CCM iko imara na Magufuli hajaleta hofu yoyote, wahoji Mbona Lowassa kasimama kuchangia makanisa?

CCM IKO IMARA NA MAGUFULI HAJALETA HOFU YOYOTE

UPOTOSHAJI unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, leo, Jumapili Desemba 18, 2016 umeendelea tena kwa gazeti moja linalokiunga mkono chama kimoja cha upinzani hususan Tanzania Bara, kuchapisha habari yenye kichwa kinachosema "JPM azusha hofu mpya CCM" na kudai ifuatavyo:

(1) Kwamba mabadiliko makubwa ya kimuundo yaliyotangazwa siku chache zilizopita na Chama Cha Mapinduzi (CCM), yamezusha hofu kwa makada wake kuwa mwanzo wa kukiua badala ya kukiimarisha.

UKWELI ULIVYO

Tangu kumalizika kwa vikao vya Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Jumanne Desemba 13, 2016 hadi sasa hakuna mwanachama, kiongozi wala mfuasi yeyote wa CCM aliyelalamika, kuhoji au kunung'unukia mabadiliko yoyote yaliyopitishwa na vikao hivyo.

Badala yake, madai ya gazeti hilo ambalo limejipambanua wazi kuwa linakisemea, kukitumikia na kutekeleza matakwa yote ya chama hicho cha upinzani huku likiwa liko huru ni habari za kufikirika kichwani, zile ambazo licha ya kutungiwa mezani pia zinaweza kuitwa kuwa za ni kuokoteza barabarani.

(2) Kwamba mabadiliko ya kupunguza Wajumbe wa Kamati Kuu kutoka 34 na kubaki 24 na Wajumbe wa NEC kutoka 388 na kubaki 158 yanalenga kukifanya chama hicho kuwa cha wachache katika ngazi za uamuzi, hatua ambayo itakuwa na athari zaidi kwa CCM.

UKWELI ULIVYO

Vikao vyote vya CCM katika ngazi zote ni vya uwakilishi, hivyo idadi ya watu siyo hoja na haina msingi wowote.

Ndiyo maana kwa mfano Kamati za Usalama na Maadili katika ngazi zote za matawi, kata, wilaya mpaka mikoa zinaundwa na wajumbe watano tu.

Kama watu watano wanaweza kuwawakilisha wana CCM wote katika mkoa mzima kwa mfano, inawezekanaje kwa wawakilishi 158 kwa mikoa 31 waonekane wachache?

Lakini pia, hivi watu 388 wanapokutana mahali hicho kinakuwa kikao au mkutano wa hadhara ambao hata mijadala yake inaweza isifanyike kwa usahihi?

Hivi inawezekana kwa watu wote hao kuchangia kwenye kikao cha siku moja au mbili tu?

(3) Madai kwamba hatua ya kila wilaya kuwa na Mjumbe wa NEC inawafanya wana CCM waone chama kimepelekwa mkononi mwao, na pia inakuwa rahisi kwake kuwapelekea wenzake mambo waliyokubaliana kwenye vikao.

UKWELI ULIVYO

Nafasi za Wajumbe wa NEC wanaowakilisha wilaya ambazo sasa zinaondolewa hazikuwahi kuwepo katika historia ya TANU, ASP wala CCM yenyewe tokea ianzishwe mwaka 1977 hadi zilipoanzishwa miaka minne iliyopita, yaani mwaka 2012 tu.

Hivi kama hazikuwepo kwa miaka yote 23 ya uhai wa TANU, miaka yote 20 ya uhai wa ASP na miaka 35 ya CCM na chama kilikuwa kinafanya vizuri katika malengo yake ya kisiasa, hivi uwepo wao wa miaka hiyo umeleta tija gani ambayo wakiondolewa itakuwa hasara?

Kuhusu madai kwamba wanapotoka kwenye vikao vya NEC walikuwa wanawapelekea wanachama kile kilichoamuliwa pia ni hisia za kufikirika vichwani mwa watu wasiohusika na chochote kile kwa CCM.

Kazi ya kuwapelekea wana CCM maamuzi mbalimbali ya NEC siyo ya Wajumbe wa NEC ila inafanywa na Katibu Mkuu wa CCM kupitia kwa makatibu wa chama hicho wa mikoa, wilaya, majimbo (kwa Zanzibar), kata, matawi na hatimaye wa mashina.

Hao ndio huifanya kazi hiyo kwa kuzingatia Ibara za 25(a), 44(2)(a) - (c), 58(2)(a) - (c), 72(2)(a) - (c), 86(2)(a) - (c) na 100(2)(a) - (c) za Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2012 inayotumika sasa.

(5)Kwamba kuondolewa kwa Wajumbe wa NEC wanaowakilisha wilaya kutaiweka CCM katika hali ngumu hasa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2019.

Inaelezwa kuwa hiyo itatokana na kwamba katika uchaguzi kama huo mwaka 2014, vyama vya upinzani vilipata wenyeviti wengi wa vijiji na mitaa, hivyo kutokuwepo kwa wajumbe hao vinaweza kufanya vizuri zaidi.

UKWELI ULIVYO

Inawezekana ikawa ni chini ya asilimia tano tu ya wajumbe wote wa NEC wanaowakilisha wilaya zao walioshiriki kwa njia moja ama nyingine, kuwafanyia kampeni wagombea uenyekiti ama ujumbe wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2014.

Badala yake, kazi hiyo ilifanywa zaidi na wanachama na viongozi wa maeneo husika kwa kusimamiwa, kuongozwa na kushirikiana kwa karibu na viongozi na watendaji wa CCM na jumuiya zake wa matawi, kata, majimbo, wilaya pamoja na mikoa.

Lakini pia, kama wapinzani walifanya vizuri wakati CCM ina wajumbe hao wa NEC wa wilaya, kwa nini waendelee kuwepo mwaka 2019 badala ya kuachana nao ili iwazuie wapinzani kufanya vizuri kama ilivyokuwa kwao mwaka 2014?

(6) Kwamba idadi kubwa ya Wajumbe wa NEC walionyesha kutounga mkono pendekezo la kuondoa nafasi za wale wanaowakilisha wilaya.

UKWELI ULIVYO

Mjadala miongoni mwa wana CCM wa kuendelea ama kutoendelea na Wajumbe wa NEC kutoka wilayani, ulianza takribani miaka miwili iliyopita huku wengi wakiwemo hadi wenyewe wakitaka waondolewe.

Chanzo na sababu za kuwepo kwa mjadala huo ni ukweli kuwa tofauti na matarajio ya kuanzishwa kwa nafasi hizo, hali ilikwenda kinyume chake na hivyo kilichokuwa kinasubiriwa na wengi ni kufika kwa wakati muafaka ili hatua zichukuliwe.

Pili, kupitishwa kwa uamuzi huo ndiko kulikoshangiliwa zaidi na wajumbe wote kuliko mambo yote mengine, hatua iliyothibitisha kuwa huenda hata wenyewe walikuwa wameelewa kwa mapana na kuunga mkono jambo hilo kwa dhati ya mioyo yao yote.

Ndiyo maana hata Mwenyekiti Rais Dk. John Pombe Magufuli alipotaka kuahirisha kikao ili wajumbe waende kula, kisha wakirudi ndipo waendelee na agenda hiyo ukumbi mzima ulipiga kelele kuomba waipitishe kwanza kama ilivyo, kisha afunge kabisa kikao ili wakitoka wasirudi tena.

(7) Madai kwamba walengwa wa mabadiliko hayo walikuwa Wajumbe wa NEC kwa madai kuwa ni chanzo cha rushwa hasa nyakati za chaguzi.

UKWELI ULIVYO

Kuondolewa kwa nafasi kadhaa za ujumbe wa NEC hakuna uhusiano wowote ule na madai ya rushwa ila ni mageuzi ya kawaida ndani ya chama.

Ni mageuzi ya kawaida ambayo yamekuwa yakifanyika kwa kuletwa au kuletwa tangu wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne hadi hii ya tano, hivyo hakuna uhusiano wowote na kulengwa mtu yeyote ila ni kutaka kukidhi malengo ya kisiasa kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa duniani kote.

(8) Kwamba eti mwaka jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wa sasa, Edward Lowassa ndiye aliyepata wadhamini wengi zaidi wakati akiwania uteuzi wa kugombea urais kupitia CCM huku wengine akiwemo Dk. John Magufuli wakihangaika.

UKWELI ULIVYO

Kila unapofika uchaguzi mkuu wa ndani ya CCM au wa dola, chama hicho kimekuwa kinatumia Katiba na Kanuni kutafuta na kuteua wagombea wa nafasi zinazoshindaniwa, lakini mwaka jana Lowassa, kutokana na uchu wake wa madaraka uliopitiliza aliamua kutozingatia chochote kati ya hivyo viwili akidhani kuwa ingemsaidia, lakini kumbe alikuwa yeye mwenyewe anajiharibia.

Mathalani, kama alikuwa akichangia mamilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa makanisa na misikiti nchini kote kuanzia mwaka 2011 - 2015, kwa nini aliacha ghafla baada tu ya kuenguliwa katika kinyang'anyiro cha kutafuta mgombea wa urais kupitia CCM?

Anataka kutuambia kuwa ujenzi wa misikiti na makanisa nchini ulikamilikia hapo ama ilikuwa gia ya kutafutia urais?

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Charles Charles
Katibu wa Habari wa Katibu Mkuu wa CCM
.
Halafu mnamkamata Maxcence Melo kwa njama za kutaka kuifungia jamii forum , huu ukweli ulivyo wenu mngeuweka jukwaa lipi kujadiliwa enyi ukoo wa panya?
Halafu inaonyesha hata mkishtushwa kutoka usingizini mtalia kwa hamaki "Lowasaaa" kwa jinsi mnavyo mhofia.
 
mkuu hunaga shuguli za kukuingizia kipato? Sidhani kama ungekuwa nazo kila saa ungeandika mada zaidi ya 5 kwa siku moja!

Tafuta kazi ya kufanya achana na chadema na Lowassa maana watanzania kwa sasa wamesha Elimika.

Mwambie Sizonje Akaze Buti maana 2020 hatu taki Hadithi za kina Bulembo kutafuta kuhurumiwa.
Buku 7 x 30 ni 210,000 kwa mwezi hii pesa inamtosha sana sababu huwa wanawatumainisha kuwapa shavu kwa baadye.
 
HUU MT

HUU MTANDAO UNAENDESHWA BILA LESENI , WOTE MNAJUA HIVYO. BADO TU MNALETA MAELEZO YENU KUPITIA MTANDAO HUU HUU?
 
Hongera thread hatakama hatukubaliani nawe, kikubwa wapo wanaopata muda wa kuisoma humu ni Kama baharini huwezi fahamu unapotupa nyanvu nini utakama, lengo ni samaki lakini huwezi kosa konokono
 
Mpasuko upo na wajumbe wengi wametolewa,na wameapiza kulipa kisasi 2020
 
Kweli nimeamini lowassa tishio.yupo kimya lakini watu ni mchecheto wa khatari
Inawauma sana kuona mtu walie mwibia kura na kumpora ushindi wake yuko kimya wakati wali amini kua jamaa hawezi kupuuzia. .Hivi unajisikiaje kumuona mtu ulie mfanyia mabaya na anakujua lkn anakaa kimya....
 
Elimu bure na kuongezeka kwa bei ya korosho na Pamba ndio maana ya kutiririka pesa kwa wanyonge.

Ila Nyumbu hawatakaa waelewe hili.

Wako bize kupangusa viatu vya Lowasa
 
Inawauma sana kuona mtu walie mwibia kura na kumpora ushindi wake yuko kimya wakati wali amini kua jamaa hawezi kupuuzia. .Hivi unajisikiaje kumuona mtu ulie mfanyia mabaya na anakujua lkn anakaa kimya....
Nimeamini lowassa ana moyo wa kiume sidhani kwa ambayo yamefanyika dhidi yake bwana Faru John kama angeweza kuvumilia hata kwa wiki moja tu.
 
Back
Top Bottom