CCM ivunjike tu

Simkubali Lowassa, lakini kama ikitokea amepewa ridhaa ya chama, mimi na kundi langu kwa pamoja tutamuunga mkono katika uchaguzi mkuu. Ieleweke wazi, Lowassa yupo chini ya CCM na kamwe hawezi kulipiza visasi kwa yeyote yule aliyewahi kuwa kinyume nae au mtu yeyote katika kambi yake. Kwa mnaosubiri CCM ivunjike, mtasubiri sana.

Rai yangu: Imarisheni vyama vyenu vya upinzani ili tuwe na ushindani, hii ya kuvizia mchezaji apate jeraha ili ndio mpate ushindi ni katika kutia huruma. Imarisheni vyama vyenu.
 

Mkuu Mkandara nimekuelewa kwa sana hapa.

Surprisingly watu hawajawahi kuliona hili. Time will tell.
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi sema na nitaendela kusema tena kuwa haya yanayotokea ndani ya chama kikongwe na tawala ni lazima yatokee ili mabadiliko yatokee. Bila haya yanayotokea watanzania hawawezi fanya mabadiliko kamwe hata iweje!! Naamini ni mpango wa Muumba wetu baada ya kuona tumelalamika sana bila kuchukua hatua, na sasa anachukua hatua yeye kwa namna yake, hakika muda wa watanzania kukombolewa umefika.......Chocheeeni kuni.
 
Mzee Mwanakijiji, uliyoyaandika ni bayana. Hatimaye yaliyotabiriwa yanaelekea kutimia. Inafurahisha na ninapata amani ya moyo kwani kupasuka kwa CCM ndiyo mwanzo wa "Tanzania Mpya". Hawawezi kukatana majina kwa upande mmoja, na hawajajiandaa kushindwa kwa upande mwingine. Uongozi kwao ni kama bidhaa, Mwenye pesa nyingi ndiye mshindi. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Last edited by a moderator:
Imekuwa kama watoto wadogo,eti Lowasa anatishia wenzie akikatwa atamleta Dr.Balali,sasa hicho ni chama ama ni genge la wavuta bangi nibangue

Kwa kauli hizi bila shaka CCM wamesha muondoa hata kwenye kujadiliwa
 

1.Fear of the UNKNOWN

2.Fear of DARING
 
vyombo vya dola vitakapoiacha ccm ijiendeshe kisiasa kama chama cha siasa, hapo hapo kitavunjika. ktk hali ilikoifikisha tanzania ni bora na nafuu sana ccm ikivunjika na kutoweka kabisa. hata kwa usalama wa taifa hili ccm haifai tena. ni bora iondoke iwe historia na tz ianze upya. naamini kama taifa tutaendelea zaidi kuliko kuwa tena chini ya utawala wa ccm
 

Na ivunjike tu! by Mizengo Pinda.
 
Shida sio CCM kufa kabisa
CCM now ni kama 'dead man walking'
shida ipo kwenye replacement tukishaizika CCM
je wananchi wanaiona na kuiamin replacement?
we umeiiona?

Hoja ya ajabu kabisa hii!

Yaani huoni walio better kuliko huyo dead man anaye walk!

Hii inashangaza sana

Tusiwe na mawazo ya aina hii
 
Ndugu yangu Pasco yawezekana mapenzi yakatufanya tusione hali halisi.

Kwa maisha ya kawaida ni lazima U-wish au kutamani au Uote kuwa na nyumba au gari au chochote kile.Na ndoto hizi zawezekana zikaja baada ya kuona mwenye nyuma ana kunyanyasa ukawa unawish ungekuwa na nyumba yako na yawezekana matamanio yako yakakupeleka kule unakotamania yaani kuwa na NYUMBA.Yawezekana jirani anakutambia na miguu minne yake yaweza kuwa Prado au benzi basi ukatamani ungekuwa na japo vitz au Suzuki na wishes zako zikigeuka kuwa ndoto na ukaifanyia kazi nina uhakika matamanio yamo yakawa kweli ukapata vitz au suzuki.

Wishes za watanzania wengi au ndoto ya watanzania ni wengi ni kuondokana na Rusbwa na ufisadi uliokithiri unaowanyima watanzania haki zao za msingi hivyo wishes zao ni pamoja na CCM kuvunjika vipandenvipande tena siyo viwili bali zaidi ya viwili.

Ndoto za watanzania wengi ni kuiondoa madarakani huyu mwizi,mbadhirifu,mfugaji wa rushwa tena kubwa,tunatamani kwa njia yoyote ile kupata uhuru wa kuwaonod hawa na moja wapo ni hawa wajamaa kusambaratika kwa namna yoyote ile ila lazima wasambaratike.

Sababu tumeshajua mbinu zao inabidi kuanza kuzifanyia kazi na mojawapo ni kutafuta plan B maana hii A yaelekea kushindwa..UHURU WA KUJIANDIKISHA tumeshanyang'anywa na hapo ndipo tunatamani vyama vya upinzani kutafuta plan B.Na siyo wao tu hata sisi dreamers na wishers tuingie tusaidiane kutafuta plan B.

Tatizo kubwa mapenzi ya watu yametufunga macho kuliko mapanzi na uzalendo wa nchi yetu.Tatizo siyo Chadema wala UKAWA tatizo watanzania hatujui nini tunataka..
 
Wengi wetu bado wanaamini kuwa kwa sababu ccm haijabadili logo yake kutoka jembe na nyundo, basi ni chama kile kile chenye kauli mbiu ya "DAIMA NITASEMA KWELI, FITINA KWANGU MWIKO" wakati sasa uongo na fitina ndizo nguzo kuu za chama!
R.I.P Mwalimu.

 
Kingunge leo kaongea maneno mazito na katoa angalizo juu ya mpasuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…