categories za watabibu

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
Jana nilikuwa naongea na mtu mmoja akawa anasema kuwa yeye anajua kutibu kwa mitishamba na karithishwa na baba yake.

Ila aliomba kuwa taarifa zisifike kanisani kwani yeye ni muumini mzuri anaujulikana. Nilishangaa sana, ila nikamuuliza kwanini? kwani kanisa lenu linakataza mitishamba, akasema hakuna mtu anaetibu kwa mitishamba pekee, eti lazima kuwe na uganga.

kufupisha hadithi ndefu, ila at the end of the day timu nzima iliokuwapo hapo ilisema hakuna utibabu wa mitishamba, wala wasiitwe wachawi kwani eti japo wote wanatumia ushirikina, lakini mchawi anaumiza na mganga anaponya.

mie nilidhani mganga anatumia mishamba na njia za kiasili (madini, mimea, wanyama au wadudu, na therapies nyingine) na mchawi ni mshirikina yoyote anaeponya au anaeumiza.
 
watu wengi wanachanganya kujua dawa za miti shamba na kuwa mganga wa kienyeji, actually ni vitu vinavyochanganya lakini tofauti ni kuwa unaweza kuwa unajua dawa za kutibu magonjwa mengi na hiyo kurisishwa ni kuelekezwa na anayejua hizo dawa.

lakini ukija pale kwenye uganga wa kienyeji kuanza kupiga ramli na kuuliza mizimu hapo ndipo linapokuja tatizo la kuambiwa ulete mbuzi mara kuku na vitu kama hivyo.

lakini kujua dawa labda Mwarubaini, arovera, majani ya mapera na dawa nyingine nyingi bila USHIRIKINA mimim sioni ni tatizo na nadhani hakuna kanisa linalopinga hilo
 
Kwa hakika hakuna tatizo lolote kujua/kutumia miti shamba, nk kama dawa. Hata hizo dawa rasmi za hospitali nyingi zinatokana na mazao ya mimea.

Issue ni kuwa wengi wa hao waganga wa kienyeji/kimila, pamoja na kutumia mazao ya mimea kutibu, wanaongezea teknolojia zao za kuagua, kuzindika, kuloga, ushirikina nk.

Ukitaka tiba tu, mtafute anayejua dawa za miti shamba/mimea. Usiende kwa mganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom