Alipojiunga na vhama chenye msimamo huo ndio unapaswa kuwa msimamo wake pia. Je mlitarajia aende huko awabadilishe msimamo uliowaleta pamoja?
Ninachokiona hapa kuna haja kubwa sana ya kutoa elimu juu ya mabadiliko. Watu wenye uelewa mdogo hawawezi kutoa hoja za kuboresha zaidi sana wanaonyesha hofu ya mabadiliko. Wanaogopa kupoteza ama kutokea kwa wasiyoyojua.
Lakini jambo la ajabu, kuna kundi moja ama kwa makusudi au kwa ujinga, linajaribu kuwaaminisha watu kwamba mtu akihama kutoka chama kimoja na kwenda kingine, basi anahama na sera, mila na mazoea ya kule alikokuwa anayapelekea kule anakoenda. Na hili ndilo linawafanya wengine waone kama Lowasa kaenda kuharibu ukawa, na ccm wanaona kama ni kete ya kuwafitinisha wapenda mabadiliko kwamba Lowasa anahamisha ushetani wa ccm na kuuambukiza kwenye UkaWa.
Watu wanapaswa kujua wahamiaji wote wanakwenda CHaDEMA kwa kuwa wameona ni chama makini chenye misingi imara na uwezo wa kuongoza mabadiliko katika nchi. Na baada ya kuona hawaridhiki na mifumo iliyopo ikiwa ni pamoja na kunyimwa fursa za kuwaza mabadiliko ndani ya vyama vyao, wanatafuta uwezekano huo nje ya ccm.
Lowasa anayetumiwa kwa mema na mabaya, amesema alitafuta fursa za kufanya mabadiliko ndani ya ccm lakini alinyimwa na akaona mahala sahihi pa kufanay hayo ni CHADEMA. Sasa kwa nini watu wasiamini kwamba anakohamia anakwenda kuungana na manguli aliowakuta kuongeza nguvu ya mabadiliko?
Kwa nini waamini kwamba Lowasa ataharibu kundi lote la waadilifu wa UKAWA, pamoja na nia yake njema na wasione kama kundi la waadilifu wa UKaWA ndiyo misngi wa mabadiliko ya kuwabadilisha wtu mmoja mmoja na chi nzime kutoka kwenye u ccm kwenda kwenye Utanzania?
Lowasa should not be an agenda now. Tumwone yeye na wageni wenzake, pamoja na wenyeji wao kwamba wanafanya kazi moja ya kulikomboa taifa kwa misingi ya UKaWA na si uozo unaonuka kule ccm.
Ccm haipaswi kupewa nafasi ya kuendelea ku create confusions na hofu eti Lowasa amehamishia ufirauni CHADEMA kwa kuwa hata yeye anasema anasimamia katiba ya Warioba? What else? Ukawa siyo ccm kila mtu aamue kufanya atakacho. Kla mmoja anafanya vile UKaWA unataka.
Pengine kwa kuwasaidia ccm, ni vizuri wakashughulika na mafisadi wao walioota magamba sugu huko ccm ambao wameapa kuendeleza ufisadi at any cost.
UKaWA, waachie wapigania ukombozi waliopo na wanaoungana na hili jeshi ili kuongeza nguvu na kasi ya ukombozi.