CCM ikishidwa uchaguzi wa udiwani Arusha, katibu mkuu wa CCM atakuwa amechangia kushidwa

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Nikiwa mwanachama wa CCM na mfuatiliaji duru la kisiasa kwa miaka mingi sana. Kwa katibu mkuu wa CCM kutokwenda kuokoa jahazi la CCM Arusha imenistajabisha sana. Imenifanya niwakumbuke makatibu wetu wakuu walio pita kabla yake. Ukizingatia yeye ni mwana wa Arusha na kikubwa zaidi alisha wahi kuwa mbunge wa Arusha mjini. Kwa mantiki hiyo, yeye atakuwa anakubalika sana kuliko kiongozi yeyote wa CCM na makada katika mji wa Arusha
 
Kinana kwa sasa hivi ana msaada wowote katika chama. Mwigulu ndie kisha kuwa katibu mkuu
 
Amedhibitisha kuwa yasemwayo na wengi kuhusu yeye ni ukweli na kuwa Arusha wanamfahamu hivyo anaoga kujitokeza hadharani kwa wanaomfahamu. Yeye mwache akatambe huko Rudewa na Njombe ambako pengine hawajui hata nini kinaendelea.
 
Nikiwa mwanachama wa CCM na mfuatiliaji duru la kisiasa kwa miaka mingi sana. Kwa katibu mkuu wa CCM kutokwenda kuokoa jahazi la CCM Arusha imenistajabisha sana. Imenifanya niwakumbuke makatibu wetu wakuu walio pita kabla yake. Ukizingatia yeye ni mwana wa Arusha na kikubwa zaidi alisha wahi kuwa mbunge wa Arusha mjini. Kwa mantiki hiyo, yeye atakuwa anakubalika sana kuliko kiongozi yeyote wa CCM na makada katika mji wa Arusha

Nina wasiwasi kama kweli wewe ni mwana CCM. Hiyo avatar yako inakusuta vibaya sana.

Tiba
 
Wewe unafikiri hata Kinana angekuja Arusha angefanya nini kinusuru CCM?

Katika hili ninamtetea Kinana.
Kinana ana akili afadhari kidogo kuliko makada wenzake kwa kuwa anajua CCM hapa Arusha ni lazima itashindwa tu, tena itashindwa vibaya sana, hivyo ni kupoteza muda, nguvu na rasilimali za CCM kupambana mahali ambapo watu wanaipenda sana CHADEMA kama mkombozi wao.
 
Nina wasiwasi kama kweli wewe ni mwana CCM. Hiyo avatar yako inakusuta vibaya sana.

Tiba

Ha ha ha Tiba.. Mie mwenyewe nilivyoiona hiyo Avatar na id jina la jamaa ikabidi nicheke tu.. JF hakuishi vituko humu..
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom