CCM: Chama Cha Mafisadi?

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Siku nyingi nyuma, nilisema hapa kuwa CCM si Chama Cha Mapinduzi bali ni Chama Cha Mafisadi. Nikaambiwa kwamba nazungumza lugha mbaya na watu kama FMES wakanijia juu sana. Asha nikaonekana mzabinazabina tu. Lakini leo naona hoja ya CCM kuwa Chama Cha Mafisadi imeshika ari, nguvu na kasi mpya. Jamani sasa hiki chama tukiite mahali kote kuwa ni "Chama Cha Mafisadi"; anayebisha atoe hoja

-Mwenyekiti wa CCM yuko kwenye orodha ya mafisadi.
-Katibu Mkuu amekuwa akihongwa na kumkumbatia fisadi Manji
-Mjumbe senior kwenye kamati ya Maadili bwana Chenge amedhihirika ni fisadi.
-Wajumbe wa Kamati Kuu wakina Mkapa, Rostam nk ni mafisadi
-CCM imepata ushindi mwaka 2005 kwa fedha za ufisadi na kuwafanyia ufisadi wananchi kwa kuwahonga mavazi na fedha
-Serikali ya CCM inaendeshwa kwa ufisadi

Asha
 
Hili linajulikana kwa kila mtu sasa kuwa CCM ni chama cha mafisadi, kama wapo watu clean ni wachache kama Dr. Shein lakini kwa CCM kuwaibia wananchi naona ni fasion, kiongozi asipoiba naona wanamuona kama sio kingozi bora maana viongozi wao wengi ni mafisadi wanaosubiri siku zao.
 
AshaNaaam nakubaliana nawe lakini pia nawapa nafasi wale wale walio kujia juu waje hapa waseme kwa uwazi je wanakubali ama wanadhani maneno yako ni mwiba mkali ?
 
The title of this thread is too general. Chama sio viongozi pekee tu bali ni pamoja na wanachama wasio kwenye uongozi, uongozi wa chama ni asilimia ndogo sana ya wanachama. Unaposema CCM ni chama cha mafisadi una maanisha kila mwenye kadi au unaongelea uongozi tu? Naamini humaanishi hivyo,huoni kuna haja ya kubadilisha hiyo heading na kuwataka radhi wana CCM wasiojihusisha na vitendo vya kifisadi?
 
Nafikiri hakuna anayeweza kukubishia hata mwenyekiti wao anaweza kusema hivyo.

Hapa lazima watanzania wabadilike, mara nyingi hakuna maendeleo yanayokuja bila kuchukua risik.

Inabidi kuchukua hatua katika hili kuhakikisha tunaondoa Mzizi huu wa UFISADI nchini dawa inaeleweka ni kuimba nyimbo za "CCM basi basi tumewasutukia hatutaki tena".

Miaka waliopewa na MAVUNO waliyoyapata nafikiri yanatosha. Kila kiongozi na MABILIONI? Wakati watanzania wakifunga mikanda?

Wamepata wapi, viwanda vyao viko wapi? Basi inatosha.
 
The title of this thread is too general. Chama sio viongozi pekee tu bali ni pamoja na wanachama wasio kwenye uongozi, uongozi wa chama ni asilimia ndogo sana ya wanachama. Unaposema CCM ni chama cha mafisadi una maanisha kila mwenye kadi au unaongelea uongozi tu? Naamini humaanishi hivyo,huoni kuna haja ya kubadilisha hiyo heading na kuwataka radhi wana CCM wasiojihusisha na vitendo vya kifisadi?

KKN, kama viongozi wengi wa juu wa chama hicho akiwemo Rais wa awamu ya tatu na pia aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wamehusishwa na ufisadi basi ni chama cha kifisadi. Je, walio bado wanachama wa chama hicho wanaendelea kuwa wanachama kwa kipi hasa kinachowavutia ndani ya chama hicho? Mimi sikioni chochote zaidi ya ufisadi ambao umejaa kila kona ya chama hicho.
 
hii ni kujikosha baada ya kutuhumiwa kuwa unatumika na ccm?

kweli mkuu umekusudia kuomba radhi
 
Brazameni hapo umesema sawa nakubaliana na wewe.. Kuna list ndefu ya vigogo wa CCM wanahujumu uchumi wetu iliyotolewa pale mwembe yanga..Na tunafahamu madudu yao mengi tuuuuu.. jinsi wanavyoiba bila huruma mali za Watanzania.Kwanini basi tusiwaite MAFISADI?? Nasikitika kusema kwamba 2010 Watanzania wengi watakuwa wamesahau waliyotutenda na kuwarudisha tena madarakani kwa "kishindo".
 
Hiyo ndiyo evolution ya CCM. Samahani sina Power Point manake ndingewachorea Evolution nzima kama ifuatavyo:

JKN - Chama Cha Mapinduzi
Jukumu - kumkomboa mwananchi.

Ruksa - Chama Cha Matapeli
Jukumu - Kuwa na ofice katika briefcase kila kona ya jiji.

BM/Pombekali - Chama Cha Mafisadi
Jukumu - Kuiba kodi za wananchi na rasilimali za nchi kwa kiburi na uharamia wa hali ya juu.

JK - Lets wait, he only got 2 yrs. I will judge him after his 1st term.

Stay tuned, we shall find out soon!
 
Not fair to generalize the whole party, maana wako watu wa maana kwenye chama na tutabanana na hawa mafisadi wachache tu,chama chetu kimetekwa na wezi, tunahitaji viongozi wa maana amasivyo,huu ndio mwanzo wa mwisho wa chama chetu tusipopambana na hawa.
 
Hao wengi ambao bado ni wasafi mbona hatuwasikii wakiwashinikiza viongozi wa juu wa CCM ili mafisadi wote wafilisiwe na kufunguliwa mashtaka ili kukisafisha chama chenu? Kulikoni mpaka mmeamua kukaa kimya?
 
Hili linajulikana kwa kila mtu sasa kuwa CCM ni chama cha mafisadi, kama wapo watu clean ni wachache kama Dr. Shein lakini kwa CCM kuwaibia wananchi naona ni fasion, kiongozi asipoiba naona wanamuona kama sio kingozi bora maana viongozi wao wengi ni mafisadi wanaosubiri siku zao.
Jamco,

Hii inajulikana wapi??
tusipende kujumisha mambo,eti kwa kuangilia manji na mtu flani,kwani wao ndio CCCM pekee,CCM yaani Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuwapo mpaka pale tutakapoamua nini kifanyike..

yaani kama ukiw ana mwenyekiti Mhuni na baadhi ya watu wanaomzunguka wakiwa ni walevi sana na wanopenda sana totoz kw muda mrefu,mathalani miaka kama 20 iliyopita na wanaendeleza libeneke hili mpaka sasa,unaweza kukiita vipi cham hicho..

i said first and narudia tena,ahc kukejeli chama cha mapinzuzi,tushindane kwa hoja
 
Nakubaliana nawe kabisa Asha ingawa mimi nadhani inabidi kiitwe Chama Cha Mafisadi na Majambazi (CCM)
 
Cha msingi ili wanachama wasijumuishwe katika uozo wa viongozi wao wa wa chama, ni kuhakikisha kuwa wanao uwezo wa kuwaweka madarakani na kuwatoa madarakani mara moja viongozi wao (wowote) mara wanapokuwa wanataka kuchafua jina la chama chao. Hadi sasa halijafanyika hilo, kwa hiyo wote ni wamoja tu hadi Chama kitakapokuwa na uwezo wa kujitoautisha na wanachama bila kujali ni nani wa la historia yake, wala fedha zake.
Kwa kweli chama ni chama cha mafisadi, i am sad to admit that too!!
Zamani tulisema ni chama cha majambazi,
hivi by the way bado jina la chama ni valid?
Manake huo ukiritimba, kungangania mambo/watu tu kwa nia ya kushikilia historia, si jadi ya mapinduzi, i think its high time wafikirie kubadilisha jina au kubadilisha tabia
 
Jamco,

Hii inajulikana wapi??
tusipende kujumisha mambo,yaani kama ukiw ana mwenyekiti Mhuni na baadhi ya watu wanaomzunguka wakiwa ni walevi sana na wanopenda sana totoz kw muda mrefu,mathalani miaka kama 20 iliyopita na wanaendeleza libeneke hili mpaka sasa,unaweza kukiita vipi cham hicho..

i said first and narudia tena,ahc kukejeli chama cha mapinzuzi,tushindane kwa hoja

Ndugu Gembe hebu tulia kidogo usihamaki. Sikiliza wanachokisema kisha pembua unayoweza kuyafanyia kazi. Yawezekana usemayo yakawa ni kweli academically lakini kihalisia yasiwe hivyo kwa sababu:
Kiongozi fisadi huchaguliwa na wanachama mafisadi.
Asipochaguliwa na mafisadi, hupigiwa debe na mafisadi.

Kwa mfumo wa uchaguzi wa ccm ulivyo, haiepukiki kuchagua viongozi mafisadi kwa sababu ndani ya ccm, ufisadi ulipewa majina kama MWENZETU n.k. Kw hiyo usitegemee vinginevyo.

CCM, kihistoria, nadhani kinaweza kuwa chama tofauti na vyama vingine duniani kwa sababu ya majukumu kilchopewa na watz. ccm ni chama pekee kilichopewa dhima za kuweka misingi ya taifa, kikashindwa. Kimepewa jukumu la kujenga demokrasia kikashindwa hata ndani yake chenyewe. Uchumi kilishindwa hata kabla hakijaanza kwa kuuwa SUKITA.

Ndani ya ccm tukajengewa dhana kuwa ujanja ndio deal. Kila mtu akawa hataki kazi tena,bali hela. Nenda white house au Lumumba uone kinachofanyika. Ni kelele kana kwamba sio ofisi iliyopewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza mustakabali wa taifa.

Ccm wameshindwa kujenga classes based on thoughts bali wamejenga based on ujanjaujanja tu.

Trace cv za viongozi na wafanyakazi wa chama kuanzia ngazi ya matawi, unaweza kuona tatizo liko wapi. Hakuna anayehubiri imani ya chama hata mmoja. Hakuna anayechaguliwa kwa ukulima wala ufanyakazi wake hodari. Ni ujanja kwa kwenda mbele huku KUSHUGHULIKIANA ikiwa ndiyo silaha kuu ya kujenga na kulinda chama.

Nadhani wakati umefika kwa hasa wanachama wasafi unaowatetea kuamua kujipembua wakasimamia na kutetea wanachokiamini ambacho sio kingine zaidi imani ya chama na WAKAJITAMBULIASHA kuwa wanaamini hivyo na wakatetea msimamo wao bila ya uoga kama alivyofanya Nyerere.

Naamini mkifanya hivyo mtarudisha ccm iliyokusudiwa na Nyerere.[/SIZE]
 
Mbona JKN (RIP) alisema sisiemu inanuka rushwa ilhali yeye alikua mwanachama?
Ikithibitika viongozi wakuu ni mafisadi, huwezi kuwatenganisha na chama.
Kumbuka vikao vya chama huendeshwa na viongozi wake.

Natambua ikiongelewa kwa ujumla inawaumiza na wasiohusika (wana sisiemu safi - ambao ni kweli wapo wengi tu). Kundi la wanasisiemu safi lina wajibu wa kusafisha chama chao, ambacho JKN alisema kilikua kinanuka rushwa (sijui leo angesemaje?).
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom