Ni imani yangu kuwa CDM watashinda kwa ushindi wa kawaida katika uchaguzi mkuu ujao. Ushindi huu wa kawaida si dalili njema kwa CDM, na hasa ukizingatia CCM wanavyohaha huku na huku kutafuta namna ya kuokoa jahazi, hata wamediriki kutoa uhai wa watu.
Watazoea, na hata ikifika 2015 kuendelea kutoa uhai kwao si issue. Hayo ni mazingira magumu sana kwa CDM kusubiri kukabidhiwa dola kikatiba. Kenya wameishi kwa kuibiana kura kwa muda mrefu sana,wakati matokeo yanaonyesha kuwa Kibaki ameshindwa, kitu ambacho hakukitarajia sana,aliamua kuiba kura ambazo tayari zimekwisha hesabiwa.
Kitendo hicho kilimfanya Moi kutamka maneno yafuatayo " Huyu mutu ya ajabu sana, wengine naiba mahindi yakiwa kwa shamba,yeye naiba ikiwa kwa stoo" .Unaweza kuona uzoefu wa nchi za kiafrika katika kusigina haki ya wanachi ya kuchagua.
Nataka kusema nini!
Washauri wa CCM ni hao hao (kenya,zimbabwe nk). Walau kwa watu wa kenya wameamka kiasi na wanaweza kuyakataa matokeo kama yamekwenda ndivyo sivyo, kwa watz bado sana.Tutaikataa ccm kwa kupiga kura tu,lakini isipokubali kuondoka hatuna plan B.
Tutajikuta tunakuwa wanyonge na kuendelea kuumia kwa miaka mingine mitano. Siku za mwizi ni arobaini,lakini siku ya arobaini akiiba kwa mtu muoga huenda tukaendelea kuhesabu ya 41. Ni wakati sasa CDM kutueleza imejipanga vipi kuhakisha matokeo halisi yanatangazwa 2015.
Naelewa kuwa kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha haki inatendeka, lakini viongoza wana nafasi nzuri zaidi kuliko sisi wanachama wa kawaida,lakini hata hivyo miongoni mwa majukumu ya kiongozi ni kuonyesha njia.