CCM Imejimaliza Rasmi na IPTL-ESCROW

CCM Imejimaliza Rasmi na IPTL-ESCROW

Porojo hizo, mlitaka umeme wa bure?

Hata kama unatumia makalio kufikiria huwezi kusapoti upuuzi wa chama chetu. CCM yetu ni janga la taifa. Viongozi wote waliotetea uovu ni wauaji. Hawa ghasia ni muuaji. Simba chawene muuaji. Waziri wa fedha (siyo mwigulu) ni wauaji
 
CCM ni janga la taifa.Leo wezi wanaambiwa waangalie jinsi ya kuandika hukumu zao.Tangu lini?Tulikosea sana kuikabidhi nchi kwa genge la wezi.

Wananchi wanaoipenda nchi hii lazima wakubali kuokokoa taifa hili na kufanya kwa ujasiri kama kule Burkinafaso,laa sivyo mkoloni mweusi hataacha kutunyonya na kutukandamiza hadi mautin.

Ni fursa kwa UKAWA na wote wasiopenda ukoloni huu ku mobilize umma kujikomboa wenyewe pasipo kutegemea fadhila za mkoloni huyu na mfumo wake.
 
Hapa kinachotokea ni kwamba kile kiburi cha wabunge wa CCM na serikali yake kutaka kutunisha misuli ili kuchukua ushindi kiburi hichi hawajaangalia kwa undani madhara yake kwa wananchi. Hakuna mjadala uliofuatiliwa kwa umakini na wananchi wengi kama huu. na kinachoumbua serikali ni kwamba kamati ya PAC si ya upinzani na wako watano tu mle na hapa inaonyesha ccm inajikataa yenyewe.

Kama Raisi atachekacheka tu na hawa vibaka basi ajue amemwachia mgombea wa CCM mzigo mkubwa wakati wa uchaguzi. Hela walizochota na zile zisizojulikana ni nyingi na kwa usalama wa chama naona CCM yenyewe kwenye vikao vyao vya ndani wawaondoe hawa wezi na ikiwezekana hatua za kisheria zichukuliwe ili imani ya wananchi irudi.

Watu kutoka Mara hawana historia ya kuiba hela za uma lakini nashangaa haya majambazi ya sasa imekuwaje
 
Kumbuka fedha za escrow ni malimbikizo ya fedha za miaka 10, sasa miaka 10 fedha zote za malipo ziwe zinapelekwa benki kuhifadhiwa unafikiri zitakuwa ndogo?

Lakini kumbuka kuwa, moja katika maafikiano yaliyopo ni ku re invest hizo fedha na kuibadili hiyo mitambo na kuongeza mingine inayotumia Gas kwa gharama nafuu ili bei zishuke. Na hilo tayari wamekubaliana na lipo kwenye harakati la kufanyika na PAP wameshatangaza kulianza.

Acha ujinga wewe, uliona wapi mtu binafsi anagawa pesa kama njugu? Tetea under five, pregnant mothers are suffering. Shame on you shame on all those who do not see white, as white
 
Halafu wabunge wa Ccm wanaimba Ccm nambari one!! Tena ndami ya ukumbi wa bhunge. Kwenye michango ya ripoti wengi ni vihiyo hawaongei. Ila kwenye kunoa midomo utadhani wamekula pilipili kichaa. Hii ni fedheha kwa taifa
 
Porojo hizo, mlitaka umeme wa bure?


Hivi wewe dada sijui bibi huo moyo wako niwakibinadam ama msukule!?
Mtake msitake aibu hii imewapata na ndio anguko lenu tupo hapa na tuombeane uzima.
 
Dah umenikumbusha hilo tukio,tuliongozwa na Tweve,sijui yupo wapi siku hizi Marry Ngowi
 
Last edited by a moderator:
Hapa kama ukimsikia vema Proff Muhongo zile ni real facts na inabidi tuzikubali hapana porojo na maneno hapa kuna vita na majungu haya tulia.
1.Wafanya biashara wenye chuki na uongozi bora wa nishati na madini hasa oil and gas.
2.wagombea urais chuki na PM wetu.wanahaha twiter nk
3.wanasheria waliokosa tenda za ufisadi kina Mkono
4 Mabenki uchwara
5.waliokosa huo mgao....
Hayo ndio CCM ife hakuna issue hapo....tutukie nchi yetu iishe kwa amani...na upendo.

Hujielewi,hujitambui na wala hufahamu kinachoendelea...vinginevyo waweza kuwa WAKALA WA SHETANI.
 
Hivi wewe dada sijui bibi huo moyo wako niwakibinadam ama msukule!?
Mtake msitake aibu hii imewapata na ndio anguko lenu tupo hapa na tuombeane uzima.

Aibu ipi? ya uongo na majungu. Narudia sijaona hoja ya maana zaidi ya majungu na drama.

Eti mtu kwenye maandiko anatoa ushauri Naibu Waziri awachishwe kazi halafu kwenye kura anakubali kuwa hana makosa yoyote. Uliona wapi hiyo zaidi UKAWA.

Hilo tu limetosha kutupilia mbali hoja zote zilizobaki za wengine. Hauwezi kuwa na ripoti ya uchunguzi halafu ukaikana ripoti yako.
 
Wacha kusema uongo.

Onesha huo wizi uko wapi? tumeona rripoti ya CAG na TAKuKURU hatujaona hata sehemu moja iliyosema kuna wizi waliougunduwa au rushwa waliyoiona katika uchunguzi wao.

Kwanini mnadanyana humu na mnadanganya umma wa Watanzania nyinyi na wabunge wenu?

Msifikiri kwa uongo ndiyo mtapata madaraka ya hii nchi, Watazania wanawaona na wanawashangaa sana watu wazima kusambaza uongo.

Onesha huo wizi uko wapi kama wewe u mkweli.

Mijitu mingine kama imerogwa watanzania akinanan au wewe peke yako? Maana ni watanzania wachache wenye mtazamo kama wako kipi hakifahamiki kwenye hizo ripoti au ww ni mtt wa muhongo acha kejeli ungejua wananchi wanahali mbaya usingetetea upuuzi huu
 
Acha ujinga wewe, uliona wapi mtu binafsi anagawa pesa kama njugu? Tetea under five, pregnant mothers are suffering. Shame on you shame on all those who do not see white, as white

Hizo hoja dhaifu sana, pregnant mother alipokosa umeme hoaspital mlisema aaah' mnauwa watoto. Sasa ana umeme, mnashindana na wawekezaji mnataka umeme wa bure.
 
Mijitu mingine kama imerogwa watanzania akinanan au wewe peke yako? Maana ni watanzania wachache wenye mtazamo kama wako kipi hakifahamiki kwenye hizo ripoti au ww ni mtt wa muhongo acha kejeli ungejua wananchi wanahali mbaya usingetetea upuuzi huu

Hata sakata la Dowans ni Watanzania wachache tuliosema uamuzi wa kufunga mitambo ya Dowans ni kulitia Taifa hasara. Matokeo, mahakama za Kimataifa zikaamuwa tuwalipe capacity charge, na umemem ambao ungezalishwa, na gharama zao zote na % ya interest. Umesahau?

Hili jambo la fedha za escrow ukweli uko wazi kabisa lakini Watanzania walio wengi wana aakili za kushikwa, hawaoni, hawasikii.

jamani hebu kuweni wa kweli wa nafsi zenu, hapo hapo unasema fedha zimeibiwa escrow, hapo hapo mtu mwingine anasema waliopewa hizo fedha wazilipie kodi aliyesema hizo fedha zimeibiwa amesha sahau anashangili kuwa hilo ni wazo zuri!

Khaa, sasa kama za wizi ukishazilipia kodi si umehalalisha? hebu kuweni wakweli wa nafsi zenu.
 
Back
Top Bottom