Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,422
- 49,037
Tofauti ya binadamu na wanyama, ipo kwenye ustaarabu, lakini kwenye mambo mengine mengi, tunashabihiana.
Wanyama wanakula kama tunavyokula wanadamu.
Wanyama wanajamihiana, kama ilivyo kwa binadamu.
Wanyama wanazaa na kufa kama ilivyo kwa wanadamu.
Mwanadamu ambaye ubinadamu wake umekamilika ana utashi ambao humtengenezea staarabu wa kutambua kuwa kila mwanadamu mwenzake ana utu kama wa kwake. Ustaarabu ndiyo humfanya authamini na kuuheshimu utu wa mwenzake, hata kama wanatofautiana katika fikra.
Wanadamu ambao ubinadamu wao umekamilika, kamwe huwezi kuwasikia wakisema kuwa eti mimi au mtu fulani ni lazima awe Rais au awe mbunge, kwa sababu anajua kuwa yeye au mwingine yeyote ni mwanadamu kama walivyo wengine, na hivyo kuna uwezekano wapo wenye uwezo kama wa kwake au hata wa kuweza kumzidi. Na tena linapokuja suala la uchaguzi, hawezi kutamka kuwa eti mtu fulani lazima awe Rais, kwa sababu anajua kuwa maamuzi ya nani awe Rais, Mbunge au diwani, ni maamuzi ya wapiga kura, ambayo yeye hana mamlaka nayo.
Kwenye nchi ambazo watu wamekamilisha ubinadamu wao, na sasa wanaishi kwenye ustaarabu, viongozi wao hata wakisikia minong'ono tu kuwa huenda wananchi wao hawawataki, mara moja au huitisha kura za maoni au hata huamua kujiondoa kwenye uongozi. Kwa sababu hawapendi wawaongoze watu ambao hawataki wawaongoze. Ndiyo maana kule Italy, kuna wakati Waziri mkuu alikuwa na mahusiano ya kimaoenzi na kahaba mmoja, minong'ono ikawa mingi dhidi yake. Waziri mkuu yule alikiri kuwa ni kweli ila alikwishaachana na huyo kahaba.
Hata hivyo aliitisha kura ya maoni kutaka kujua kama baada ya kufanya kosa hilo, bado wananchi wanataka awaongoze. Pale UK, kila mara tunasikia viongozi wakuu wakijiuzulu baada ya kujiridhisha kuwa wananchi wanaowaongoza hawaridhiki na uongozi wao.
Hali hiyo, leo imetokea USA, baada ya baadhi ya wamarekani kuonesha kuwa na mashaka na Biden kuendelea kuwa na uwezo thabiti kutokana na umri wake, kwa ustaarabu mkubwa katangaza kuwa hatagombea tena Urais.
Sasa ukija kwa Afrika, ni balaa tupu. Viongozi wengi wa Afrika, na waafrika walio wengi kwa ujumla, bado hawana ustaarabu wa kibinadamu. Wengi bado wana tabia zinazokaribiana na wanyama. Wanyama, walio wengi, mwenye nguvu ndiye mwenye haki ya kula zaidi, kutawala kundi lote, kumiliki na majike yote. Tabia hizo bado zipo sana kwa Waafrika. Ndiyo maana hata hapa kwetu CCM, wanaCCM walio wengi na viongozi wa CCM, huwa wanaamini ni wao tu ndio wenye haki ya kuongoza kwa sababu wana nguvu za dola, ndiyo maana ukiwapinga au kukosoa, watakuteka, watakutesa, watakufilisi, wakati fulani hata kukuua. Bado wanaamini kuwa mwenye maguvu ndiye mwenye haki ya kutawala, kama ilivyo kwa wanyama. Kinachoitwa demokrasia, kwa CCM na viongozi wao, kwao hakina maana. Ndiyo maana watatumia Polisi, wasiojulikana na hata majambazi ili tu wasalie madarakani.
Wazungu walio wengi wamekwishapita kwenye hatua hii ya ubinadamu wa mtu mweusi, japo wapo wazungu wachache, kama akina Putin, na huko Asia, bado wanakaribiana na watu weusi. Wazungu walio wengi ni jamii iliyostaarabika ambapo utu wa mwanadamu hupewa sana thamani. Ndiyo maana, leo hii mwingereza au mmarekani akitekwa na maharamia, serikali zao zipo tayari kutumia hata mabilioni ya pesa ili kumwokoa huyo mtu mmoja, wakati hapa kwetu mtu tu kuikosoa Serikali, anaweza kutekwa au hata kuuawa, na mwili wake kutupwa kwenye viroba baharini au kutupwa kwenye mbuga za wanyama ili awe chakula cha fisi.
Au mtu mwenye ulemavu wa ngozi anauawa ili viungo vyake vipelekwe kwa mchawi eti vikatengenezewe dawa ili mtu aweze kuwa mbunge au kiongozi wa Serikali. Yaani mtu hathamini kabisa uhai wa yule binadamu mwenzake anayeenda kumwua, sawa kabisa na mnyama ambaye yupo tayari kumwua mnyama mwenzake ili ashibishe tumbo lake, bila ya kufikiria thamani ya uhai wa yule mnyama mwenzake.
Wapo waafrika wachache sana, kama Nelson Mandela, ambaye hata wazungu walimstaajabia sana kwa hekima na ustaarabu wake, lakini viongozi wa Afrika walio wengi, ni laana tupu, hapa kwetu, ndiyo zaidi.
Ukisikia mtu anasema eti mtu fulani lazima awe Rais, au chama fulani lazima kishinde uchaguzi, au mtu fulani ni lazima awe mbunge, utambue kuwa huyu ubinadamu wake bado haujakamilika. Bado ni mnyama. Maana mwanadamu mstaarabu anatambua kuwa hakuna mwanadamu hata mmoja anayemiliki hisia na maamuzi ya watu wengine, ndiyo maana watu wastaarabu huwa wanafanya uchaguzi ili kujua maamuzi na hisia za walio wengi. Kama unajua kuwa mtu fulani ni lazima awe Rais, mbunge au diwani, au unajua kuwa CCM lazima itashinda uchaguzi, kuna haja gani ya kufanya uchaguzi?
CCM wakemeeni au hata kusitisha uwanachama wa watu ambao ubinadamu wao bado haujakamilika, maana huko huko CCM inaonekana ndiko walikojaa.
Wale ambao ni binadamu ambao ubinafamu wao umekamilika, heshimuni utu, na maamuzi ya watu wengine kwani ninyi hamna tofauti yoyote dhidi yao katika utu tuliopewa na Mungu, hata kama tunatofautiana katika mambo madogo madogo.