kwamtoro
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 4,922
- 3,234
Nikiwa mwanachama wa CCM na mfuatiliaji duru la kisiasa kwa miaka mingi sana. Kwa katibu mkuu wa CCM kutokwenda kuokoa jahazi la CCM Arusha imenistajabisha sana. Imenifanya niwakumbuke makatibu wetu wakuu walio pita kabla yake. Ukizingatia yeye ni mwana wa Arusha na kikubwa zaidi alisha wahi kuwa mbunge wa Arusha mjini. Kwa mantiki hiyo, yeye atakuwa anakubalika sana kuliko kiongozi yeyote wa CCM na makada katika mji wa Arusha