Huu ni utabiri wangu na mtakuja kuukumbuka. Ni kweli ulio wazi kwamba Watanzania wengi wameichoka CCM, lakiji wanashindwa kuiondoa madarakani kwa sababu Mwenyekiti wao ambaye ndiye Rais was nchi ndiye mwenye madaraka ha kuunda na kuisimamia Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC).
NEC ndiyo inaamua kumtangaza mshindi yoyote inavyotaka. Matokeo ya urais ndio kabisa hayatakiwi kuhojiwa.
Hivi kama chama kinapendwa na wananchi, mbona kimejitwisha madaraka makubwa kiasi cha kuvuruga demokrasia?
CCM wajue hata Mugabe hakupanga kujiuzulu kipindi hiki, hakujua kama jeshi litamgeuka, alidhani mambo yatakuwa shwari hadi afie ikulu.
Nyerere hakuwa mjinga kuruhusu vyama vingi hata kama wengi hawakuvitaka.
CCM hawataki mabadiliko ya Katika maana wanajua iliyopo inawalinda. Wanadhani wataishi milele madarakani, lakini ipo Sikh wataondoka madarakani kwa aibu kama Mugabe.