Mkuu Mwiba, hiyo "mentality" ya kwamba wao wamebeba "matofali" basi nyie mtabeba "nondo" haina siha njema sana kwa Taifa! Mnakusudia kuchukua "Dola" na mnaahidi kusimamia "Utawala wa sheria", hivyo nashauri mtumie zaidi wanasheria wenu nguli kupambana na huo uharamia wa CCM mahakamani! Maendeleo ya kidigitali yanawawezesha kupiga picha na hata kurekodi matukio yote ya kihalifu kama mfano wa picha uliyoibandika! Pale mahakama itakapoonekana kuwabeba hao CCM, basi mtakapochukua hiyo "Dola" itawapa ari zaidi ya kufumua mfumo mzima wa kimahakama ili kuhakikisha zinatoa haki sawa kwa wote bila kuangalia cheo au uwezo wa mtu! Tafakari