Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,231
- 113,608
Sasa hivi kila dalili zinaelekea kuonyesha kuwa watu wameshaukubali utawala mpya wa Kikwete licha ya malalamiko ya mizengwe iliyojitokeza katika zoezi la uhesabuji wa kura.
Ni wachache sana ambao wanakataa kuutambua uhalali wa utawala huu. Wengi wameshakubali yaishe na wameshaamua kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Kwa mtindo huu CCM na serikali zake zitaendelea kuchezea watu kwa vile wanajua tu wepesi wa kusahau na kukubali yaishe. Nami nasema kwa mtaji huu tujiandae kutawaliwa na CCM kwa muda mrefu sana.
Yahifadhini haya maneno yangu kwa marejeo ya baadaye.