Ccm inatwanga maji kwenye kinu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm inatwanga maji kwenye kinu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Sep 25, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,180
  Likes Received: 417,601
  Trophy Points: 280
  Kama umekuwa ukikifuatilia kwa karibu Chama Cha Mapinduzi utabaini hawataki midahalo kwa sababu hawana mkakati wa kupambana na ufisadi na vile vile hawana nia ya kufutilia mbali hii dhuluma ya ufisadi kwa raia wote wa Tanzania.

  Ukizipembua hoja za ahadi zote za CCM utaona ya kuwa wanalenga kututupia changa la ahadi kemukemu za miundo mbinu ili tusahau kero nzito za ufisadi.

  Hakuna mahali popote pale ambapo CCM imekuwa tayari kujinadi, kuzungumzia au kukiri kuwa ufisadi ndiyo chimbuko la umasikini hapa nchini.

  Jitihada zao za kuombaomba misaada huko nje na wakati wanatoa misamaha ya kodi ya zaidi ya Tshs 700 bilioni kwa mwaka kwa wachimbaji migodi wakubwa ni fedheha kwa taifa wakati mwananchi wa kawaida alipodai msamaha wa kodi kwenye mshahara aliambulia punguzo la asilimia moja tu!

  Mgeni anapewa asilimia mia moja za msamaha wa kodi na mikopo nafuu ikiwemo ruzuku ili ahamishe utajiri wa Nchi hii kwa bei poa.

  Mimi simwelewi Spika wa Bunge anayemalizia muda wake pale anapodai elimu na afya bure haviwezekani wakati kodi hazikusanywi ipasavyo kutokana na ujanja wa kupindisha sheria na kuwabagua wazawa kwa kuwakandamiza.

  Elimu ya juu ili iwe bureee kabisa zinahitajika ongezeko la Tshs 38 Bilioni katika bajeti ya serikali. Sasa hili lina shida gani kama bilioni 700 za bwereta anaachiwa mwekezaji bomu aishie nazo kwao na mali ghafi zetu ambazo wala hafanyi jitihada yoyote ya kuzisindika hapa ncini ili kuongeza thamani yake, kujaziliza kodi zaidi na kutunisha mfuko wa ndani wa ajira za kitaalamu zaidi.

  Ama kwa hakika, Tanzania bila CCM kweli yawezekana na safari hii tusikubali kabisa kudanganyika na ahadi hewa au usanii wa CCM.

  JK ajiandae kuandika hotuba ya kihistoria ya kumkabidhi Dr. Slaa nchi naye Dr. Slaa kazi yake ya kwanza ni kulipiga marufuku Bunge letu tulilojiundia wenyewe kukufuru kwa kujiita eti nalo ni tukufu na kama Bunge ni tukufu je MWENYEZI MUNGU ATAKUWAJE KAMA SIYO KUTAFUTA LAANA?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  bunge tukufu.... Nina hakika sio wote watukufu mle ndani .
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitwanga maji kwenye kinu yatabaki...ni container hiyo, nafikiri wanamwanga kwenye mchanga!
   
Loading...