mama kubwa
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 6,527
- 10,538
Pole Genta yupo aliewatuma ndio maana walipoingia mitini wale wengine aliwaita wapumbavu. Hili goma kinara wake ni Sizonje.
Daah GENTAMYCINE umeongea ukweli. Lakini huyo mwenyekiti wenu hashauriki na ndo maana kuna haya mambo yanayoendelea. Anajiona ana akili kuliko mtanzania yeyote.. Hapo ndio anapokosea. Siku mukulu akikubali kushauriwa na siku watanzania tutapoacha unafiki kama GENTAMYCINE alivyo basi tutapiga hatua kubwa ya maendeleo..
Aibu gani? Kushawishi ni aibu? Mbona Lissu alimshiwishi Nape kuhama na kuingia chadema? Lobing hipo kite.
Nikakumbuka ule usemi mashuhuri kuwa hata saa mbovu kuna wakati inasema ukweli. Asante Gentamycine kwa post mujarabu.
Hongera Gentamycine kwa upeo wako mkubwa wa ushauri na wa kuona mbali.Bandiko hili ni zuri sana na limejaa ushauri mwanana ambao unapaswa kufanyiwa kazi haraka.CCM tunaipenda,lakini wapo watendaji wengi sana wa hovyo na wabovu wachumia tumbo kuanzia mashinani mpaka ngazi ya taifa, ambao wanakichafua sana chama.Kazi ya kukisafisha chama ni kubwa na inatakiwa kufanywa haraka, tena bila huruma,vinginevyo 2020 itakuwa chungu.
Tunajuaje? Hii hakuna ushahidi wa pesa.ni kauli tu. Hakuna sehemu yo yote inayoonyesha kupeana pesa.
Ya ccm nimeichoma moto kupitia kampeni ya mange kimimbaKadi unayo?!
Kawatuma yeye mwenyeweMm ni CCM, but to speak the TRUTH, evidences za videos tena zina sauti ni mbaya sana sanaaaa... Nassary aka Dogo Janja hapa naona kacheza muziki wa dunia ya kwanza, ushauri wangu kwa Mh. Rais wangu JPM, fukuza RC Arusha, DC na Mkurugenzi Arumeru, hapo utaonekana umepinga rushwa kwa vitendo, and this will PROVE kwa wananchi na wana CCM wenzangu kuwa uzembe hautakiwi ktk kazi..
Sbb hapo kuna uzembe mkubwa sana from RC, DC Arumeru, Mkurugenzi Arumeru wote wazembe kabisa na kiukweli wamekidhalilisha sana Chama chetu CCM.. THIS IS MY FEELINGS.. Fukuza hawa, and uaminifu na uzalendo wako kwa wananchi wetu Mh. Rais utapanda kwa kasi drastically, siasa ni mchezo so Mh. Rais huu ni ushauri wangu..
Fukuza hawa, wametuchafua wazi wazi, CCM mpya ya sasa haitaki uzembe wa aina yoyote.. and utaona jinsi HILI LITASAIDIA MNO MNO 2020
Mungu mbariki Mh. Rais wetu, Mungu ibariki CCM yetu..
Ni kweli kabisa Sisi ambao tunasema ukweli unaonekana ni mapandikizi kumbe ndo wafia chama. Kukicha wataamka kutoka usingizini wakati huo muda utakuwa hautoshiHuko nyuma nilipokuwa naandika mambo humu tena ya Kuikosoa CCM lakini nikiwa na maana moja kubwa tu ambayo kwa bahati mbaya sana ' Wapumbavu ' wachache waliojawa na ' Unafiki ' mkubwa na uliotukuka kabisa walikuwa wakinikejeli, kunitusi, kunikashifu huku wakisema kuwa Mimi GENTAMYCINE ni mwana CHADEMA na nakumbuka kila mara niliwahi kuwaambia kuwa ipo siku ' mtanielewa ' na ' mtanikumbuka ' na hatimaye sasa yametimia.
Nilishamwambia hadi Mwenyekiti wetu Taifa kuwa awe makini sana kwani humo humo ndani ya CCM yetu kuna ' Mamluki ' wengi ambao wanamchafua na kumuharibia ili baadae aharibikiwe na waje kumcheka hakunisikia.
Nilishawahi kueleza mapungufu kabisa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye sifichi na sioni aibu kusema kuwa ni mmoja kati ya Watu ninaowajua in and out na kuna siku nilisema humu humu JF kuwa kama kuna Mtu ambaye tokea ' Teuzi ' za CCM za Wagombea Urais 2015 alikuwa hampendi, hamtaki na akimdhihaki sana Mgombe wa Urais Rais wa sasa wa JMT Dkt. Magufuli alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuna siku moja tukiwa nae katika Nyumba jirani na ilipo Hotel ya Kebby's Mwenge alionge a' Kauli ' moja ambayo siku niliposikia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na JPM nilianza kumuonea mno ' huruma ' JPM kwani nilianza kujua nini kitakuja.
Nilishawahi kusema humu humu tena kwamba kuna Wana CCM wenzetu wanadhani kumpamba, kumsifu na kumpa matumaini hewa Mwenyekiti wetu Rais Dkt. Magufuli kutakisaidia Chama chetu lakini pia kutawasaidia Wao kuendelea kula ' bata ' ndani ya Chama wakati ukweli ni kwamba akina Sisi GENTAMYCINE ambao tunakosoa baadhi ya mambo yawezekena ndiyo tukawa na ' uchungu ' wa kweli kabisa na CCM yetu na Magufuli wetu ila kila mara ' Mwanamume ' nabaki kuambulia ' Kashfa ' na ' Kejeli ' kumbe wakiwa wamesahau kuwa Mimi ndiyo ' Malaika ' mwema wa Mungu niliyepo duniani Kukomboa, Kurekebisha na Kunyoosha.
Nilishawahi humu humu kuandika kwamba hakuna Kipindi ambacho Chama chetu Tawala cha CCM kimepata Msemaji ' goi goi ' kama sasa na nikatoa sababu zangu nyingi sana za Kitaaluma na Kiuweledi kwamba Bwana Hamphrey Polepole ' hatoshei ' hapo na kuna siku ' ataharibu ' na ' kuboronga ' zaidi lakini kama kawaida nikapuuzwa na kukejeliwa lakini alichokifanya Polepole majuzi baada ya kuwasikia akina Nassari na Lema juu ya ' Kashfa ' ya aibu katika Chama sasa ndiyo ' kimeigharimu ' CCM kwani kama Polepole angekuwa ' ameiva ' hasa Kimawasiliano, Kipropaganda na Kimkakati ' asingekurupuka ' kuwajibu vile akina Nassari na Lema ambao nao sasa wakaamua kumwaga kila kitu hadharani na sasa tunaaibika.
Nasikia leo kuna ' Mpuuzi ' mmoja hivi anajiandaa kuzungumza na Press ili eti kufanya ' counter ' juu ya walichosema akina Nassari na Lema hivyo nichukue nafasi hii kumwambia tu kwamba asipoteze huo muda na hizo juhudi bali labda kikubwa ambacho anatakiwa kukifanya ni kuandika haraka sana Barua ya Kujiuzuru ' madaraka ' yake lakini pia upesi sana aende mwenyewe Ofisi za TAKUKURU ili ' mashtaka ' rasmi dhidi yake yaanze ili muda wowote tuwe tunaenda kumsalimia / kumsabahi akiwa Gerezani anatumikia ' Kifungo ' chake.
Mwisho nimwombe sana Mheshimiwa Mwenyekiti wetu Taifa wa CCM na Rais wangu Mpendwa kabisa wa JMT Dkt. Magufuli kwamba siku zingine awe anaingia humu JamiiForums na angalau basi aweze kuona Sisi akina GENTAMYCINE, wana CCM makini, wakweli na wawazi wenzangu bila kusahau hata wale Watanzania wenye mapenzi mema nae na kwa nchi wanasema nini au wanamshauri nini. Humu Jamvini JF kuna Watu wana maono ya mbali na wanajua mambo pengine hata kuliko hao ambao wako nae karibu ila ' tunadharaulika ' wakati kiukweli haya tunayoyaibua wala hatutaki tulipwe au tupewe fadhila yoyote bali tumekomazwa na ' Uzalendo ' wa ukweli kwa nchi na taifa.
" hata Kichaa au Mwendawazimu kuna wakati huwa anaongea mambo ya msingi na ambayo yanaweza pia kukuoa au kukusaidia katika maisha yako hivyo tuache kuwadharau kwa sababu tu ya hali zao kwani kila Mtu yupo hapa duniani kwa makusudi yake Mwenyezi Mungu "
Sijui GENTAMYCINE nitaficha wapi Mimi ' aibu ' hii ya Arusha!
Nawasilisha.