Wasi wasi wa mleta mada ni wa kweli kabisa, kuna kila dalili kuwa CCM haitakuwa tayari kuondoka Ikulu kwa sanduku la kura.
Mfano mmojawapo mkubwa kabisa ni haya mauaji ya polisi yanayoendelea nchi nzima, kwenye shughuli za CDM, huo ulikuwa mpango mahsusi wa CCM, kutaka kukipakazia Chadema kuwa ni chama cha fujo, ili baadaye vibaraka wa CCM, kina Tendwa wakifute.
Bahati nzuri sana kwa CDM, tukio la picha zilizoonyesha polisi wakimsulubu Mwangosi kule Nyololo, hadi kutoa roho yake, limeiokoa CDM, na mpango huo mchafu, uliokuwa ukiratibiwa kwa karibu na msajili wa vyama.
Ili kuamini kuwa ule ulikuwa mpango mahsusi wa chama tawala, hadi hivi leo, si Kamuhanda wala Mwema, waliokubali kujiuzuru, na bosi wao JK, hajawafukuza kazi ingawa ni dhahiri mauaji yale yalikuwa ya makusudi kabisa.
Kwa maana hiyo, huo ni ushahidi tosha CCM wanajua kabisa, uwezekano wa kushinda uchaguzi wa 2015, ushakuwa finyu sana, sawasawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Sasa nini cha kufanya, ni kuongeza awareness kwa wananchi kuwa CCM, hawatakuwa tayari kuondoka Ikulu kirahisi.
Kwa hiyo kazi kubwa ya kufanyika kuanzia sasa hadi 2015, ni kutoa elimu ya hali ya juu ya kulinda kura hadi wakati wa kutangaza matokeo. Ninaamini hata wao wakishajua mbinu zao zote za kubaki madarakani zinajulikana, wataanza kujiandaa kisaikolojia kuondoka Ikulu.
Na wao hawatakuwa wa kwanza kukabidhi nchi kwa upinzani. Jirani zetu Zambia wamefanya hivyo, hivi karibuni. Ghana, Kenya, Malawi, weshawahi kufanya hivyo. Sioni kwa nini isiwezekane kwa wa-TZ.
La muhimu ni wananchi kujipanga tayari kwa kupokea mabadiliko. MUNGU IBARIKI TANZANIA.