi, au Ndesamburo, Mbowe, Diallo, Raza, au Salum wa kiwanda cha kusokota nyuzi.

Ninachopinga ni Wanasiasa hasa wanaotumikia wananchi kama watumishi wa Serikali; Wabunge, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Makatibu wakuu, kifupi mtu yeyote ambaye ni mtumishi wa umma (Serikali) anapaswa kuacha biashara zake na ashike moja, nalo ni utumishi wa umma mpaka pale atakapoacha kazi yake kama mwajiriwa wa Serikali na kulipwa mshahara na walipa kodi wa Tanzania.

Nilipoandika CCM ni mali ya Wakulima na Wafanyakazi, ni kutokana na Imani yangu asili iliyotumika kuunda CCM. CCM ni chama kilichoshika Usukani wa nchi kutokana na msukumo wa Wakulima na Wafanyakazi. nikauliza kwa kina nawe ukanishukuru kwa dhati, kwa nini WanaCCM wanaendelea kuwaachia Mafisadi waendelee kufanya maamuzi watakayo ndani ya chama?

Ninachojengea hoja ni utupu wa vita vya Wapiganaji kudai kuwa wao lengo lao ni kung'oa mafisadi ndani ya CCM na wanaolilia kuwang'oa tunawajua, ni kundi la Lowassa, Rostam, Chenge na Mkapa.

Lakini, Tanzania au hat CCM yenyewe, ina matatizo mengi sana ya kimfumo ambayo ni kauli miaka nenda rudi zimekuwa zikitumika kulaghai Watanzania kuwa sasa kuna nuru na sura mpya.

Naomba sana usome ile makala ya Mwanakijiji inayozungumzia mfumo wa Utawala wa Kifisadi. Ukishausoma ndipo utaelewa ni kwa nini nimewagangamalia hawa "Wapiganaji"!

Kuna mengi mabovu Tanzania ambayo wala hayahitaji kuhubiriwa kwenye majukwaa, bali ni vitendo na msukumo unaohitajika, je Wapiganaji wako wapi kufanya hilo?
 
- Na ninaikataa kwa nguvu moja hoja yako ya msingi kwamba wapiganaji 11 ndio mwanzo wa our national misery, ninasema hapana! na ninakuomba tu upunguze jazba na wapiganaji, maana wakibadili mawazo tutakwisha mkuu.

Respect.

FMEs!

FMES,

Ni wapi niliposema kuwa Wapiganaji ni chimbuko la Matatizo yetu?

Sina jazba na Wapiganaji, nina jazba na Kauli zisizoendana na vitendo au utashi kwa manufaa ya Taifa ambalo tayari limeshakwisha!

Unadai wakibadili mawazo tutakwisha, je wao ndio pekee wenye uwezo wa kuleta Mapinduzi dhidi ya Unyonge na Umasikini Tanzania? Kwa kauli yako kuwa wakibadili mawazo tumekwisha, unaudhihirishia wazi umma kuwa kinachogombaniwa ndani ya CCM ni Uongozi wa nchi na si Maslahi ya nchi!
 
Rev. Kishoka,

Kila nikirudi mtandaoni naona hii thread imesha kua. Huku kwetu ngumu sana maana mara umeme hakuna na pia internet ni aghali sana. Inabidi kutumia internet mchana tu.

Hongera kwa uchambuzi wako wa kina kwenye hii thread na mwenye kuelewa ataelewa. Ila Rev. Kishoka nakushauri muanze kuyatekeleza baadhi ya haya mnayoyaandika huku wilayani. Naamini watu kama nyie mkiamua kufanya kweli ujinga mwingi ulioko huku wilayani unaweza kupungua.

FMES hachukii ufisadi na badala yake hapa anatuchezea ngoma tu. Kama anachukia ufisadi basi aanze na Malechela ambaya hata mwalimu alimwita ni mhuni na hakuweza hata kujitetea. Lakini CCM walivyo wajinga wakamfanya Makamu mwenyekiti wa chama. Ameongeza mbinu mbalimbal za CCM kuiba kura huko kwenye majimbo.

Ukija Sitta ndio sahau kabisa kuanzia kule CDA mpaka hata pale TIC ambko alifanya ufisadi mkubwa sana. Mambo ya kwamba eti usalama wa taifa ni usanii tu. Mtu anayechukua milioni nane kwa mwezi kwa ajili ya kupanga nyumba huyo hana uzalendo wowote kwa sisi walala hoi huku vijijini. Hivi ni dawa gani inayouzwa milioni mbili? Aliforge receipt huyo Sitta.

Mtu kama Shelukindo, ameua mashirika mangapi ya umma kabla ya kuwa mbunge?

Dr. Mwkyembe, vipi alipohalalisha mauaji ya Wapemba mwaka 2001, hakujua ni makosa? Aliona cheo cha kuwa mbunge Eat Africa ni bora zaidi kuliko haki ya wananchi? Aliponunua ghorofa y NBC pale Tukuyu wakati hakuwa mfanyakazi wa NBC hakuona kwamba huo ni ufisdi? Wakati huo alikuwa mjumbe wa board ya NBC.

Kuna mengi ya hawa wapiganaji wa FMES ambayo hayako sawa. Wanaunganishwa na kitu kimoja, wako hatarini kudondoshwa kwenye majimbo yao kwasababu hakuna walichofanya na sasa wanatumia vita ya ufisadi kama njia ya kuonewa huruma.

Dr. Slaa ni kweli ni mpambanaji wa vita vya ufisadi maana anataja na majina na kutoa na ushahidi. Hawa wengine kazi zo kuzua majungu kibao. Msanii wetu hapa aliulizwa ataje mafisadi gani wakiondoka CCM, chama kitabaki clean bila mafisadi, akashindwa kujibu.

FMES, sina ugomvi na wewe ila kama kweli unachukia ufisadi acha kuandamana na mafisadi kila wanapokuja huko USA. Kama rais anachukia ufisadi kweli si ufisadi ungeisha? Chenge kwanini bado yuko bungeni? Lakini JK akija huko FMES ndio wa kwanza kugongeshana naye glass.
 
Ina maana walipoandika Magazetini kwua Spika anakaa kwenye nyumba binafsi ni Uzushi? Je walipodai kuwa ana stakabadhi za malipo ya matibabu zisizoeleweka nazo ni uzushi? kama ni uzushi, mbona hajatoa taarifa au tamko kukanusha?
National Assembly Speaker Sitta happy with CAG`s decision

2009-05-03 16:57:05
By Staff Reporter, Dodoma

The Speaker of the National Assembly Samuel Sitta said recent clearance of his office by the Controller and Auditor General (CAG) over allegations of embezzlement of funds shows that people bent on ``tarnishing his name in the public will not succeed.``

He told The Guardian on Sunday in an exclusive interview in Dodoma over the weekend that he was happy the National Audit Office has revealed the truth over the matter and justice done.

On April, 25 2008, Sitta announced in Parliament that he received allegations that he had embezzled about 60million/- while in Bangalore, India, on December 21, 2007 for treatment. The Speaker`s treatment involved an operation administered on him.

He said, without naming those accusing him, the tendency to create unfounded claims to tarnish people`s image was normal in politics.

``I am sure those fond of creating allegations against others will continue doing so.

All this is dirty politics but we will not be deterred by their behaviour,`` he said, adding that such people have even claimed that he sometimes used Bunge funds to tour his constituency.

Sitta explained that the funds allocated for his office are administered by two special officials. He said even when he travels it is the same people who process the funds, observing all financial procedures.

There are reports in political circles that the ``victims`` of the Bunge decision on Richmond scam in early 2007 had soon started to wage a campaign against Sitta as revenge, hoping he loses in the general elections next year.

Speaking to reporters last Monday in Dodoma Controller and Auditor General (CAG) Ludovick Utouh said his office audited all the Bunge accounts but could not find any irregular payment or embezzlement that the Speaker was being associated with.

``We did our audit work very thoroughly but we did not see anything that would suggest something was done out of the required financial procedures,`` CAG Utouh was quoted as saying.
  • SOURCE: Sunday Observer
 
My dear Friend FMES,

Kwa heshima na taadhima kubwa, naomba utuambie hawa "Wapiganaji" unaowatetea kuwa wanapigana dhidi ya vita vya Ufisadi, ni Ufisadi wa namna gani?

Umesema vita vya Ufisadi viko vingi, naomba utupe mnyumbulisho wa hivyo vita, ni vita gani "wapiganaji" wanapigana na ni kwa faida ya nani?

Je Ufisadi ni nini? Ni Kiwira, Richmond na EPA na hata ongeza Rada, IPTL, ATCL, TRL, TICTS na Buzwagi pekee?

Je uzembe, hujuma na ufujaji katika Serikali Kuu, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Serikali za Mikoa, Wilaya na vyombo vingine kama Ripoti ya Mdhibiti Mkuu viko sehemu gani ya vita hivi unavyodai vya Wapiganaji?

Ripoti ya Benki ya Dunia inasema Tanzania imeshindwa kujijenga na kuwa fanisi kwa kutosha ili ipewe misaada na mikopo ya bei nafuu na riba ndogo, na hivyo kupoteza sifa hiyo na upendeleo huo maalum kwa miaka mitatu ijao, je Wapiganaji wako tayari kuamka na kutaka Uwajibikaji?

Deni la Taifa limeongezeka marudufu na tunaambiwa tusiwe na hofu, lakini deni hili ni Asilimia 33 ya pato la Taifa ikiwa na maana kuwa katika kila Shilingi 100 tunayopata, shilingi 33 ni deni, kabla ya kuondoa gharama nyingine za uzalishaji na matumizi ili tupate salio la Akiba.

Je deni hili linaloongezeka kila siku, Wapiganaji wana mpango gani kulisitisha na kulipunguza?

Tofauti kati yangu na wewe ni mtazamo wa lipi ni la muhimu na manufaa kwa Taifa la Tanzania.

Kama Wabunge wanashindwa kufanya kazi zao na kuwajibika ipaswavyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na si ya katiba ya Chama kiwe CCM, CHADEMA, CUF au TLP, hao kwangu, hawafai kutuongoza Watanzania. Wanatuhujumu Watanzania kwa kuweka maslahi ya Chama chao kwanza na si maslahi ya Taifa. Maslahi ya Taifa yanafanywa kuwa ni kisingizio.

Umezungumzia hapo juu kuhusu vyama vya Siasa Marekani na Obama. Heri wao wanajulikana msimamo wao na wanafanya kazi kwa juhudi kwa manufaa ya nchi kwanza na chama kupokea hongera kutokana na ufanisi wa Serikali na si Chama.

Hivyo mategemeo yangu ambayo yalikuwa ni kuwaona "wapiganaji" wakipigana pande zote za vita dhidi ya Umasikini na Unyonge, bado hayajatimizwa na nionavyo ni kuwa vita ya kuondoa Unyonge wa Maendeleo ya kweli kwa Taifa letu, imegeuzwa kuwa ni vita ya Watu wasioelewana ndani ya Chama.

Ukweli ni kuwa ukisoma kinachofanywa na Mafisadi na Wapiganaji, utaona kinachogombewa si kwa manufaa ya Tanzania, la hasha! Ni kwa manufaa yao na Chama chao ya kutaka kujua ni nani ayashike madaraka ya nchi na hili chimbuko lake ni Ugombea Urais 2005 na matokeo yake!

- Mchungaji, nimesema hivi kabla hujaelewa wapiganaji wanachopigania, unahitaji kuelewa hapa JF tunapigania nini hasa?

- Matatizo ya benki ya dunia na madeni na Tanzania hayawezi kuwa ni ya wapiganaji 11 walioanza vita only three to four ago.

- Wapiganaji 11 hawawezi kupigania maovu yote ya nchi hii kwa wakati mmoja, kwanza ni mengi mno maana yameanza toka awamu ya kwanza wengi wao wakiwa shule za msingi, sasa pole pole tusaidiane nao wayafikie yote, lakini lazima tuwape time ya kutosha.

- Mkuu Yesu alikuwa na wananfunzi 12, lakini walichoandika hakifafani, sasa mimi na wewe sio lazima tuwe na mawazo sawa on wapiganaji wanachopigania, lakini ninasema hivi wapiganaji wasingekuwepo hata hii deabte tusingekua nayo, ninasema hivi Mungu awape nguvu an busara zaidi wapiganaji hawa 11 wazidi kulisaidia hili taifa, ambao limeoza kwa muda mrefu sana sasa, toka awamu zilizopita zote zilikuwa zimeoza ndio kwanza wapiganaji wanajaribu kunyoosha sasa, sio rahisi lakini tukiwapa support yaani mimi na wewe Mchungaji watafanikiwa tu kutukomboa.

Respect.

FMEs!
 
Rev. Kishoka,

1. FMES hachukii ufisadi na badala yake hapa anatuchezea ngoma tu. Kama anachukia ufisadi basi aanze na Malechela ambaya hata mwalimu alimwita ni mhuni na hakuweza hata kujitetea. Lakini CCM walivyo wajinga wakamfanya Makamu mwenyekiti wa chama. Ameongeza mbinu mbalimbal za CCM kuiba kura huko kwenye majimbo.

- Engineer kama ninavyosema, kila ukifungua mdomo wako ni pumba na more pumba, mimi sio mbunge wako wala mkuu wako wa wilaya sasa nikiwa fisadi au nisipokuwa ni uamuzi wangu sio wako mkuu,

- Una tabia moja usipokuwa na hoja uanaaza kurusha rusha majina ya watu what Malecela has to do na this? Halafu unasema ya Mwalimu na uhuni wa Malecela, sasa Mwalimu kama alikuwa msafi aliwezaje kwua na waziri wa nje muhuni? Samaki wakiwa wameoza si huwa ni wote, meaning kwamba kama Malecela alikuwa mhuni basi Mwalimu alikuwa ndiye professor wa uhuni, au?

- Ya kuiba kura na Malecela, hivi ni kwa nini hakuiba kura za Tarime?

Ukija Sitta ndio sahau kabisa kuanzia kule CDA mpaka hata pale TIC ambko alifanya ufisadi mkubwa sana. Mambo ya kwamba eti usalama wa taifa ni usanii tu. Mtu anayechukua milioni nane kwa mwezi kwa ajili ya kupanga nyumba huyo hana uzalendo wowote kwa sisi walala hoi huku vijijini. Hivi ni dawa gani inayouzwa milioni mbili? Aliforge receipt huyo Sitta.

- Sitta ni fisadi na huku mafisadi nao wanampiga vita aondolewe uspika, huku ni fisadi mwenzao, it does not make any sense mkuu!, wazee wa ngwasuma wanasema acha kudandia treni kwa mbele!

FMES, sina ugomvi na wewe ila kama kweli unachukia ufisadi acha kuandamana na mafisadi kila wanapokuja huko USA. Kama rais anachukia ufisadi kweli si ufisadi ungeisha? Chenge kwanini bado yuko bungeni? Lakini JK akija huko FMES ndio wa kwanza kugongeshana naye glass.

- Mkuu Engineeer sijui unaishi wapi na wewe hujui ninapoishi, huko USA huwa ninakwenda sana, ninaamini ni kuvunja sheria za JF ku-speculate ID au location ya member mwingine bila idhini yake.

- Ya Chenge kuwepo bungeni hayanihusu, na sijui kama Jk ni mmoja wa wapiganaji 11, ni kweli JK ni rafiki yangu pia tena longtime sana akiwa hana hata ambitions za kuwa rais, sasa ya kugongeshana glasi naona yanakuuma sana mpaka umeyasema, mkuu acha wivu na chuki maana haziwezi kukusaidia anything, wala haviwezi kulisaidia taifa letu.

- Mkuu Engineer sina la kukusaidia na matatizo yako ya binafsi na mimi, ninasema Dr. Mwakyembe bado kwangu ni shujaa wa taifa, kama ana mapungufu basi yaweke hapa kwa facts na utuambie mgombea wako atafanya nini tofauti na DR, lakini hizi rants za personal unapoteza muda bure tu mkuu!

Respect.

FMEs!
 
FMES,

Ni wapi niliposema kuwa Wapiganaji ni chimbuko la Matatizo yetu?

Sina jazba na Wapiganaji, nina jazba na Kauli zisizoendana na vitendo au utashi kwa manufaa ya Taifa ambalo tayari limeshakwisha!

Unadai wakibadili mawazo tutakwisha, je wao ndio pekee wenye uwezo wa kuleta Mapinduzi dhidi ya Unyonge na Umasikini Tanzania? Kwa kauli yako kuwa wakibadili mawazo tumekwisha, unaudhihirishia wazi umma kuwa kinachogombaniwa ndani ya CCM ni Uongozi wa nchi na si Maslahi ya nchi!

- Mkuu Mchungaji kama kweli huamini kwamba wapiganaji ndio wenye jawabu la matatizo yetu mengi as a nation for now, basi usingekua na tatizo nao, ninasema hivi wapiganaji ni good people tena wenye good intentions kwa taifa, Mungu awape nguvu na busara zaidi ili waweze kuendelea kupigania taifa na masilahi yetu wananchi,

- Na sisi wananchi tuwape support, tushirikiane nao ili waweze kulisaida taifa letu, kushindana nao na kuwakatisha taama haiwezi kutusaidia wananchi wala taifa, hawagombei power maana wanazo tayari hizo power, Sitta ni speaker wa bunge letu tayari sasa anagombea power ipi tena kwa kupinga ufisadi?

Ninasema Mengi ni tajiri wa ajabu sana sasa kwa kupigania taifa dhidi ya mafisadi anatafuta nini kama sio kujitoa tu kwa ajili ya taifa lake? Tuwe na shukrani jamani, haya mambo hayakuwepo huko nyuma hivi mmesahau kwamba huko nyuma hawa wapiganaji wangeishia kisiwa cha Mafia walikoishia kina Seif Bakari na wenzake? Na huyu Rais Kikwete pia apewe heshima japo kidogo, maana kama sio yeye huu uhuru wa wabunge na viongozi wetu wa vyama vya siasa usingekuwepo,

- Ni kweli tuna matatizo mengi sana, lakini la ufisadi ndio namba moja likitatuliwa hili basi mengine yote yatajiondoa yenyewe, sasa tuwape support wapiganaji badala ya kutaka kushindana na kuwaponda, hatuwezi kupata hata baraka za Mwenyezi Mungu kama hatuwezi kuwaheshimu na kuwaunga mkono wapiganaji.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Unakumbka vita dhidi ya Uhujumu na Ulanguzi wa Uchumi wilivyopiganiwa na Sokoine? Je baada ya kamata kamata Uhujumu na Ulanguzi uliisha? Jibu ni Hapana na ndio maana leo tunaendelea na vita ileile.

Mwinyi alikuja na Fagio la Chuma, Mkapa akaunda tume ya Warioba, kwenye utawala wa Kikwete, kumeundwa tume ya Chifupa ya madawa ya kulevya, tume ya Bomani kuhusu madini, kamati ya Bunge ya Richmond, tume ya wizi BOT ya EPA hata tume ya Zombe!

Tume na Kamati hizi zimefanya kazi na kuwasilisha mapendekezo yao Serikalini. Utekelezaji wa mapendekezo ni sifuri!

Ripoti ya Warioba bado inapata vumbi na utando wa Buibui, tangu itolewe na aliyepelekwa mahakamani alikuwa ni Kiula na wenzake wawili ambao kesi imefutwa na sasa wako huru. Wengine wote waliotajwa kwenye Ripoti ya Warioba hawajaguswa na si ajabu wengine ndio hao hao waliohusika na EPA.

Kwenye utawala wa Kikwete;
  • Wafanya biashara ya madawa ya kulevya hawajakamatwa wala kushughulikiwa kwa namna yeyote.
  • Mkataba wa Buzwagi na mingine ya madni ambayo ina kasoro na iliingiwa kwa vitendo vya hujuma haijasitishwa.
  • Waliohujumu ATCL na kuingia mkatgaba uliotia hasara nchi, wamepewa vyeo vipya.
  • Wahujumu wa Benki Kuu pamoja na kufikishwa mahakamani, kesi zao ni dhaifu mno na matokeo yake yatakuwa kama yale ya Kiula.
  • Yona, Mramba, Mgonja wamefikishwa mahakamani kwa Uzembe na Matumizi mabaya ya madaraka, Lowassa, Chenge, Karamagi na Msabaha pamoja na kuwepo ushahidi tosha wa makosa yao ya kiutendaji, bado wako huru na wanapewa heshima kubwa na kuogopewa.
  • Rostam ambaye kampuni yake ilinunua mkataba feki, kaendelea kupokea malipo badala ya kusitisha mkataba. Imechukua muda mrefu kwa mkataba wa Richmond kusitishwa hata baada ya Kamati ya Mwakyembe kubaini kuwa ulikuwa na walakini. Rostam alishindwa kutumia busara na kuliokoa Taifa, akafikiria tumbo lake na hata leo hii, bado ni mjumbe wa CC, NEC na Mbunge na hajapewa karipio la wazi.
Sasa kama mtiririko huu unaoonyesha ushahidi tosha wa ubutu na udhaifu kuhusiana na kesi za uhujumu na ufisadi kutoka Serikali kuu na hata ndani ya Chama, iweje tuendelee kushangilia kuwa "Wapiganaji" wanapigana vita sahihi?

Je kama leo hii ni takriban karibu miaka 26 tangu vita vya Uhujumu vya Sokoine, bado tunaendelea na vitendo vilevile tena kwa ustadi kutokana na udhaifu wa Sheria na mfumo wetu wa kiutawala, je huoni kuwa Wapiganaji ni sawa na mfa maji?

Unaposema kuwa Vita ya Ufisadi bila kuainisha ni Ufisadi gani kuwa ndio vita kuu ya kwanza, kamwe usitegemee utaweza kushinda hiyo vita kwa maana Watanzania tumeshanogewa na Ufisadi kwa namna moja au nyingine na kama mbinu za vita dhidi ya Umasikini na Unyonge havitabadilishwa na kuangalia mfumo na si watu, Wajukuu wako na wangu watakuwa kwenye JF yao miaka 40 kutoka leo hii wakiongelea kitu ambacho mimi na wewe Babu zao wanakiongelea na kubishana leo hii!

Kinachohitajika kufanyika na Wapiganaji kwanza ni kuleta mabadiliko ya mfumo wa Utawala ambao utagusa mfumo wa Siasa, mfumo wa Sheria na mfumo wa Uchumi kama tunataka kushinda vita dhidi ya Ufisadi.

Leo akifungwa Lowassa na Karamagi, kesho atatokea Mosha na Mapunda, nao watacheza libeneke mpaka tushangae.

Nimekuuliza mahali uliposema kuwa hawa 11 wanashindana na 5000, je ni mbinu gani za medani wanazotumia kuvuna wapiganaji wapya au kukaribisha wasio na upande waje kwao au wale walioko kwa mafisadi wahamie kwao?

Maana picha hii, ina kasoro kubwa sana. Ama Wapiganaji hawakubaliki ndani ya Chama na vita vyao havieleweki, au kila mtu mwenye nguvu na mamlaka ya maamuzi na kura ndani ya CCM ambaye si Mpiganaji basi yeye ni Fisadi!

La mwisho, Katika hawa 11, kuna wawili tuu ambao wao hawatadhurika na "life after action", Kilango na Kimaro na hivyo wao vita wanavyopigana hata kama vina makosa fulani ni vita vya kweli kwa manufaa ya Taifa na si kutetea maslahi yao binafsi.

Kilango na Kimaro, hawana wasiwasi wa kupoteza majimbo na Ubunge wao, na hata kama wakipoteza Ubunge, wao hawategemei Ubunge kuwapa riziki.

Wengine waliobakia, wao kazi zao ziko hatarini pamoja na maslahi yao, na njia pekee ya kujionyesha kwa wananchi wao ni kupiga kelele za Ufisadi kitu ambacho ni udaku ulio bora masikioni mwa watu.

Waambie Wapiganaji, waache kupigana dhidi ya watu, wapigane dhidi ya mfumo, wateleweka!

Sasa ukikaa kitako na kutafakari ninachikiongea sasa, labda unaweza kunielewa na kama kuna "Mpiganaji" ambaye bado haelewei ninachokisema, waambie wanitumie barua pepe kishoka70@yahoo.com niwapige msasa na kuwaeleza kwa nini vita vyao ni mbofumbofu!
 
Rev. Kishoka,
Ninakubaliana na wewe kabisa kuwa hii dhana ya hawa wanaoitwa 'wapiganaji' imesimama katika kulinda na kuhifadhi maslahi binafsi na hasa madaraka waliyokuwa nayo. Ukiangalia kwa makini from the body language hakuna dhamira ya kweli kwa yale wanayoyaongea rather than ni jinsi gani watarudi tena Dodoma kama wabunge. Ina kisiwa kuwa uchaguzi mkuu ujao wa 2010 utakuwa mgumu kwa maana baadhi ya wabunge licha ya kuwepo wagombea kutoka kambi za upinzani, hofu kubwa ya upinzani ipo ndani ya wanachama wenyewe kwa wenyewe ndani ya CCM. Hii hofu inazidi kukua kwa jinsi zinavyojijenga kambi za mivutano ndani ya CCM.
Hivyo basi, wale ambao ni waoga inabidi watafute namna ya kupiga kelele kadri inavyowezekana ili wasikike na kupata attention ya wapiga kura wao dhidi ya yeyote atakayejitokeza kupingana nao. Hili kundi la 'wapiganaji liko tayari hata kuhamia upande wowote ule iwe ni wa ndani ya CCM au nje ya CCM ili mradi tu lihakikishiwe kuwa 'wapiganaji' watarudi tena Dodoma next year kama wabunge.

To be sincere, ubunge ni kiti kinachotafutwa kwa udi na uvumba hasa kwa wale wanaojua ni namna gani wananufaika kwa kuwa wabunge.
 
FMES,

Unakumbka vita dhidi ya Uhujumu na Ulanguzi wa Uchumi wilivyopiganiwa na Sokoine? Je baada ya kamata kamata Uhujumu na Ulanguzi uliisha? Jibu ni Hapana na ndio maana leo tunaendelea na vita ileile.

- Mchungaji, vita vya wahujumu uchumi huwezi linganisha na vita ya sasa ya mafisadi, wahujumu uchumi walikuwa wauza colgate na sabuni za palmolive mtaani sio wezi wa kama mafisadi wa EPA mkuu, huu mfano ni batili kabisa on the ishu ya vita vya ufisadi.

Mwinyi alikuja na Fagio la Chuma, Mkapa akaunda tume ya Warioba, kwenye utawala wa Kikwete, kumeundwa tume ya Chifupa ya madawa ya kulevya, tume ya Bomani kuhusu madini, kamati ya Bunge ya Richmond, tume ya wizi BOT ya EPA hata tume ya Zombe! Tume na Kamati hizi zimefanya kazi na kuwasilisha mapendekezo yao Serikalini. Utekelezaji wa mapendekezo ni sifuri!

- Hoja nzito na nzuri, lakini hazina uhusiano wowote na wapiganaji na vita vya ufisadi, absolutely nothing to do with!

Ripoti ya Warioba bado inapata vumbi na utando wa Buibui, tangu itolewe na aliyepelekwa mahakamani alikuwa ni Kiula na wenzake wawili ambao kesi imefutwa na sasa wako huru. Wengine wote waliotajwa kwenye Ripoti ya Warioba hawajaguswa na si ajabu wengine ndio hao hao waliohusika na EPA. Kwenye utawala wa Kikwete;
  • Wafanya biashara ya madawa ya kulevya hawajakamatwa wala kushughulikiwa kwa namna yeyote.
  • Mkataba wa Buzwagi na mingine ya madni ambayo ina kasoro na iliingiwa kwa vitendo vya hujuma haijasitishwa.
  • Waliohujumu ATCL na kuingia mkatgaba uliotia hasara nchi, wamepewa vyeo vipya.
  • Wahujumu wa Benki Kuu pamoja na kufikishwa mahakamani, kesi zao ni dhaifu mno na matokeo yake yatakuwa kama yale ya Kiula.

- Again ni maneno mazuri sana, lakini nothing to do na vita vya ufisadi, labda BOT na Buzwagi, lakini watuhumiwa wa EPA wako mahakamani sasa sijui ni wapiganaji wanaotakiwa kwenda kuwashitaki or what?
    • Yona, Mramba, Mgonja wamefikishwa mahakamani kwa Uzembe na Matumizi mabaya ya madaraka, Lowassa, Chenge, Karamagi na Msabaha pamoja na kuwepo ushahidi tosha wa makosa yao ya kiutendaji, bado wako huru na wanapewa heshima kubwa na kuogopewa.
    • Rostam ambaye kampuni yake ilinunua mkataba feki, kaendelea kupokea malipo badala ya kusitisha mkataba. Imechukua muda mrefu kwa mkataba wa Richmond kusitishwa hata baada ya Kamati ya Mwakyembe kubaini kuwa ulikuwa na walakini. Rostam alishindwa kutumia busara na kuliokoa Taifa, akafikiria tumbo lake na hata leo hii, bado ni mjumbe wa CC, NEC na Mbunge na hajapewa karipio la wazi.
    Sasa kama mtiririko huu unaoonyesha ushahidi tosha wa ubutu na udhaifu kuhusiana na kesi za uhujumu na ufisadi kutoka Serikali kuu na hata ndani ya Chama, iweje tuendelee kushangilia kuwa "Wapiganaji" wanapigana vita sahihi?
  • - Mchungaji, ona sasa unaongelea Lowassa, Msabaha, na Karamagi ambao wamejiondoa uongozi baada ya kupigwa mawe mazito sana na wapiganaji, hivi kwa nini baada ya wapiganaji kuwatosa hawa uongozini, wewe na Chadema hamkuandamana wafikishwe kwenye sheria?
  • - Unaongela kusitishwa kwa mkataba wa Richimonduli, mbona hukubali kwamba bila wabunge wapiganaji huo mkataba nani angeusitisha mkuu? ndio maana mwanzoni nilikuambia kwamba uko mis-informed mkuu, ndio maana yanakuwa malumbano hewa, I mean kama hujui kuwa Richimonduli ilisitishwa na wapiganaji, na kwamba Lowassa, Msabaha na Karamagi hawana uwaziri leo kwa sababu ya wapiganaji, then unafikiri kweli Mchungaji tunaweza kuelewana hapa?
  • - You are mis-informed mkuu tena big time na huwezi kaa tu chini na kusubiri wapiganaji wakufanyie kila kitu! Wewe na Chadema yako mmelifanyai nini taifa na hivi vita zaidi tu ya kutaja majina ya mafisadi? Ni wapiganaji ndio waliyoyafanyia kazi hayo majina mkuu, sasa onyesha shukrani japo kidogo kuliko mashambulizi hewa!
Je kama leo hii ni takriban karibu miaka 26 tangu vita vya Uhujumu vya Sokoine, bado tunaendelea na vitendo vilevile tena kwa ustadi kutokana na udhaifu wa Sheria na mfumo wetu wa kiutawala, je huoni kuwa Wapiganaji ni sawa na mfa maji? Unaposema kuwa Vita ya Ufisadi bila kuainisha ni Ufisadi gani kuwa ndio vita kuu ya kwanza, kamwe usitegemee utaweza kushinda hiyo vita kwa maana Watanzania tumeshanogewa na Ufisadi kwa namna moja au nyingine na kama mbinu za vita dhidi ya Umasikini na Unyonge havitabadilishwa na kuangalia mfumo na si watu, Wajukuu wako na wangu watakuwa kwenye JF yao miaka 40 kutoka leo hii wakiongelea kitu ambacho mimi na wewe Babu zao wanakiongelea na kubishana leo hii!

- Sasa tizama Mchungaji wewe unakubali mwenyewe kwamba wa-Tanzania tumeshanogewa na ufisadi, sasa huoni sababu ya wapiganaji kupata shida maana wote tumezoea ufisadi kwa maneno yako mwenyewe, ni tabia tumeizoea toka awamu ya kwanza miaka 45 iliyopita, leo unategemea wapiganaji in three years tu wawe wamesafisha uozo uliodumu kwa miaka 45 ya uhuru?

Kinachohitajika kufanyika na Wapiganaji kwanza ni kuleta mabadiliko ya mfumo wa Utawala ambao utagusa mfumo wa Siasa, mfumo wa Sheria na mfumo wa Uchumi kama tunataka kushinda vita dhidi ya Ufisadi.

- Mchungaji, how could this be possible kufanyika in only four years za wapiganaji kuwemo vitani na ufisadi? Wapiganaji wameanza na ufisadi kwanza mkuu ndio tatizo sugu linalobeba matatizo yote uliyoyataja hapo juu, sasa tuwape msaada mkuu wapiganaji, maana ndio the only hope tuliyonayo sasa hivi as a nation, unajua fika kwamba huko Chadema hakuna hope kabisa!

I mean wawakilishi wa Chadema kina Zitto hawawezi kupigana na mafisadi wa Dowans, sasa tuwa-support tu wapiganaji mkuu watusaidie taifa!

Leo akifungwa Lowassa na Karamagi, kesho atatokea Mosha na Mapunda, nao watacheza libeneke mpaka tushangae. Nimekuuliza mahali uliposema kuwa hawa 11 wanashindana na 5000, je ni mbinu gani za medani wanazotumia kuvuna wapiganaji wapya au kukaribisha wasio na upande waje kwao au wale walioko kwa mafisadi wahamie kwao?

- Mchungaji you are asking for too much kutoka kwangu, sasa wapiganaji unataka waweke siri za strategy zao za kivita, sasa watawashinda vipi mafisadi? Hivi kweli unafikiri wapiganaji hawakujua kwamba mafisadi wanaenda kumkaanga Spika? Wakati Rostam alishamwambia Kinana mapema sana kwamba Lowassa au Chenge lazima washike uspika, kabla ya kikao? Ni strategy za wapiganaji ndio zilizomuokoa Spika mkuu!

- Labda wewe ungeweka strategies zenu huko Chadema namna ya kuwasiadia wapiganaji na hivi vita mkuu, tunataka umoja maana bila umoja hatuwezi kushinda hivi vita!

Maana picha hii, ina kasoro kubwa sana. Ama Wapiganaji hawakubaliki ndani ya Chama na vita vyao havieleweki, au kila mtu mwenye nguvu na mamlaka ya maamuzi na kura ndani ya CCM ambaye si Mpiganaji basi yeye ni Fisadi!

- Mchungaji vipi wapiganaji kutokubalika ndani ya chama liwe tatizo lako au la wapiganaji? Off course wapiganaji hawakubaliki ndani ya chama kwa sababu ulizozisema mwenyewe kwamba wa-Tanzania wote tumezoea ufisadi, sasa utashangaa kwamba wapiganaji hawakubaliki ndani ya chama chao mkuu, kwani hukumbuki jinsi Yesu alivyoambiwa na wauza nguruwe kuondoka mara moja kwenye eneo lao baada ya kuharibu biashara yao kwa kuwarusha mashetani wabaya katika nguruwe wao wa biashara?

La mwisho, Katika hawa 11, kuna wawili tuu ambao wao hawatadhurika na "life after action", Kilango na Kimaro na hivyo wao vita wanavyopigana hata kama vina makosa fulani ni vita vya kweli kwa manufaa ya Taifa na si kutetea maslahi yao binafsi. Kilango na Kimaro, hawana wasiwasi wa kupoteza majimbo na Ubunge wao, na hata kama wakipoteza Ubunge, wao hawategemei Ubunge kuwapa riziki.

- Again mis-informed mkuu hawana wasi wasi wa kupoteza majimbo yao kwa sababu ya kazi kubwa waliyowafanyia wanachi wao, ndio maana sasa hivi jiko huku USA na Mama Kilango, hana wasi wasi na jimbo lake akiwatafutia wananchi wake masilahi yao, sasa atapoteza vipi kazi yake?

- Na besides, CCM inajua kwamba hawa hata wakitoka na kugombea na chama kingine hawana tatizo, kwa hiyo ukiwafanyia kazi wanajimbo huwezi kuwa na wasi wasi hata siku, unless hukuwafanyia kazi wananchi, na you are damn right kwamba hawa wabunge hawategemei ubunge kwa riziki zao ndio maana wanaweza kusimama kidete on ufisadi.

Wengine waliobakia, wao kazi zao ziko hatarini pamoja na maslahi yao, na njia pekee ya kujionyesha kwa wananchi wao ni kupiga kelele za Ufisadi kitu ambacho ni udaku ulio bora masikioni mwa watu. Waambie Wapiganaji, waache kupigana dhidi ya watu, wapigane dhidi ya mfumo, wateleweka! Sasa ukikaa kitako na kutafakari ninachikiongea sasa, labda unaweza kunielewa na kama kuna "Mpiganaji" ambaye bado haelewei ninachokisema, waambie wanitumie barua pepe kishoka70@yahoo.com niwapige msasa na kuwaeleza kwa nini vita vyao ni mbofumbofu

- Mchungaji, wapiganaji wote wako sawa katika upiganaji, labda tofauti yao iko kwenye kusimamia kazi zao majimboni hilo sio tatizo la wapiganaji wote, lakini ninashukuru kwamba sasa wamekubaliana kuweka nguvu yao pamoja na kupigana pamoja na majuzi wameanza kule kwa Mpiganaji Seleli, that was great idea.

- Naona unajaribu kuwagawa wapiganaji na maneno ya wakoloni kwamba wengine ni better than wengine, no mkuu wote wako sawa katika vita hii, na hawapigani na watu kama unavyodai, ila wanapigana na vitendo viovu vya mafisadi kwa taifa na hasa wananchi wa Tanzania yaani mimi na wewe, sasa haya maneno yako sio shukrani kwa sacrifice wanazojitoa nazo!

- Finally, unaongea wazi nia na madhumuni yao na hizi never stop attacks, kumbe unataka wapiganaji wakutafute kuomba ushauri, kwanza unawaponda halafu unadai wakutafute, maaan wewe ndiye bingwa wa upiganaji ufisadi Tanzania na record yako iko wazi jinsi unavyojua kupambana na ufisadi,

Mchungaji ni makosa sana hasa mbele ya Mungu, kujaribu kuwashusha hadhi bin-adam wengine ili ujipandishe wewe, that is wrong sio tu kisiasa hata kidini mkuu it is wrong!

Mungu Aibariki Tanzania.

Respect and Out!

Field Marshall Es!
 
Rev. Kishoka,
Ninakubaliana na wewe kabisa kuwa hii dhana ya hawa wanaoitwa 'wapiganaji' imesimama katika kulinda na kuhifadhi maslahi binafsi na hasa madaraka waliyokuwa nayo. Ukiangalia kwa makini from the body language hakuna dhamira ya kweli kwa yale wanayoyaongea rather than ni jinsi gani watarudi tena Dodoma kama wabunge. Ina kisiwa kuwa uchaguzi mkuu ujao wa 2010 utakuwa mgumu kwa maana baadhi ya wabunge licha ya kuwepo wagombea kutoka kambi za upinzani, hofu kubwa ya upinzani ipo ndani ya wanachama wenyewe kwa wenyewe ndani ya CCM. Hii hofu inazidi kukua kwa jinsi zinavyojijenga kambi za mivutano ndani ya CCM.
Hivyo basi, wale ambao ni waoga inabidi watafute namna ya kupiga kelele kadri inavyowezekana ili wasikike na kupata attention ya wapiga kura wao dhidi ya yeyote atakayejitokeza kupingana nao. Hili kundi la 'wapiganaji liko tayari hata kuhamia upande wowote ule iwe ni wa ndani ya CCM au nje ya CCM ili mradi tu lihakikishiwe kuwa 'wapiganaji' watarudi tena Dodoma next year kama wabunge.

To be sincere, ubunge ni kiti kinachotafutwa kwa udi na uvumba hasa kwa wale wanaojua ni namna gani wananufaika kwa kuwa wabunge.

Mkuu mbona naona inakuwa rahisi zaidi kurudi Dodoma kama wakimuunga mkono Rostam and co? Mimi naona hawa wapiganaji wanaangalia maslahi ya taifa zaidi kuliko maslahi yao binafsi. Kama wangekuwa na maslahi binafsi si wangeanza kumtukuza Rostam tu, au kujiunga na camp ya mafisadi na kula hela za wizi. Naona it is simpe kurudi bungeni, kujineemesha kwa kuwa on mafisadi side, ni muhimu tukiwapongeza wapiganaji, kwa kuwa wanachopigania zaidi ni maslkahi yetu wadanganyika.
 
- Mchungaji, vita vya wahujumu uchumi huwezi linganisha na vita ya sasa ya mafisadi, wahujumu uchumi walikuwa wauza colgate na sabuni za palmolive mtaani sio wezi wa kama mafisadi wa EPA mkuu, huu mfano ni batili kabisa on the ishu ya vita vya ufisadi.

Field Marshall Es!

Mkuu Mzee FMES, Heshima mbele!

Vita ya wahujumu uchumu haikuwa ya wauza colagate na sabuni, ilikuwa njama kubwa ya Mapapa waliokuwa wanahodhi bidhaa kwa kuzitoa kwenye soko na kusababisha upungufu wa kila kitu. Kumbuka ni katika kipindi hiki zilifanyika njama za kumpindua Mwalimu.
 
Last edited:
Field Marshall Es,
Mkuu ujumbe mzito sana unaoutoa hapa, hasa kwa mtu kama Mchungaji inanipa shida na wasiwasi sana na imani yake kwani yeye kama mchungaji anafahamu vita ya YESU...Yesu alikabiriana na Utawala mzima wa Pilato sii majeshi tu hadi wananchi wenyewe Wayahudi na matokeo yake alishindwa kimwili, lakini ujumbe wake ulifika.. Leo hii dunia nzima ina waumini wake wasiopungua billioni mbili zaidi ya utawala wowote duniani. Sasa tumejifunza kipi kutokana na hadithi nzima ya maisha ya Yesu! - bila shaka, NENO ndilo muhimu kuliko mtutu wa bunduki!
Wanachofanya Wapiganiaji ni kidogo sana lakini matunda yake yanaweza kutuonyesha sote njia na tukaelewa uharamu wa matendo ya Mafisadi ambao hadi leo hii nasoma mada zinazowatukuza. Ujumbe bado haujafika kwa kina Ndivyo Tulivyo, hivyo kazi yao bado kabisa, ndio kwanza inaanza!
 
- Mkuu Mchungaji kama kweli huamini kwamba wapiganaji ndio wenye jawabu la matatizo yetu mengi as a nation for now, basi usingekua na tatizo nao, ninasema hivi wapiganaji ni good people tena wenye good intentions kwa taifa, Mungu awape nguvu na busara zaidi ili waweze kuendelea kupigania taifa na masilahi yetu wananchi,

- Na sisi wananchi tuwape support, tushirikiane nao ili waweze kulisaida taifa letu, kushindana nao na kuwakatisha taama haiwezi kutusaidia wananchi wala taifa, hawagombei power maana wanazo tayari hizo power, Sitta ni speaker wa bunge letu tayari sasa anagombea power ipi tena kwa kupinga ufisadi?

Ninasema Mengi ni tajiri wa ajabu sana sasa kwa kupigania taifa dhidi ya mafisadi anatafuta nini kama sio kujitoa tu kwa ajili ya taifa lake? Tuwe na shukrani jamani, haya mambo hayakuwepo huko nyuma hivi mmesahau kwamba huko nyuma hawa wapiganaji wangeishia kisiwa cha Mafia walikoishia kina Seif Bakari na wenzake? Na huyu Rais Kikwete pia apewe heshima japo kidogo, maana kama sio yeye huu uhuru wa wabunge na viongozi wetu wa vyama vya siasa usingekuwepo,

- Ni kweli tuna matatizo mengi sana, lakini la ufisadi ndio namba moja likitatuliwa hili basi mengine yote yatajiondoa yenyewe, sasa tuwape support wapiganaji badala ya kutaka kushindana na kuwaponda, hatuwezi kupata hata baraka za Mwenyezi Mungu kama hatuwezi kuwaheshimu na kuwaunga mkono wapiganaji.

Respect.

Field Marshall Es!
Mkuu FMES,Saluti Mkuu! Hapo juu nakunukuu ukisema "tatizo kuu ni ufisadi na likitatuliwa matatizo mengine ya taifa letu yatajiondoa yenyewe", ndivyo ilivyo Mkuu? Sio kwamba ufisadi (malfeseance) ni matokeo ya matatizo makuu ya Taifa letu tokea na kabla ya Uhuru? Sio kwamba kwa namna moja au nyingine ufisadi umetokana na mfumo wa uchumi aliotuachia mkoloni ukichanganya na mfumo aliojaribu kuujenga Mwalimu? Mkuu FMES hebu jiulize toka uhuru hadi leo 'njia kuu za uchumi' kwa kusema ukweli nani kazishikilia? Na huyo aliyezishikilia ana hulka gani? Jaribu ku refresh your memory seke seke la watu kupanga mawe miaka ile alfajiri RTC na NDL lilisabababishwa na nini na nani walifaidi na kwa njia gani? Vibali vya 'import' na 'exchange control' benki kuu nani alifaidi miaka ile? Mkuu jiulize toka tupate uhuru hadi leo nani hasa wamekuwa wakifaidi cream ya uchumi wa inji hii? Jiulize miaka ya sitini,sabini hadi themanini ni kundi gani la watanzania lilikuwa likisomesha watoto oxford na cambridge? hapa nazungumzia miaka hiyo. Sorry to mention names na Mungu anisamehe hebu jiulize Mkuu FMES unadhani kina Jeetu Patel, Rajani , Andy Chande, Lord Rajpar et al ( wakati huo kina RA wananyonya) wameanza na kula hutu tu vijisenti twenu mnatopigia kelele hutu twa EPA na Kagoda,tujisenti ambatwo kwao ni chicken feed? is that what you think Mkuu? Mkuu tuache kuangalia tulipoangukia tutafute tulipojikwaa. Leo hii tutaona ufisadi ndilo tatizo kuu,si kweli hata kidogo,tatizo ni mfumo wa uchumi.Nchini Rwanda si kwamba wenye hulka ya ufisadi hawapo,la asha wamejaa tele lakini mfumo wa uchumi unawazuia kufisadi.Hata ukiwachinja hao ambao leo unawaita mafisadi bila kubadili mfumo wa uchumi tutaendelea kulalama tu hadi mapambazuko na kwa taarifa yako hata umlete Chadema/CUF/TLP madarakani leo so long as mfumo ni huu tulionao sahau mafanikio! Ndio maana nasema ifikie pahala tuweke politic pembeni tutafute hard nosed solutions za matatizo yetu,tukishayatatua ndo turudi kwenye mchezo wa siasa.Salaam Aleikum, nakutakia Swaum njema Mkuu FMES kama umefunga!
 
MODS hii mada imepindishwa haya yote yapelekwe kule kwa MJJ topic ya "wapiganaji" hapa ni Kamati kuu na yatokanayo ndo tunahitaji kujua
 
Back
Top Bottom