CCM aibu hii ya Arusha ibebeni wenyewe Mimi simo

CCM aibu hii ya Arusha ibebeni wenyewe Mimi simo

Nakuelewa, he is not ready Brother ..... wrong and right are defined moyoni mwa mtu, na he knows wrong and right, na hataki. Mfano, kwenye hotuba yake Arusha alisema sukari ilikuwa 5000 alipoingia madarakani? I was like? real? sasa hapa tunafanyaje ndugu? na watu wote wa karibu hawamwambii ukweli, walio karibu wakiweka msimamo labda italeta mabadiliko, lakini kama watu wa karibu hawafanyi hivyo, ni vigumu sana kwa sisi huku!!!!

Asante Uttoh2002, "if the mountain cannot move to John then we must make John move to the mountain"
 
Huko nyuma nilipokuwa naandika mambo humu tena ya Kuikosoa CCM lakini nikiwa na maana moja kubwa tu ambayo kwa bahati mbaya sana ' Wapumbavu ' wachache waliojawa na ' Unafiki ' mkubwa na uliotukuka kabisa walikuwa wakinikejeli, kunitusi, kunikashifu huku wakisema kuwa Mimi GENTAMYCINE ni mwana CHADEMA na nakumbuka kila mara niliwahi kuwaambia kuwa ipo siku ' mtanielewa ' na ' mtanikumbuka ' na hatimaye sasa yametimia.

Nilishamwambia hadi Mwenyekiti wetu Taifa kuwa awe makini sana kwani humo humo ndani ya CCM yetu kuna ' Mamluki ' wengi ambao wanamchafua na kumuharibia ili baadae aharibikiwe na waje kumcheka hakunisikia.

Nilishawahi kueleza mapungufu kabisa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye sifichi na sioni aibu kusema kuwa ni mmoja kati ya Watu ninaowajua in and out na kuna siku nilisema humu humu JF kuwa kama kuna Mtu ambaye tokea ' Teuzi ' za CCM za Wagombea Urais 2015 alikuwa hampendi, hamtaki na akimdhihaki sana Mgombe wa Urais Rais wa sasa wa JMT Dkt. Magufuli alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuna siku moja tukiwa nae katika Nyumba jirani na ilipo Hotel ya Kebby's Mwenge alionge a' Kauli ' moja ambayo siku niliposikia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na JPM nilianza kumuonea mno ' huruma ' JPM kwani nilianza kujua nini kitakuja.

Nilishawahi kusema humu humu tena kwamba kuna Wana CCM wenzetu wanadhani kumpamba, kumsifu na kumpa matumaini hewa Mwenyekiti wetu Rais Dkt. Magufuli kutakisaidia Chama chetu lakini pia kutawasaidia Wao kuendelea kula ' bata ' ndani ya Chama wakati ukweli ni kwamba akina Sisi GENTAMYCINE ambao tunakosoa baadhi ya mambo yawezekena ndiyo tukawa na ' uchungu ' wa kweli kabisa na CCM yetu na Magufuli wetu ila kila mara ' Mwanamume ' nabaki kuambulia ' Kashfa ' na ' Kejeli ' kumbe wakiwa wamesahau kuwa Mimi ndiyo ' Malaika ' mwema wa Mungu niliyepo duniani Kukomboa, Kurekebisha na Kunyoosha.

Nilishawahi humu humu kuandika kwamba hakuna Kipindi ambacho Chama chetu Tawala cha CCM kimepata Msemaji ' goi goi ' kama sasa na nikatoa sababu zangu nyingi sana za Kitaaluma na Kiuweledi kwamba Bwana Hamphrey Polepole ' hatoshei ' hapo na kuna siku ' ataharibu ' na ' kuboronga ' zaidi lakini kama kawaida nikapuuzwa na kukejeliwa lakini alichokifanya Polepole majuzi baada ya kuwasikia akina Nassari na Lema juu ya ' Kashfa ' ya aibu katika Chama sasa ndiyo ' kimeigharimu ' CCM kwani kama Polepole angekuwa ' ameiva ' hasa Kimawasiliano, Kipropaganda na Kimkakati ' asingekurupuka ' kuwajibu vile akina Nassari na Lema ambao nao sasa wakaamua kumwaga kila kitu hadharani na sasa tunaaibika.

Nasikia leo kuna ' Mpuuzi ' mmoja hivi anajiandaa kuzungumza na Press ili eti kufanya ' counter ' juu ya walichosema akina Nassari na Lema hivyo nichukue nafasi hii kumwambia tu kwamba asipoteze huo muda na hizo juhudi bali labda kikubwa ambacho anatakiwa kukifanya ni kuandika haraka sana Barua ya Kujiuzuru ' madaraka ' yake lakini pia upesi sana aende mwenyewe Ofisi za TAKUKURU ili ' mashtaka ' rasmi dhidi yake yaanze ili muda wowote tuwe tunaenda kumsalimia / kumsabahi akiwa Gerezani anatumikia ' Kifungo ' chake.

Mwisho nimwombe sana Mheshimiwa Mwenyekiti wetu Taifa wa CCM na Rais wangu Mpendwa kabisa wa JMT Dkt. Magufuli kwamba siku zingine awe anaingia humu JamiiForums na angalau basi aweze kuona Sisi akina GENTAMYCINE, wana CCM makini, wakweli na wawazi wenzangu bila kusahau hata wale Watanzania wenye mapenzi mema nae na kwa nchi wanasema nini au wanamshauri nini. Humu Jamvini JF kuna Watu wana maono ya mbali na wanajua mambo pengine hata kuliko hao ambao wako nae karibu ila ' tunadharaulika ' wakati kiukweli haya tunayoyaibua wala hatutaki tulipwe au tupewe fadhila yoyote bali tumekomazwa na ' Uzalendo ' wa ukweli kwa nchi na taifa.

" hata Kichaa au Mwendawazimu kuna wakati huwa anaongea mambo ya msingi na ambayo yanaweza pia kukuoa au kukusaidia katika maisha yako hivyo tuache kuwadharau kwa sababu tu ya hali zao kwani kila Mtu yupo hapa duniani kwa makusudi yake Mwenyezi Mungu "

Sijui GENTAMYCINE nitaficha wapi Mimi ' aibu ' hii ya Arusha!

Nawasilisha.
Wewe ni mnafiki. Polepole ni jiniasi anakuzidi sana kiakili na weledi. CCM ipo pahala pazuri sana kuliko kipindi chochote kwa sasa. Kila mwananchi anaelewa umuhimu wa CCM ya sasa. Yaani huku kitaa ni chereko chereko!
 
Mm ni CCM, but to speak the TRUTH, evidences za videos tena zina sauti ni mbaya sana sanaaaa... Nassary aka Dogo Janja hapa naona kacheza muziki wa dunia ya kwanza, ushauri wangu kwa Mh. Rais wangu JPM, fukuza RC Arusha, DC na Mkurugenzi Arumeru, hapo utaonekana umepinga rushwa kwa vitendo, and this will PROVE kwa wananchi na wana CCM wenzangu kuwa uzembe hautakiwi ktk kazi..

Sbb hapo kuna uzembe mkubwa sana from RC, DC Arumeru, Mkurugenzi Arumeru wote wazembe kabisa na kiukweli wamekidhalilisha sana Chama chetu CCM.. THIS IS MY FEELINGS.. Fukuza hawa, and uaminifu na uzalendo wako kwa wananchi wetu Mh. Rais utapanda kwa kasi drastically, siasa ni mchezo so Mh. Rais huu ni ushauri wangu..

Fukuza hawa, wametuchafua wazi wazi, CCM mpya ya sasa haitaki uzembe wa aina yoyote.. and utaona jinsi HILI LITASAIDIA MNO MNO 2020

Mungu mbariki Mh. Rais wetu, Mungu ibariki CCM yetu..
 
Cocochannel where are you? I miss you so much, come baby, come please.
Today Jf is so cool, I'm here waiting for you baby mwaaah.
Kapewa za uso asubuh nazani yuko kwa DAB kushtaki kampitia Le kubwa jingaz
 
Nimepata kuandika mara kadhaa Mh. Rais wa JMT aangalie waliomzunguuka wakoje na yeye lakini nadhani ujumbe huo hajafanikiwa kuupata! Niliandika anaweza kuwa na nia njema sana na napenda kuamini hivyo lakini genge la majambazi na wezi waliomzunguuka wananipa shaka kuamini katika nia yake njema. LAZIMA TUKWAME

Mkuu uko sahihi kwa 100% na nakubaliana nawe. Yaani kila nikiyakumbuka yale maneno ya Kejeli ambayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alikuwa akiyatoa kwa Mwenyekiti Taifa CCM Magufuli wakati alipoteuliwa na akifanya Kampeni halafu nikasia tena ' Kamteua ' kuwa RC Arusha nilijua tu ya kwamba kuna ' hatari ' inakuja na sasa imetimia rasmi. Hakuna Mtu ambaye hampendi na wala hamkubali kabisa Mwenyekiti na Rais Magufuli kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha Gambo na hili Mimi kama Mimi GENTAMYCINE nina uhakika nalo kwani nimewahi kuyasikia hayo maneno yakitoka ' mubashara ' katika ' Kinywa ' cha Mrisho Gambo na nina uhakika hata Yeye mwenyewe akisoma haya ' maandiko ' yangu hapa hatoyabishia kwani anajua sijakosea na huwa sibahatishi bali huwa nina uhakika na mambo yangu.
 
Yanaweza kukusaidia "kukuoa" au kukusaidia ktk maisha hapo mkuu hapajatulia
 
Hivi mnajua nilifika tawi la CCM ilala pale kufatilia kadi yangu. Nilipanga niludi week hii kuchukua kadi sasa naona aibu hawa vijana kina Mnyeti na Gambo sio kwamba wana uchungu na CCM lah hasha wanauchungu na Madaraka wanachotaka wao ni kutafuta kiki kwa Rais wapande vyeo watu kama hawa sio wazuri wanaweza kukugeuka anytime.
 
Gambo anafanya mchezo na machalii wa Ara, hizo propaganda zake za kitoto apeleke Dodoma, huko sehemu zenye makoloni ya CCM wasiojielewa
 
Wewe ni mnafiki. Polepole ni jiniasi anakuzidi sana kiakili na weledi. CCM ipo pahala pazuri sana kuliko kipindi chochote kwa sasa. Kila mwananchi anaelewa umuhimu wa CCM ya sasa. Yaani huku kitaa ni chereko chereko!
kufa na tai shingoni dada
 
Back
Top Bottom