Watanzania tuliwaamini kwa kauli mbiu ya nguvu zaidi, kasi zaidi na ari zaidi lakini sasa tunayoshuhudia ni tofauti na mbaya zaidi ni ukiukwaji wa haki, ufisadi na rushwa kushika kasi zaidi lakini pia mauaji ya raia wasio na hatia kufanywa na polisi, haya yametokea Igunga, Arusha, Arumeru, Tarime, Kagera, Iringa, Morogoro, Mbeya na maeneo mengine ya Tanzania lakini vitisho, kejeli na mateso wanayofanyiwa Watanzania wanaodai haki kama ilivyotokea kwa Dr. Ulimboka. CCM imekaa kimya wakati haya yanatokea zaidi wanatumia muda mwingi kuwasakama viongozi wa CHADEMA, lakini je kero hizi zote chanzo ni CHADEMA? Je sisi Watanzania CHADEMA ndio tuliowapa dhamana? CCM msipoliona hili hamtufai 2015.