CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Apr 8, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - The dataz nilizozipata leo kutoka ndani ya CCM, ni kwamba Kamati Kuu ya chama hicho inatazamiwa kukutana rasmi hivi karibuni, hapa jijini Dar-Es-Salaam, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri yetu Mh. Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa dataz hizo:-

  1. Tarehe 17-18, April 2009 kutakuwa na kikao cha Sekretariat.

  2. Tarehe 19, April 2009 itakuwa ni kikao cha Kamati ya Maadili.

  3. Tarehe 20-21, April 2009 itakuwa ndio kikao rasmi cha Kamati zote, kwenye Kamati Kuu ya CCM.

  - Kikao hiki kinapewa umuhimu mzito sana na wataalamu wengi wa mambo ya siasa nchini kutokana na mivutano mikubwa sana inayoendelea kwa chini chini, baina ya makundi mbali mbali yanayowania uongozi wa juu wa chama hicho, yakiwa pia na lengo la uongozi wa juu wa Jamhuri yetu, ifikapo Mwaka 2010.

  Je kikao hiki kweli kitaweza kubadilisha kitu chochote, kuweka muongozo sahihi, au kusimamia masilahi ya taifa kwa manufaa ya umma? Tunakisubiri kwa hamu kubwa sana kikao, na kuanzia leo tutajaribu kuwaletea yale yote muhimu yanahusiana na kuelekea kwenye hiki kikao, huku tukiendelea kujadiliana mengineyo yanayokaribiana na hiki kikao, tukiangalia zaidi masilahi ya taifa.

  Mungu Aibariki Tanzania.

  Wazee wa sauti ya umeme Field Marshall Es!
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu, tunashukuru sana data ulizotuwekea, naomba tu niseme kuwa tusiiwekee matumaini makubwa hivyo isije ikawa usanii kama ule wa Azimio la Butiama - that never happened.
  Kama una dondoo kuhusu ajenda basi utuhabarishe, shukrani!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kigogo alia makundi CCM :Tuesday, 07 April 2009 16:17

  Na Gladness Mboma

  Majira

  KATIBU wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Amos Makalla amesema makundi mengi yanayojengwa ndani ya chama hicho ni ya tangu mwaka 2000 hadi 2005 ambayo kwa sasa yamegeuzwa kuwa miradi.Bw. Makalla alitoa kauli hiyo jana.

  "Inashangaza sana mpaka sasa watu wanaendeleza makundi na visasi ya uchaguzi mkuu wa tangu mwaka 2000 hadi 2005 na hayo makundi ndiyo yanayorudisha nyuma chama na si kitu kingine.

  "Ukitaka kuwa mwanasiasa mzuri unatakiwa kupunguza maadui na kuongeza marafiki. Ni lazima tuwe kitu kimoja, makundi hayajengi bali yanabomoa," alisema. Alisema makundi hayo yamekuwa yakichukua ajenda ya kupambana na rushwa na ile ya ufisadi ambayo ni ya CCM, huku wengine wakiwa wamesahau madhambi yao.

  Bw. Makalla alisema alishangazwa na kauli ya Waziri Mstaafu Bw. Hassy Kitine aliyoitoa hivi karibuni kwa vyombo vya habari kwamba Serikali inaendeshwa kwa makundi na Idara ya Usalama wa Taifa inapwaya.

  "Bw. Kitine akumbuke kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliojisahahu huku akijua ana madhambi makubwa ambayo leo angekuwa ameozea gerezani kwa kashfa ambayo iliwahi kumkumba ya matibabu ya mkewe. Je, anakumbuka?

  "Kitine asitufanye Watanzania wasahaulifu. Je, anaweza kuwa miongozi mwa watu wasafi? Ieleweke ajenda ya kupambana na rushwa na ufisadi ni ya CCM kama chama na si kikundi cha watu wachache," alidai. Alisema wapo wana-CCM ambao sasa wameamua kuibuka na kuikosoa Serikali wakati wangekuwa vijijini au magerezani kwa kashfa ambazo ziliwahi kuwakumba enzi za uongozi wao.

  Wakati huo huo, Bw. Makalla amedai Rais Jakaya Kikwete ataendelea kuwa Rais 2010, kwani wapinzani hawajawa tayari kwa urais bali wanataka kuokoteza mitaa, vitongoji mwaka huu na mwakani wanajipanga kwa ubunge na udiwani na si urais. Aliwataka viongozi kutofanya mikutano ya ndani na badala yake wafanye mikutano mikubwa ya hadhara na kuzungumza na umma kile ambacho Serikali imefanya.

  ___________
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,467
  Trophy Points: 280
  Asante FMES kwa taarifa hizi. Uzuri wa nchi yetu, ni nchi ya chama kimoja kwa demokrasia ya vyama vingi, hivyo sasa ni macho na masikio yetu katika vikao hivi bila kujali vyama-jina vilivyopo ambao viongozi na mashabiki wote ni kinachoendelea kwenye chama dola-CCM ndicho kinachoamua mastakabali wa nchi yetu.

  Pamoja na ajenda kuwa siri, ajenda kuu ni safari ya kuelekea 2010, tayari wapiga firimbi wa hamelini wameshapuliza kipenga wanataka watu wapishe njia ili iwe nyeupe kwa mkulu, huku wapenda demokrasia ya kweli, wakisisitiza chama ni katiba sheria taratibu na kanuni, huku wakitilia mkazo hakuna kanuni waka taratibu ambazo hazijaandikwa.

  Pia ni kikao muhimu cha watu kunyooshewa vidole kama wasaliti wa 'utaratibu wetu tuliojiwekea' dhidi ya utekekezaji wa katiba ya chama katika nafasi ya kushika usukani wa dola.

  Endelea kutuhabarisha huku tukifuatilia kwa makini.

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi.....Kidu/gu/mu!.
   
 5. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika hali ya sasa hivi Kikao cha Kamati Kuu CCM siyo issue zaidi kuliko kikao cha Bunge au Baraza la Wawakilishi. Msuguano ni katika mstakabala wa wananchi wa Zanzibar na Tanganyika Sasa hili si suala la CCM na Kamati zake. Hata kidogo!!!!!
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Susuviri heshima mbele sana,

  - Maneno yako ni kweli sana, lakini kumbuka as a nation yaani Tanzania, this is all we have for political stimulation kwa wale tunaojali, mpaka siku tutakapofikia kunapotakiwa hatuna choice bali ku-deal na what we have yaani vikao kama hivi, cha muhimu ni kupata the best of important information out of it, kwa sababu Chiligati hawezi kuzitoa, bila kutanguliwa, tunapowawahi na dataz huwa tunawaweka kwenye positon ya kuwalazimisha kusema wazi yaliyojiri, kwa kawaida huwa hawapendi ksuema yote.

  - Cha muhimu ni kujua kiongozi gani huko kwenye vikao vyao anajali masilahi ya taifa, na nani ni fisadi, na nani anaenda kulala usingizi tu.

  Respect.

  FMES!
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama hawana ajenda ya kuwaondoa viongozi na wanachama waliooza kwa kashfa katika chama basi ni usanii tu na wasubiri kunyolewa 2010.Kinachosikitisha hata mafisadi ni wajumbe wa vikao hivyo sijui JK atawadhibiti vipi.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  I love this observation
   
 9. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawana jipya hawa..watakutana then its business as usual! if anything they will have a photo of rostam and mwakyembe shaking hands in front of kikwete na waandishi kuonyesha ccm bado wapo pamoja...yetu macho!
   
 10. S

  Son of the Soil Member

  #10
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani ndugu...ni yale yale tu, sitarajii jipya
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  FMES nakubaliana na wewe lakini naomba kuuliza niprocess gani itatumika katika ku-identify kiongozi fisadi etc kwa kuwa hivi sasa kuna a lot of spin out there!
   
 12. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145


  Wee bwana wee wewe Makala toa hoja na sio mtu, siku zote huyo Hassy wenu mungeweza kumtia jela lakini mnaendeleza porojo tu pia mkikubaliana kukosoana basi hamtakuwa na kulindana kama ilivyo hivi sasa, tafadhali badilikeni nyie msije kuta treni imekuacheni
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hakuna chombo chenye nguvu za juu kisiasa nchini kama Kamati Kuu ya CCM. Hii ni mojawapo ya masalia ya mawazo ya kikomunisti ambayo CCM inapenda kushikiria kwa majivuno. KK ina nguvu kuliko Bunge, Mahakama, Jeshi au chombo kingine chochote. Inabidi usome Katiba ya CCM uweze kuelewa nguvu hiyo.

  Pia tukumbuka mkutano huu kama utafanyika jinsi hiyo unakuja siku chache baadaya kuhoji kwa nguvu zote ni nani anaiongoza CCM.

  Kwa wale walioko Bongo watakuwa wamesoma makala yangu ya kujibu hotuba ya RAis Kikwete kwenye gazeti la Mwanahalisi leo na pia makala ya Tanzania Daima leo. Yote ni katika kuendeleza hoja kuwa aidha CCM ibadilike au ijikute inabadilishwa. Uwezekano wa hilo la kwanza kwa kweli bado ni finyu.

  Tatizo ni kuwa composition iliyopo sasa ya KK siamini kama inaweza kuchukua hatua dhidi ya watu wanaotuhumiwa ufisadi. Naamini wao wako zaidi makini kuhakikisha kunautulivu kwenye chama kuliko kitu kingine (nimelieleza hilo kwenye makala ya "Nani ameguke kutoka CCM" - Sijui TD wametumia kichwa gani cha habari).

  Naaamini lolote litakalotokea itakuwa ni kupeana "makaripio makali" na kujaribu kusuluhisha mvutano ndani ya CCM. Wakati wowote CCM inatishiwa uhai wake, hadhi yake au jina lake, CCM will always act. Kumbuka Ibara 15:1
   
 14. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #14
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sisiem sisiem, chondechonde mnatumaliza...

  Kuna wakati watu tulikuwa na matumaini sana na vikao na baadaye maamuzi ya CCM. Wakati huo umepita (Rejea Kikao cha Butiama hivi karibuni), kwani hata sisiem wenyewe hawajui kama wana dhamana kubwa katika nchi hii hivyo wanatakiwa kuwa makini sana na mustakabali wa taifa hili. Hao wanaoijidai wameshika hatamu ndio haohao waliochangia kiasi kikubwa kwa nchi hii kuwa masikini wa kutupwa...

  Ukisoma Mwanhalisi la leo waweza kulia.. Nanukuu "... Ni kashfa ipi utataja nchini kwetu isiiguse CCM kama chama au wanachama wake mmoja mmoja? Ipi? Nani kaifikisha nchi hii kwenye umaskini wa kujitakia kwa sababu ya kuzembea matumizi ya raslimali za Taifa? Nani? Si ni CCM na viongozi wake kuanzia kwenye uwindaji wa kitalii, uchimbaji madini, ubinafsishaji mashirika ya umma..."

  Kama ndio haohao, (na ndio haohao) chini ya uongozi huu huu wa sasa, hakuna kitu hapa. Napenda kutofautiana hapa, CCM hawana maslahi ya Taifa, wana maslahi yao tu (hasahasa ya mafisadi... maana ndugu zangu wengi kule mashambani ni wanaCCM, lakini humabulia patupu)... tukielekea uchaguzi Mkuu, maslahi ya hao wachache yanatatizwa, hivyo wanakutana ili kuendelea kutugawanyisha umaskini.

  Mungu ibariki Tanzania, isipokuwa CCM.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Toba! hili kundi la wezi na mafisadi sijui linapanga nini tena saa hizi
   
 16. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #16
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania Daima, 08 Aprili 2009, Ukurasa wa 10: Makuwadi wa Ufisadi CCM Wameguke
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Asante Sekenke!
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  This will never ever happen in CCM government!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi WaTanganyika mnakubaliana na hizi kauli za kuwa Vyama vya upinzani hamjawa tayari ?
  Maana Zenji kasi yao wanasema hata wakiamshwa usiku wa manane kupiga kura basi Sultani CCM haoni ndani ni out tena anatupwa mbali sana ,na kila siku ziendavyo ndivyo inavyozidi kuwekwa pembeni na kuambiwa imetosha baba ,Wazenji wanataka kuizima na kuipunguza CCM EMPIRE na kuibakiza huko Tanganyika ,ila juhudi zikifanywa hata baadhi ya mikoa wanaweza kuipunguza CCM EMPIRE ,yaani Mikoa mitatu mikuu ikipunguzwa basi itakuwa hatua si ndogo ,tuikomboe Kilimanjaro Arusha,Mtwara ,Tanga ,Dar es salaam,Mwanza ,Mbeya na Kagera na mikoa mingine kumega mega ,mbona 2015 Usulutani wa CCM utakuwa umebakiza mikia tu.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Huo ndiyo ukweli Susuviri. Kinaweza kikawa ni kikao kingine kitakachojaa usanii wa hali ya juu na hakuna lolote la maana litakaloamuliwa.
   
Loading...