CCM isipowaondoa "Mafisadi" itashindwa kutimiza ahadi - Tutaiacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM isipowaondoa "Mafisadi" itashindwa kutimiza ahadi - Tutaiacha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, May 13, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nilianza kusikia kwamba 'kujivua gamba' kwa ccm, ni kuwaengua viongozi watatu wa ngazi za juu za chama hicho (majina yalitajwa), na walipewa muda wa siku 90 kufanya hivyo. Baadae nikawa nasoma humu jamvini kuwa, tafsiri hiyo ya awali ilibadilishwa, na sivyo hivyo. Baada ya hapo sikuwa na uhakika 'kujivua gamba' ni nini hasa tena, mpaka jioni hii nilimpomwona kijana Nnape akihutubia wana ccm, na kutoa tafsiri ya 'kujivua gamba'.

  Kutokana na Nnape, ccm ni chama kilichotawala takriban miaka 50, kwa hivyo kwa muda wote huo kimekuwa kizee, hivyo kinahitaji 'kujivua gamba'.

  Alisema, "Kujivua gamba ni kuongeza uwezo wa ccm kuwa karibu na wanachama wake". Baada ya kusema hivyo alipigiwa vigelegele na kina mama.

  Nilijiuliza hivi ni kwa nini hao kina mama wanapiga vigelegele? Je wanafahamu kuwa hiyo ni version nyingine ya kujivua gamba tofauti na ile iliyotolewa na Nnape mwenyewe na katibu wa ccm?

  Itakuwa ni vizuri kama chama tawala kitakuwa karibu na wananchi. Hata hivyo ni vizuri zaidi kuthibiti watu na vitendo ambavyo vinaweka chama tawala mbali na wananchi. Hapa ina maana kwamba, ili 'kujivua gamba' iwe ya kweli, na sio tu hotuba za majukwaani, version zote mbili hazina budi kutekelezwa.
   
 2. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kujivua gamba kuna version moja tu, hiyo remix hatuijui, watanzania wana akili siku hizi wanjua kila kinachoendela, ila hao kina mama inabidi wafundwe ili waache kushangilia kifo chao.
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Kweli ccm imekwisha,iko ICU,nimeangalia watu walioudhuria,siamini kwa wingi wao kama wanafika200,sijuhi wakiiona halaiki ya CDM wanajisikiaje,siyo siri CCM wanahaibika sana
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mbona ccm hao hawaji shinyanga ,kahama, bk, karagwe. Tuwachanechane tuwatupe
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyo aliwachagulia hiyo slogan nafikiri aliamka na hangover ya kangara. That was a wrong and stupid slogan. Nyoka ni nyoka tu hata ajivue gamba ni wa kumwogopa.
  So hakuna jipya hapo kwenye chama cha magamba
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli kua uyaone leo wamebadilisha version ya kujivua gamba, hata mie nimemsikia huyu Nape, lakini siku nyingine watakuja wa version ya kuwa kujivua gamba ni kuwaomba wananchi waichukie CDM hebu tusubiri tuone, time will tell
   
 7. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Phrase "Kujivua Gamba" ni kauli iliyomtoka JK kwa bahati mbaya akijaribu kuwafurahisha hadhira yake siku ya kuadhimisha miaka 34 ya Chama Cha Mafisadi (CCM). Ingekuwa ktk hotuba yake aliyoandaliwa na wasaidizi wake (kama ilivyo kawaida ya viongozi wetu Vilaza kama yeye) kusingekuwa na maneno hayo maana phrase yenyewe ina kasoro kibao bila kujali utekelezaji wake usiowezekana. Sababu zangu ni hizi zifuatazo:-
  1. Nyoka ni kiumbe anayeogopwa na wanadamu kwa mabaya yake kutokana na uwezo wake wa kudhuru watu kwa kuuma na sumu yake kali. Hata pale anapokuwa anatumika ktk ngoma lengo huwa kuwashangaza watu tu na si kuhamasisha upole wake kwa binadamu. Jiulize iweje kurekebisha kasoro za muda mrefu ktk chama kufananishwe na nyoka kujivua magamba?
  2. Tangu nimesikia jina JK sijawahi kushuhudia kauli thabiti na ikafuatiwa na utekelezaji kutoka kwake. Hata waliompamba sana ili apate urais walitumia sifa za kijinga kama ni kijana, hajanunua nyumba za serikali zilipouzwa, anasomesha watoto wake hapahapa nchini, ni handsome, ni mweupe, sura yake itapendeza kwenye noti n.k.
  3. Kwa mtazamo wangu namwona JK kama wale watu wanaotenga wenzao ktk makundi mawili tu ya Marafiki na Maadui. Ukiwa rafiki yake atakulinda daima na ukiwa adui atakutesa ile mbaya kuhakikisha unakiona cha moto. Yeye hana watu wa kati (wale ambao si marafiki wala maadui lakini wanaostahili kutendewa haki). Angalia ulinzi wake kwa watu kama Hosea, Rostam, Karamagi, Lowasa na wengine wanaoonekana kuwa rafiki zake tangu zamani ulinganishe na watu kama Sitta, Magufuli, Babu Sea nk wanaotafsiriwa kama wasiokuwa wake. Rostam angekuwa ndiyo Spika hata kumfikiria Anna Makinda anaweza kusingekuwapo. Angalia wanaopelekwa Mahakamani kwa ufisadi. Mramba, Mgonja, Liyumba nk wanaoonekana si wake na angalia kina RA, Manji nk walio wake wanavyoendelea kupeta wakati hata wao walinufaika.
  4. Kwa ufupi watanzania jiandaeni kwa mshangao ujao kwani kama mnadhani JK ana mpango wowote kwa ajili ya Taifa hili au CCM mmeliwa! Wenye akili tunajua angekuwa na jeuri ya kumwadabisha yeyote katika ufisadi katika hayo magamba ambayo yeye ni mmojawapo angeshaanza zamani. JK ni mwoga haswa. Hata ripoti ya Richmond ilisomwa na kina Mwakyembe kwa kuwa aliogopa kuizuia vinginevyo ingezuiliwa mapema. Samahani kwa kusema hili lakini JK na CCM ni ma-Bogus haswa!
  5. Ukitaka kujua JK ni Bogus angalia inayoitwa mipango yake ya uchumi halafu usikie mtu anakwambia alisoma na ku-graduate BA Economics.
  Nimechoka kumzungumzia huyu jamaa na labda sasa ifikie wakati watanzania tutumie muda wetu kuwaelimisha wanaoshabikia ulaji wa CCM wajue kuwa Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi pamoja na kasoro zao mbalimbali wanaokekana kuwa na mipango ya kupambana na umasikini wakati sisi tunachekacheka tu kila wakati na viongozi wetu Vilaza. Wenzetu wanapiga hatua sisi tupo na akina Nape wetu vimeo tunashangilia wakicheza viduku na vibajaji majukwaani. Tukubali ukweli kwamba kwa JK na CCM tulichapia haswa na bora next time tuchague kwa kuangalia merits za mtu na si kelele za TOT na magazeti ya Rostam.
  Huko jumuiya ya Afrika Mashariki tunaenda kuwa mambumbu wa kutupwa na hatutaweza kushindana na jirani zetu kwa lolote.
  Guys! Mark my words... hawa wajinga wanatuteketeza na bahati mbaya baadhi yetu tunawashangilia na kuona sifa kuhusishwa nao.
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Teh teh! wanaujua moto wa huko, hata Arusha sidhani kama watarusha miguu yao huko manake itakuwa full kuzomewa, nimecheka sana wakati Nape akielezea remix ya kujivua gamba..... ITV news leo saa mbili usiku
   
 9. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sisiemu wana weweseka hawajui wataingia kwa staili gani ili watoke kisiasa, Nape aliona akisema kujivua gamba ni kufukuza mafisadi alifikiri hiyo song itajibu, ilipobuma ameamua kutoka na verse nyingine lakini bado ngoma imebuma.

  Kwa staili hii ya kubadilisha maana ya kujivua gamba kila siku, akifanya mikutano mitano maana itakuwa imebadirika mara tano! Na hapo ndopo atakapo gundua kuwa kivuli cha nguvu ya umma kinavyomkaribia. Atazomewa huyo mpaka atajuta kujipendekeza pendekeza bila kujiandaa!
   
 10. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280

  Asante kaka
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Malaria Sugu, nilijua tu ile 'Artequin' ingekufaa. Si unaona unavyo-function sasa? lakini tujipe siku mbili tatu ili tuwe na uhakika kama malaria yote itakuwa imeisha!
   
 12. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Du Mkuu Mpaka wew? kweli hama tuu bado hujaamini kuwa hizo ni bla bla tuu sasa atatekelezaji uku akijua ameshikwa pabaya huyo mwenyekiti wenu? alipenda uraisi wa dezo sasa zile hela zinamtokea puani na ukizingatia alimwambia amkanye nape la sivyo ataweka azarani madudu yoooteee.

  Mbaya zaidi inawezekana hawa jamaa ni mafya kweli kweli kipindi kile hata wabunge wa ccm walikua wakitaka hela wanawaona na kusign kiasi halichochukua ikiwa ni ushaidi so je huyo mwenyekiti wako amesign vingapi kwao? na amechukua ngapi? inatisha wee utaumiza kichwa bure ila mziki ndio hua

  Nakupa ongera kwa kuanza kushtuka coz umepata matusi mengi kwa kuonyesha uzalendo wako ndani ya kidumu fikra za wajinga na wao wanakucheka tuu
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha,siku hizi kuna mtu kaiba password yake so ana ongea
  mambo yenye kichwa
   
 14. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 868
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  welcome back malaria sugu..tatizo ni mwenyekiti wenu hana nia ya dhati ya kuwafukuza mapacha watatu mana watamuanika asilani..cha msingi karibu cdm tupambane na ccm.
   
 15. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kada wa cdm atupwa vbaya uchaguz wa rais chuo cha ardh dsm
   
 16. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naoana sasa umeanza kuwa na ubongo timilifu!! Hongera kwa point. Tena nenda kamchape nayo hii msg kwenye fb wall yake.
   
 17. k

  kayumba JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka kusema kujivua gamba kukitekelezwa kwa tafsiri yao ya mwanzo ndiyo ungekuwa mgawanyiko wa ccm! Na sasa siku zinavyopita hilo linazidi kudhihiri. Baada ya vikao vya kujivua magamba na mikutano ya sekeretarieti mpya iliyofuatia nashawishika kuamini hata kujivua gamba kukisitishwa basi ccm haitakuwa ile ile ya siku zote. Vindonda vilivyosababishwa na mambo ya magamba hata vikipona basi makovu yatakuwa makubwa sana kiasi cha kufanya sura isitamanike.

  Uzuri wa haya yote ni kuwa ccm wamejichimbia kaburi wenyewe!
   
 18. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ha,haaa kidumu fikra za wajinga ........... Malizia basi
   
 19. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mwenyekiti nae ni fisadi sasa nae ajifukuze uanachama? Itakuwa sawa na kukatatawi la ti ulolikalia. Kama hauelewi unachoongea umepotea ndugu yangu
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  MS ccm wamewatoa waislamu wameingiza wakristo tupu, mfumo kristo umerudi
   
Loading...