CCM haijamtoka Lowassa akilini

CCM haijamtoka Lowassa akilini

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
Tabora/Manyoni/Dar. Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa jana alizua sintofahamu baada ya kusema; "CCM oyee", kauli iliyowafanya wananchi hao kukaa kimya na walipoona akicheka waliitikia "oyeee" huku nao wakicheka na kumshangilia.

Ingawa ilitokana na ulimi kuteleza, yeye mwenyewe alisema alitamka neno CCM kama utani ili kubaini ni wananchi wangapi wanaokishabikia chama hicho kati ya waliojitokeza uwanjani hapo kumsikiliza wakati tayari amekwishaeleza jinsi chama hicho tawala kilivyoshindwa kuliletea taifa maendeleo.

Msindai kama Lowassa

Wakati Lowassa akieleza kwamba alisema hayo kwa utani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai aliyekihama chama hicho na kujiunga na Chadema, alitoa mpya baada ya kukiombea kura chama chake hicho cha zamani badala ya Ukawa kwenye mkutano wa hadhara.

Msindai alitoa mpya hiyo juzi jioni wakati akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Manyoni Magharibi na Mashariki uliofanyika Manyoni mjini kwa tiketi ya Ukawa.

Baada ya kuwanadi wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani wa majimbo hayo, Msindai ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM Tanzania, aliwaomba wakazi wa Manyoni akisema:

"Mpeni kura Lowassa ni mchapakazi na mwadilifu, anauchukia umaskini ataikomboa nchi yetu na kura zote za Rais, wabunge na madiwani wapeni wagombea wa Chama cha Mapinduzi."

Baada ya tamko hilo, uwanja ulilipuka kwa kelele na minong'ono ndipo kiongozi mmoja aliponyanyuka na kwenda alipokuwa Msindai ameketi na ni kama alimwambia: "Hapa ni Ukawa si CCM."

Alipopata maelekezo hayo, Msindai alisimama na kusema: "Ninaomba radhi, unajua koo limekauka, hebu kwanza naomba mnipe maji nipooze koo."

Alipoletewa maji na kuyanywa, aliendelea kuomba radhi na kusema: "Ndugu zangu, ulimi uliteleza... si mnajua tumetoka huko hivi karibuni Uccm haujatutoka sawasawa," alisema na kuamsha kicheko kwa mashabiki waliokuwa wakimsikiliza.

Akizungumza kwa simu jana, Msindai alikiri kuombea kura wagombea wa CCM kwenye mkutano wa Ukawa lakini alisema kuwa ulimi uliteleza na kwamba aliomba radhi na watu walimwelewa.

Hata hivyo, Msindai alikazia kusema kuwa Watanzania wanataka mabadiliko kwani hata mgombea wa CCM, Dk John Magufuli katika hotuba zake amekuwa akisema anataka kuona Tanzania ikibadilika.

"Watanzania watabadilika ikiwa Dk Magufuli atatimua watu wote kwenye mfumo wa utawala na kuleta mabadiliko ya kweli, lakini kama watu watabakia walewale, watamwangusha," alisema Msindai.

Alipoulizwa utayari wa Watanzania kubadilika, Msindai alisema Ukawa ndiyo watakaoleta mabadiliko ya kweli kwa kuwa watawaondosha watu wote na kuleta watu wapya kwa ajili ya kufanya kazi," alisema.

Alisema CCM ya sasa siyo ile ya (Julius) Nyerere na imebadilika na haitumikii tena wananchi na kwamba, Dk Magufuli ni mwenye hasira hivyo anakosa sifa.

Mmoja wa makada wa Chadema Mkoa wa Singida, Paschal Mlaki alieleza kushangazwa na kuteleza kwa Msindai akisema ana wasiwasi na waliokuja kwenye chama hicho. "Mimi ni kada wa Chadema hapa Singida, hakuna asiyenijua, ukweli hili limetukwaza wengi... hivi inaingia akilini kweli uko mkutano wa Ukawa ukatangaza CCM?

"Watu wanatumia gharama zao kufanya maandalizi, wanataka kupata vitu vya Ukawa halafu anakuja kututangazia haya!"

Chanzo: Mwananchi
 
Lowassa Asema CCM Oyee Viwanja vya Sabasaba



UKAWA%2B4.PNG



11988751_10156014242005158_6772900682278766512_n.jpg

mmmmh stellah massawe so cute :rockon:
 
Kumbuka kwamba asilimia 50 ya kura zake zitatoka kwa wanaCCM. Hiyo sio kwamba alikosea - huyu bwana ni master politician.
 
Mzee alikuwa anapima upepo!hajaamini kama nyomi yote ile ni ya ukawa!
 
Mzee anakumba ndugu zake walio mkuza wa CCM

Hawezi maana hao ndugu ZAKE WA ZAMANI wanakumbatia sana UFISADI na sasa amekimbia hiyo DHAMBI ya kuwadanganya Watanzania kwa ahadi hewa na kuibiwa.
 
wanaompigia kura wengi wao wanatoka ccm sasa ni lazima awasalimie
 
Hajakosea kitu,
hata wewe unaweza kumkumbuka mtu aliyekuudhi miaka ya zamani
ili ageuke aangalie mafanikio yako.
 
Namimi kuna jamaa yangu kaniambia hili,nadhani sio ajenda kubwa.....hapa ni kusonga mbele na nguvu ya umma mpk ikulu.
 
Alikua anapima kama kuna ccm pale kumbe Hamna.nyomi yote ile ya ukawa
 
Siku hizi ameanza kupoteza kumbukumbu!

Kuna uwezekano alikuwa anadhani anahutubia mkutano wa CCM.

Kazi kweli kweli!

Tena sasa hivi ana afadhali tangu ahamie UKAWA naona anakuwa imara kuliko alivyokuwa ccm. Nadhani ccm walikuwa wanamfanya awe bubu na zezeta kumkosesha jukwaa la kupigia siasa.
 
Back
Top Bottom