CCM ilioza, CHADEMA/UKAWA inaoza!

CCM ilioza, CHADEMA/UKAWA inaoza!

Wakati akimnadi mgombea urais wa CCM, Benjamin Mkapa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alipata kusema, “CCM ni kama kokoro. Linabeba samaki, wakubwa kwa wadogo. Linabeba hata takataka.”

Kauli ya Mwl. Nyerere ilitoka baada ya nchi kuingia kwenye mageuzi ya kisiasa na kiuchumi bila kuwepo kwa misingi imara ya kupambana na changamoto za soko huria la kiuchumi na kisiasa.

Mwaka 1925, Mahatma Gandhi aliwahi kuorodhesha Seven Social Sins, mojawapo ilikuwa ni politics without principle. He went on to say having politics without truth(s) to justly dictate the action creates chaos, which ultimately leads to failure and violence.

Kwa kukosekana na misingi imara ya kisiasa, CCM ilijikuta ikivamiwa na wanachama/viongozi ambao wana kila aina ya uchafu na hawana maadili. CCM ilikuwa ni kama mzoga ambao ulikuwa unavuta mainzi na mafisi. Kukaibuka kaulimbiu inayosema; ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri.’

Uchafu wa kisiasa na kukosekana maadili kilipekea kuibuka kwa kikundi kinachojiita wanamtandao (party cartel). Wanamtandao kimsingi kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa ni chama ndani ya CCM katika msingi wa kupata nguvu na madaraka ya juu nchini kwa njia yoyote.

Kama ilivyo kawaida, Mtandao una maisha mafupi, Mwaka 2012 ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa maisha ya wanamtandao kama party cartel within CCM.

Baada ya uteuzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Magufuli, tumeshuhudia kumeguka kwa wanamtandao ambapo pande lingine kwa sasa linatafuta maisha yenye heri ndani ya CHADEMA/UKAWA.

CHADEMA ambayo ilikuwa tofauti na CCM kwa sasa imeanza kuvaa mavazi ya CCM ya mwaka 1995. CHADEMA imeanza kuachana na misingi yake ya kupambana na ufisadi na kwa kufanya hivyo, inakuwa kama mzoga unaovutia mainzi na mafisi ya kisiasa. Kauli mbiu iliyokuwa CCM inayosema ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri’ kwa sasa imeanza kupata nafasi ndani ya CHADEMA/UKAWA.

Kwa sasa ndani ya CHADEMA/UKAWA hakuna vetting na tunaambiwa mwanachama anayeijiunga leo hana tofauti na yule aliyejiunga miaka 20 iliyopita. unaweza kujiunga leo na kupewa uongozi leo. Dhana ya makapi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Dk. Slaa ndani ya CHADEMA sio hoja tena.

Wapiga kura makini nchini kwa sasa wako kwenye limbo. Wapiga kura makini kwa sasa wanakabiliwa na zoezi la kuchagua shetani mzee (CCM) chini ya Magufuli au shetani kijana(CHADEMA/UKAWA) chini ya Lowassa.

Kwa sasa siasa za Tanzania huwezi kuzitofautisha na upuuzi ambao huwezi kuepuka kwenye sanduku la kura!

Kampeni za mwaka huu zitakuwa ni kivutio chenye matokeo yale yale!

Kiongozi umeongea ukweli kabisa. Mimi mwenyewe hapa niko njia panda kabisa maana wote hao wanafanana.
 
Mkuu,
Hii nadhani ni inferiority complex yako!

Ni wapi nilijifanya kama mjanja?

Fikra zako haziakisi ukweli!
Wapi nimekutaja wewe nguchilo? huna la maana zaidi ya kujinafikisha kwa watawala ukitumaini kurushiwa makombo!
 
Lengo lako nini haswa?wananchi tunataka kuiondoa CCM kwanza.Mengine tutashughulikia baada ya kazi hii muhimu.
 
Wakati akimnadi mgombea urais wa CCM, Benjamin Mkapa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alipata kusema, “CCM ni kama kokoro. Linabeba samaki, wakubwa kwa wadogo. Linabeba hata takataka.”

Kauli ya Mwl. Nyerere ilitoka baada ya nchi kuingia kwenye mageuzi ya kisiasa na kiuchumi bila kuwepo kwa misingi imara ya kupambana na changamoto za soko huria la kiuchumi na kisiasa.

Mwaka 1925, Mahatma Gandhi aliwahi kuorodhesha Seven Social Sins, mojawapo ilikuwa ni politics without principle. He went on to say having politics without truth(s) to justly dictate the action creates chaos, which ultimately leads to failure and violence.

Kwa kukosekana na misingi imara ya kisiasa, CCM ilijikuta ikivamiwa na wanachama/viongozi ambao wana kila aina ya uchafu na hawana maadili. CCM ilikuwa ni kama mzoga ambao ulikuwa unavuta mainzi na mafisi. Kukaibuka kaulimbiu inayosema; ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri.’

Uchafu wa kisiasa na kukosekana maadili kilipekea kuibuka kwa kikundi kinachojiita wanamtandao (party cartel). Wanamtandao kimsingi kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa ni chama ndani ya CCM katika msingi wa kupata nguvu na madaraka ya juu nchini kwa njia yoyote.

Kama ilivyo kawaida, Mtandao una maisha mafupi, Mwaka 2012 ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa maisha ya wanamtandao kama party cartel within CCM.

Baada ya uteuzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Magufuli, tumeshuhudia kumeguka kwa wanamtandao ambapo pande lingine kwa sasa linatafuta maisha yenye heri ndani ya CHADEMA/UKAWA.

CHADEMA ambayo ilikuwa tofauti na CCM kwa sasa imeanza kuvaa mavazi ya CCM ya mwaka 1995. CHADEMA imeanza kuachana na misingi yake ya kupambana na ufisadi na kwa kufanya hivyo, inakuwa kama mzoga unaovutia mainzi na mafisi ya kisiasa. Kauli mbiu iliyokuwa CCM inayosema ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri’ kwa sasa imeanza kupata nafasi ndani ya CHADEMA/UKAWA.

Kwa sasa ndani ya CHADEMA/UKAWA hakuna vetting na tunaambiwa mwanachama anayeijiunga leo hana tofauti na yule aliyejiunga miaka 20 iliyopita. unaweza kujiunga leo na kupewa uongozi leo. Dhana ya makapi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Dk. Slaa ndani ya CHADEMA sio hoja tena.

Wapiga kura makini nchini kwa sasa wako kwenye limbo. Wapiga kura makini kwa sasa wanakabiliwa na zoezi la kuchagua shetani mzee (CCM) chini ya Magufuli au shetani kijana(CHADEMA/UKAWA) chini ya Lowassa.

Kwa sasa siasa za Tanzania huwezi kuzitofautisha na upuuzi ambao huwezi kuepuka kwenye sanduku la kura!

Kampeni za mwaka huu zitakuwa ni kivutio chenye matokeo yale yale!

Well said.
 
Kiongozi umeongea ukweli kabisa. Mimi mwenyewe hapa niko njia panda kabisa maana wote hao wanafanana.

Usisimame njia panda .kazi ni kumwondoa nduli ccm kwanza.mengine tutaweka sawa baadae.wape wagombea wa UKAWA kura yako.saa ya ukombozi ni sasa.
 
Mkuu,Kwa sasa siwezi kusema kama CHADEMA ni tawi la CCM lakini ninachofahamu, kilichoifanya CCM kufika hapa ilipo ndio kile kimeanza kujitokeza ndani ya CHADEMA/UKAWA.
Ndugu muda wowote tutayaona mengi ya ccm cdm, ndio maana najisemea ukombozi wa tz bado
 
Yote uliyoongea ilikuwa kuzuga tu, msingi wa yote uko paragrafu ya mwisho...chuki zako kwa Lowassa.

I wish ningekuwa na chuki kwa Lowassa, sina affiliation na chama chochote na wala sifuati mkumbo lakini pia sina mihemko katika kufanya maamuzi. Niliyosema ni utashi wangu na nitasimamia hapo.

Misingi ya ukawa haipo tena, wimbo wao dhidi ya ufisadi umekufa ghafla, sasa wanatafuta mbinu za kusafisha uchafu ulioletwa toka CCM A. Nilukuwa muumini mzuri wa siasa zao, lakini sasa basi....
 
It is now over 50 years and it is time for change but what's change...

Change...(to whom it may concern)

After you've done a thing the same way for two years, look it over carefully. After five years, look at it with suspicion. And after ten years, throw it away and start all over.

He who rejects change is the architect of decay. The only human institution which rejects progress is the cemetery.

Few can accept happiness if it means change. We want the life we have now, only happier. It's the most unhappy people who most fear change.

When the winds of change blow, some people build walls and others build windmills.

Those who expect moments of change to be comfortable and free of conflict have not learned their history.

The man who never alters his opinion is like standing water, and breeds reptiles of the mind.

All changes, even the most longed for, have their melancholy; for what we leave behind us is a part of ourselves; we must die to one life before we can enter another.

To exist is to change, to change is to mature, to mature is to go on creating oneself endlessly.

He that will not apply new remedies must expect new evils; for time is the greatest innovator.

The only man I know who behaves sensibly is my tailor; he takes my measurements anew each time he sees me. The rest go on with their old measurements and expect me to fit them.

CCM just has to go...
 
Mimi ilikua niwapigie ukawa kura zote kuanzia urais mpaka udiwani,lakini kitendo cha kumleta lowassa kura Yangu ya urais imerudi kwa magufuli,nitawapa ukawa kura ya ubunge na udiwani,kama ukawa watakua wanafikili ninavyofikili Mimi basi ni heri tu,Mimi nafikili ukawa wanamtumia lowasa ili kupata viti vingi vya ubunge na udiwani tu,

huku wakijua kabisa kwamba swala la urais kwa lowasa halipo,yaani ccm wakukate,wakuite makapi fisadi mgonjwa,halafu uende ukawa hata wananchi wakupigie kura zote za urais wewe ccm hawakupi urais,si wanakujua madhambi yako ,

na this time naungana na ccm goli la mkono ikibidi poa tu, lowasa sio! huyo ni wakutumiwa tu kama alivyomtumia kikwete halafu akamwaga,ukawa nanyie mtumieni halafu mnamwaga! kimeo hicho !

Umenena poa sana mkuu na hata ikibidi ubunge hatuwapi tutawapa tu udiwani, kwasababu wametulaghai sana, kama leo wanaachana na itikadi ya ufisadi tunategemea wabunge wao wakaseme nini juu ya ufisadi? mie zote kwa CCM ..potelea potea, CCM sahivi inapendeza wakati Ukawa sahivi inakera
 
Mkuu,
Nani amekuambia ninataka kulala au nilipo ni usiku?

Utai-delete vipi CCM wakati kifaa cha kui-delete ulikisema hivi,

Baada ya mwanaJF kusema hivi,

Kwenye thread hii,

Tutaendelea kukukumbusha!

Ndio maana nasemaga wewe ni kima tu kwakuwa huna uwezo wa kupambanua nyakati na mazingira!!!

Fukunyua post zangu zoote za humu na ninakiri awali nilikua CCM na nimeitetea sana CCM humu but sasa nimebadilika!!!

Hata JK alimsifu sana EL alipokua CCM leo anamponda!!!

Hata akina Taylor walisifiwa na magharibi lkn leo wanamhenyesha ICC!!!

Sauli aliua sana watumishi wa Mungu but mwishowe akawa mhubiri wa injili!!!!

Kigeni kwako nini??
 
Kuna tofauti kati ya uanaharakati na siasa..na huwa kuna tatizo tunapo-deal na wanaharakati feki kama muanzisha mada..

Hamna msingi wowote uliokiukwa kwa usajili uliofanyika mpaka hivi sasa..na kwa taarifa yako vita dhidi ya ufisadi imo kwenye ilani ya CDM...Honestly, kama kuna watu hawawezi kuzungumzia 'ufisadi' basi ni CCM...CCM wanazungumzia kuanzisha 'mahakama ya rushwa', what for? tatizo la rushwa haliwezi kutatuliwa na mahakama 'special' kushughulika nayo....

Wakati wanamtandao wanamuingiza Kikwete madarakani haikuwa issue ya kuzungumzia, pengine kwa sababu CCM ilikuwa inarudi madarakani, lakini inaonekana ni issue pale ambapo uwezekano wa CCM kurudi madarakani unazidi kuwa mdogo!!!...any campaign needs not just a campaign team but also campaign funds mobilized from different sources such as friends, relatives, from fundraising and even 'loans'....

Unavyozungumzia maadili, sijui shetani mzee na kijana, huko ni kutapatapa, ni kama mtu aliyesombwa na mafuriko halafu anatafuta pa kushikilia...CCM wamefanya kitu gani cha maana kushughulikia rushwa na ufisadi hadi wanyooshee wengine vidole kuhusu maadili?...huyo 'shetani kijana' ni lini kahujumu uchumi wa Tanzania? Ni lazima tuwe na vyama vikubwa viwili+ hii nchi ili twende sawa kwenye utendaji kazi na uwajibikaji.....mambo ya chama kimoja kutawala zaidi ya nusu karne ni 'old tradition', it is holding us back, it needs to end....

Mtu akisema siasa za Tz ni upuuzi, hiyo ni subjective view, na hasahasa ni kwa wale wasiolelewa political dynamism, tactics and strategies....hatuwezi kutoa chama chenye mizizi ilikomaa kwa miaka 50+ na ambacho kina-control almost everything katika hii nchi kwa kutumia walewale tuliokua nao bila kukivunja vipande vipande...historia inaonyesha kuwa ndivyo ilivyotokea kwa Zambia, Kenya, Nigeria n.k....na ndio CHADEMA wanachokifanya hapa Tanzania...'splitting CCM like pieces of firewood'

Baada ya kuanzishwa kwa multi-partism 1992, ni wanaCCM ndio walioanzisha vyama vya siasa kama CDM...na imekuwa kawaida kwa CDM kusajili wanaCCM, tatizo usajili wa mwaka huu (wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu wawili+) umewachanganya sana CCM..kwahiyo wanarusha kila aina ya vijembe mfano 'makapi' kupooza hasira zao lakini wapi?....mbona hawajawahi kusema 'makapi' toka 1992...kwanini waseme 2015?
 
Wakati akimnadi mgombea urais wa CCM, Benjamin Mkapa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alipata kusema, “CCM ni kama kokoro. Linabeba samaki, wakubwa kwa wadogo. Linabeba hata takataka.”

Kauli ya Mwl. Nyerere ilitoka baada ya nchi kuingia kwenye mageuzi ya kisiasa na kiuchumi bila kuwepo kwa misingi imara ya kupambana na changamoto za soko huria la kiuchumi na kisiasa.

Mwaka 1925, Mahatma Gandhi aliwahi kuorodhesha Seven Social Sins, mojawapo ilikuwa ni politics without principle. He went on to say having politics without truth(s) to justly dictate the action creates chaos, which ultimately leads to failure and violence.

Kwa kukosekana na misingi imara ya kisiasa, CCM ilijikuta ikivamiwa na wanachama/viongozi ambao wana kila aina ya uchafu na hawana maadili. CCM ilikuwa ni kama mzoga ambao ulikuwa unavuta mainzi na mafisi. Kukaibuka kaulimbiu inayosema; ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri.’

Uchafu wa kisiasa na kukosekana maadili kilipekea kuibuka kwa kikundi kinachojiita wanamtandao (party cartel). Wanamtandao kimsingi kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa ni chama ndani ya CCM katika msingi wa kupata nguvu na madaraka ya juu nchini kwa njia yoyote.

Kama ilivyo kawaida, Mtandao una maisha mafupi, Mwaka 2012 ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa maisha ya wanamtandao kama party cartel within CCM.

Baada ya uteuzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Magufuli, tumeshuhudia kumeguka kwa wanamtandao ambapo pande lingine kwa sasa linatafuta maisha yenye heri ndani ya CHADEMA/UKAWA.

CHADEMA ambayo ilikuwa tofauti na CCM kwa sasa imeanza kuvaa mavazi ya CCM ya mwaka 1995. CHADEMA imeanza kuachana na misingi yake ya kupambana na ufisadi na kwa kufanya hivyo, inakuwa kama mzoga unaovutia mainzi na mafisi ya kisiasa. Kauli mbiu iliyokuwa CCM inayosema ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri’ kwa sasa imeanza kupata nafasi ndani ya CHADEMA/UKAWA.

Kwa sasa ndani ya CHADEMA/UKAWA hakuna vetting na tunaambiwa mwanachama anayeijiunga leo hana tofauti na yule aliyejiunga miaka 20 iliyopita. unaweza kujiunga leo na kupewa uongozi leo. Dhana ya makapi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Dk. Slaa ndani ya CHADEMA sio hoja tena.

Wapiga kura makini nchini kwa sasa wako kwenye limbo. Wapiga kura makini kwa sasa wanakabiliwa na zoezi la kuchagua shetani mzee (CCM) chini ya Magufuli au shetani kijana(CHADEMA/UKAWA) chini ya Lowassa.

Kwa sasa siasa za Tanzania huwezi kuzitofautisha na upuuzi ambao huwezi kuepuka kwenye sanduku la kura!

Kampeni za mwaka huu zitakuwa ni kivutio chenye matokeo yale yale!

This is the best analysis of what is going on in CHADEMA with respect to what was going on in CCM i have read so far. Well done Mkuu. I have been trying to find exact words to express what you have written for so long, yet have always come up short.

If Slaa was still around in CDM, i would have hopes of anything to change.., as of Now CHADEMA is more team lowassa than it is CHADEMA, and we all know their mantra..., Ikulu at all costs.NO PRINCIPLES. As we have learned, even those we thought had little principles in CHADEMA, had a price.., and apparently their price is a promise of getting to IKULU.., at all cost...,

I disagree, I will always disagree, and i will make myself as clear as possible, whatever is going on in CHADEMA now is the most shameful political act our country has ever been through.., and it's amazing to see CHADEMA with its leaders, standing in front of Tanzanians with a straight face and swallow about every principle and public stance they have made over the past 10 years and expect the same Tanzanians to vote them in. They must think Tanzanians are baboons, with brains of 5 years olds.
 
Mbona hamtaki kuambiwa ukweli?

Sifa kuu ya kiumbe kinachotaka kuangamia..,

We perish the moment we stop taking criticism. Yani kuna mabushuti CHADEMA wanaamini hakuna kosa wanaweza kufanya.., Jambo la Ajabu kabisa.
 
Mkuu,
Wewe ulishasema hoja zangu ni nyeupe kama makamasi lakini cha kushangaza bado unataka kusikia zaidi hgoja nyeupe kama makamasi!

Badala ya kusikia majibu yenye hoja nyeupe kama kamasi, majibu ya hoja yako ulishawahi kujibu wewe mwenyewe ambapo ulisema katika thread hii,

Kwenye comment namba 16 ulisema,

Kwa hiyo unataka nini zaidi wakati umejijibu mwenyewe?
Mkuu wafuasi wa ukawa ni kama nyumbu.leo watasema hili kesho watageuka.ukawa chini ya slaa ilikua tishio kwa ccm,lakini ukawa hii ya sumaye na mngeja? Uchaguzi utaisha tatehe 24!
 
Kila anayehama anadai kaonewa alikotoka! Siyo wapambanaji wa kweli ni misukumo ya natakwa yao tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom