CCM imetelekeza Wazee katika Huduma za Afya

kizuiani

Member
Jul 12, 2020
73
130
Ni ukweli usiopingika kuwa wazee nchini hutambulika kuanzia miaka 65 yaan ELDER ADULTS katika kuwagawa katika makundi ya tiba. Kundi hili la above 65 yrs linashambuliwa sana na magonjwa ya kuambukiza kutokana na upungufu wa kinga zao mwilini.

Hali hii hupelekea kuugua magonjwa mara kwa mara haswa mfumo wa hewa yaani pneumonia bacterial, viral na hata fungal. Pia matatizo ktk mfumo wa mifupa kwao ni km maisha yao ya kila siku. Wajukuu leo nimeamka shingo ,mgongo na kiuno vyote vinauma. Ni kauli common kuzisikia kwa hawa wazee.

Wazee hawa wengi hawana bima. Ukiitafuta bima yake kuipata inahitaji huruma ya muumba ktk hali ya kuugua kwake. Wengi huishia kutafuta barua za utambuzi ili kupata exemption health services ambayo huishia ngazi ya zahanati. Kuanzia kituo cha afya mpaka MNH hakuna cha msamaha kwa wazee bali itahitaji huruma ya muumba.

Nampongea sana mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu kwa kuliona hili na hatimaye kuwaweka wazee wote nchini kuingia kwenye mfumo wa Bima bila masharti yoyote. Hakika wazee watapata ahueni.

CHAGUA TUNDU LISSU ILI BABU NA BIBI ZETU WAPATE BIMA NA HATIMAYE TUEPUKE GHARAMA

Kama kijana nitampigia Lissu kura yangu ili babu na bibi zangu wasiteseke tena kutafuta barua serikali za mitaa. Wanadharirika sana.
 
Back
Top Bottom