CCM Arusha kwatifuka: Mary Chatanda akataliwa; yeye asema "sing'oki"

Hiyo ni CCM bana wanatekeleza sera za chama kwa vitendo.


Tangu uchaguzi uishe hawa wanagombana na walianza vita ya maneno sasa ni ngumi. Inawezekana kweli ndo wamenza kutekeleza sera kwa vitendo tena live
 
Vita ya panzi furaha ya kunguru. kwa hiyo wasiamuliwe hawa acha wasambaratike kabisa na kila mmoja akimbilie njia yake ili wanachama walioachwa bila mchungaji waje CDM wenyewe kwenye chama cha wastaarabu
 
my God i wish niipate video hii itakuwa poa sana ila kama kweli huyu mama adabu ipo pembeni kidogo kama kaolewa lazima mme awe bondia loh?
 
nahisi kuna mengi zaidi ya haya yanayoibuka huku ugambani,tuwe wavumilivu tu...

Uko sahihi, maana jipu ndo linaanza tu kutoa dalili ya kupasuka, hatujui usaha uliochanganyika na damudamu hutoa harufu mbaya zaidi ya dalili za mwanzoni
 
Hii sasa kali kwani dalili hizi ni mbaya kwa CCM inayojitahidi kujisafisha kwa maji taka hali inayodhihirisha kwamba gamba jipya linaanza kukomaa bila wao kujua. Sasa sijui likimomaa watajivua tena au watabadili ngozi isiwe ya magamba tena. Huu urais utawatoa watu roho. Ila ukweli TUUSEME JAMANI BERNALD MEMBE HAUWEZI URAIS LABDA WAMCHAGUE AKINA DADA TU kwani nchi yetu si ya kufanyia majaribio na wasanii. Tuwe makini kuhakikisha ile white house yetu aingii comedian mwingine bali comedian wakaigize kwenye TV na nchi iongozwe na watu serious
 
Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa CCM, wote wanaochochea vurugu watafukuzwa chamani, wamfukuze Membe basi.
 
Hapa JF kuna vituko sana,kama mtoa mada kapotosha au kaandika bila uhakika hiyo ni aibu...

Kama wewe unataka kupotosha pia hiyo ni Aibu.Jamani tujaribu kulinda heshima ya Jukwaa letu ,tuache ushabiki usio na mpango

mkuu kamanda nadhani jf ni jamvi lenye hekima na kisima cha fikra. Mchana nimepita jumuiya nyingine,nkaona ujumbe ila nikakaa kimya kwa kuwa no research no right to speak,ila nkapata ujumbe wa Arusha,wakasema mwanamama chatanda,amtandika mjumbe Millya,pia pitia pale kwa 'WANABIDII' pale google utaona mada kama iyo. Cha muhimu tuwaombee hawa watu maana wamefikia mwisho,wamechanganyikiwa. Dini yangu inasema kuwa ni laana kumtusi mtu aliyepakwa mafuta ya Krisma. Chatanda uliwatusi viongozi wa dini na mwisho wako ni mbaya sana! Pia umeongeza laana ya kumpiga mdogo wako Millya,apo mwanamke kampiga mwanaume ambaye kwa utamaduni wa mwafrika ni kichwa cha familia,shauri yako!
 
Jamani CCM sasa imefika pabaya. Watu wanatunishiana misuri, wanatwangana na kutukanana hakuna wa kuwakemea. Hiki sasa si chama bali genge la watu wasiokuwa na mwelekeo. Bado huko Dar huenda Katibu wa CCM wa mkoa bwana Kilumbi Ng'enda akatwangana na Bwana idd Azzan. Kila mtu ndani ya CCM ana sharubu kama kambale. Hakuna wa kumkemea mwenzake. Kama ni nyumba basi imebaki na watoto tu!! Jamani hiki ni Chama tawala sasa ikiwa mambo yenyewe ndiyo hayo ya kupigana mnapata wapi muda wa kupigania wananchi ili wawe na hali bora? Mnapata wapi muda wa kutekeleza ilani yenu ya mwaka 2010 iliyosheheni ahadi lukuki? Hivi huyu Millya ndiye yule alipigwa na Ole Sendeka na kisha Ole Sendeka akashinda kesi? Huyu Chatanda si ndiye aliyeleta mtafaruku wakati wa uchaguzi wa Meya? Chatanda na Millya wote wazee wa matukio!
Ningefurahi km wangetoana ngeu kabisa, the Good thing nikwamba KAMANDA MILLYA AMESHINDA!
 
Kila habari ya ccm sasa hivi ni km unaangalia movie ktk screen ya 3d, haya ccm mumekula nyama za wananchi wenu sasa mwakulana mwenyewe....ngoja tuone mwisho wake.
 
Back
Top Bottom