CCM chama bora Afrika

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Sifa Kubwa 10 Kudhihirisha kuwa CCM ni Chama Bora Barani Afrika

1. CCM ni Chama chenye mtandao mpana mpaka ngazi zote za chini nchi nzima. Kiongozi wa chini kabisa katika jamii yetu ni mjumbe wa shina wa CCM. Kabla ya kumwona kiongozi yeyote katika ngazi ya chini, wa kwanza kumwona ni kiongozi wa CCM. Hakika ni mtandao pekee mpana barani Afrika!

2. CCM ni Chama kilichohimili na kustahimili mikikimikiki na misukosuko ya mabadiliko ya kisiasa pasipo kuyumba wala kutetereka. Vyama vingine vikongwe vimesambaratika vibaya. Mathalani UNIP cha Zambia, MCP cha Malawi, KANU na NARC vya Kenya, NDC cha Ghana, Socialist Party (PS) cha Senegal na SLPP cha Sierra Leone, na vinginevyo. Hakika huu ni uimara na umadhubuti wa pekee barani Afrika!

3. CCM ni Chama kilichoonesha uwezo na ukomavu mkubwa katika kusuluhisha migogoro na tofauti ndani ya Chama kwa njia za amani, maelewano, maridhiano na kusameheana kupitia vikao halali vya Chama. Hakika hii ni demokrasia ya pekee na ya kuigwa barani Afrika!

4. CCM ni Chama kilichoweza kubadilishana viongozi kwa mchakato ulio wazi, wenye ustaarabu mkubwa na wa demokrasia ya kweli ndani ya Chama na Serikali, pasipo uhasama wala vurugu zozote tokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere alipong'atuka 1985, na tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanza upya 1992. Hakika hii ni historia pekee na ya kuigwa barani Afrika.

5. CCM ni Chama kilichomudu kuimarisha na kuviwezesha vyama vingine kukomboa nchi zao kusini mwa jangwa la Sahara. Mathalani FRELIMO cha Msumbiji na MPLA cha Angola (1975), ZANU-PF cha Zimbabwe (1980), NRM cha Uganda (1986), SWAPO cha Namibia (1991) na ANC cha Afrika Kusini (1994), na vinginevyo. Hakika huu ni mchango mkubwa na wa kipekee katika historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

6. CCM ni Chama chenye kutetea, kulinda na kuimarisha amani, utengamano na umoja wa kitaifa nchini, na kuleta maelewano baina ya vyama, sambamba na viongozi wake kujihusisha bega kwa bega katika kuyapatanisha makundi yanayohasimiana katika nchi jirani na kwingineko barani Afrika. Hakika huu pia ni mchango wa pekee barani Afrika!

7. CCM ni Chama chenye uzoefu mkubwa wa kuwekeza na kuendesha miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa mali zao. Hii ni pamoja na kulinda na kuhifadhi magari ya thamani kubwa pasipo kujali itikadi za wamiliki. Hakika huu ni uzalendo na utaifa wa pekee na wa kuigwa barani Afrika!

8. CCM ni Chama kilichoweza kutoa viongozi mahiri na waliotukuka katika ngazi ya kitaifa na Kimataifa kwenye nyanja mbalimbali. Mathalani kwa uchache, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Salim Ahmed Salim, Balozi Ali Mchumo, Rais wa Bunge la Afrika Getrude Mongella na wengineo. Hakika hii ni sifa ya pekee na ya kujivunia barani Afrika!

9. CCM ni Chama kinachohamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kila siku pasipo kusubiri nyakati za uchaguzi. Tunawaona viongozi wa CCM wakituhimiza kila siku kufanya kazi kwa bidii. Hakika jambo hili ni nadra sana kuliona kwingineko barani Afrika!

10. CCM ni Chama kilichoonesha dhamira ya kweli kuhusisha na kuutambua mchango wa wanawake katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, ikiwa pamoja na uwepo wa wanawake wa kutosha katika Baraza la Mawaziri na kuwapa vyeo vya juu jeshini. Hakika huu ni mfano pekee na wa kuigwa barani Afrika katika usawa wa kijinsia.

Na: Gwandumi G.A. Mwakatobe (0714 - 511622)
(Mfuatiliaji na Mchambuzi wa Masuala ya Kitaifa na Kimataifa)
 
CCM ni Chama bora Afrika katika yafuatayo:
1. Chukua chako mapema- kila kiongozi anakwapua mali na kujilimbikizia kwa kwenda mbele

2.Chama cha mafisadi
3. Chama kilicho jaa waongo, wanao thubutu kusimamia uovu, kusema uongo alimradi walinde maslahi yao

4. Chama cha wezi, waliodiriki kuchota mamilioni ya pesa ilikupata ushindi wa kishindo!

5. Chama kinacho baka demokrasia, kwa kutumia nguvu za dola kuwatishia watu walio kinyume yao kwa kuwapiga mabomu kusambaratisha mikutano yao, kuwamwagia tindikali!

6. Chama cha kulindana na Umwenzetu hata kama mtu kaiba, kafanya kosa la wazi analindwa kwa nguvu zote ama kuhamishwa toka ponti A kwenda B badala ya kuwajibishwa

7. Chama cha Kimafya.. sipendi kueleza mengi.. rejea Kolimba na nduguze..

8.Chama chenye mipango mibovu isiyo jali wananchi wake, wakati watu umasikini unazidi kushamiri wao wanawazia kutengeneza mamilionea 100 na fukara milioni 38!!!!!

9. Chama cha kisanii, kila kitu kwao ni funika kombe mwanaharamu apite, kelele zikidi, ni kuunda tume juu ya tume, na tume ya tume ya tume hadi jua lizame hakuna ufanisi utokanao na tume yoyote ile zaidi ya kutapanya mali zetu!

10. Chama kilicho kosa muelekeo, kilichotingwa na mawazo mgando na hakika kina elekea kuliangamiza Taifa, kwa kuwekeza hela nyingi katika Siasa na propoganda badala ya kuwekeza katika elimu na uzalishaji!

11 Naam chama cha wasanii.. ahadi lukuki utekelezaji sifuri!

12....
13.....
14...

Endelezeni wakuu.. hakika CCM ina sifa zote!
 
Duh! ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira...kweli kuna watu wamepumbazika hata uwezo wa kuchanganua mambo hawana!
 
Mtu mmoja anayependa kujitangaza na kutetea ujinga bila kujua kuwa wanae watakuja kuwa wafanyakazi wa watoto wetu. Thinks very low... not smart enough to see how things should be, but rather seeing them as they are, and thinking that is how they should be.!
 
FD,
Bora umesema ukweli,naona toka upate ajira katika serikali yetu unakuwa online muda mrefu..hakuna jipya huko
 
Si kweli kuwa CCM ni chama bora bali ni ni ktk contest ya vyama vilivyoko Afrika ambavyo vimejaa migogolo kama vyama vya Lyatonga,ukabila kama Chadema na udini kama CUF.sasa the best choice among altenatives parties is CCM.Wanachama wa ccm hawatoki nje ya watanzania ndio mana ata mienendo yao inaonyesha haswa tabia za watanzania,
 
Huyu mhurumieni, anatafuta namna ya kufika walipofika wenzake akina Tambwe na Akwilombe ili naye aanze kutembea na Makamba kwenye misafara.
 
Gwandumi Mwakatobe ana historia ndefu ya maisha ya dhuluma na wengi wana hisi ana uonjwa wa akili . Hana haya wala soni katika maisha yake yote .Gwandumi ni opportinist wa nguvu na mtu wa kupenda kuhurumiwa .Once he was kiongozi wa CCM alikuwa anakaa maeneo ya Chuo .Akaamua kutaka afahamika basi akaingia katika hakati akafukuzwa kwenye ile nyunmba ya mwana CCM mwenzake .

Akawa hana pa kuishi na watoto sisi tukamuonea huruma tukamkusanya .Akaenda kujinga na NYF siku zile ikawa inakufa basi akaingia kwenye chombo kimoja cha harakati. Watu wakamwamini sana na kumuonea huruma hata kumsaidia maisha maana walidhani ana akili ya maendeleo .

Akapewa pesa na The Leadership Forum kwenda kuelezea Demokrasia huko mikoani yaani kuwaeleza vijana wawe tayari kujiunga na mageuzi bila ya kujali ni Chama gani wanaishia ila washiriki Siasa . Jamaa akatia pesa ndani na kuanza kukusanya watu ili baadaye aje kuanzisha Chama .

Gwandumi ndiye kwenye kile chama marehemu cha HAMAS.Alipewa usajili wa muda na kwa kuwa akili hamzitosh akaanza matusi basi usajili ukaishia pale pale na akapewa onyo na Tendwa .

Gwandumi kama kajisalimisha CCM ni njaa yake . Sina hakika kama zile pesa Mbowe alizo kula kesha rudisha maana alimfanya Chuma ulete ama ATM hadi baadaye watu walispo sema huyu ni njaa kali .

Yaani mateso yote na chhuki zote kwa CCM leo Gwandumi unasema haya ama umeandikiwa ?
Unakumbuka niliko kuokota na kukusaidia ukilia CCM wanakumaliza kisa ume cross na kuwa na mawazo huru ?

Huyu ana njaa sana ila zaidi ni confused officer mimi namjua kwa maandiko sura na kukaa naye hata jana nilikuwa naye hapa Dar na makaratasi mkononi ila sikujua ndiyo haya alikuwa kaandaa .
 
Huyu mhurumieni, anatafuta namna ya kufika walipofika wenzake akina Tambwe na Akwilombe ili naye aanze kutembea na Makamba kwenye misafara.
KTK Hili kitila Nyamaza bcs historia inakuhukumu,Pia nachokiona yoyote hapa JF ambae hatakua na mawazo -ve ktk kila kitu anaonekana hayawani.

Nilitegemea angejibiwa na wengine kwa kupinga kile au sifa alizo toa na si kujibiwa kwa hoja mpya.
 
Gwandumi Mwakatobe anaweza kuwa ni mjinga wa wajinga, inawezekana kabisa IQ yake ni below 70, kwa sababu baadhi ya mambo anayosema kama ingekuwa kweli basi leo Tanzania ingekuwa mbali sana.

"7. CCM ni Chama chenye uzoefu mkubwa wa kuwekeza na kuendesha miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa mali zao. Hii ni pamoja na kulinda na kuhifadhi magari ya thamani kubwa pasipo kujali itikadi za wamiliki. Hakika huu ni uzalendo na utaifa wa pekee na wa kuigwa barani Afrika"

Hii inaonesha kuwa uwezo wakti wa kutumia akili yake na macho yake ni mdogo sana, ni mdogo kupita kiasi, This is very foolish argument!
 
KTK Hili kitila Nyamaza bcs historia inakuhukumu,Pia nachokiona yoyote hapa JF ambae hatakua na mawazo -ve ktk kila kitu anaonekana hayawani.

Nilitegemea angejibiwa na wengine kwa kupinga kile au sifa alizo toa na si kujibiwa kwa hoja mpya.

Wewe weka hoja hapa; mimi si mtu wa kuogopa historia yangu. Sema usikike, what are you trying to say exactly?
 
Kitila this guy si Mtoto wa Mkulima ni mtoto wa mafisadi ama connections na mafisadi ndiyo kila siku ana mawazo ama ya Gwandumi .Anyway mwache aseme tumsikie kama ana hoja kama hana aache tuichambue hoja ya mchovu mwenzake Gwandumi .
 
kujipendekeza kwa huyu jamaa ni ujinga na ni hatari kubwa sana. Yeye kwa mtazamo wake finyu aliokuwa nao anafikiri CCM itampa ulaji kwa kuandika matapishi yake hapa. Wazazi na ndugu zake kule Mbeya wanakufa tokana na upuuzi wa CCM.

CCM ni chama bora barani Africa kwa kuwanyima wananchi wake demokrasia ya kweli bali kuwapanda woga na uwongo kama hawa akina Mwakatobe. Tanzania hakuna amani kama CCM inavyosema bali Tanzania kuna WOGA, watu wanaogopa kudai haki zai kisheria kwa kuhofia kwamba CCM watatumia vyombo vya dola kama polisi, usalama wa taifa nk kuwapiga na kuwafunga.

Kwa msingi huo viongozi wa CCM na watoto wao wanaweza kufanya upuzi wanavyotaka huku wakijua kwamba Watanzania ni waoga.

Mwakatobe nadhani inabidi uwe mkweli na wala usiwe mwoga na manafiki. Kangi ulinkonyofu fijo gwe setani ugwe. Angukukoma une.
 
....kwa kweli na hasara na njaa zote wanazotutia bado kuna watu wanasifia hawa mafisadi,kazi ipo kweli kweli!
 
Kidumu chama cha mapinduzi!! Mapinduzi kwa namna ya kuibia taifa rasilimali, rushwa, dhuluma, uuaji, ukiritimba, ujambazi, ujangili...niendelee jamani?

Huyu Gwandumi ni wa kuombewa...kweli CCM ni chama bora huku ikiwa na track record kama hii:

-uuaji wa viongozi wa kweli na haki (Sokoine, Kolimba, Mwaikambo)

-uwekezaji usio na msingi kwa kutumia mali ya Umma (Sukita)

-rushwa (kuanzia wakati wa Kiula, Mramba etc)

-Ujangili (wanyamapori skendo za kina Ndolanga na aliyemfuatia, Severre)

-Ufuska (BWM,JK,Majogo,etc)

-Ujambazi (IGPs Mahundi, Mahita)

Yaani listi ni ndefu tena iliyoanzia zama za Mwalimu. Yaani hata ukandamizaji wa upinzani na ufisadi naona uvivu kuviongelea. A piece of advise to my dear Mwakatobe: Just shut the hell up!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom