CCM: Dharura Kamati Kuu & NEC, Kuna Nini Huko?

Apr 27, 2006
26,588
10,375
- Wakuu JF heshima mbele sana, According to the dataz nilizozinasa sasa hivi, ni kwamba Mwenyekiti wa CCM taifa ameitisha vikao vya dharura, yaani Kamati Kuu ya CCM Tarehe 28/3/10 na kingine cha NEC Tarehe 8/4/10 na kwamba ameamuru vikao vyote vifanyike Dar, Karimjee Hall,

- Kinachotisha hapa according to the dataz ni agenda ya hiyo mikutano miwili muhimu ambazo inasemekana anazo yeye mwenyewe kinyume na kawaida ya kutayarishwa na Katibu Mkuu, ambaye inaelezwa aliachwa solemba na Mkulu, alipojaribu kuitisha Secretariat ili ku-set agenda ya hivi vikao!

- Tayari kuna viongozi wameanza kuingiwa na homa kali kuhusiana na hii dharura, ambayo inaaminika kwamba kuna la mgambo nyuma yake kutokana na lugha ya ukali aliyoitumia Mkulu! Hali ya hewa ikitulia nitamwaga some more dataz sasa hivi noma, aahhggrr JF Where we dare mwanangu!

Respect.

Field Marshall Es = Wazee Wa Sauti Ya Umeme!
 
Hakuna lolote katika hizi mikutano ambazo hazina mwelekeo wowote. CCM ni kundi la watu ambao wameunganishwa na "one common interrest"; Madaraka. Hawana wanachokiamini pamoja, hawana falsafa, hawana mwelekeo! Ni vitofauti vya hapa na pale tu visivyokuwa na impact yoyote katika mustakabali wa taifa hili.

Jambo kubwa hapa ni jinsi ya kugawana madaraka bila kuingiliana, hakuna jipya!
 
- Tayari kuna viongozi wameanza kuingiwa na homa kali kuhusiana na hii dharura, ambayo inaaminika kwamba kuna la mgambo nyuma yake!
Field Marshall Es = Wazee Wa Sauti Ya Umeme!


Hawa jamaa walionakiliwa na Tanzania Daima hapo chini wanahisa kubwa sana October, hawawezi kupuuzwa. Unajua wakiamua Kuchangua mbadala wao na kusema ni fulani na wakawaelekeza waumini wao walekeze ncha za pen zao Oktoba huko chochote kinaweza kutokea, labda ameamua kuchukua ajenda yao ambayo imekuwa ajenda ya tulio wengi kwa muda mrefu.

Tanzania Daima

Makanisa yamjadili Kikwete

na Betty Kangonga

VIONGOZI mbalimbali wa madhehebu ya dini wamefanya kikao cha siri na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa madarakani viongozi wote waliohusika katika kashfa mbalimbali kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kikao hicho kinachofanyika Dar es Salaam, kinawakutanisha viongozi wa dini zaidi ya 160 kutoka sehemu mbalimbali nchini wanaotathmini hali ya siasa na kushuka kwa kiwango cha elimu.

Vyanzo mbalimbali vya habari kutoka ndani ya kikao hicho, vililiambia gazeti hili kuwa kikao hicho cha siku tatu kilifunguliwa na kiongozi mmoja maarufu wa dini. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema viongozi hao walijiridhisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kuwachukulia hatua wanachama wake waliohusishwa na kashfa mbalimbali huku wakiachwa kuendelea na nafasi zao.
 
this is very dangerous tz nchi yangu unakwenda wapi mbona unatutia machungu wenzako??yaani maskini tunabebeshwa magunia ya misumari na kupigwa bakola kweli tutafika!!duh!sijui bwana tumekata tamaa kabisa na maisha haya inasikitisha sana hv kwann mkulu anashindwa kuwachukulia hatua hwa mafisadi!yaani ujambazi,ajali,umaskini vyote vyetu sie wananchi ambao ni kundi kubwa kwann tunawaacha wachache watutawale?wanatugeuza wanavyotaka mbaya zaidi familia zao zipo ulaya na kwa watoto wao waliopo bongo wana kazi za maana na wana pesa!umaskini huu!inauma sana!
 
WanaJF naomba kuuliza swali moja hapa.

Kuna mtu yeyote humu anamchukulia huyu kiongozi "Serious?"

Jaribu kutafakari hizi sentensi mbili halafu utoe uzito wake. Ipi ni serious zaidi ya nyingine.

1 - Mwenyekiti wa CCM aitisha mkutano wa dharura, (March, 2010).

2 - Mwalimu J.K. (RIP and we miss you) aitisha mkutano wa dharura, (30yrs ago or today).
 
Kuna uhusiano wowote na utabiri wa Sheikh Yahya niliousikia leo (Radio Clouds, taarifa ya saa 12 joni)?
-Uchaguzi utaahirishwa
-Karume ataongezewa muda na blah blah nyingine kama kaiwaida ya watabiri

Can these dots be connected?
 
Yale yale JK hana ubavu wa kufoka anajua kuti alilokalia akitikisika kidogo tu linakatika atabakia hivyo hivyo tumzoee
 
Kuna uhusiano wowote na utabiri wa Sheikh Yahya niliousikia leo (Radio Clouds, taarifa ya saa 12 joni)?
-Uchaguzi utaahirishwa
-Karume ataongezewa muda na blah blah nyingine kama kaiwaida ya watabiri

Can these dots be connected?

Inaweza ikawa kweli; unganisha pia na suala la independent candidates.
 
Tujadili mambo yaliyoandikwa katika ''Mwananchi'',''Nipashe'',''Raia Mwema'',''Majira'',''Uhuru'',''Habari Leo'',''The Guardian'',nk.
Hakuna sababu ya kujadili hizi speculation.
 
Tujadili mambo yaliyoandikwa katika ''Mwananchi'',''Nipashe'',''Raia Mwema'',''Majira'',''Uhuru'',''Habari Leo'',''The Guardian'',nk.
Hakuna sababu ya kujadili hizi speculation.
Kwa nini unayaamini sana hayo magazeti huna habari wakati mwingine source za habari zao zinatoka JF na waandishi wao wengi wapo humu.
 
Hhahahah moto umewaka mpaka Octoba safari ni mwendo. Mbona mnasahau kama CCJ walipozindua chama chao Mwenyekiti wa muda alisema machache ambayo lazima yawaguse WA CCM. Mkulu anataka kujua nani anajiengua CCM na nani anabaki aanze kupanga baraza lake la mawaziri na wala nchi mapeeeemmmaa kabla hakujakucha. Hivi Why do people believe in whatever Sheikh Yahya says? Huyu mtu yupo kwenye business asitake kutuendeshea nchi yetu na mazingaombwe yake. Halafu eti vyombo vya habari wanamwita kumuhoji ili iwe vipi hii ni nonsense.
 
Tujadili mambo yaliyoandikwa katika ''Mwananchi'',''Nipashe'',''Raia Mwema'',''Majira'',''Uhuru'',''Habari Leo'',''The Guardian'',nk.
Hakuna sababu ya kujadili hizi speculation.
Ganesh,
Tuletee hizo issues zilizoandikwa kwenye hayo magazeti. JF ni mahali ambapo habari huvunjika kabla ya kunaswa na hayo magazeti.
 
Ganesh,
Tuletee hizo issues zilizoandikwa kwenye hayo magazeti. JF ni mahali ambapo habari huvunjika kabla ya kunaswa na hayo magazeti.

hana jipya,

hivi kwa Tanzania ya sasa kuna mwandishi wa maana aliyebakia kwenye hayo magazeti?, habari zinaanzaga kujadiliwa humu na baada ya muda ndio zinaingia kwenye hayo magazzeti
 
Kuna watoto wakisikia wazazi wanaongea wanaenda kusema kwa majirani kinachozungumzwa, au wazazi wanawaambia nenda kaseme?
 
Hakuna kitu chochote kinachofanyika serikalini ambacho kinaweza kukufanya uichukulie serikali na viongozi wake serious. It is all the rot. Viongozi wote wakuu wanakaa ofisini less than 25% ya muda wa kazi wakati mwingine wote uliobaki wako safarini wakila parallel allowances za kuhudhuria vikao, seminas, kongamanos, warshas, etc..., who is doing the thinking for the country. Uki disect vitu vinavyoendelea serikalini utajua kuwa nchi inaenda kama nguruwe tu!
 
Back
Top Bottom