CCM aibu hii ya Arusha ibebeni wenyewe Mimi simo

CCM aibu hii ya Arusha ibebeni wenyewe Mimi simo

CCM inabidi ibadilike kwakweli sa hivi ni mda wa kuweka watu wazalendo na ambao bongo zinachemka ila kukumbatia watu wanaofikiria matumbo yao tu kwa zama hizi za teknolojia hizi aibu hazitatuacha kwakweli

Bora useme Wewe Mkuu labda wanaweza kukusikia kwani Mimi nimeimba humu JF ila naambulia tu kuitwa mwana CHADEMA na haya yote au huu udhaifu nimeshawahi kuusema na kuuonya huko nyuma katika threads na posts zangu ila ninapuuzwa na nadharauliwa lakini namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa ' tunu / shani ' hii ya Kipekee kabisa ya kuweza kuyaona yanayokuja mapema sana na kutoa ushauri wangu. Aliyebarikiwa amebarikiwa tu hata kama ' utamdharau ' na ' kumpuuza ' vipi.
 
Wewe ni mnafiki. Polepole ni jiniasi anakuzidi sana kiakili na weledi. CCM ipo pahala pazuri sana kuliko kipindi chochote kwa sasa. Kila mwananchi anaelewa umuhimu wa CCM ya sasa. Yaani huku kitaa ni chereko chereko!
Daaaah mnafrahishagaaa sanaaa
 
Wewe ni mnafiki. Polepole ni jiniasi anakuzidi sana kiakili na weledi. CCM ipo pahala pazuri sana kuliko kipindi chochote kwa sasa. Kila mwananchi anaelewa umuhimu wa CCM ya sasa. Yaani huku kitaa ni chereko chereko!

Ningeshangaa sana na mno kama ' Uzi ' huu usingechangiwa na ' Wapumbavu ' wengi mliojazana hapo Chamani Mnazi Mmoja ambao mnadhani kumdanganya, kumficha na kumpamba Mwenyekiti Taifa mnamsaidia Yeye na Chama wakati ukweli ni kwamba kwa uhalisia uliopo sasa na hili la akina Nassari na Lema kuna uwezekano mkubwa coming to 2020 CCM tukawa na Mlima mrefu wa Kupanda kuliko ule ambao tulikuwa nao mwaka 2015.

Na nilikuwa nawataka na nawasubiria sana ' Wapumbavu ' wa aina yako ili ' niwanyooshe ' vizuri Kihoja na silaha pekee ambayo GENTAMYCINE nimepewa na Mwenyezi Mungu ni ' akili, maarifa na upeo ' peke yake. Bora Mimi ' Mnafiki ' mmoja ninayejipambanua, muwazi na mkweli kuliko nyie ' Wanafiki ' lundo mnaojidanganya hapo Mnazi Mmoja.

Maneno yangu haya ya leo mtayakumbuka mwaka 2020. Yangu macho!
 
Mimi kwa ukweli wa moyo wangu sitofautishi walivhofanya wakina Gambo, Mnyeti, na Yale anayoyafanya malaika mtukufu.
Staili waliyoitumia wakina Mnyeti na Gambo kina tofauti gani na zile rushwa za vyeo zinazotolewa na mtukufu?
Rejea rushwa ya vyeo ambayo kingereza inaitwa patronage corruption ilivyofanya kazi kwa
1; Anna Mghwira
2: Kitila mkumbo
3: lyatonga Mrema
4: Humphrey pole pole
5; Ibrahim Lipumba
Na hao ni kwa uchache. Jamani naomba tofauti kama mnaziona
KAMA ALIVYO BABA NDIVYO WALIVYO WATOTO.
 
Katika watu waliomlaumu rais na jeshi la wananchi ni mm hasa kitendo cha kuchafua hafla ya jeshi kwa kuingiza siasa kwenye ujio wa utata wa hao madiwani toka cdm. Kimsingi udhiafu mkubwa ni wa rais au ndiye nahodha wa hilo ziezi.

Jambo jingine nje ya mada ni hii tabia ta taasisi za umma za uchunguzi kukaa ofisini eti wanangoja wapelekewe ushahidi. Hao akina Nassari na Lema wamehubiri zaidi ya wiki wana ushahidi na wakaomba wamuone rais au takukuru kumwaga ushahidi.

Badala yake kiburi kikatawala kisa ni wapinzani wamesema na eti wapinzani wanachukuliwa wanampinga na kumchafua rais. Hilo limekolezwa na yaliyomkuta Lissu na wapi vidole vinaelekezwa. Kama rais/serikali haitachukua hatua tofauti ya awamu hii na iliyipita kwenye rushwa hazitachekana. Ni wakati sasa kujisafisha kwani ni sifa mbaya kwa rais/serekali na nchi.
 
Huwezi nielewa, ingawa natamani sana unielewe, tuna wajibu wa kumwombea kwa sababu ni rais wetu, maamuzi yake yanatuathiri, Kitendo cha Bashite, Clouds na Treatment ya Nape, kinazihirisha kwamba hayupo tayari kusikiliza ushauri wa mtu, there is nothing you can do, HATAKI, PERIOD.
Maombi yamedunda kwa jamaa
 
Huko nyuma nilipokuwa naandika mambo humu tena ya Kuikosoa CCM lakini nikiwa na maana moja kubwa tu ambayo kwa bahati mbaya sana ' Wapumbavu ' wachache waliojawa na ' Unafiki ' mkubwa na uliotukuka kabisa walikuwa wakinikejeli, kunitusi, kunikashifu huku wakisema kuwa Mimi GENTAMYCINE ni mwana CHADEMA na nakumbuka kila mara niliwahi kuwaambia kuwa ipo siku ' mtanielewa ' na ' mtanikumbuka ' na hatimaye sasa yametimia.

Nilishamwambia hadi Mwenyekiti wetu Taifa kuwa awe makini sana kwani humo humo ndani ya CCM yetu kuna ' Mamluki ' wengi ambao wanamchafua na kumuharibia ili baadae aharibikiwe na waje kumcheka hakunisikia.

Nilishawahi kueleza mapungufu kabisa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye sifichi na sioni aibu kusema kuwa ni mmoja kati ya Watu ninaowajua in and out na kuna siku nilisema humu humu JF kuwa kama kuna Mtu ambaye tokea ' Teuzi ' za CCM za Wagombea Urais 2015 alikuwa hampendi, hamtaki na akimdhihaki sana Mgombe wa Urais Rais wa sasa wa JMT Dkt. Magufuli alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuna siku moja tukiwa nae katika Nyumba jirani na ilipo Hotel ya Kebby's Mwenge alionge a' Kauli ' moja ambayo siku niliposikia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na JPM nilianza kumuonea mno ' huruma ' JPM kwani nilianza kujua nini kitakuja.

Nilishawahi kusema humu humu tena kwamba kuna Wana CCM wenzetu wanadhani kumpamba, kumsifu na kumpa matumaini hewa Mwenyekiti wetu Rais Dkt. Magufuli kutakisaidia Chama chetu lakini pia kutawasaidia Wao kuendelea kula ' bata ' ndani ya Chama wakati ukweli ni kwamba akina Sisi GENTAMYCINE ambao tunakosoa baadhi ya mambo yawezekena ndiyo tukawa na ' uchungu ' wa kweli kabisa na CCM yetu na Magufuli wetu ila kila mara ' Mwanamume ' nabaki kuambulia ' Kashfa ' na ' Kejeli ' kumbe wakiwa wamesahau kuwa Mimi ndiyo ' Malaika ' mwema wa Mungu niliyepo duniani Kukomboa, Kurekebisha na Kunyoosha.

Nilishawahi humu humu kuandika kwamba hakuna Kipindi ambacho Chama chetu Tawala cha CCM kimepata Msemaji ' goi goi ' kama sasa na nikatoa sababu zangu nyingi sana za Kitaaluma na Kiuweledi kwamba Bwana Hamphrey Polepole ' hatoshei ' hapo na kuna siku ' ataharibu ' na ' kuboronga ' zaidi lakini kama kawaida nikapuuzwa na kukejeliwa lakini alichokifanya Polepole majuzi baada ya kuwasikia akina Nassari na Lema juu ya ' Kashfa ' ya aibu katika Chama sasa ndiyo ' kimeigharimu ' CCM kwani kama Polepole angekuwa ' ameiva ' hasa Kimawasiliano, Kipropaganda na Kimkakati ' asingekurupuka ' kuwajibu vile akina Nassari na Lema ambao nao sasa wakaamua kumwaga kila kitu hadharani na sasa tunaaibika.

Nasikia leo kuna ' Mpuuzi ' mmoja hivi anajiandaa kuzungumza na Press ili eti kufanya ' counter ' juu ya walichosema akina Nassari na Lema hivyo nichukue nafasi hii kumwambia tu kwamba asipoteze huo muda na hizo juhudi bali labda kikubwa ambacho anatakiwa kukifanya ni kuandika haraka sana Barua ya Kujiuzuru ' madaraka ' yake lakini pia upesi sana aende mwenyewe Ofisi za TAKUKURU ili ' mashtaka ' rasmi dhidi yake yaanze ili muda wowote tuwe tunaenda kumsalimia / kumsabahi akiwa Gerezani anatumikia ' Kifungo ' chake.

Mwisho nimwombe sana Mheshimiwa Mwenyekiti wetu Taifa wa CCM na Rais wangu Mpendwa kabisa wa JMT Dkt. Magufuli kwamba siku zingine awe anaingia humu JamiiForums na angalau basi aweze kuona Sisi akina GENTAMYCINE, wana CCM makini, wakweli na wawazi wenzangu bila kusahau hata wale Watanzania wenye mapenzi mema nae na kwa nchi wanasema nini au wanamshauri nini. Humu Jamvini JF kuna Watu wana maono ya mbali na wanajua mambo pengine hata kuliko hao ambao wako nae karibu ila ' tunadharaulika ' wakati kiukweli haya tunayoyaibua wala hatutaki tulipwe au tupewe fadhila yoyote bali tumekomazwa na ' Uzalendo ' wa ukweli kwa nchi na taifa.

" hata Kichaa au Mwendawazimu kuna wakati huwa anaongea mambo ya msingi na ambayo yanaweza pia kukuoa au kukusaidia katika maisha yako hivyo tuache kuwadharau kwa sababu tu ya hali zao kwani kila Mtu yupo hapa duniani kwa makusudi yake Mwenyezi Mungu "

Sijui GENTAMYCINE nitaficha wapi Mimi ' aibu ' hii ya Arusha!

Nawasilisha.
BILA SUPPORT YA POLISI NA VYOMBO VYA USALAMA SSM NI WEPESI KAMA UNYOYA
 
Mtu hata kama humpendi Gambo au Mnyeti huwezi taka mtu ajiuzulu kwa tuhuma za vi photoshop vya kutengeneza kwenye vyoo vya ofisi za chadema Arusha.Ushahidi wa mahakama au takukuru ndio waweza mtia hatiani mtu.Watu wanasema walipewa mamilioni !!! Na watu wengine humu wanasema ndiyo walipewa!! Uliziona hizo pesa wakipewa? Hata hivyo viphoto shop koko vya Lema na Nassari havionyeshi.Watu wanadakia humu walipewa!!!! Gambo and Munyeti are there to stay.Hatoki mtu ng`ooo.CCM tuachieni wenyewe wengine akina team lowasa mlio chadema endeleeni na yenu.Kama mnataka kurudi CCm rudini tu lakini mambo ya photoshop za chadema waacheni wenyewe.ya ngoswe mwachie ngoswe.
 
Mimi kwa ukweli wa moyo wangu sitofautishi walivhofanya wakina Gambo, Mnyeti, na Yale anayoyafanya malaika mtukufu.
Staili waliyoitumia wakina Mnyeti na Gambo kina tofauti gani na zile rushwa za vyeo zinazotolewa na mtukufu?
Rejea rushwa ya vyeo ambayo kingereza inaitwa patronage corruption ilivyofanya kazi kwa
1; Anna Mghwira
2: Kitila mkumbo
3: lyatonga Mrema
4: Humphrey pole pole
5; Ibrahim Lipumba
Na hao ni kwa uchache. Jamani naomba tofauti kama mnaziona
KAMA ALIVYO BABA NDIVYO WALIVYO WATOTO.

Kwa hawa angalau ukimtoa Lipumba. Hao wengine ana haki japo ukiwa na mtazamo wa kiitikadi unakwazika.
 
Mm ni CCM, but to speak the TRUTH, evidences za videos tena zina sauti ni mbaya sana sanaaaa... Nassary aka Dogo Janja hapa naona kacheza muziki wa dunia ya kwanza, ushauri wangu kwa Mh. Rais wangu JPM, fukuza RC Arusha, DC na Mkurugenzi Arumeru, hapo utaonekana umepinga rushwa kwa vitendo, and this will PROVE kwa wananchi na wana CCM wenzangu kuwa uzembe hautakiwi ktk kazi..

Sbb hapo kuna uzembe mkubwa sana from RC, DC Arumeru, Mkurugenzi Arumeru wote wazembe kabisa na kiukweli wamekidhalilisha sana Chama chetu CCM.. THIS IS MY FEELINGS.. Fukuza hawa, and uaminifu na uzalendo wako kwa wananchi wetu Mh. Rais utapanda kwa kasi drastically, siasa ni mchezo so Mh. Rais huu ni ushauri wangu..

Fukuza hawa, wametuchafua wazi wazi, CCM mpya ya sasa haitaki uzembe wa aina yoyote.. and utaona jinsi HILI LITASAIDIA MNO MNO 2020

Mungu mbariki Mh. Rais wetu, Mungu ibariki CCM yetu..

Kumbe ' Shujaa ' wa kweli sipo tu peke yangu. Safi sana Mkuu na nakubaliana na yote uliyoyasema hapo ila na Wewe sasa jiandae kuambiwa kuwa ni Mwana CHADEMA kama ambavyo GENTAMYCINE ambaye nilimpigania humu JF Rais Magufuli wakati wa Kampeni hadi nikitukanwa na hata kutishiwa ili tu Kipenzi changu Dkt. Magufuli awe Rais lakini leo Mimi huyu huyu naitwa Mnafiki na Msaliti.

Ipo siku Wana CCM mtanielewa na mtajua kuwa Mwenyezi Mungu amewapeni ' Zawadi ' ya thamani kabisa ya GENTAMYCINE ila mnaipuuza na kuidhihaki. Hakuna ambacho huwa nakileta au nakitolea ufafanuzi humu JF kisije / kisitokee.
 
Mtu hata kama humpebndi gambo au mnyeti huwezi taka mtu ajiuzulu kwa tuhuma za vi photoshop vya kutengeneza kwenye vyoo vya ofisi za chadema Arusha.Ushahidi wa mahakama au takukuru ndio waweza mtia hatiani mtu.Watu wanasema walipewa mamilioni !!! Na watu wengine humu wanasema ndiyo walipewa!! Uliziona hizo pesa wakipewa? Hata hivyo viphoto shop koko vya Lema na Nassari havionyeshi.Watu wanadakia humu walipewa!!!! Gambo and Munyeti are there to stay.Hatoki mtu ng`ooo.CCM tuachieni wenyewe wengine akina team lowasa mlio chadema endeleeni na yenu.Kama mnataka kurudi CCm rudini tu lakini mambo ya photoshop za chadema waacheni wenyewe.ya ngoswe mwachie ngoswe.
tafuta miwani labda una shida ya macho. au wewe ni " Mnyeti" kaacha Nyeti za ccm wazi .pwaahhhhh
 
Mtu hata kama humpebndi gambo au mnyeti huwezi taka mtu ajiuzulu kwa tuhuma za vi photoshop vya kutengeneza kwenye vyoo vya ofisi za chadema Arusha.Ushahidi wa mahakama au takukuru ndio waweza mtia hatiani mtu.Watu wanasema walipewa mamilioni !!! Na watu wengine humu wanasema ndiyo walipewa!! Uliziona hizo pesa wakipewa? Hata hivyo viphoto shop koko vya Lema na Nassari havionyeshi.Watu wanadakia humu walipewa!!!! Gambo and Munyeti are there to stay.Hatoki mtu ng`ooo.CCM tuachieni wenyewe wengine akina team lowasa mlio chadema endeleeni na yenu.Kama mnataka kurudi CCm rudini tu lakini mambo ya photoshop za chadema waacheni wenyewe.ya ngoswe mwachie ngoswe.
Magamba yanaruka na kukanyagana
 
Back
Top Bottom