CCM itang'oka kwa aibu kama Mugabe

CCM itang'oka kwa aibu kama Mugabe

Huu ni utabiri wangu na mtakuja kuukumbuka. Ni kweli ulio wazi kwamba Watanzania wengi wameichoka CCM, lakiji wanashindwa kuiondoa madarakani kwa sababu Mwenyekiti wao ambaye ndiye Rais was nchi ndiye mwenye madaraka ha kuunda na kuisimamia Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC).
NEC ndiyo inaamua kumtangaza mshindi yoyote inavyotaka. Matokeo ya urais ndio kabisa hayatakiwi kuhojiwa.
Hivi kama chama kinapendwa na wananchi, mbona kimejitwisha madaraka makubwa kiasi cha kuvuruga demokrasia?
CCM wajue hata Mugabe hakupanga kujiuzulu kipindi hiki, hakujua kama jeshi litamgeuka, alidhani mambo yatakuwa shwari hadi afie ikulu.
Nyerere hakuwa mjinga kuruhusu vyama vingi hata kama wengi hawakuvitaka.
CCM hawataki mabadiliko ya Katika maana wanajua iliyopo inawalinda. Wanadhani wataishi milele madarakani, lakini ipo Sikh wataondoka madarakani kwa aibu kama Mugabe.
nalo neno
 
Ishu ya Zimbabwe kamwe na haitokuja kufanana hata kama CCM ikitoka madarakani: why
ZANU pf ambacho ndicho chama cha Mugabe ndicho kilichoona Mugabe aachie ngazi wakiongozwa ZDF.
wanachama wa ZANU pf pamoja na bunge walitaka kupiga kura za kutokua na imani ni kiongozi wao wa chama ambaye pia ni rais. Hii ni kutokana na
Umri wake, hali ya kiuchumi kuzorota, maisha ya wananchi na kushuka kwa thamani ya shilingi.
Baada ya Mugabe kumwandikia barua spika wa bunge kuwa amejiuzuru kwa hiyari wananchi walishangilia kwa furaha si kwasababu ZANU pf imeondoka madarakani Bali ni kwasababu mzee Mugabe amepumzika, Hata atakayemrithi Mugabe kwa mujibu wa taarifa ni aliyekua makamu wake wa rais kabla kumtimua na kumfuta uanachama kwa shinikizo la mkewe bi Grace Mugabe.
Kilichotokea Zimbabwe ni Mugabe kukosa support ya vyombo vya usalama. Nyengine zote kuhusu ZANU PF ni blaa blaaa tu. Hao viongozi wa ZANU ndio wamekosa imani na Mugabe kiasi hicho ndani ya kipindi cha wiki 1 na kumgeuka? Kama ex VP asingekuwa na support ya vyombo vya usalama basi mpaka leo Mugabe angebakia kuwa raisi kwa unafiki wa viongozi wa chama tawala. Haya ndiyo yanayoikumba siasa za Africa in general. Utashangaa watu wanavyokugeuka ndani ya sekunde wanapojihisi hawatishiwi na maisha yao. Africa inaongozwa kwa vitisho na ukweli ni kwamba it's not worth loosing your life to gain popularity! Play your cards right.
 
Back
Top Bottom