CCM isimsimamishe SIYOI Arumeru ili kunusuru chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM isimsimamishe SIYOI Arumeru ili kunusuru chama

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mwanajamii, Mar 2, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Naomba niandike ukweli na mtizamo wangu kwa chama cha mapinduzi (CCM) kuhusiana na yanayojili katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru mashariki.

  Hakuna atakayekataa ukweli kwamba ushindi wa SIYOI SUMARI kwa kiasi kikubwa umetokana na nguvu ya fedha alizopewa na mmoja wa makada wa CCM anayetuhumiwa kwa ufisadi ambaye pia ni mkwe wake EDWARD LOWASSA. Hili limejionyesha wazi na hadi sasa watuhumiwa wengine waliokuwa wakigawa fedha wanaendelea kuhojiwa.

  SIYOI ni mgeni katika siasa za Tanzania hana uzoefu zaidi ya kubebwa na jina la baba yake na upo uwezekano wa yeye kushindwa kumudu purukushane na mitikisiko toka kwa upinzani hasa CHADEMA ambao kwa sasa wanafurahia ushindi wake. CHADEMA wanamuona ni dhaifu dhidi ya mgombea wao JOSHUA NASARI na kwa vyovyote vile endapo atasimamishwa kugombea, ushindi kwao ni lazima.

  MY TAKE:

  i) CCM wanatakiwa kuwa makini katika hili ili kukinusuru chama na endapo watamsimamisha watakiweka
  chama katika mazingira magumu ya kuendeleza matumizi ya fedha na undugu katika siasa zao.

  ii) Katika kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kutumia nguvu kubwa kujisafisha na kurejesha "credibility"
  kwa wananchi, naona ni vyema kamati kuu isimteue SIYOI na badala lake wamweke mtu mwingi bila kujali
  kama watashinda au la vinginevyo jinamizi la rushwa na nguvu ya mafisadi ndani ya chama itaendelea
  kukibomoa chama hicho.

  Nawasilisha.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Haa! mimi nilifikiri chama kinaendeshwa kwa kanuni na taratibu zake ktk kumpata mgombea. Kumbe kwenu mnachungulia nani anamtaka nani! Nyerere alikufa na hili lichama lenu.
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Chama kijisafishe kwa sioi peke yake mbona ndani ya chama wengi wachafu au wewe huoni.Sema kama unampenda aliyeshindwa tukuelewe sio kusafisha chama kwa kumwondoa mtu itakuwa ni unafiki
   
 4. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio na mimi naposhangaa hapo, au wamsimamishe mtoa mada!
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa uma maana gani?
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NAKUHAKIKISHIENI CCM WAKIFANYA KOSA ULILOSHAURI HAPA WATALISIKIA JIMBO HILO KWENYE BOMBA,EDWARD RICHMOND ANA USHAWISHI WA HALI YA JUU KWENYE JIMBO LILE NA SOTE TUNAJUA KUWA SIOI NI MKWE WAKE KWA VYOVYOTE EDWARD NDIO ALIMSHAURI AGOMBEE NA ANAMPA FULL SUPPORT .LEO HII CCM WAKISEMA WANAMTEMA TUU KUNDI ZIMA LA EL BILA EL KUJIWEKA HADHARANI LITASAMBARATIKA NA KUIUNGA MKONO CDM KWA HIYO CDM ITASHINDA KWA KISHINDO JAPO SIO LAzIMA WASHINDE KWANI WATZ WANA MAMBO YAO WANAYAPENDA KAMA UBWABWA,KOFIA ,KANGA NA AHADI HEWA NA UKIYAWEZA HAYA BASI UNAWATEKA NA KUWABURUZA
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ii) Katika kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kutumia nguvu kubwa kujisafisha na kurejesha "credibility"
  kwa wananchi, naona ni vyema kamati kuu isimteue SIYOI na badala lake wamweke mtu mwingi bila kujali
  kama watashinda au la vinginevyo jinamizi la rushwa na nguvu ya mafisadi ndani ya chama itaendelea
  kukibomoa chama hicho.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  siyoi ni gamba jipya
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  chiligati alisema mgombea atateuliwa kesho
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SIOI NI MASTER PLANER WA EDWARD RiCHMOND
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kujikosoa ni muhimu ili uweze kujisahihisha.hapa kuna kila sababu ya kujikosoa na kujishihisha ili watu wakuamini
   
 12. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  ndg vgl unataka kusema ninh mbona sikusomi ? Una uhusiano wowote na sarakikya ?
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hata kama jimbo litapotea upinzani haijalishi, kundi la EL likisambaratika pia haijalishi. Tumechoka na madudu wanayoyafanya bhana.... kila kitu pesa tu au jina la mtu?
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  rushwa rushwa rushwa kila siku,tena leo dogo anaendeleza rushwa,,,,watanzania bana
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sina uhusiano na mgombea yeyote wala wanaowaunga mkono ila ninachoshwa na makundi ndani ya chama na nguvu za wachache wenye fedha wanaoonekana kufanya wanavyotaka ndani ya chama huku magamba waliyonayo yameng'ang'ania bila kuyavua.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [h=6]Goodluck Mwangomango
  [/h] [h=6]Kama tulishinda Igunga, hatuwezi shindwa Arumeru Mashariki. Lakini tunatakiwa kupambana na rushwa kwa vitendo. Round ya kwanza tuliyasikia ya arumeru, marudio ya leo tumesikia waliokamatwa wakitoa rushwa. Chama kisipo chukua maamuzi sahihi kupitia CC tutakuwa tumejidharirisha wenyewe kwa wananchi.[/h]
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [h=6][/h] [h=6]HIVI NDIVYO CCM ITAJIJENGEA UHALALI WA KUWA CHAMA KIONGOZI KWA TAIFA.

  Mwalimu J.K. Nyerere, Baba wa Taifa, aliwahi kusisitiza

  "Pasipokuwa na haki hapawezi kuwa na amani".
  ...
  [/h]
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tanzania imefanikiwa kuwa nchi yenye amani na utulivu kutokana na sera zake zinazoweka mbele uhuru, haki, usawa na utu. Lazima CCM iendeleze sera hizi kwa nguvu zote. Katika kipindi cha sasa cha uchumi wa soko ambapo kuna mwelekeo wa watu wachache kulimbikiza mali kwa wingi na wananchi walio wengi kuachwa kwenye kingo za umaskini, ni muhimu kwa CCM kujitokeza wazi wazi upande wa wanyonge.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ziendeleze msimamo thabiti wa kulinda na kutetea maslahi ya chama dhidi ya maslahi ya ubinafsi na maslahi ya taifa dhidi ya maslahi ya vikundi vya kibinafsi. Hivi ndivyo CCM itajijengea uhalali wa kuwa chama kiongozi kwa taifa.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika uchaguzi wa mwaka 2010 CCM walipoteza majimbo mengi si kwa sababu chama hakipendwi bali udhaifu waliokuwa nao wagombea wao ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa hawakubaliki kwa wananchi. WENJE alishinda kutokana na kauli chafu za MASHA kuwadhalau wazee wa Mwanza kwamba Ubunge wake hautokani na kura zao bali fedha zake. Musoma mjini MATHAYO alishindwa na NYERERE kwa sababu aligeuza chama kuwa cha kifamilia na wanafamilia hao walifanya matukio ya ajabu ikiwemo kuchukua wake za watu kwa madai ya wangewafanya nini. Maeneo mengi ndivyo ilivyokuwa... hii hali itaendelea mpaka lini? Kwa hali hii na mifano niliyotoa sitashangaa nikiona Arumeru nako CCM inaangukia pua.
   
Loading...