CCM Arusha kwatifuka: Mary Chatanda akataliwa; yeye asema "sing'oki" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Arusha kwatifuka: Mary Chatanda akataliwa; yeye asema "sing'oki"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, May 19, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Leo majira ya saa kumi na nusu kumetokea vurugu hapa CCM mkoani Arusha, baada ya vijana kumtoa Mary Shitanda kwenye mkutano wekiimba hatukutaki ondoka zako.

  Baada ya kuona watu wanazidi kumzonga alichukuliwa na kuingizwa ndani na askari kanzu waliofika hapo na kufunga milango. Kuna wandishi wa startv na Ch 10 walibahatika kuingia ndani.

  Sijajua hasa chanzo ni nn?..nimeona twitter JMakamba anapuuza taarifa hizi, kudundwa si lazima fimbo au mawe, maneno makali ni kichapo tosha. vurugu zimetokea, labda kama atapuuza na tbc1

  [​IMG]

  HALI si shwari chama tawala mkoani Arusha mara baada ya gari la Katibu wa CCM hapa, Mary Chatanda kunusurika kuchomwa moto na baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM).Wanachama wa umoja huo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha waliandamana katika Jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Arusha, wakishinikiza Chatanda pamoja na Mjumbe wa Baraza la Vijana mkoani Arusha, Mrisho Gambo "wajivue gamba".

  Hali hiyo ilijitokeza jana katika jengo la makao makuu ya chama hicho wakati Kikao cha Kamati ya Siasa Mkoa kikiendelea ambapo, hali iliyosababisha dereva wa gari la katibu huyo wa CCM kulitoa nje ya jengo hilo na kisha kulikimbiza mahali kusikojulikana.

  Vijana hao walikuwa wameshika mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakipaza sauti zilizokuwa zikimtaka Chatanda kuondoka katika nafasi yake ya uongozi kwa madai kwamba amekuwa akikivuruga CCM mkoani Arusha.

  Wakizungumza na waandishi wa habari, wanachama hao kutoka wilaya za Monduli, Longido, Arusha, Arumeru, Karatu na Ngorongoro walisema pamoja na wao kutoa malalamiko mbalimbali juu ya Chatanda na Gambo, lakini uongozi wa CCM taifa umekuwa ukiwakumbatia viongozi hao na kudai sasa wamechoka.

  Walisema malaliko yao kuwa Chatanda amekuwa akikivuruga chama chao ikiwa ni pamoja na kusababisha kukosa ushindi wa Jimbo la Arusha Mjini lililoenda kwa Chadema huku wakisema kwamba ikiwa atakataa kung'oka watajua cha kufanya.

  "Hatumtaki Chatanda na hatumtaki Mrisho Gambo hawa watu kwanza ni wasaliti, lakini pia wamechangia sisi kushindwa kuchukua jimbo hili kwani walikuwa wanaiunga mkono Chadema tunataka waondoke mara moja hadi kieleweke," ilisikika sauti ya mmoja wa vijana hao.

  Miongoni mwa jumbe ambazo zilikuwa zimeandikwa kwenye mambango hayo ni "Chatanda umehujumu uchaguzi kwa siasa zako za makundi zilizojaa chuki, ubinafsi na ubabe usio na manufaa kwa Chama Cha Mapinduzi", "Chatanda kwa siasa zako za ubabe umetuchonganisha na viongozi wa dini", na nyingine kadha wa kadha.

  Hali hiyo ilisababisha Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, James Ole Millya aliyekuwa kwenye kikao cha kamati ya siasa kutoka nje na kwenda ukumbini kuwatuliza wanachama hao, lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

  Akizungumza na wanachama hao, Milya aliwataka wapunguze jazba na kusema kuwa yeye ni mjumbe ametumwa kusikiliza madai yao hivyo wampatie na kisha taufikisha ujumbe huo.

  "Jamani ninawaomba mtulie sidhani kama mtafanya fujo ninaomba mnipatie ujumbe mnitume niufikishe jamani nami nitaufikisha tulieni jamani," alisema Milya

  Hata hivyo, ushawishi wa Milya haukuzaa matunda na kuamua kurudi kikaoni kwani wanachama hao waliendelea kupaza sauti zao kwa wakidai kuwa wanamtaka katibu huyo aondolewe mkoani Arusha kwa kuwa amekuwa akiingilia uamuzi wa umoja wao na kuendelea kumkubatia Gambo.

  "Mheshimiwa tunakipenda sana chama chetu na tunakuheshimu sana, tunaomba Chatanda aondoke la sivyo tutachoma gari lake, tukikutana nalo tutamondoa kwa nguvu," alisema kwa jazba mmoja wa vijana hao.

  Vijana wavamia kikao cha kamati ya siasa
  Wakati hayo yakiendelea wanachama hao walikosa uvumilivu na kisha kuvamia ofisi ambapo Kikao cha Kamati ya Siasa mkoa kilipokuwa kikifanyika huku wakitishia kubomoa mlango kitendo kilichosababisha viongozi mbalimbali wa CCM mkoani hapa kuhaha kutuliza tafrani hiyo.

  Maafisa usalama wakiwemo askari kanzu walikuwa wametanda katika maeneo ya jengo hilo huku wengine wakionekana wakizungumza na viongozi wa UVCCM kujua chanzo cha vurugu hizo.

  Chatanda ajifungia ukumbini
  Hadi tunakwenda mitamboni, Chatanda alikuwa bado amejifungia ndani ya ukumbi wa mkutano na hakuna taarifa yoyote ya CCM Mkoa aliyotolewa kuhusiana na tukio hilo.

  Tuhuma dhidi ya Chatanda kutoka ndani ya chama chake zimekuja siku chache tangu ashutumiwe kuwa mmoja wa waliosababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa mkoani Arusha baina ya vyama vya CCM na Chadema.

  Mgogoro huo unafuatia Chadema kupinga katibu huyo wa CCM wa Mkoa wa Arusha kushiriki katika vikao vya Baraza la Madiwani na kupiga kura ya kumchagua meya wa Jiji la Arusha, hali Iliyosababisha maandamano makubwa ambayo yalisababisha vifo vya watu watatu.

  Wakati CCM wakidai kuwa Chatanda ni mjumbe halali wa vikao vya baraza hilo, Chadema wamekuwa wakipinga kwa maeleo kwamba mwanamama huyo ni mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga hivyo hana sifa ya kushiriki vikao vya Arusha.

  source: Gazeti la mwananchi

  marychatanda.jpg
  Mary Chatanda​
   
 2. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heee! wao kwa wao? watasema chanzo chadema
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu natamani kufika eneo la tukio.
   
 4. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  safi sana,hiyo ndio madhara ya ile damu iliyomwagika february
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Wenyewe wameanzana tena si alitetewa huyo kuwa ni mjumbe halali wa vikao vya chama cha magamba mkoa wa aArusha sasa imekuwaje tena
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Siku yake imefika!! maboss wake(CCM) wanamgeuka!!!
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,961
  Trophy Points: 280
  Harufu ya damu itawamaliza huwa haipotei bure.
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  MARY CHITANDA si ndie yule aliyechonganisha chadema na ccm?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mnara wa Babeli
   
 10. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ccm mkoa wa Arusha,wamepigana,wakimpinga katibu wao Mary Chitanda,katika ugomvi huo chitanda amejeruhiwa,wapo kwenye hapa ccm mkoa
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Kesho watasema ni vijana wa CDM waliopewa sh 500 kila mmoja ili wakavuruge kikao cha ccm.
   
 12. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Crashwisa, very good, ila tulia tumia simu yako piga picha tukio zitume kwa member yeyote hapa.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kuna mwandishi wa tbc kasema chanzo ni ukumbi..zogo linaenelea na sikia wakisema mleteni huku
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Funny Vijana wa-CCM kumbe wawezi kulala milele naona siku hizi hata Malaria Sugu anatoka Usingizini
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wangekata shingo kabisa huyoo mama ptuuuuuuuuu
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Watasema chadema wamewaingilia kwenye vikao vyao
   
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,864
  Trophy Points: 280
  Leta story mkuu,ilikuwaje?
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,961
  Trophy Points: 280
  Wangemtegua mguu kabisa.
   
 19. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kwa nini hawakumtupa dirishani umma ukamdaka wakagawana vipande na wakamtengeneza vizuri.
   
 20. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  wanapenda sana kupigana,kwanza huyo mary tunasikia anapiga bwanake
   
Loading...