CCM ilioza, CHADEMA/UKAWA inaoza!

CCM ilioza, CHADEMA/UKAWA inaoza!

Vetting ulitaka wakutangazie? ... ww ni katika Vatican mafiaz ... beneficiaries wa mfumo unaonufaisha nchi za magharibi plus mabeberu wa dunia hii ... Chagua UKAWA kwa maslahi mapana ya Watanzania ... Nukushi zako ziweke baada ya miaka mitano tutafanya tathmini tena ... for now CCM must go to hell ...

Wakati akimnadi mgombea urais wa CCM, Benjamin Mkapa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alipata kusema, “CCM ni kama kokoro. Linabeba samaki, wakubwa kwa wadogo. Linabeba hata takataka.”

Kauli ya Mwl. Nyerere ilitoka baada ya nchi kuingia kwenye mageuzi ya kisiasa na kiuchumi bila kuwepo kwa misingi imara ya kupambana na changamoto za soko huria la kiuchumi na kisiasa.

Mwaka 1925, Mahatma Gandhi aliwahi kuorodhesha Seven Social Sins, mojawapo ilikuwa ni politics without principle. He went on to say having politics without truth(s) to justly dictate the action creates chaos, which ultimately leads to failure and violence.

Kwa kukosekana na misingi imara ya kisiasa, CCM ilijikuta ikivamiwa na wanachama/viongozi ambao wana kila aina ya uchafu na hawana maadili. CCM ilikuwa ni kama mzoga ambao ulikuwa unavuta mainzi na mafisi. Kukaibuka kaulimbiu inayosema; ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri.’

Uchafu wa kisiasa na kukosekana maadili kilipekea kuibuka kwa kikundi kinachojiita wanamtandao (party cartel). Wanamtandao kimsingi kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa ni chama ndani ya CCM katika msingi wa kupata nguvu na madaraka ya juu nchini kwa njia yoyote.

Kama ilivyo kawaida, Mtandao una maisha mafupi, Mwaka 2012 ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa maisha ya wanamtandao kama party cartel within CCM.

Baada ya uteuzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Magufuli, tumeshuhudia kumeguka kwa wanamtandao ambapo pande lingine kwa sasa linatafuta maisha yenye heri ndani ya CHADEMA/UKAWA.

CHADEMA ambayo ilikuwa tofauti na CCM kwa sasa imeanza kuvaa mavazi ya CCM ya mwaka 1995. CHADEMA imeanza kuachana na misingi yake ya kupambana na ufisadi na kwa kufanya hivyo, inakuwa kama mzoga unaovutia mainzi na mafisi ya kisiasa. Kauli mbiu iliyokuwa CCM inayosema ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri’ kwa sasa imeanza kupata nafasi ndani ya CHADEMA/UKAWA.

Kwa sasa ndani ya CHADEMA/UKAWA hakuna vetting na tunaambiwa mwanachama anayeijiunga leo hana tofauti na yule aliyejiunga miaka 20 iliyopita. unaweza kujiunga leo na kupewa uongozi leo. Dhana ya makapi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Dk. Slaa ndani ya CHADEMA sio hoja tena.

Wapiga kura makini nchini kwa sasa wako kwenye limbo. Wapiga kura makini kwa sasa wanakabiliwa na zoezi la kuchagua shetani mzee (CCM) chini ya Magufuli au shetani kijana(CHADEMA/UKAWA) chini ya Lowassa.

Kwa sasa siasa za Tanzania huwezi kuzitofautisha na upuuzi ambao huwezi kuepuka kwenye sanduku la kura!

Kampeni za mwaka huu zitakuwa ni kivutio chenye matokeo yale yale!
 
Mchuano ni kati ya tingatinga na dereva vipi hapo??

Tunataka kusikia hoja na uwezo wa wagombea kuongoza na sio siasa zenu za majungu na kimaskini!!!

Tunahitaji Rais ambae atakuwa Kiongozi na Sio Manager!!!!
Mkuu,
Wewe ulishasema hoja zangu ni nyeupe kama makamasi lakini cha kushangaza bado unataka kusikia zaidi hoja nyeupe kama makamasi!

Badala ya kusikia majibu yenye hoja nyeupe kama kamasi, majibu ya hoja yako ulishawahi kujibu wewe mwenyewe ambapo ulisema katika thread hii,

Kwenye comment namba 16 ulisema,
Wewe unaamini bali Mimi ninajua kwa hakika Lowassa ni mgonjwa taabani asiyeweza kubeba bilauri kwa dakika hata 5!!!

Malipo ni hapa hapa duniani wamechezea Sana jasho la watanzania hao bado yule joka lenye makengeza IPO siku Mungu atamrarua akomeshe jeuri yake kwa watanzania.
Kwa hiyo unataka nini zaidi wakati umejijibu mwenyewe?
 
He he heee! Ha ha haaa! Are you one of the wapiga kura makini?
CCM hawaishiwi vituko.
 
We mgonjwa kalale hizi hashuo zako hazisaidii kitu!!!
hapa ni ku delete CCM tu hiyo Pombe yako imwage tu haina wanywaji!!!
Kama kuna watu wanaumizwa na ngoma ya UKAWA, huyo Ng'wamapalala kaumia si mchezo. Ukikusanya post zake zote anazoanzisha humu bila kupumzika, unaona kabisa alivyoathirika na bado. Ngoma ya UKAWA ni nzito na kama nilivyowahi kusema humu, CCM inamomonyolewa hatua kwa hatua, hizi za sasa ni rasha rasha tu, zinakuja zitakazowafanya wazimie kabisa. Kwa kuanzia, tusubiri vichwa vikuu vya habari Jumatatu...hakuna mtu atayekuwa tena na hamu wala muda wa kupoteza akifuatilia ngonjera na mipasho ya kesho Jumapili Jangwani...stay tuned!
 
Mkuu,
Wewe ulishasema hoja zangu ni nyeupe kama makamasi lakini cha kushangaza bado unataka kusikia zaidi hoja nyeupe kama makamasi!

Badala ya kusikia majibu yenye hoja nyeupe kama kamasi, majibu ya hoja yako ulishawahi kujibu wewe mwenyewe ambapo ulisema katika thread hii,

Kwenye comment namba 16 ulisema,

Kwa hiyo unataka nini zaidi wakati umejijibu mwenyewe?

Ubaya wa JF it keeps records.,jamaa kama kaumbuka fulani hivi..
 
huwezi kusema UKAWA NA Lowassa ni shetani kijana hilo halijathibitishwa hivyo unakua unaspeculate tu. in the other hand CCM wamedhihirisha ushetani wao kwa miaka 54. hivi CCM wana mbinu gani ya kututoa kwenye umasikini ambayo hawakutumi kwenye hiyo miaka 54? kibaya zaidi mwenyekiti wake hajui kwanini tu masikini.
 
Mkuu, tatizo kuna serious divide sasa hivi not only social but mental divide na utaweza kudadavua kupitia comments tu chini katika thread hii .. mtu anajibu kifupi hatafakari ulichosema au kuelewa hata 10%. It's a serious problem and what you see is degeneration of ethics, morals and thinking capacity. We are facing a bleak future!
Mkuu,
Hili la baadhi ya wanaJF kutoa comment za kijinga kijinga haliwezi kunizuia/kutuzuia kuongea hoja zenye msingi wa kujenga katika fikra pana.

Ninaamini kwenye mkusanyiko kama Jamiiforums hawakosekani pia wajinga na wapumbavu!

Tutaelimishana pole pole!
 
CCM A vs CCM B...
Vita baina ya UKAWA vs CCM imekufa ghafla, sasa tunashuhudia CCM A ikipambana vikali na CCM B. Nionavyo mimi, CCM A tayari imejisafisha na kupeleka makapi yote CCM B. October tutashuhudia CCM A mpya. CCM B itakuwa chama pinzani na kitajitenga na UKAWA kwa vile madhumini ya kuwa pamoja hayakufikiwa.

Kura yangu siwezi kumpa Lowassa kamwe.
 
Huyu ni ccm tumpuuze.
Mkuu,
Tatizo ni kwamba wewe hujampuuza ndio maana umefikia hatua ya kutoa comment baada ya kusoma mada.

Hao wengine wataanza vipi kumpuuza kama wewe unayependa kuwa kiongozi wao hujampuuza mtoa mada?
 
Haha siku nyingi kalikua kanajifanya ni kamwanaharakati kumbe uchwara kama yule aliyekauka mwili polepole!!!

Anajifanyaga yupo neutral kumbe ni kuwadi mkubwa wa CCM!!!
Obsession, fixation or inferiority complex?
 
Hivi wanaofananafanana na nyumbu kati ya makundi haya;

images
...
images
...
images

na haya;

images
...
images
...
images

Ni yapi? Nilikuwa nauliza tu...

Ninavyojua nyumbu hufanana, tena sana tu.

Mkuu,
Mimi nadhani wanapotumia neno nyumbu hawana maana ya kufanana mavazi bali wana maana ya kufanya jambo bila kuhoji na kuchanganua matokeo ya kile wanafanya/wanataka kukifanya.
 
Hapo uliposema shetani mzee na kijana nakubaliana na wewe, kweli wale tunaoangalia sera tupo mjia panda, ukitazama kila pande hakuna nafuu huku mabadiliko tukiyataka japo hatuoni kutuwakilisha kwenye mabadiliko hayo.
 
We mgonjwa kalale hizi hashuo zako hazisaidii kitu!!!

hapa ni ku delete CCM tu hiyo Pombe yako imwage tu haina wanywaji!!!
Mkuu,
Nani amekuambia ninataka kulala au nilipo ni usiku?

Utai-delete vipi CCM wakati kifaa cha kui-delete ulikisema hivi,
Wewe unaamini bali Mimi ninajua kwa hakika Lowassa ni mgonjwa taabani asiyeweza kubeba bilauri kwa dakika hata 5!!!

Malipo ni hapa hapa duniani wamechezea Sana jasho la watanzania hao bado yule joka lenye makengeza IPO siku Mungu atamrarua akomeshe jeuri yake kwa watanzania.
Baada ya mwanaJF kusema hivi,
Mimi nnaamini Lowassa ni mgonjwa kwa sasa na afya yake si kama ile ya miaka 10 nyuma.
Kwenye thread hii,
Tutaendelea kukukumbusha!
 
CCM A vs CCM B...
Vita baina ya UKAWA vs CCM imekufa ghafla, sasa tunashuhudia CCM A ikipambana vikali na CCM B. Nionavyo mimi, CCM A tayari imejisafisha na kupeleka makapi yote CCM B. October tutashuhudia CCM A mpya. CCM B itakuwa chama pinzani na kitajitenga na UKAWA kwa vile madhumini ya kuwa pamoja hayakufikiwa.

Kura yangu siwezi kumpa Lowassa kamwe.

Yote uliyoongea ilikuwa kuzuga tu, msingi wa yote uko paragrafu ya mwisho...chuki zako kwa Lowassa.
 
Vetting ulitaka wakutangazie? ... ww ni katika Vatican mafiaz ... beneficiaries wa mfumo unaonufaisha nchi za magharibi plus mabeberu wa dunia hii ... Chagua UKAWA kwa maslahi mapana ya Watanzania ... Nukushi zako ziweke baada ya miaka mitano tutafanya tathmini tena ... for now CCM must go to hell ...
Mkuu,
Bahati mbaya huwa sijadili siasa katika mlengo wa kidini.

Kama nikitaka kujadili dini huwa ninaingia kwenye jukwaa linalohusu masuala ya kidini.

Bahati mbaya hili ni jukwaa la siasa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom