Wewe unapenda sana kuzungumzia mstakabala wa CCM Zanzibar, lakini mbona hukamilishi story yako kwa kueleza nini mbadala- sasa. Wacha nikusaidie kidogo. CUF haimo kabisa mawazoni mwa Wazanzibari walio wengi. Kama CCM inapigwa chini, ujue CUF inapata kipigo mara mbili. CUF (katika hali yake ya hivi sasa) siyo chama ambacho Wazanzibari wanakikubali. Huo ndio ukweli wa mambo.
Napenda kuzungumzia uhai wa Sultani CCM kwa sababu ameshafikishwa ukingoni na dalili za wazi zinaonekana ni wakati tu umibakia wa kubwagwa na chini ,Chama mbadala sio Mzanzibari bali dunia nzima inajua kuwa ni CUF ,naona unauliza mbona mchana haukuitwa usiku ?
CUF sasa hivi ina nguvu kuliko wakati wowote ule kule Zanzibar hilo halitaki mjadala ,maana uchumi wa dunia umetetereka na ujue na CCM nayo haina mshiko ,huo ndio ukweli ,halafu kule hivi sasa wananchi hawatizami uchumi wa Nchi wala umeme upo au haupo maana siku mbili hizi wamewawashia umeme na maji kwa sababu ya uchaguzi wa magogoni ,yaani mambo yenu ya kitoto kabisa ,jamani wakati wa kupewa peremende umekwisha na hilo ndio moja litakaloelezwa katika huo mkutano wa mafisadi kuwa wakati wa kubebana umekwisha na hautarejea tena ,watu wanakwenda mbele ,hivyo kitakachozungumzwa huko ni kuwa uchaguzi unaokuja utakuwa wa haki na usawa mambo ya kutegemea polisi na majanjawids umepitwa na wakati aliyepora ndio keshapora ,kwa ufupi awamu ya Kikwete na Karume ndio awamu ya mwisho kutumia mbinu za kukwapua kura na kubadilisha matokeo ,kwa chaguzi zijazo kila chombo kitatakiwa kuchunga dhamana yake ,usifananishe Tanzania na Zimbabwe au Kenya au Nchi zingine za Kiafrika utakuwa unakosea sana, Tanzania namna inavyotaka sifa haswa huyu JK Mrisho basi utaona mambo yatakavyowabadilikia jamaa zako ambao wanaona ,mbinu za kutumia polisi kukimbia na masanduku ya kura utazidi kutumika na kuwanufaisha wafuasi wa Sultani CCM.
CCM imeshasoma kuwa Nchi haiwezi kuendeshwa na matokeo ya wizi na kulazimisha utawala ,maana kufanya hivyo itakuwa hata heshima baina yao inapungua ,tumeona ni jinsi gani CCM imeweza kutwaa madaraka katika uchaguzi uliopita ,malipo yake ndio haya tunayopigiana nayo makelele ,maendeleo hakuna ,viongozi wote wameingia kwa rushwa hakuna anemsikia mwenziwe kila mmoja ni mbabe ,hakuna anaemsikiliza Kikwete kwa vitendo maana wote asiejua hili analijua lile ,viongozi wanaogopana kila mmoja anamwona mwenziwe ana marazi ya umeta.
Tusiandikie mate sikiliza dongo litakalorushwa na Kikwete yaani mtashangaa ,yeye mwenyewe atajiweka katika kundi la kuwa yupo tayari kushindwa au kukubali matokeo yatakavyokuwa ,lakini kwiba hakwibi tena ,atatizama hatima ya Mwenyezi Mungu itakavyoangukia akishinda au akishindwa ataamini kuwa haki imetendeka na ndio gumzo kubwa atakalowaambia wenziwe wakiwemo CCM-Zanzibar kuwa haiwezekani kila siku waambiwe ni wezi ni lazima uchaguzi uendeshwe kwa haki bila ya manung'uniko kutoka upande wowote atakae shinda awe ameshinda kwa ridhaa ya wananchi na sio nguvu za dola.
Hivyo kama unategemea internate za ofisi na ulaji wa CCM basi anza kufungasha na kutafuta mradi utakaokuwezesha kuonekana tena hapa JF la si hivyo ndio utupe buriani kabisa.