CCM amueni kati ya hawa wawili

CCM amueni kati ya hawa wawili

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,494
Reaction score
57,871
Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania utakubaliana na mimi kuwa nchi hii imekuwa ikikosa viongozi wazuri kwa sababu tu ya rushwa , ushabiki usio na maono na upenzi tu.

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza watangaza nia wa chama cha mapinduzi na nafikiri kama hauendeshwi na siasa za ushabiki,upenzi, wivu,chuki na fedha utakubaliana na mimi kuwa wagombea wenye maono na wanaotakiwa kuwekwa na kupambanishwa na chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi huu ni Prof Muhongo , January Makamba.

Hapa ninaelezea wagombea walioonyesha kuwa na maono mazuri ya Tanzania tuitakayo huko mbeleni na wamejipambanua vizuri kimpakakati kwenye kuyafikia maono yao kwenye HOW. Nasema hivi kwa sababu nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu wa siasa za Marekani na sehemu za ulaya na nilichokuja kugundua kwa wale binadamu wenzetu ni kuwa wanaangalia sana how utakavoenda kutekeleza sera zako na sio tu uzuri wa sera. Na hapa ndo nchi nyingi za kiafrika tumekuwa tunafeli siku zote kwa sababu hatuwapimi wagombea kwa njia na mikakati yao ya kutekeleza sera zao bali uzuri tu wa sera zao na uwezo wao wa kuyazungumzia matatizo ya wananchi.

Najua wapenzi wa watangaza nia wengine mtanisema vibaya ila naomba tu leo niwajadili hawa na kutoa hitimisho mwishoni juu ya nani wa kupewa bendera ya chama chao ili akiwakilishe kwenye uchaguzi mkuu.

Kusema ukweli hawa wagombea wote wameonekana kuwa watu wa facts na reality na sio porojo na maneno matamu tu. Wote kwa pamoja wamejitanabaisha kuwa sio watu wa maneno maneno bali ni issues tu.wote kwa pamoja wamejionyesha kuwa wana maono mazuri na wanatumia vizuri exposure yao katika kuitengeneza Tanzania ijayo.

Wote wanaonekana hawana mda na mtu wala visasi na mtu kitu ambacho ni kikubwa sana kwa chama cha mapinduzi kwa wakati huu na ujao. Ka kifupi kama mtu alisikiliza hotuba ya kingunge wakati lowassa anatangaza nia Arusha na maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na Membe wakati anatangaza nia huko kwao Lindi atakubaliana na mimi. N I ukweli usiopingika kuwa endapo team lowassa watashika nchi kuna watu lazima watakimbia nchi na likewise Membe akishika nchi ni lazima upande wa pili watafute sehemu ya kwenda. Na kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania utagundua ugomvi wa hizi timu mbili ndo zimeupa shida sana utawala wa sasa.

Napenda kumalizia kwa kuonesha wapi ambapo mimi naona Prof Muhongo amemzidi bwana January Makamba. Sehemu pekee ambayo Prof Muhongo amemzidi January Makamba ni kwenye uwezo wa kuongoza, kusimamia mambo kwa weredi wa hali ya juu na utendaji kwa ujumla.

Sisemi hivi ili kumsifia tu Prof Muhongo ila kila mtu anakubali kuwa huyu Prof amekaa kwenye system kwa miaka miwili tu ila alivoisimamia Tanesco hasa kwa miradi ya usambazaji vijijini hadi kufikia asilimia 38 wakati anaondoka huu ni utendaji wa kutukuka na kipekee sana unaomfanya astahili kupewa tuzo ya heshima na raisi. Pili ni alivosimamia sekta ya gesi kwa kipindi hiki kifupi huku akikataa kuwapa watu wababaishaji vitalu na kusimamia upatikanaji wa schoralships kwa watanzania wengi inasemekana zaidi ya 100 kwa ajili tu ya kuifanya nchi ije kuwa na wataalam wa kusimamia hii sekta(hapa napenda kumfananisha na kagame anavofanya Rwanda).

Hizo ndo sifa ambazo Prof Muhongo anaonekana kumzidi January Makamba na January anaitaji kupewa mda kidogo ili aweze kuprove how strong he is kwenye huo upande.

Napenda kusisitiza kuwa watu wa kambi zingine mtanisamehe sana,wengi wagombea wenu wnapata popurarity only kwa kuisemea rushwa tu na kupambana na wala rushwa ila sio kwenye vision ya kuitengeneza Tanzania imara kwenye uchumi na mikakati ya kutekeleza sera zao na kuifikia iyo vision.

Nilisema kwenye post moja humu kuwa CCM iandae timu imara ya kufanya kazi na Prof MUHONGO na kwa kuanzia mwampe Salim Ahmed Salim kuwa makamu wake. Leo napenda kutoa ushauri kwa Prof mwenyewe kuwa Mungu akikubariki uingie magogoni mambo ya nje mpeleke January akajijenge zaidi, na January najua utasoma hii post naomba sana ufanyie kazi ilo eneo nililokuomba ulithibitishe kwa watanzania ili mda ukifika Prof akistep down upewe kijiti uendeleze vision bora kwa taifa la Tanzania.

MUNGU ibariki TANZANIA na WATANZANIA WOTE.

MUNGU wabariki Prof Muhongo na January Makamba.
 
"watanzania tuakapimwe akili"- Mdau wa JF.

Jitu limhusika katika ufisadi miezi michache tuu iliyopita hata mwaka haujaisha lakini leo anapigiwa debe awe rais wa nchi.
 
Muhongo kama ameshindwa kuzuia wizo WA mabilioni ya Escrow yaliyoibiwa na maofisa walio chini ya wizara yake ndiyo anaweza kuongoza nchi.
 
"watanzania tuakapimwe akili"- Mdau wa JF.

Jitu limhusika katika ufisadi miezi michache tuu iliyopita hata mwaka haujaisha lakini leo anapigiwa debe awe rais wa nchi.

Tunatakiwa kuwa makini zaidi, tunapotoa maoni yetu kuhusu Raisi ajaye kwa weledi, umakini, uwezo wake wa kifikra na maono yake ya baadae. Bila jaziba na siasa chafu za kuchafuana bila ushahidi wala fact zozote! Prof. Muhongo anafaa zaidi kwa uwezo wake alioonyesha kwa muda wa miaka miwili na nusu tu, maono yake yatatufikisha Tanzania tunayoitaka.
 
Tatizo tuna viongozi wa ajabu,wanajua kuongea au walioongea points si watendaji,wasiojua kuongea ni mafisadi.
Ukawa ndo jibu
 
Hongera kwa kuandika...

Huyu kweli ni wa kupewa hongera tu kwa kuandika, hivi ana underestimate nguvu ya ukawa eeh, yaani kusimamisha Muhongo au Makamba ni bora hata uchaguzi tusifanyike tu kuokoa hizo fedha, tunamwachia tu Dr.Slaa aende zake Magogoni
 
Prof Muhongo is too educated to vie for presidential post while January is too young to lead us
 
Muhongo kama ameshindwa kuzuia wizo WA mabilioni ya Escrow yaliyoibiwa na maofisa walio chini ya wizara yake ndiyo anaweza kuongoza nchi.
Ameshindwa kuzuia kivipi????
Labda nikueleze tu,waziri na msimamizi wa sera kwenye wizara. Kwenye escrow lile suala lilikuwa nje ya mikono ya waziri ndo mana hujaona hata sehemu moja ikiwemo kwenye ripoti ya CAG wala kwenye list ya watu walioingiziwa fedha na hata kwenye list ya wati walioonekana kukiuka maadili na kuitwa tume ya maadili jina la PROF MUHONGO.
kwenye escrow baada ya hukumu kutoka correspondence zilikuwa baina ya Katibu Mkuu wa wizara KAMA MTENDAJI MKUU wa WIZARA, Mwanasheria Mkuu na BOT.
Sasa katibu mkuu alimuandikia Mwanasheria Mkuu kumuuliza hela zilipwe au vipi mwanasheria Mkuu kama mshauri no 1 wa serikali kwenye mambo ya sheria akasema zilipwe na kama ulifuatilia ilionekana katibu mkuu aliuliza mara nyingi as je hela zilipwe au vipi na mwanasheria mkuu akainsist hela zilipwe, sasa hata kama wewe ungekuwa Prof Muhongo ungefanya nini? Una mamlaka hayo?
 
Tafadhali niambie udhaifu wa hotuba ya mwigulu mchemba
Mwigulu ni mzuri ila aliniangusha kwa kweli. ile haikuwa ni hotuba ya kiongozi anayeelezea vision yake bali anayeelezea how ametoka kwenye umaskini na maisha magumu na how anavocritisize mfumo huu. haikuwa hotuba yenye maono iliyojikita kwenye sera na mikakati ya kutekeleza sera zake.
 
Sasa hivi ni zamu ya Lowasa,hao wengine wasubiri muda wao ukifika tutawafikiria
Naona utakuwa ni wakati wa visasi kukomoana na kuonyeshana sie tumewashinda na tunaendesha nchi. Hakutakuwa na lolote la maana kwa Tanzania tuitakayo huko mbeleni.
 
Lord denning

Binafsi nimependa saana hoja yako lakin tatzo lako umeandika katik mkono mmoja umesahau kwamb kikatib si kwamb kkila rais atatoka CCM na hakunaushahid wa kuonyesh kwamb ccm ndo wtatoa rais mwaka huu. Uchambuz wako naomb ufany kam uchambuz wa uteuzi wa nafasi ya wagombea katik chama na sio katik nafasi ya rais
 
Last edited by a moderator:
Huyu kweli ni wa kupewa hongera tu kwa kuandika, hivi ana underestimate nguvu ya ukawa eeh, yaani kusimamisha Muhongo au Makamba ni bora hata uchaguzi tusifanyike tu kuokoa hizo fedha, tunamwachia tu Dr.Slaa aende zake Magogoni
Ndugu tunashindanisha sera zenye maono na mikakati thabiti ya kutekeleza sera husika and not otherwise. So far sijaona sera na mikakati ya ukawa, sijaona mtangaza nia yeyote wa ukawa akijielezea na kuelezea sera na mikakati yake iliyobase kwenye vision bora???? Kwa nini nijadiri watu ambao sioni kama wamejipanga vizuri???
Huu ndso ulikuwa wakati wa ukawa kuonyesha how democratic, strong na walivo na vision kwa hii nchi kwanza kwa kutuletea watu mbalimbali kwenye vyama vyao ili tuone walivo na resource nyingi na za kutosha ila otherwise ndo ule niliosema ushabiki tu.
 
Ndugu tunashindanisha sera zenye maono na mikakati thabiti ya kutekeleza sera husika and not otherwise. So far sijaona sera na mikakati ya ukawa, sijaona mtangaza nia yeyote wa ukawa akijielezea na kuelezea sera na mikakati yake iliyobase kwenye vision bora???? Kwa nini nijadiri watu ambao sioni kama wamejipanga vizuri???
Huu ndso ulikuwa wakati wa ukawa kuonyesha how democratic, strong na walivo na vision kwa hii nchi kwanza kwa kutuletea watu mbalimbali kwenye vyama vyao ili tuone walivo na resource nyingi na za kutosha ila otherwise ndo ule niliosema ushabiki tu.

Mkuu unajua ilani ya uchaguzi ni nini? je unajua kila chama kina ilani yake ya uchaguzi? je unajua kuwa mgombea anauza ilani ya chama husika? je unajua kwamba alichoongea muhongo na makamba si ilani ya uchaguzi ya ccm ila ni mambo yao binafsi? Wajanja tunachojua walichoongea ni mbwembwe, ilani ya chama haijatoka bado, so walichoongea ni useless for now, subiri time will tell

Halafu Je unajua chama cho chote cha siasa ndoto yake ni kushika dola? yaani uwe na nia ya kushika dola halafu umsimamishe muhongo au makamba? unamwacha Makongoro Nyerere, then you are not serious!!
 
Back
Top Bottom