umejibia hoja vema mkuu ila tunaweza kutofautiana kimawazo ambayo ni haki yetu ila FACTS lazima ziheshiwe ili kulinda ukweli wa majadiliano,umemsia president Magufuli kwa kuleta maendeleo ILA please nipe mradi mmoja alioutekeleza kwenye awamu yake,mradi ambao umeleta mabadiliko kwa common man on the street,sio sisi middle class wenye uwezo kidogo;achilia miradi ambayo iliasisiwa na awamu ya nne na utekelezaji wake ukaanza yeye kaja kuumalizia,ninahitaji mradi uliobuniwa naye,na ukautekeleza na matunda yake yanaonekana,kumbuka kuwa Ubungo sio ubunifu wake and I can put my head on the bock ule ni uchafu Fulani pale,Reli inasuasua na mvua ikinyesha kidogo miundo yake inashindwa kabisa kuhimili ,mradi ile wa umeme KUKAMILIKA kwenye uongozi wake kwangu ni ndoto;kampeni za korosho zote ni za kisiasa mkulima wa korosho hadi leo bado anamaumivu,reli ya dar to moshi inasuasua,mradi wa bomba la mafuta Uganda to tanga naona kama unafifia.
Ukisema anatekeleza miradi ya Kikwete unakosea hata kama imeasisiwa awamu ya4.
Nipende kusema kuwa bila dhamira ya kweli, utekekezaji unaousema haungelikuwepo na hakuna cha kumfanya.
Emb turud awamu ya4 miradi kababe iliyotekelezwa ikakamilika uitaje kwa majina.
Huyu wa awamu ya5 Tanzania nzima ninaona inefumuliwa inajengwa: Nyerere dam,Standard g railway, Dar huko miradi kibao, Dodoma huko, barabara kuunganisha mikoa, barabara za mjini, mikataba ya madini kufumuliwa, kukaba mafisadi.
Mambo hayo nimeyataja kwa uchache kwasababu sijatuliza kichwa.
Kwa kuwa tawala zote kwa awamu ninazijua, nitaeleza kifupi mapungufu ya kila awamu.
Enzi za awamu ya kwanza, Nyerere alijitahidi kuanzisha mashirika ya Umma, lakin alikuwa hana meno, mafisadi aliwagwaya hadi kumchomekea hayati Moringe adili nao, matokeo yake yanafahamika, baada ya hilo gharika mafisadi walianza kudai fidia nk nk kwasababu kulikuwepo na mwanya wa kusheria, wakaibana serikali kuwalipa fidia.
Awamu ya pili siiongelei maana ilikuwa kama utawala wa mpito.
Awamu ya tatu ndiyo sura za mafisadi zilijidhihirisha kwa kuwa hapakuwa na sheria madhubuti kuwabana, pesa ilibanwa kishenzi, nyongeza za mishahara ilikuwa ni kiduchu mno, oesa mfukoni hakuna ukiangalia s.sleep usishangae kuona nyongeza ya sh.5,000!
Awamu ya4 ni ya makundi na udini kuruhusiwa, misikiti kuanza kujengwa hata maofisini na kwenye visima vya mafuta.
Salamu za madhehebu kwenye kadannasi zikaasisiwa.
Sijasikia salamu za namna hiyo Bungeni, salamaleko, sijui Yesu asifiwe!
Makundi yalipewa baraka halisi za huyu mwenzetu ama kinyume chake.
Tuliokula chumvi kwa kuona tawala zote tangia uhuru nitakuwa mwizi wa fadhila nikimsema tofauti Magufuli.
Kuanzia utawala wa Mwinyi hadi huu, wanatawala kipindi kifupikifupi mno, hivyo impact ya kila utawala unadisplay awamu hiyo hadi awamu nyingine inayofuata siyo ajabu.
Lakini watawala wote tunawapima kwa uthubutu wao wa kuchukua hatua za kuleta maendeleo pamoja na uzuiaji ama utokomezaji wa mianya ya rushwa ambayo waTz walikuwa wametopea na kuwa ni kama utamaduni halisii.
Kwa hiyo mkuu,mimi imani yangu ipo sana kwa utawala wa awamu hii, hasa akiendelea bila kubadilika.
Akibadilika huku mbele ya safari basi nami nitabadili msimamo na mtazamo wangu.
Sishabikii chama chochote kwa sasa.
Mkuu nineandika kama summary, nikitulizana ndiyo ninaweza kukuwekea details za niliyoyaandika. Alamsiki.
Sent using
Jamii Forums mobile app