CCM isimsimamishe SIYOI Arumeru ili kunusuru chama

CCM isimsimamishe SIYOI Arumeru ili kunusuru chama


Goodluck Mwangomango


Kama tulishinda Igunga, hatuwezi shindwa Arumeru Mashariki. Lakini tunatakiwa kupambana na rushwa kwa vitendo. Round ya kwanza tuliyasikia ya arumeru, marudio ya leo tumesikia waliokamatwa wakitoa rushwa. Chama kisipo chukua maamuzi sahihi kupitia CC tutakuwa tumejidharirisha wenyewe kwa wananchi.


Tena ni kujidhalilisha kwa kiasi kikubwa na kuendelea kujijengea mazingira magumu kwa chaguzi zijazo ukiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Naomba niandike ukweli na mtizamo wangu kwa chama cha mapinduzi (CCM) kuhusiana na yanayojili katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru mashariki.

Hakuna atakayekataa ukweli kwamba ushindi wa SIYOI SUMARI kwa kiasi kikubwa umetokana na nguvu ya fedha alizopewa na mmoja wa makada wa CCM anayetuhumiwa kwa ufisadi ambaye pia ni mkwe wake EDWARD LOWASSA. Hili limejionyesha wazi na hadi sasa watuhumiwa wengine waliokuwa wakigawa fedha wanaendelea kuhojiwa.

SIYOI ni mgeni katika siasa za Tanzania hana uzoefu zaidi ya kubebwa na jina la baba yake na upo uwezekano wa yeye kushindwa kumudu purukushane na mitikisiko toka kwa upinzani hasa CHADEMA ambao kwa sasa wanafurahia ushindi wake. CHADEMA wanamuona ni dhaifu dhidi ya mgombea wao JOSHUA NASARI na kwa vyovyote vile endapo atasimamishwa kugombea, ushindi kwao ni lazima.

MY TAKE:

i) CCM wanatakiwa kuwa makini katika hili ili kukinusuru chama na endapo watamsimamisha watakiweka
chama katika mazingira magumu ya kuendeleza matumizi ya fedha na undugu katika siasa zao.

ii) Katika kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kutumia nguvu kubwa kujisafisha na kurejesha "credibility"
kwa wananchi, naona ni vyema kamati kuu isimteue SIYOI na badala lake wamweke mtu mwingi bila kujali
kama watashinda au la vinginevyo jinamizi la rushwa na nguvu ya mafisadi ndani ya chama itaendelea
kukibomoa chama hicho.

Nawasilisha.

Rekebisha kwanza anaitwa Sioi na siyo SIYOI .....
 
"Ndugu wajumbe napenda kuwakumbusha jambo moja muhimu kabla ya kupiga kura, leo hatuchagui mbunge, mnachofanya ni kupiga kura za maoni. Mgombea atateuliwa na kikao cha Kamati Kuu Machi 3, mwaka huu," alisema Chiligati.

Hapa ndipo wanapotakiwa kufanya kweli.
 
Mie nashangaa wanaosupport walaji rushwa na watoa rushwa CCM sijui mnaenda wapi.Hivi akishinda kwa sababu ametoa pesa kwanza anazirudishaje?Yaleyale ya Posho. Vijana mlioko ndani ya CCM acheni kushabikia rushwa,rushwa inaua haki.Jamaa eh watanzania tutakwisha,hivi Sioi atazirudishaje pesa alizotoa? Au anategemea kuteauliwa kuwa Waziri ili awe waziri wa 10%?Tumekwisha inabidi tuamke.AKina mama wa Arumeru acheni kupokea hizo elfu mbili mbili hazinunui hata kilo ya sukari!! Khanga baada ya miezi kadhaa zimekwisha lakini matatizo yako pale pale tumieni haki yenu ya msingi kumpigia kura mtu mwenye uwezo wa kuwakilisha jimbo na Watanzania wote,tulio nje ya Arumeru tutawashukuru sana.
 
ii) Katika kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kutumia nguvu kubwa kujisafisha na kurejesha "credibility"
kwa wananchi, naona ni vyema jinamizi la rushwa na nguvu ya mafisadi ndani ya chama likaendelea
kukibomoa chama hicho.
Kumbe CCM inatumia nguvu kubwa kujisafisha ili kurejesha credibility?!.

Kumbe ni jinamizi la rushwa na ufisadi ndivyo vinavyoibomoa CCM?!.

You are very wrong na huu ni ukweli mchungu kwa wana CCM, wapinzani na wana Arumeru ambao for the sake ya uchaguzi huu, wao ndio wawakilishi wa Tanzania kama indicator ya uchaguzi wa 2015!.

Rushwa na ufisadi sio jinamizi kwa CCM bali ndio order of the day. Zamani wapenzi wa CCM walihudhuria mikutano ya hadhara kwa mapenzi yao kwa chama chao, sasa kabla hujahudhuria mkutano kwanza lazima upewe t-shirt na kofia, upatiwe bahasha ya nauli, ukodiwe fuso la kukupeleka na kukurudisha, baada ya mkitano lazima ukalishwe pilau na kupewa bahasha nyingine ya kifungua kinywa kesho yake!. Watu wanahudhuria mikutano ya CCM kwa vivutio ila ya Chadema wanahudhuria kwa mapenzi yao.

CCM imesurvive sio kwa kupendwa bali kulelewa na mabwana wa grand corruption!. Fedha za Kagoda ndizo zimempeleka JK Ikulu!. Mafisadi wakuu ndio wamekihodhi chama, hivyo rushwa na ufisadi ndizo nguzo kuu za CCM kwa sasa!. CCM imesimama kwenye Rushwa, imesimama kwenye ufisadi hivyo rushwa na ufisadi ndizo nguzo kuu zilizokishikilia chama, na badala ya kukidhoofisha kama unavyodhani, ndizo zinazo kiimarisha na kitatawala milele!.

Sio ndilo zao la CCM na ndiye atakayechaguliwa Arumeru kama kielelezo cha nguvu ya rushwa na ufisadi kwenye chaguzi zetu!.

CCM lazima itamsimamisha Sioi itake isitake kwa vile bado inalitaka jimbo hilo!. Chini ya hapo ni kulitoa jimbo hilo sadaka!.
 
Gamba ukilipaka rangi haliwi jipya, litakuwa gamba lenye rangi..na gamba likiwa jipya haliitwi kipusa..litakuwa gamba tuu...So Gamba hung'olewa likatoka na shina lake..Sasa kama shini kumegandana hata kama utumie nini, hapo hapajalegea ni kuumizanatuu..So sioi kama apo carried na Gamba lililong'ang'ania shinani..Still ni gamba tuuu....Chadema for better country
 
Ugeni wa siasa za Tanzania ndo ukoje? Siasa hii hii ambayo hata mpigadebe kituoni anaweza kuwa mwanasiasa mzuri kuliko mvaa suti ndani ya V8? Kipi kigumu katika siasa ya Tanzania?

Kaweza sugu ambaye alikuwa mchanga pia!
 
CCM haiwezi kushinda bila kutumia pesa? hawaamini kwenye hoja bali nguvu ya wenye nacho.
Kama hauko kwenye system na huna nasaba na wenye nacho bora ujitoe ccm na urudi kuangalia ndugu zako wanaoumia kwa sababu ya mfumo huu mbovu huenda ni ndugu zako,tuache kujipendekeza kwa walionacho na walio kwenye system,Taifa ni letu sote na naomba tuanzie Arumeru dhidi ya walionacho na nguvu ya umma.
 
Jamani acheni tu hivo hivo...sisi tunamtaka SIYOI na EL Arumeru ili tukuonesheni sisi CHADEMA ni nani hasa katika siasa za Arusha...Karibu ulingoni Siyoi mwenyeji wako ni kijana Nassari
 
Naomba niandike ukweli na mtizamo wangu kwa chama cha mapinduzi (CCM) kuhusiana na yanayojili katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru mashariki.

Hakuna atakayekataa ukweli kwamba ushindi wa SIYOI SUMARI kwa kiasi kikubwa umetokana na nguvu ya fedha alizopewa na mmoja wa makada wa CCM anayetuhumiwa kwa ufisadi ambaye pia ni mkwe wake EDWARD LOWASSA. Hili limejionyesha wazi na hadi sasa watuhumiwa wengine waliokuwa wakigawa fedha wanaendelea kuhojiwa.

SIYOI ni mgeni katika siasa za Tanzania hana uzoefu zaidi ya kubebwa na jina la baba yake na upo uwezekano wa yeye kushindwa kumudu purukushane na mitikisiko toka kwa upinzani hasa CHADEMA ambao kwa sasa wanafurahia ushindi wake. CHADEMA wanamuona ni dhaifu dhidi ya mgombea wao JOSHUA NASARI na kwa vyovyote vile endapo atasimamishwa kugombea, ushindi kwao ni lazima.

MY TAKE:

i) CCM wanatakiwa kuwa makini katika hili ili kukinusuru chama na endapo watamsimamisha watakiweka
chama katika mazingira magumu ya kuendeleza matumizi ya fedha na undugu katika siasa zao.

ii) Katika kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kutumia nguvu kubwa kujisafisha na kurejesha "credibility"
kwa wananchi, naona ni vyema kamati kuu isimteue SIYOI na badala lake wamweke mtu mwingi bila kujali
kama watashinda au la vinginevyo jinamizi la rushwa na nguvu ya mafisadi ndani ya chama itaendelea
kukibomoa chama hicho.

Nawasilisha.

Kwa mchezo huu tutafika kweli
 
ii) Katika kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kutumia nguvu kubwa kujisafisha na kurejesha "credibility"
kwa wananchi, naona ni vyema kamati kuu isimteue SIYOI na badala lake wamweke mtu mwingi bila kujali
kama watashinda
au la vinginevyo jinamizi la rushwa na nguvu ya mafisadi ndani ya chama itaendelea
kukibomoa chama hicho.

Nawasilisha.
Sijakuelewa yaani CCM waweke mtu yeyote bila kujali kushindwa....duh! nayo ni maoni kwa nini wasijitoe kabisa ili kunusuru makundi na aibu watakayoipata, kwa ninavyoona CCM kupata 30% itakuwa kazi.
 
Waache bwana,wewe tangu lini CCM wanasikia ushauri? ni kama sikio la kufa bana.
 
Hata kama jimbo litapotea upinzani haijalishi, kundi la EL likisambaratika pia haijalishi. Tumechoka na madudu wanayoyafanya bhana.... kila kitu pesa tu au jina la mtu?
Tatizo lenu mulim-under estimate mamvi.
 
Back
Top Bottom