CCM haitaiacha ikulu kwa kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM haitaiacha ikulu kwa kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SAGANKA, Sep 18, 2012.

 1. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni imani yangu kuwa CDM watashinda kwa ushindi wa kawaida katika uchaguzi mkuu ujao. Ushindi huu wa kawaida si dalili njema kwa CDM, na hasa ukizingatia CCM wanavyohaha huku na huku kutafuta namna ya kuokoa jahazi, hata wamediriki kutoa uhai wa watu.

  Watazoea, na hata ikifika 2015 kuendelea kutoa uhai kwao si issue. Hayo ni mazingira magumu sana kwa
  CDM kusubiri kukabidhiwa dola kikatiba. Kenya wameishi kwa kuibiana kura kwa muda mrefu sana,wakati matokeo yanaonyesha kuwa Kibaki ameshindwa, kitu ambacho hakukitarajia sana,aliamua kuiba kura ambazo tayari zimekwisha hesabiwa.

  Kitendo hicho kilimfanya Moi kutamka maneno yafuatayo " Huyu mutu ya ajabu sana, wengine naiba mahindi yakiwa kwa shamba,yeye naiba ikiwa kwa stoo" .Unaweza kuona uzoefu wa nchi za kiafrika katika kusigina haki ya wanachi ya kuchagua.

  Nataka kusema nini!

  Washauri wa CCM ni hao hao (kenya,zimbabwe nk). Walau kwa watu wa kenya wameamka kiasi na wanaweza kuyakataa matokeo kama yamekwenda ndivyo sivyo, kwa watz bado sana.Tutaikataa ccm kwa kupiga kura tu,lakini isipokubali kuondoka hatuna plan B.

  Tutajikuta tunakuwa wanyonge na kuendelea kuumia kwa miaka mingine mitano. Siku za mwizi ni arobaini,lakini siku ya arobaini akiiba kwa mtu muoga huenda tukaendelea kuhesabu ya 41. Ni wakati sasa CDM kutueleza imejipanga vipi kuhakisha matokeo halisi yanatangazwa 2015.

  Naelewa kuwa kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha haki inatendeka, lakini viongoza wana nafasi nzuri zaidi kuliko sisi wanachama wa kawaida,lakini hata hivyo miongoni mwa majukumu ya kiongozi ni kuonyesha njia.
   
 2. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu umefanya Uchambuzi Mzuri sana, kwa kuongezea machache ni kwamba;Ikumbukwe kuwa kuna walioapa kuilinda Serikali ya CCM kufa na kupona,Hawa wana uhakika wa kwenda Lunch Marekani na Dinner wakaenda Swiss kabla ya Kwenda London Kulala.. Hawa wana watoto wao wanaosoma huko huko ambao hawakuwahi kusikia njaa tangu kuzaliwa kwao.. Ama hao watoto wana watoto wao ambao wanataka nao wakija kuwa na watoto wao wawe kama wao. Watu hawa Kuwanyang'anya Ikulu si kazi ndogo.. Ni kazi ya KUFA NA KUPONA: Sasa kama ambavyo wao waliapa kuilinda Serikali ya CCm isiondoke madarakani KUFA NA KUPONA basi CHADEMA nayo inahitaji watu WALIO TAYARI KUFA NA KUPONA ili haki itendeke.

  Sina mpango wa kuwajibia viongozi wangu lakini kwa hali inavyoonekana na umakini wao wanaendelea na maandalizi ya kuweka na ama wameshaweka plan B. Hata hivyo what i believe ni kwamba si sahihi sana kuweka Silaha zako za kivita machoni pa adui yako kwa sababu atang'amua na kutengeneza silaha kali kukushinda wewe.

  Thanks very much!
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Nyie nao naona mmeanzisha thread ya kujifurahisha,peleka hii kwenye jukwaa la jokes.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tayari Jumuia ya Kimataifa wanazo taarifa za ndani zaidi juu ya mpango wa CCM kung'ang'ania madaraka au hata kujichagulia 'kukasimu' uongozi kwa JWTZ nje kabisa ya maelekezo ya katiba.

  Wewe ngoja tu utaona kitu gani watakachofanyiwa wakati huo na hawa wadau wa demokrasia kote duniani endapo
  CCM watarogwa kufuata hizo ndoto zao za maangamizi.
   
 5. M

  MTZmakini Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri chama cha mapinduzi kitaondolewa kwa mapinduzi; hili linakuja
   
 6. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Pindi watanzania watapo fahamu wanacho kihitaji ndipo watakapo fahamu adui yao ni nani? Nachukizwa sana pale naposikia wanasiasa hata hao wa CHADEMA wanapo ipa jina serikali iliyopo madarakani na Kuivimbisha kichwa kwa kuiita SERIKALI YA CCM.
  Jina hilo lina wafanya wabweteke na kudhani bila wao Tanzania haiwezekani
   
 7. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimekupata vema Deus, kuna siku niliomba wapenda haki tukutane,ulikuwa miongoni mwa waliochangia ile mada.Ilichangiwa na watu 150,waliotumia vichwa na vifua kuchangia hawakuzidi watano, wengine wengi walitumia viuno,kutumia kichwa, kifua na kiuno ni jambo la kifalsafa,nadhani unanielewa.Wengi watashabikia cdm hadi siku ya uchaguzi,baada ya matokeo ya dhuluma wanafanya nini.Watz wengi wamebaki kulalamika tu bila kuchukua hatua,ccm ya sasa sio ya kulalamikia tu, inahitaji vifua vikiongozwa na vichwa.Deus mimi na wewe tunaelewa kuwa haki haiombwi bali inadaiwa na kupiganiwa,katika haya mawili ya mwisho ni watz wangapi wanaweza kufanya hivyo. Katika vurugu za uchaguzi kenya uliweza kuona hata wanawake wanapigania haki,hapa kwetu ccm kwa vitisho tu vya kawaida wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwazuia akina mama kuhudhuria mikutano ya cdm,hawa watadai haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa?
   
 8. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Majebere watu wanajifurahisha na wake zao na si kwa hoja.Ukinielewa nitashukuru.
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hao pia ni binadamu kama ss wanaweza pewa donge nono wakatuacha kwenye mataa...

  Mimi nilishajipa jukumu hili ila tu under condition CDM hawataruhusu fisadi kugombea hiki kiti..Basi ikiwa hivyo CCM wafanye watakalo watambike matambiko yote na kunyanyua silaha zao zote wanazojua hawawezi badilisha matokeo maana nature yote imeelekezwa kutii amri yangu hii halali na hao wa mataifa ni sehemu ya nature.
   
 10. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Hivi kama wakibaki ikulu na wabunge hawana sisawa na bunduki bila risasi??
   
 11. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...wewe anzisha yako ya kujichukiza...
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naweza kusoma kitu fulani katika Uongozi wa Kitaifa Chadema ukiongozwa na kamanda Mbowe. Mambo kadhaa ambayo yamenifikirisha kwa busara yao na umakini wao ni kama ifuatavyo:
  1. Kashfa ya utoroshwaji pesa na kuzificha Uswiss hawaligusii, limeachwa kiporo kwa wakati wake ukiwadia kulipua.
  2. Viongozi ndumila kuwili chamani wanafukuzwa mapema ili wasijeambukiza uozo kwa wengine
  3. Mabomu yaliyoandaliwa na CCM kuilipukia Chadema kama Shibuda na wenzake wanayachukua kwa tahadhari kubwa kwa manufaa ya chama.
  4. Jitihada kubwa ni kukijenga chama kuanzia matawini huko vijijini ambako CCM hujivunia, ndo maana tunaona CCM wanahaha kuvuruga uanzishwaji wa matawi Chadema vijijini kwani ngome ya CCM sasa inasambaratika.
  5. Kutambulika kimataifa, haya matawi ya huko ng'ambo ni njia tu ya kufikisha ujumbe kwa mataifa, majuzi tumeshuhudia Katibu Mkuu Chadema kuhudhuria mkutano wa kimataifa huko Ujerumani, maana yake sauti ya Chadema yaanza sikika kimataifa.
  6. Mauaji yanayofanya na serikali ya CCM yamesaidia kuitangaza zaidi Chadema Kimataifa, na hivyo ni dalili tosha ya kuanza kujulikana jitihada za Chadema kunusuru uchumi wa taifa letu na huduma bora kwa watanzania.
  7. Kashfa ya kuficha pesa Uswiss kwa viongozi waandamizi na wastaafu wa serikali ni ishara tosha ya uovu wa viongozi tulio nao tosha kwa jumuiya ya kimataifa badala ya kuelekeza nguvu kujenga nchi wao wanaliibia taifa pesa na kuzificha nje ya nchi.
  8. Mbinu chafu katika Uchaguzi mkuu uliopita ulivyoshuhudiwa na jumuiya ya mataifa kutamka wazi kuwa vyombo vya dola vimeisaidia CCM kushinda unazidikupata nguvu kutokana na Serikali kuendeleza ubabe kwa wapinzani kutumia vyombo vya dola.
  9. Matumizi ya dola dhidi ya raia wasio na hatia na mauaji yanayoendelea nchini yanazidi kuwaamsha wapiga kura udhalimu unaofanywa na serikali inayoongozwa na CCM.
  10. Historia inajieleza wazi jumuiya ya kimataifa inavyosaidia kudhoofisha tawala dhalimu kwa njia mbalimbali.
   
 13. gwakipanga

  gwakipanga JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 472
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Swala la msingi ila nashangaa watu wengine wanaona kama joke. Hili swala la ccm kugoma kutoka ikulu tulitegemee kutokea, maana kuna watu wanaona kwamba wao wamezaliwa kwa ajili ya kutawala aswa viongozi wa kiafrika. Nahii utaona jinsi gani serikali inavyo tumia nguvu kubwa na pesa nyingi kwenye chaguzi ndogo. Hiyo inatokana na hofu ya watawala kwa vile wanajua kwamba chini ya utawala wao hawakutenda haki, hiyo wanaogopa mkono wa chuma kuwashukia.
  Lakini kubaki ikulu kwa ccm itategemea nguvu ya umma imeamasika kiasi gani. Umma ndiyo utaoamua kama sasa basi, ccm tupeni ikulu yetu. Na kwa vile ccm watata kuficha maovu yao ili wasikutane na mkono wa chuma hawata kubali kuachia ikulu kiraisi. Ila isipo tumika busara ya wanachama wachache walio ndani ya ccm, basi tunaweza kushudia umwagikaji wa kutisha ktk ardhi Tanganyika. Ila tuomembe Mungu hayo yasitokee, hekima na busara zitumike kwa wale wanayoitakia mema Tanganyika. Viongozi wa ccm kumbukeni kwamba Tanganyika ni ya kwetu sote hata sisi watoto wa makabwela ambao tunaishi uwamishoni kwa kumkimbia mkoloni mweusi aliye mbaya zaidi karl peters.
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Kabisa KakaKiiza! Watakuwa na mfano ya kitu!
  Yani wanaccm watacheka pasipo majibu!
   
 15. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  CCM wapo radhi kuua raia wote, kuliko kuiachia Ikulu. Ikulu ikichukuliwa na CDM, viongozi wengi wa ccm watafia jela
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Bahati mbaya watanzania si waarabu. Mbowe alisema juzi kuwa watanzania ni wapole kupitiliza, na hawana munkari wa kimapinduzi na ndio maana hata CCM wakifanya mizengwe wanajua tu vumbi litapoa na maisha yatasonga.

  CDM wafanye lipi la ziada zaidi ya kujaribu kuamsha watanzania waliolala bila mafanikio? Wasilaumiwe CDM maana watanzania ndio wanaopiga kura na kwa kudra CDM ikaongoza, na kwa makusudi CCM ikaiba, na kwa woga na upumbavu watanzania wakakaa kimya wakilalamikia tumboni. Mwenye jukumu la mwisho ni mwananchi.
   
 17. I

  Iramba Junior Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa naamini maneno ya kiongozi wa CDM Mh. Mbowe ambayoamekuwa akiyasema mara kwa mara sehemu tofauti ya kwamba Taifa la Tanzanialimejaa watu ambao ni “Timidly”. Uoga huu wote wa nn? Mbona mbona unasemaUMESHAFUNGWA kabala hata mechi aijaanza! Tuamke jamani, kama kweli watu ambaomna uwelewa wa kutosha mnakuwa na mtazamo kama huu, hakika ukombozi wetu nikazi kubwa!

  Jamani njia pekee ya kushinda ni confidence na siyo kuanza kuweka elements of failures! Kwa taarifa yako ni kwamba ukisikiliza kauli za Pinda aliyoitoa Mwanza pale alipozomewa alopomwambia Wenje kwamba hawa ndiyo wananchama wenu mtakaposhika dola, Mh Sitta CDM ina safu nyembamba kuongoza nchi, n.k. hizi ni ishara tosha kwamba wako prepared pyschologically kushindwa!
  Tuamke!

   
 18. Mcheza Karate

  Mcheza Karate JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 691
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  Nani aachie ikulu? Nyie mna wivu nini? Au mna majungu yenu? Tutawaua wote lakini si kuachia ikulu

  mnanionea wivu ninavyopiga misele ya ULAYA?, au mnaona wivu mwanangu RIZ 10alivyonunua magari(zile semi treler).?

  Mnataka wajomba zangu wasipate maisha mazuri eeh? Hamjui mi nina utitiri wa watoto? Wakale wapi?

  Acheni majungu bana alaaaaaaa!!!!
   
 19. miftaah

  miftaah Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani hao CCM wamebashiriwa Ikulu na Mwenyezi Mungu hadi kiama?.....wataondoka tu hata kwa kufanya mapinduzi itabibi yafanyike mna kaondoka Firauni ijekua wao hata uasi wa Firauni hawajaufikia...wataondoka kivyovyote.
   
 20. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ukifikiria ujumbe ulioletwa hapa na hali halisi nina uhakika unashikwa na tumbo la kuharisha. Anza kutafuta kazi nyingine ya kufanya kuanzia 2015, serikali ijayo haitahitaji walamba viatu ili wapate mkate wao.
   
Loading...