CCM amebaki Abrahaman Kinana

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Chama cha mapinduzi kimekwisha kabisa.,Sio tena chama cha siasa.

Amebaki katibu mkuu,Abrahaman Kinana pekee anayefanya kazi ya siasa.Hakuna mwingine. Mwenyekiti anatumia kofia ya urais kukisaidia chama.

Naibu katibu mkuu anatafuta credit ya urais kupitia unaibu waziri. Katibu wa itikati hana hoja,hana mvuto.Amebaki kuvizia ziara za katibu mkuu wake Jumuiya ya wazee ilikurupua ikarudi kujifungia.

UVCCM ndio hamna kitu,ni sufuri.Hata viongozi wake hawajulikani,amebaki kiongozi wa chipukizi anayevamia midahalo na kushambulia wahusika.

Hata mikoani hawapo kabisa,wakifanya mkutano bila Kinana watu hawaendi,wanabaki wao na nyimbo zao na watoto wanatumia nafasi hiyo kupata disco vumbi la bure.

Ni hakika CCM sasa hakiendeshwi kama chama cha siasa,kimekwisha. Hakuna mbunge anayeweza kufanya ziara ya mafanikio jimboni mwake,labda Deo Filikunjombe. Hope,not later than next year CCM itaanza kuachia uongozi wa nchi.
 
Mwenyekiti wao amebaki tu kusafiri kila kukicha kuomba kuomba pesa, sijui alisoma wapi kwamba misaada inayotokana na kodi za wananchi wengine kama wa kwake hapa nchini iliweza kuondokana na umaskini. eti mwenyekiti anafurahia mapokezi makubwa huko china, nadhani miaka michache ijayo Tanzania kutakuwa na watoto wenye asili ya kichina wengi sana.
 
Wewe unadhani huyu anafanya kazi za chama? ...anafanya kazi zake kwa mgongo wa chama ila hapo anazuga kupata protection!
 
Kweli jamaa kwisha habari yao, hakuna mbunge ataerudi bungeni, name hii ni sababu ya usaliti.
 
Hahahahahaaaaaaaa! Huku ni kujifariji kweli. Eti CCM kabaki Kinana tu! Mbona sasa huwa mnalialia na akina Makonda, Mwigulu, Nape, Mangula, Kikwete, Sitta nk?
 
Kinana siyo juha kama dr slaa siasa zake anafanya kwa mipango.
Kweli kabisa Mkuu. Dr Slaa kachoka sana. Nadhani ni kutokana na laana ya kupora mke wa Mtu na kuacha kazi ya Mungu. Cheki hapa chini
image.jpg
 
Mwenyekiti wao amebaki tu kusafiri kila kukicha kuomba kuomba pesa, sijui alisoma wapi kwamba misaada inayotokana na kodi za wananchi wengine kama wa kwake hapa nchini iliweza kuondokana na umaskini. eti mwenyekiti anafurahia mapokezi makubwa huko china, nadhani miaka michache ijayo Tanzania kutakuwa na watoto wenye asili ya kichina wengi sana.
View attachment 199555
 
Chama cha mapinduzi kimekwisha kabisa.,Sio tena chama cha siasa.

Amebaki katibu mkuu,Abrahaman Kinana pekee anayefanya kazi ya siasa.Hakuna mwingine. Mwenyekiti anatumia kofia ya urais kukisaidia chama.

Naibu katibu mkuu anatafuta credit ya urais kupitia unaibu waziri. Katibu wa itikati hana hoja,hana mvuto.Amebaki kuvizia ziara za katibu mkuu wake Jumuiya ya wazee ilikurupua ikarudi kujifungia.

UVCCM ndio hamna kitu,ni sufuri.Hata viongozi wake hawajulikani,amebaki kiongozi wa chipukizi anayevamia midahalo na kushambulia wahusika.

Hata mikoani hawapo kabisa,wakifanya mkutano bila Kinana watu hawaendi,wanabaki wao na nyimbo zao na watoto wanatumia nafasi hiyo kupata disco vumbi la bure.

Ni hakika CCM sasa hakiendeshwi kama chama cha siasa,kimekwisha. Hakuna mbunge anayeweza kufanya ziara ya mafanikio jimboni mwake,labda Deo Filikunjombe. Hope,not later than next year CCM itaanza kuachia uongozi wa nchi.

Hii hadithi yako nzuri sana, enhe Hii hadithi yako yakufikirika inatufundisha nini?
 
Back
Top Bottom