CCM isipowaondoa "Mafisadi" itashindwa kutimiza ahadi - Tutaiacha

Tangu lini Ngedere akamfukuza Nyani kwenye Shamba la mahindi?
Fupa kalishindwa Fisi ataliweza Mbwa kweli?

Nimeipenda hii. Inaeleza wazo zima kwa ufasaha. Nyani kwa umbile ni mkubwa kuliko ngedere. Wote ni wavamizi katika shamba la mahindi. Ngedere kwa umbile na nguvu zake ndogo, hawezi kumfukuza nyani kwenye shamba. Ngedere anakula mahindi shambani kwa ridhaa ya nyani. Nyani akicharuka, anaweza kumfukuzia ngedere mbali. Ngedere akitaka kushiba, itabidi ale mahindi kimya kimya, bila kumbughudhi nyani.
 
kuna ile kauli wanapenda kuitumia sana ccm kwa wenzao...wamekosa mwelekeo. naona hii inafaa kuwa kauli mbiu yao...chama mufilisi wa mwelekeo
 
Hahahaha, Malaria Sugu! Inaonesha unadalili ya kupona malaria, nakushauri uendelea kumalizia dozi ya dawa unayotumia utapona Mkuu. Upo wapi wema wa CCM? Yapo wapi maendeleo yaliyoletwa na CCM? Wapo wapi viongozi wazelendo wa CCM? Jibu unalo wewe mwenyewe. Wewe na mimi tulikomboe taifa sasa!Tuoneshe uzalendo wetu sasa.
 
Back
Top Bottom