Huko nyuma nilipokuwa naandika mambo humu tena ya Kuikosoa CCM lakini nikiwa na maana moja kubwa tu ambayo kwa bahati mbaya sana ' Wapumbavu ' wachache waliojawa na ' Unafiki ' mkubwa na uliotukuka kabisa walikuwa wakinikejeli, kunitusi, kunikashifu huku wakisema kuwa Mimi GENTAMYCINE ni mwana CHADEMA na nakumbuka kila mara niliwahi kuwaambia kuwa ipo siku ' mtanielewa ' na ' mtanikumbuka ' na hatimaye sasa yametimia.
Nilishamwambia hadi Mwenyekiti wetu Taifa kuwa awe makini sana kwani humo humo ndani ya CCM yetu kuna ' Mamluki ' wengi ambao wanamchafua na kumuharibia ili baadae aharibikiwe na waje kumcheka hakunisikia.
Nilishawahi kueleza mapungufu kabisa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye sifichi na sioni aibu kusema kuwa ni mmoja kati ya Watu ninaowajua in and out na kuna siku nilisema humu humu JF kuwa kama kuna Mtu ambaye tokea ' Teuzi ' za CCM za Wagombea Urais 2015 alikuwa hampendi, hamtaki na akimdhihaki sana Mgombe wa Urais Rais wa sasa wa JMT Dkt. Magufuli alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuna siku moja tukiwa nae katika Nyumba jirani na ilipo Hotel ya Kebby's Mwenge alionge a' Kauli ' moja ambayo siku niliposikia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na JPM nilianza kumuonea mno ' huruma ' JPM kwani nilianza kujua nini kitakuja.
Nilishawahi kusema humu humu tena kwamba kuna Wana CCM wenzetu wanadhani kumpamba, kumsifu na kumpa matumaini hewa Mwenyekiti wetu Rais Dkt. Magufuli kutakisaidia Chama chetu lakini pia kutawasaidia Wao kuendelea kula ' bata ' ndani ya Chama wakati ukweli ni kwamba akina Sisi GENTAMYCINE ambao tunakosoa baadhi ya mambo yawezekena ndiyo tukawa na ' uchungu ' wa kweli kabisa na CCM yetu na Magufuli wetu ila kila mara ' Mwanamume ' nabaki kuambulia ' Kashfa ' na ' Kejeli ' kumbe wakiwa wamesahau kuwa Mimi ndiyo ' Malaika ' mwema wa Mungu niliyepo duniani Kukomboa, Kurekebisha na Kunyoosha.
Nilishawahi humu humu kuandika kwamba hakuna Kipindi ambacho Chama chetu Tawala cha CCM kimepata Msemaji ' goi goi ' kama sasa na nikatoa sababu zangu nyingi sana za Kitaaluma na Kiuweledi kwamba Bwana Hamphrey Polepole ' hatoshei ' hapo na kuna siku ' ataharibu ' na ' kuboronga ' zaidi lakini kama kawaida nikapuuzwa na kukejeliwa lakini alichokifanya Polepole majuzi baada ya kuwasikia akina Nassari na Lema juu ya ' Kashfa ' ya aibu katika Chama sasa ndiyo ' kimeigharimu ' CCM kwani kama Polepole angekuwa ' ameiva ' hasa Kimawasiliano, Kipropaganda na Kimkakati ' asingekurupuka ' kuwajibu vile akina Nassari na Lema ambao nao sasa wakaamua kumwaga kila kitu hadharani na sasa tunaaibika.
Nasikia leo kuna ' Mpuuzi ' mmoja hivi anajiandaa kuzungumza na Press ili eti kufanya ' counter ' juu ya walichosema akina Nassari na Lema hivyo nichukue nafasi hii kumwambia tu kwamba asipoteze huo muda na hizo juhudi bali labda kikubwa ambacho anatakiwa kukifanya ni kuandika haraka sana Barua ya Kujiuzuru ' madaraka ' yake lakini pia upesi sana aende mwenyewe Ofisi za TAKUKURU ili ' mashtaka ' rasmi dhidi yake yaanze ili muda wowote tuwe tunaenda kumsalimia / kumsabahi akiwa Gerezani anatumikia ' Kifungo ' chake.
Mwisho nimwombe sana Mheshimiwa Mwenyekiti wetu Taifa wa CCM na Rais wangu Mpendwa kabisa wa JMT Dkt. Magufuli kwamba siku zingine awe anaingia humu JamiiForums na angalau basi aweze kuona Sisi akina GENTAMYCINE, wana CCM makini, wakweli na wawazi wenzangu bila kusahau hata wale Watanzania wenye mapenzi mema nae na kwa nchi wanasema nini au wanamshauri nini. Humu Jamvini JF kuna Watu wana maono ya mbali na wanajua mambo pengine hata kuliko hao ambao wako nae karibu ila ' tunadharaulika ' wakati kiukweli haya tunayoyaibua wala hatutaki tulipwe au tupewe fadhila yoyote bali tumekomazwa na ' Uzalendo ' wa ukweli kwa nchi na taifa.
" hata Kichaa au Mwendawazimu kuna wakati huwa anaongea mambo ya msingi na ambayo yanaweza pia kukuoa au kukusaidia katika maisha yako hivyo tuache kuwadharau kwa sababu tu ya hali zao kwani kila Mtu yupo hapa duniani kwa makusudi yake Mwenyezi Mungu "
Sijui GENTAMYCINE nitaficha wapi Mimi ' aibu ' hii ya Arusha!
Nawasilisha.