Ukiachana na kutofanyika lile kafara la kukimbiza moto mwaka huu.....ukiachana na makada muhimu kutoonekana kwenye harakati hizi za kampeni ...kuna mambo bado yanafikirisha sana... Je hii ni coincidence ama ni matokeo ya wapanga mipango duni?
Mwanzoni mwa mwezi huu ccm katika kujiandaa na kampeni ilikuja na wazo la kukodi wasanii ili waisaidie kwenye kampeni zake...Jumla ya wasanii wapatao 200 wakakodisha kwa malipo yasiyojulilana...lakini ninini kilitokea!?
Kile kilichopaswa kuwa tukio kubwa la ukaribisho wa wasanii 200 kwenye jukwaa la kampeni la ccm ..kilikuja kufunikwa na tukio la mshereheshaji mmoja kupishana lugha na mmojawapo wa wasanii waalikwa...kilichotokea baada ya hapo ni utoto na upuuzi mtupu...na hili ndio likawa tukio lililochukua sura ya tamasha na kufunika kabisa tukio asili
Mipango ilikuwa mingi...likaja tukio la viongozi wa dini kufanya kilichoitwa kongamano la amani kwa udhamini wa cccm...hapo viongozi husika husika wakaingizwa kwenye mtego wa kusifu na kuabudu mema mengi yaliyofanywa awamu ya tano chini ya amiri jeshi mkuu..
Hili tukio nalo impact yake ikawa so negative...badala ya jamii kujadili muktadha wa mrejesho wa matarajio ya tukio ...mjadala ukawa viongozi wa dini kuwa na upande waziwazi kwenye maswala ya kisiasa badala ya kuwa neutral kwakuwa ni viongozi wa watu wa itikadi zote hivyo kuonesha upande ni sawa na ama kuwabagua waumini au kuwachanganya
Wasanii na viongozi wa dini hawapaswi kamwe kujichanganya na mambo ya kisiasa kwakuwa wanahudumia jamii yenye itikadi zote...huku ni kujiharibia maisha hasa kwa wasanii ambao baadhi yao wameharibu nyimbo zao nzuri kwa tukio la malipo kiduchu huku wakijipunguzia mashabiki na wapenzi
Matukio mawili kwenye uzinduzi wa kampeni pale Dodoma nayo yakafunika tena uzinduzi wenyewe..jamii ikahamishiwa tena kwenye matukio yatokanayo bila kupangwa na kuacha tukio muhimu la kupanga lililoandaliwa kwa gharama kubwa
Matukio ya Diamond kuzuiwa kufika jukwaa kuu na makonda kuzuiwa kukaa jukwaa la viongozi wa ccm ndio yamechukua nafasi ya mijadala kwenye tukio la ufunguzi....kumbuka makonda ndio mlezi wa Diamond
Ni kimavi gani hiki!? Ni gundu la wapi hili? Je litakoma ama ndio mwanzo wa muendelezo wa matukio yasiyopangwa wala kutarajiwa kutokea kwenye majukwaa ya kampeni ya ccm? Matukio ambayo ndio yatachukua nafasi ya mijadala....na kufunika matukio muhimu ya kutangaza sera na kuvutia wananchi wawachague....
Naona unalazimisha kuweka vioja kwenye hoja. Ungekua makini sana, ilikupasa kujadili zaidi kampeni za CHADEMA kuliko za CCM. Mpaka sasa watu wanajiuliza kuhusu mwitikio mdogo wa wananchi kwenye kampeni za CHADEMA Dar es Salaam, is it COINCIDENCE? Chama kimepoteza mvuto? Au mgombea wenu hakubaliki?
Ukiacha kanda ya ziwa, Dar es salaam ndo inayofuatia kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura. Hata Lowassa kura zake nyingi alizipatia Dar. Sasa kwa hali hii kweli kuna matumaini yoyote ya ushindi? Maana kanda ya ziwa kwa vyovyote vile, CHADEMA hawawezi kuishinda CCM kama ilivyokua 2015.
Sasa badala ya kupoteza muda wako kwa kusema CCM ina gundu eti kwasbbu Diamond na Makonda wamezuilwa kupanda jukwaani, sijui wasanii wamekatana mitama, viongozi wa dini wameunga juhudi. Nadhani ungejikita kujadili kwanini CHADEMA haina mkakati wa kuleta hamasa kwa Wananchi ambao ndo wapiga kura. Maana hayo yote uliyoyajadili ni matukio ambayo yametokea kwenye mikakati ya CCM kuleta hamasa kwa Jamii ili kuwashawishi wawapigie kura.
Mikakati ya CHADEMA ya kampeni ilivyo ya hovyo, Utadhani labda nyinyi ndo mmejenga SGR, Flyover, Vituo vya Afya, Barabara, Madaraja n.k. Kwahiyo, hamna pressure kabisa na Uchaguzi kwasababu wananchi wanajionea mliyoyafanya. Kumbe agenda kubwa mliyonayo ni kupigwa risasi, watu kutekwa n.k na agenda moja ya uhuru wa vyombo vya habari imeshawaponyoka maana juzi mmekitimua chombo kimoja cha habari kwenye mkutano wenu. Kwahiyo hamuwezi kujipambanua tena kama ni watetezi wa vyombo vya habari.