Elections 2010 CCM inakwangua fedha serikalini kwa ajili ya kuwanunua wapiga kura

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
3,950
Kwa wale mlio Tanzania mnafahamu kuwa kwa miezi miwili sasa,wafanyakazi wa serikali wamekuwa wanakatwa mishahara yao,na fedha zinadaiwa kupelekwa kwenye kampeni.majibu ya serikali ni kuwa kuna tatizo kwenye system ya ulipaji wa mishahara(c'mon!).
Wafanyabiashara wakubwa na wakati wamelazimishwa kuchangia si chini ya 50M kugharamia kampeni za CCM(CCM kanusheni hili).wengi ninaowafahamu wamekiri na ahadi yao ni kurudisha gharama zao baada ya uchaguzi(watazirudishaje?)
Wakuu wa idara zote za serikali wame-amriwa kurudisha OC serikalini,pamoja na mafungu yote ya serikali kwenda kwenye idara za serikali yamezuiwa kwa miezi mi-2 sasa.kwa kifupi idara za resikali ziko ICU kugharamikia uchaguzi.
wakuu wa vitengo serikalini wameamriwa kuchangia 2M kwenda kwenye kampeni za CCM,kama kuna mkuu wa kitengo hapa athibitishe hilo.
Safari/warsha/semina/posho za aina zozote zile zimezuiliwa huko serikalini,wafanyakazi wa serikali ni mashahidi wa hili,wachache sana wanaopata fedha hizo, hadi zithibitishwe na makatibu wakuu wa wizara kwa amri maalum toka Ikulu.(je walikuwa wapi kudhibiti matumizi ya fedha za serikali miaka mi 4 iliyopita?kwa nini wazuie hadi matumizi ya msingi?).
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa sehemu pekee inayotumia fedha za serikali sasa ni IKULU.hivi uchaguzi si ulitengewa bajeti yake?kwa nini nchi nzima iichangie IKULU/HAZINA kufanikisha uchaguzi?
Je?
  1. wafanyakazi wa Tanzania wana sababu gani kuipigia kura serikali isiyowajali kwa kiasi hiki?
  2. Ndugu na jamaa wanaowategemea wafanyakazi hawa kwa maisha yao ya kila siku wana sababu gani ya kuendelea kuikumbatia CCM?
  3. CHADEMA,CUF,TLP,kwa nini msitumie mwanya huu mkubwa kabisa kujenga hoja ya matumizi mabovu ya fedha za UMMA kwenye uchaguzi huu yanayofanywa na CCM?

nionavyo mimi wafanyakazi kadhaa nilioongea nao,si chini ya kumi,wamekata tamaa ya maendeleo chini ya CCM,wengi wanataka mabadiliko,wako tayari kumpigia slaa kura hata kama hawampendi/hawamkubali ili mradi mabadiliko yatokee(CHADEMA mnalijua hili?)

makada wa chadema,fanyeni hima kusambaza hizi taarifa kuwa wafanyakazi wanakatwa mishahara kufidia gharama za CCM

PIA MUWAULIZE CCM/KIKWETE sababu za kutumuia fedha karibu zote za serikali kugharamia UCHAGUZI tu!kuna sababu gani mpiga kura akanunuliwa kwa fedha nyingi kiasi hicho?
 
Mkuu wanaogopa kivuli chao, wanaona haya kushuka ndo maana kwa gharama yoyote wanang'ang'ania madaraka. Halafu ati afya na elimu bure haiwezekani!
 
Hii taarifa nilishaanza kuinusa last week.
wizara ya viwanda na biashara walipewa OC ya shs milion kumi wakati bajeti inagusa to 200 millions. wahasibu na vitengo vya fedha serikalini wanawakimbia wafanyakazi maana hayo maswali wanashindwa kuyajibu.

Hivi najiuliza kwamba baada ya uchaguzi na kuiweka chadema madarakani hawa ccm watatoa wapi hizo fedha za kurejesha?
Hivi wanaccm ambao hata hizo ada hamlipii mnadhani fedha za kuendeshea kampeni zenu na kuwahonga wapinzani sugu zinatoka wapi?
SFO ya tanzania mnaliona hili, UwT mnaliona hili pia hata Hazina mnalijua hili. je mchango wenu kwa Taifa ni upi hapo? Kama chama kinapendwa basi huwa hata gharama ya uchaguzi huwa ndogo. ila kama kinalazimisha ushindi tutajuta na kuporomoka kwa uchumi baada ya uchaguzi.

tufanye historia sasa au la kizazi kitatulaumu

Kimweri, asante sana kwa kutupa mwanga na ukweli katika hili. CCM inaonekana kufanya kila kitu ili kubaki madarakani, ikiwa ni pamoja na kutumia jasho na nguvu ya watanzania masikini. Kwa muda huu mchache uliobakia tufanye hima kuwafikishia wananchi wengi ujumbe huu.
 
Hatudanganyiki mwaka huu. Waache wamwage fedha kila kaya, kura yangu ni siri yangu.
 
Eeee Mungu wangu wee nakulilia uiokoe TZ na watu wake. Tenda muujiza kwa kuwaamsha WaTanzania kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya kura hapo Octoba 31.
 
kwa wale mlio tanzania mnafahamu kuwa kwa miezi miwili sasa,wafanyakazi wa serikali wamekuwa wanakatwa mishahara yao,na fedha zinadaiwa kupelekwa kwenye kampeni.majibu ya serikali ni kuwa kuna tatizo kwenye system ya ulipaji wa mishahara(c'mon!).
Wafanyabiashara wakubwa na wakati wamelazimishwa kuchangia si chini ya 50m kugharamia kampeni za ccm(ccm kanusheni hili).wengi ninaowafahamu wamekiri na ahadi yao ni kurudisha gharama zao baada ya uchaguzi(watazirudishaje?)
wakuu wa idara zote za serikali wame-amriwa kurudisha oc serikalini,pamoja na mafungu yote ya serikali kwenda kwenye idara za serikali yamezuiwa kwa miezi mi-2 sasa.kwa kifupi idara za resikali ziko icu kugharamikia uchaguzi.
Wakuu wa vitengo serikalini wameamriwa kuchangia 2m kwenda kwenye kampeni za ccm,kama kuna mkuu wa kitengo hapa athibitishe hilo.
Safari/warsha/semina/posho za aina zozote zile zimezuiliwa huko serikalini,wafanyakazi wa serikali ni mashahidi wa hili,wachache sana wanaopata fedha hizo, hadi zithibitishwe na makatibu wakuu wa wizara kwa amri maalum toka ikulu.(je walikuwa wapi kudhibiti matumizi ya fedha za serikali miaka mi 4 iliyopita?kwa nini wazuie hadi matumizi ya msingi?).
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa sehemu pekee inayotumia fedha za serikali sasa ni ikulu.hivi uchaguzi si ulitengewa bajeti yake?kwa nini nchi nzima iichangie ikulu/hazina kufanikisha uchaguzi?
Je?

  1. wafanyakazi wa tanzania wana sababu gani kuipigia kura serikali isiyowajali kwa kiasi hiki?
  2. ndugu na jamaa wanaowategemea wafanyakazi hawa kwa maisha yao ya kila siku wana sababu gani ya kuendelea kuikumbatia ccm?
  3. chadema,cuf,tlp,kwa nini msitumie mwanya huu mkubwa kabisa kujenga hoja ya matumizi mabovu ya fedha za umma kwenye uchaguzi huu yanayofanywa na ccm?

nionavyo mimi wafanyakazi kadhaa nilioongea nao,si chini ya kumi,wamekata tamaa ya maendeleo chini ya ccm,wengi wanataka mabadiliko,wako tayari kumpigia slaa kura hata kama hawampendi/hawamkubali ili mradi mabadiliko yatokee(chadema mnalijua hili?)

makada wa chadema,fanyeni hima kusambaza hizi taarifa kuwa wafanyakazi wanakatwa mishahara kufidia gharama za ccm

pia muwaulize ccm/kikwete sababu za kutumuia fedha karibu zote za serikali kugharamia uchaguzi tu!kuna sababu gani mpiga kura akanunuliwa kwa fedha nyingi kiasi hicho?

hii inaonyesha ni namna gani ccm na viongozi wake wasivyokuwa na maadili na ubunifu wa kuweza kuikwamua tanzania hapa ilipo. Kama ccm haikuwa na fedha za kutosha mamilioni ya picha, mabango, t-shirt, kofia, khanga n.k vilikuwa vya nini?

haya tena wafanyakzi kazi kwenu, kwanza walikataa kuongeza mishahara haid hapo dr slaa alipowatishia nyau ndipo wakatoa nyongeza bila waraka. Kama hali yenyewwe ya kiuchumi serikalini ndio hiyo kweli baada ya uchaguzi wafanyakazi wataendelea kulipwa nyongeza ya mishahara?
 
Inawezekana sehemu kubwa ya fedha inachotwa na wale wanaoona watoke serikalini na mafedha ya wizi. Lazima nyingi zinaishia kwenye akaunti za vigogo wa CCM.
 
Kwa wale mlio Tanzania mnafahamu kuwa kwa miezi miwili sasa,wafanyakazi wa serikali wamekuwa wanakatwa mishahara yao,na fedha zinadaiwa kupelekwa kwenye kampeni.majibu ya serikali ni kuwa kuna tatizo kwenye system ya ulipaji wa mishahara(c'mon!).
Wafanyabiashara wakubwa na wakati wamelazimishwa kuchangia si chini ya 50M kugharamia kampeni za CCM(CCM kanusheni hili).wengi ninaowafahamu wamekiri na ahadi yao ni kurudisha gharama zao baada ya uchaguzi(watazirudishaje?)
Wakuu wa idara zote za serikali wame-amriwa kurudisha OC serikalini,pamoja na mafungu yote ya serikali kwenda kwenye idara za serikali yamezuiwa kwa miezi mi-2 sasa.kwa kifupi idara za resikali ziko ICU kugharamikia uchaguzi.
wakuu wa vitengo serikalini wameamriwa kuchangia 2M kwenda kwenye kampeni za CCM,kama kuna mkuu wa kitengo hapa athibitishe hilo.
Safari/warsha/semina/posho za aina zozote zile zimezuiliwa huko serikalini,wafanyakazi wa serikali ni mashahidi wa hili,wachache sana wanaopata fedha hizo, hadi zithibitishwe na makatibu wakuu wa wizara kwa amri maalum toka Ikulu.(je walikuwa wapi kudhibiti matumizi ya fedha za serikali miaka mi 4 iliyopita?kwa nini wazuie hadi matumizi ya msingi?).
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa sehemu pekee inayotumia fedha za serikali sasa ni IKULU.hivi uchaguzi si ulitengewa bajeti yake?kwa nini nchi nzima iichangie IKULU/HAZINA kufanikisha uchaguzi?
Je?
  1. wafanyakazi wa Tanzania wana sababu gani kuipigia kura serikali isiyowajali kwa kiasi hiki?
  2. Ndugu na jamaa wanaowategemea wafanyakazi hawa kwa maisha yao ya kila siku wana sababu gani ya kuendelea kuikumbatia CCM?
  3. CHADEMA,CUF,TLP,kwa nini msitumie mwanya huu mkubwa kabisa kujenga hoja ya matumizi mabovu ya fedha za UMMA kwenye uchaguzi huu yanayofanywa na CCM?

nionavyo mimi wafanyakazi kadhaa nilioongea nao,si chini ya kumi,wamekata tamaa ya maendeleo chini ya CCM,wengi wanataka mabadiliko,wako tayari kumpigia slaa kura hata kama hawampendi/hawamkubali ili mradi mabadiliko yatokee(CHADEMA mnalijua hili?)

makada wa chadema,fanyeni hima kusambaza hizi taarifa kuwa wafanyakazi wanakatwa mishahara kufidia gharama za CCM

PIA MUWAULIZE CCM/KIKWETE sababu za kutumuia fedha karibu zote za serikali kugharamia UCHAGUZI tu!kuna sababu gani mpiga kura akanunuliwa kwa fedha nyingi kiasi hicho?

HONGERA KWA HARAKATI ZAKO ,najua unamatumaini sana na ahadi kibao kuwa utapewa kitengo flani baada ya ushindi wa CHADEMA.sidanganyiki na ushawishi wako kwa kila unavyojaribu kunijaza chuki yako kwa CCM.UNACHUKI KWA AJILI YA INTEREST ZAKO.
 
Siyo kwamba tunakuzoza lakini, P/se! JP achana na majibu kama wimbo wa taarabu, Mipasho. Jibu hoja kwa mifano na ukweli badala ya njia hii.

Wizara ziko hoi bila sababu ya kueleweka miezi 3 baada ya kupitishwa kwa bajeti. Hiyo ni nini?

Mwezi wa 9 Wizara ya elimu ilipata 10 milioni kama OC kiasi kwamba hakuna hata mwalimu aliyepewa likizo! Hata Wastaafu wakanyimwa pesa za nauli.

Sasa hudanganyiki nini? CCM ni mzazi wa nani hapa JF

CCM wanasema ni serikali yao. Watuambie pesa zinakwenda wapi?
 
Alafu mtasema CCM wana uzalendo na nchi hii.
Ata Nyerere alisema anayetoa rushwa/fedha kuingia ikulu tumwogope kama Ukoma bse akiingia madarakani kazi ya kwanza ni namna ya kuridusha izo pesha.So Watz tukiirudisha CCM madarakani manake kuna kufunga mkanda kwa mwaka mzima hali ya kifedha ikiwa ndivyo sivyo bse watakuwa wanafukia mashimo
 
hili la fungu la other charges kwa wizara zote kupunguzwa ni style nyingine ya EPA,hii siyo siri japo sijui mkakati ukoje wa kure-imburse au ndiyo hazitarudishwa! Kwa uchafu unaofanyika sasa CCM hawawezi kukubali kushindwa maana haya yote yatakuwa unearthed na huo mdiyo utakuwa mwanzo na mwisho wa chama cha mapi.....Pia ni ukweli usiopingika kuwa kama CCM itashindwa katika nafasi ya urais itakuwa ni mwanzo wa mwisho wake!
 
Ooh! hivi sisi wadanganyika tutaepuka lini na hili jini CCM! inauma sana, inakera sana, inachosha mno, inaumiza kupita kawaida, I hate the animal so called CCM! himahima jamani 31 Oct tukawapige chini.
 
Kwa wale mlio Tanzania mnafahamu kuwa kwa miezi miwili sasa,wafanyakazi wa serikali wamekuwa wanakatwa mishahara yao,na fedha zinadaiwa kupelekwa kwenye kampeni.majibu ya serikali ni kuwa kuna tatizo kwenye system ya ulipaji wa mishahara(c'mon!).
Wafanyabiashara wakubwa na wakati wamelazimishwa kuchangia si chini ya 50M kugharamia kampeni za CCM(CCM kanusheni hili).wengi ninaowafahamu wamekiri na ahadi yao ni kurudisha gharama zao baada ya uchaguzi(watazirudishaje?)
Wakuu wa idara zote za serikali wame-amriwa kurudisha OC serikalini,pamoja na mafungu yote ya serikali kwenda kwenye idara za serikali yamezuiwa kwa miezi mi-2 sasa.kwa kifupi idara za resikali ziko ICU kugharamikia uchaguzi.
wakuu wa vitengo serikalini wameamriwa kuchangia 2M kwenda kwenye kampeni za CCM,kama kuna mkuu wa kitengo hapa athibitishe hilo.
Safari/warsha/semina/posho za aina zozote zile zimezuiliwa huko serikalini,wafanyakazi wa serikali ni mashahidi wa hili,wachache sana wanaopata fedha hizo, hadi zithibitishwe na makatibu wakuu wa wizara kwa amri maalum toka Ikulu.(je walikuwa wapi kudhibiti matumizi ya fedha za serikali miaka mi 4 iliyopita?kwa nini wazuie hadi matumizi ya msingi?).
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa sehemu pekee inayotumia fedha za serikali sasa ni IKULU.hivi uchaguzi si ulitengewa bajeti yake?kwa nini nchi nzima iichangie IKULU/HAZINA kufanikisha uchaguzi?
Je?

  1. wafanyakazi wa Tanzania wana sababu gani kuipigia kura serikali isiyowajali kwa kiasi hiki?
  2. Ndugu na jamaa wanaowategemea wafanyakazi hawa kwa maisha yao ya kila siku wana sababu gani ya kuendelea kuikumbatia CCM?
  3. CHADEMA,CUF,TLP,kwa nini msitumie mwanya huu mkubwa kabisa kujenga hoja ya matumizi mabovu ya fedha za UMMA kwenye uchaguzi huu yanayofanywa na CCM?

nionavyo mimi wafanyakazi kadhaa nilioongea nao,si chini ya kumi,wamekata tamaa ya maendeleo chini ya CCM,wengi wanataka mabadiliko,wako tayari kumpigia slaa kura hata kama hawampendi/hawamkubali ili mradi mabadiliko yatokee(CHADEMA mnalijua hili?)

makada wa chadema,fanyeni hima kusambaza hizi taarifa kuwa wafanyakazi wanakatwa mishahara kufidia gharama za CCM

PIA MUWAULIZE CCM/KIKWETE sababu za kutumuia fedha karibu zote za serikali kugharamia UCHAGUZI tu!kuna sababu gani mpiga kura akanunuliwa kwa fedha nyingi kiasi hicho?
.

Nina ndugu zangu wanne serikali nimewapigia simu sasa hivi baada ya kusoma habari hii na wako idara tofauti tofauti na marafiki zangu wawili wamesema hakuna jambo kama hilo huko serikalini. wanasema huo ni uongo hakuna jambo kama hilo serikalini ni propaganda za kueneza kampeni chafu kwa ajili ya kutafuta ushindi.
 
Watanzania tuepuke habari za kutungwa na zingine zikidaiwi zimefanyiwa utafiti zinaweza kutufanya kuacha kuchagua wagombea tunaowakubari.
 
Kwa wale mlio Tanzania mnafahamu kuwa kwa miezi miwili sasa,wafanyakazi wa serikali wamekuwa wanakatwa mishahara yao,na fedha zinadaiwa kupelekwa kwenye kampeni.majibu ya serikali ni kuwa kuna tatizo kwenye system ya ulipaji wa mishahara(c'mon!).
Wafanyabiashara wakubwa na wakati wamelazimishwa kuchangia si chini ya 50M kugharamia kampeni za CCM(CCM kanusheni hili).wengi ninaowafahamu wamekiri na ahadi yao ni kurudisha gharama zao baada ya uchaguzi(watazirudishaje?)
Wakuu wa idara zote za serikali wame-amriwa kurudisha OC serikalini,pamoja na mafungu yote ya serikali kwenda kwenye idara za serikali yamezuiwa kwa miezi mi-2 sasa.kwa kifupi idara za resikali ziko ICU kugharamikia uchaguzi.
wakuu wa vitengo serikalini wameamriwa kuchangia 2M kwenda kwenye kampeni za CCM,kama kuna mkuu wa kitengo hapa athibitishe hilo.
Safari/warsha/semina/posho za aina zozote zile zimezuiliwa huko serikalini,wafanyakazi wa serikali ni mashahidi wa hili,wachache sana wanaopata fedha hizo, hadi zithibitishwe na makatibu wakuu wa wizara kwa amri maalum toka Ikulu.(je walikuwa wapi kudhibiti matumizi ya fedha za serikali miaka mi 4 iliyopita?kwa nini wazuie hadi matumizi ya msingi?).
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa sehemu pekee inayotumia fedha za serikali sasa ni IKULU.hivi uchaguzi si ulitengewa bajeti yake?kwa nini nchi nzima iichangie IKULU/HAZINA kufanikisha uchaguzi?
Je?

  1. wafanyakazi wa Tanzania wana sababu gani kuipigia kura serikali isiyowajali kwa kiasi hiki?
  2. Ndugu na jamaa wanaowategemea wafanyakazi hawa kwa maisha yao ya kila siku wana sababu gani ya kuendelea kuikumbatia CCM?
  3. CHADEMA,CUF,TLP,kwa nini msitumie mwanya huu mkubwa kabisa kujenga hoja ya matumizi mabovu ya fedha za UMMA kwenye uchaguzi huu yanayofanywa na CCM?

nionavyo mimi wafanyakazi kadhaa nilioongea nao,si chini ya kumi,wamekata tamaa ya maendeleo chini ya CCM,wengi wanataka mabadiliko,wako tayari kumpigia slaa kura hata kama hawampendi/hawamkubali ili mradi mabadiliko yatokee(CHADEMA mnalijua hili?)

makada wa chadema,fanyeni hima kusambaza hizi taarifa kuwa wafanyakazi wanakatwa mishahara kufidia gharama za CCM

PIA MUWAULIZE CCM/KIKWETE sababu za kutumuia fedha karibu zote za serikali kugharamia UCHAGUZI tu!kuna sababu gani mpiga kura akanunuliwa kwa fedha nyingi kiasi hicho?

-----------
Aibuu....
Kuna mshikaji fulani anafanya kazi Shirika la Taifa la Utangazaji linalomiliki Runinga inayojiita ya Taifa yaani TiiiBiiiSiiii, yaani mwezi uliopita mishahara walikuwa wanisikia tu kwenye Taarifa, hakuna kulipwa. Hadi jamaa wanatoa washikaji upepo ku-cover angalau nauli na msosi. Tusiendelee kutetea ufidhuli huu...wanaumia ndugu zetu, watoto ma wamama ambao ndugu zao hawana chanzo kingine cha hela zaidi ya ajira hii iliyoko chini ya serikani ya Chama hiki kinachoenda kufa...
 
baba yangu kabla ya kuaga dunia (RIP) aliwahi kuniasa kwamba uongo na fitina ni sumu ya kupata maendeleo. Daima tuwe wakweli kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
 
Watanzania tuepuke habari za kutungwa na zingine zikidaiwi zimefanyiwa utafiti zinaweza kutufanya kuacha kuchagua wagombea tunaowakubari.

Lakini wewe ukiwapigia ndugu zako wanne wanaofanyakazi serkali ya chama cha mafisadi (CCM) si habari za kutungwa. Ah! Akili za kisogoni hizo!!!! lol
 
HONGERA KWA HARAKATI ZAKO ,najua unamatumaini sana na ahadi kibao kuwa utapewa kitengo flani baada ya ushindi wa CHADEMA.sidanganyiki na ushawishi wako kwa kila unavyojaribu kunijaza chuki yako kwa CCM.UNACHUKI KWA AJILI YA INTEREST ZAKO.

HATUJITOI MUHANGA KWA AJILI YA KUICHUKIA CCM AU KWA AJILI YA INTEREST BINAFSI KAMA NINYI MNAVYOFANYA NDANI YA CCM. BADALA YAKE TUNAKERWA NA KUUMIZWA NA UMASKINI WA TANZANIA NA WATANZANIA KATIKATI YA UTAJIRI NA NEEMWA YA KILA AINA ARDHI KUBWA NA SAFI KWA KILIMO, MITA ZA MARABA MIA NANE ZA FUKWE, MBUGA ZA WANYAMA NA VIVUTIO VYA UTALII, MADINI YA KILA AINA N.K. LAKINI KUTOKANA NA TAMMAA YA KUJILIMBIKIZIA MALI YA VIONGOZI WA CCM TANZANIA NA WATANZANIA WANASHINDWA KUUTUMIA UTAJIRI ULIOPO KUJIONDOA KATIKA LINDI LA UMASKINI.

MFANO HAI NI MILIONI MIA MOJA INATOSHA KUJENGA SHULE MOJA YA SEKONDARI YENYE MAABARA, MAKATABA, NYUMBA ZA WAALIMU NA VIFAA MUHIMU VYA KUFUNDISHIA. HIVYO BILIONI 133 ZILIZOIBIWA KATIKA EPA ZINGETOSHA KUJENGA SHULE 1330.

KATIKA MWAKA BAJETI YA 2010/11 SERIKALI INATOA MISAMAHA YA KODI HUSUSAN KWA MAKAMPUNI YA MAFUTA KWA KIWANGO KINACHOFIKIA 2.7 YA PATO LA TAIFA (GDp0 BADALA YA KIWANGO KINACHOPENDELEZWA NA WACHUMI CHA 1%. HIVYO MISAMAHA HIYO KUFIKIA BIOIONI 700 BADALA YA BILIONI 200 TU. HIVYO SERIKALI INAKOSESHWA KIASI CHA BILIONI 500 KILA MWAKA KUTOKANA NA VIONGOZI NA SERIKALI ZA CCM KUTOKUWA MAKINI.

FEDHA HIZO ZINATOSHA KUJENGA SHULE SEKONDARI 5000 KILA MWAKA. HADI MWAKA 2009 TANZANIA INA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI, BINAFSI, ZA KAT, ZA DINI N.K JUMALA YAKE NI 4102 TU. HIVYO UINAWEZA KUONA NI FEDHA KIASI GANI INAPOTEA KUTOKANA NA WIZI WA VIONGOZI WA CCM KUSHIRIKIANA NA VIBAKA UCHUMI WANAWAITA WAWEKEZAJI.
 
HONGERA KWA HARAKATI ZAKO ,najua unamatumaini sana na ahadi kibao kuwa utapewa kitengo flani baada ya ushindi wa CHADEMA.sidanganyiki na ushawishi wako kwa kila unavyojaribu kunijaza chuki yako kwa CCM.UNACHUKI KWA AJILI YA INTEREST ZAKO.
wewe mwenye upungufu wa mawazo na hoja,JIFUNZE kusoma kilichoandikwa na ku-analyse,bila kumtazama aliyeandika kwanza,hiyo itakusaidia sana kuondokona na ujinga unaotaka kuulea.sihitaji kukujaza chuki kwa CCM kwani sina sababu ya kufanya hivyo,nimetoa taarifa ya kinachoendelea serikalini ili ujue kinachoendelea.wewe kukaa juani ukiwa umevaa nguo za kijani na njano,ni uamuzi wako.watoto wakp.wa ndugu zako kukosa elimu bora ni uamuzi wako.kukosa afya na huduma za msingi ni uamuzi wako.
Mimi nimeamua huu ndio uwe mwisho wa upuuzi,wakati mataifa mengine yanafikiria jinsi ya kupambana na "future" sie tumekaa tunalaumu shida za "past".
Kama unaipenda CCM kama unavyopenda Arsenal au yanga then pole sana,kwani Politics goes beyond love/lust.WAKE UP
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom