CCM itatawala nchi kwa karne nzima

Uoga na ujinga wa watazamia nia ni mtaji kwa chama cha mwalimu magufuli et al
 
Mkuu nakubaliana na baadhi ya hoja zako. Ni kweli baadhi ya watanzania ni wajinga na waoga. Hata hivyo ujinga na uoga wa watu hawa unapaswa kukomeshwa kisiasa, lakini hakuna hatua za maana toka kwa wanasiasa wetu. Mathalani, CCM kwenye chaguzi zote wanafaidi ujinga wa kabila furani toka kanda ya ziwa, CCM wanafaidika na mikoa ya Shinyanga, Geita, Mwanza na Simiyu. Hili linaendelea tangu mfumo wa wa vyama vingi uanze, lakini hakuna hatua za maana toka vyama vya upinzani kujikita kwenye mikoa hiyo, hatimaye kuvunja vunja nguvu za CCM zinazowapa kiburi kwenye ukanda huo. Maana wingi wa watu wa mikoa hiyo, ndiyo unaoamua mshindi. Si hivyo tu, vyama hivi ni lazima vionyeshe kujitambua, visimamie AJENDA zao, ijulikane na ionekane kweli vinasimamia. haiwezekani Leo unasema furani fisadi, kesho unamfanya mgombea wako. Kitendo cha aina hiyo ni dharau kwa wapiga kura.
 
Kaka hesabu ni ujinga tu kwa ujumla wake.
Ila tofauti na wengi wanavyofikiria kuhusu huu ujinga mimi naenda mbali Zaidi mpaka kwa wanasiasa ambao wapo waliosoma (tusiwaite wajinga) na wenye uelewa mpana. Hawa wanasiasa hawajaweza kuwa na uwezo wa kuisoma jamii na kuwahubiria kile wanachokihitaji. Mfano ni mitaji wanayoitumia katika siasa zao kwa lengo la kuiteka jamii husika. Hawajaweza kujua kuwa habari hizi haziwafikii asilimia kubwa ya watanzania na pia hawajaweza kujua kuwa watanzania wengi si wakereketwa wa habari. Tweeta, fesibuki, jf nk. hata hilo bunge live ambalo walichukulia kama mtaji, sidhani kama kuna hata asilimia tano ya wapiga kura walikuwa wanaangalia bunge live
Mfano mzuri ni wanawake ambao wengi hupiga kura, hawa hawafuatilii chochote katika siasa Zaidi ya maigizo na tamthilia kwenye TV. Ukitumia mtaji kama mauaji (tena unaweka na picha) katika siasa hapo ndo hata hutawapata kabisa kwa kuwa akishaona habari za mtu kuuwawa tu basi hawezi soma mpaka mwisho.
Kwa hiyo huu ujinga wa watz ni wa wote, usidhani aliyeenda shule anakuwa tofauti na asiyeenda shule, ni kila mmoja kwa namna yake.
Ukiwa kwenye mtandao waweza jua sasa watz wanaamka, kumbe hata siyo wapiga kura.
Kuna mzee mmoja clip yake nishaipoteza, alikuwa anahojiwa kuhusu rushwa ya chumvi na nguo wakati wa uchaguzi, alisema: HIVI NDO PEEKEE NAWEZA PATA, WAKIONDOKA HAPA WAKIRUDI WANATUFUNGA JELA MAANA WANAKUWA TAYARI NA MAMLAKA



 
Chadema ilipopata fursa ya kukamata dola ikatuletea fisadi na hivyo watu wakaamua kwa dhati na kiakili mno kuwa ni lazima waibakishe CCM.

Kwa mantiki hii CCM lazima itawale milele !

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
Id yako inasawiri ulivyo
 
suala la uoga Mimi nakataa.
vita sio suluhisho mzee.tumeona nchi nyingi zilizotaka kujikomboa kwa vita mpaka Leo hakuna amani.
kikubwa NI NEC.huru.wansnchi waamue wanamtaka nani kihalali.demokrasia ichukue nafasi .tatizo CCM wanataka kufanya kwamba Wao ndo wana haki peke yao ya kuongoza.
hawakumbuki kama nchi hii NI ya demokrasia.mabavu uonevu hila.si mahala pake.
unakubalika tuonyeshe kweli unakubalika.sio KWA njia ya wizi na vitisho na umwagaji damu.
 
Yes! Woga pia ni tatizo kubwa linalochangia CCm kuwepo madarakani hadi leo. Sijui chanzo cha huu woga ni nini. Naamini hakuna nchi yenye raia waoga kama Tanzania. Ni kama laana.
ujinga mkuu ..ukiwa mjinga nirahisi kutawaliwa na hofu kwa sbabu unakuwa upo upon tu hutambui umuhimu wakuipigania haki yko pindi unapo pokonywa ..wazee wetu walikuwa wnakamatwa na kwenda kuuzwa kama watumwa na mabepari walioshika mtutu mmoja wa bunduki huku wao wakiw wamekusanywa kwa wingi kama kuku huku wakiwa hawana maamuzi yyote Yale kwaajili ya ukombozi wao ...na ccm wanajua kabisa kuwa watanzania niwaoga na wajinga ndio maana inapofika nyakati za uchaguzi mkuu huwa wanaitumia TV ya taifa kuonyesha vita ya kagera kwa mantik yakuwatia hofu watanzania..na kwa hilo wamefaulu
 
Mkuu Ngabu nakuunga mkono asilimia 100, woga wetu ndio umasikini wetu
 
CCM ni chama dume. Viva CCM viva Magufuli. Chadema tupa kule
 
watanzania niwaoga mkuu ..tena waoga haswaa njia yakukitoa chama tawala madarakani sio hiyo moja tu ykukitegemea chama pinzani ..kwa haya yaendeleayo sasa ktk nchi hii ingekuwa ni nchi nyingine sasa hvi tungeshaskia waasi wapo msituni ...hiii nchi RAIA wake sis ni mazoba kabisa
 
habari njema kwa wauaji na watoa makafara wakisikia kutawala karne nzima, utamu wa damu ya mwanadamu unawafanya wajilambe midomo saaa hii wakisoma hii thread
 
Kwani hujui ilo? Kwa sasa ni miaka 57 tokea imeanza kutawala
 
Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.
Wewe binafsi unaweza kuzipiga na polisi katikati ya bara bara? Acha ujinga wa kuhamasisha na kuchochea vurugu. Mnachochea vurugu halafu watu wakipigwa risasi mnaanza kuwalaumu polisi.

Nonsense kabisa!
 
Tupambane na polisi kwa sababu gani kwa mfano?
Tukiitoa ccm madarakani ni chama gani kinaweza kuongoza nchi?
Kwani Ccm imeweza? Miaka karibu 60 ya kuongoza nchi bado mnambwela tu!
 
Kwanini unataka kupigana na Polisi?

Polisi wanapiga kura?

Tatizo lako lipo ktk box la kura

Wapo wanaoipigia kura CCM na ni wengi.

Huwezi kushinda uchaguzi kwa kupigana na Polisi.
Nina mashaka na IQ yako. Unakijua unachoongea au?
 
Kwa kiasi uko sawa lakini utaipataje tume huru?! Amini usiamini ni mpaka damu tena ya kutosha!! CCM hawawezi kukubalia tume huru wanajuwa watakuwa wameisha!!

Pili ni kuhusu nchi zilizopiga hatua na hasa Africa ktk chaguzi huru na hata ki uchumi ni zile walizouana na kupinduana kwa sana . Nchi za Africa magharibi sasa hivi wako vizuri , mpinzani akishinda anapewa bila shida mf. Nigeria, Senegal, Ghana, na zile zilizojaribu kung'ang'ania viongozi walifurushwa na ECOWAS. Lakini Africa mashariki, tunajifanya tuna amani na huku tunaongozwa na madikteta, wasiotaka upinzani kwao sawa na uasi .
Sasa udikteta utauondoa kwa sala ???!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…