Capital Gain Tax ni nini?

Capital Gain Tax ni nini?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,262
Reaction score
18,706
Baba yangu ameuza nyumba hapa Musoma mjini kwa sh mil 80. Nyumba ilikua na hati na vizuri na amenipa jukumu la kukamilisha zoezi la uuzaji na kuhakikisha mnunuzi anamaliza process zake vizuri.

Tuliyemuuzia akataka kufanya transfer kwenda kwenye jina lake.

Halmashauri wakatuomba kitu kinaitwa evaluation ambapo wakathaminisha nyumba na kusema ina thamani ya Mil 134.

Nyumba ina mwaka kama mmoja toka iishe.

Sasa baada ya kumalizana na hamashauri, wananiambia niliyemuuzia haweza kubadili jina kama sijalipa Capital Gain Tax.

Baada ya kupeleka docs TRA , wananiambia capital gain Tax ni 10% ya market value ambapo kwa mimi ni 10% ya mil 134 sawa na Mil 13.

Wakuu hapa nimechanganyikiwa naona kama naibiwa au wanajitisha nitoe rushwa.

Nimejaribu kugoogle napata maana nyingine hata kwa Tanzania na hakuna online calculator kwa Tanzania kujua nahitaji kulipa kiasi gani.

Wakuu Capital Gain Tax ni nini?

Mbona ni kubwa kiasi hiki? Ni afadhali tusingeuza nyumba. Tuibakize iwe ya urithi?
 
Baada ya kupeleka docs TRA , wananiambia capital gain Tax ni 10% ya market value ambapo kwa mimi ni 10% ya mil 134 sawa na Mil 13.
Pole sana mkuu kwa usumbufu huo.
====
Sasa kama market value ni hiyo, wanakataje tena 10%!? Kumbe na mimi nahitsji shule kujua ni vigezo gani hawa watoza kodi huwa wanatumia kuweka viwango vya kodi.
 
Ukiangalia kwenye website ya TRA wanasema capital gain ni faida ambayo mwuzaji ameipata.

Kwa hiyo kwa uelewa wangu kama.market value ni kubwa kuliko pesa nilitopolea kwa mauzo maana yake sikutakiwa kulipa.. ni kama nilipata hasara.

Asante sana Mkuu, kwa elimu hii. Basi mrudishiwe 13.4 mil yenu kama mlikuwa mmeisha lipa. Halafu hao wanaweka market value kubwa hivyo maana yake wao sasa ndiyo wanasababisha mfumuko wa bei! Mimi nilitegemea, anayeuza bidhaa kwa bei ya chini alitakiwa kupongezwa na kupewa zawadi kwa kitendo chake cha kishujaa cha kudhibiti mfumuko wa bei. Sasa yeye eti ndiye anaadhibiwa...! Watu wakodi jamani ebu tupe elimu ya kutosha. Maana bila kutupa elimu yenu hii tunaweza kuanza kuwawazia mambo ambayo uwenda si sahihi!

Kwa mara nyingine asante sana Tabutupu kwa elimu hii ya capital gain.
 
Mkuu onavyo onekana TRA ni tatizo.. kubwa sana kwa wananchi
Asante sana Mkuu, kwa elimu hii. Basi jamaa arudishiwe 13.4 mil yake kama alikuwa ameisha lipa. Halafu hao wanaweka market value kubwa hivyo maana yake wao sasa ndiyo wanasababisha mfumuko wa bei! Mimi nilitegemea, anayeuza bidhaa kwa bei ya chini alitakiwa kupongezwa na kupewa zawadi kwa kitendo chake cha kishujaa cha kudhibi mfumuko wa bei. Sasa yeye eti ndiye anaadhibiwa...! Watu wakodi jamani ebu tupe elimu ya kutosha. Maana bila kutupa elimu yenu hii tunaweza kuanza kuwawazia mambo ambayo uwenda si sahihi!

Kwa mara nyingine asante sana Tabutupu kwa elimu hii ya capital gain.
 
TRA ni jangaaa sana.. hapo ungejua toka mwanzo kuna kitu ungefanya, kima hesabu. Jamaa angeilipa huko kwa huko ndani kwa ndani, ila ndio ivyo hukujuaz washataka fungu lao la kumi. Ila pia unaeza kataa ndio maana kuna meza ya majadiriano.. hao ndio wa kucheza nao hao..
 
Mkuu ipo hivi: Kwa mfano ulinunua nyumba kwa 80,000,000 halafu ukaja kuiuza kwa kwa 90,000,000 utapata faida ya 10,000,000. Hivyo capital gain tax ni 10,000,000×10% = 1,000,000. ...Hakikisheni kwenye gharama zenu za kuinunua hiyo nyumba zinakuwa kubwa ili kupunguza faida. Kwa mfano kama mliinunua kwa 80,000,000 lazima kuna gharama zingine mliingia kama vile ukarabati, dalali, etc. Ongezeni hizi gharama kwenye nyumba ili nyumba ionekane iliwacost hela ndefu. Gharama ya ununuzi ikiwa kubwa mtajikuta mmelipa kodi ndogo sana.
 
Baba yangu ameuza nyumba hapa Musoma mjini kwa sh mil 80. Nyumba ilikua na hati na vizuri na amenipa jukumu la kukamilisha zoezi la uuzaji na kuhakikisha mnunuzi anamaliza process zake vizuri.

Tuliyemuuzia akataka kufanya transfer kwenda kwenye jina lake.

Halmashauri wakatuomba kitu kinaitwa evaluation ambapo wakathaminisha nyumba na kusema ina thamani ya Mil 134.

Nyumba ina mwaka kama mmoja toka iishe.

Sasa baada ya kumalizana na hamashauri, wananiambia niliyemuuzia haweza kubadili jina kama sijalipa Capital Gain Tax.

Baada ya kupeleka docs TRA , wananiambia capital gain Tax ni 10% ya market value ambapo kwa mimi ni 10% ya mil 134 sawa na Mil 13.

Wakuu hapa nimechanganyikiwa naona kama naibiwa au wanajitisha nitoe rushwa.

Nimejaribu kugoogle napata maana nyingine hata kwa Tanzania na hakuna online calculator kwa Tanzania kujua nahitaji kulipa kiasi gani.

Wakuu Capital Gain Tax ni nini?

Mbona ni kubwa kiasi hiki? Ni afadhali tusingeuza nyumba. Tuibakize iwe ya urithi?

Capital gain ni mojawapo ya income tax. Kodi hii hutozwa kwa mtu ambaye amegain faida baada ya kudispose asset yake ie property, share, bonds,au stock.

Sheria ya kodi inatumia neno “ realisation of asset” badala ya neno capital gain.

Kodi hii huchajiwa kwa kuchukua amount ya mkataba wa mauziano au valuation REport whichever is greater. Mkuu valuation Report ya nyumba yako ni 134M na rate ya kodi hapo ni 10% ambayo italeta 13M.

Lakini ukokotoaji wa percent unajumuisha expenditures ulizotumia kwenye kupata nyumba hiyo. Hivyo basi TRA watatoa hizo expenses kutoka kwenye hiyo 134M.

Let say costs ulizotumia kumantain hiyo nyumba ni 90M hivyo gain itakuwa 134M-90M.Hivyo gain ni 44M ambapo 10% yake ni 4M
 
Baba angu ameuza Nyumba hapa musoma mjini kwa sh mil 80. Nyumba ilikua na hati na vizuri .. na amenipa jukumu na jukamilisha zoezi la uuzaji na kuhakikisha mnunuzi anamaliza process zake vizuri.

Tuliye mwuzia akataka kufanya transfer kwenfa kwenye jina lake.

Halmashauri wakatuomba kitu kinaitwa evaluation ambapo wakadhaminisha nyumba na kusema ina thamani ya Mil 134.

Nyumba ina mwaka kama mmoja toka iishe.

Sasa baada ya kumalizana na hamashauri , wananiambia niliye mwuzia haweza kubadili jina kama sijalipa Capital Gain Tax.

Baada ya kupeleka docs TRA , wananiambia capital gain Tax ni 10% ya market value ambapo kwa mimi ni 10% ya mil 134 sawa na Mil 13.

Wakuu hapa nimechanganyikiwa naona kama naibiwa au wanajitisha nitoe rushwa.

Nimejaribu ku google napata maana nyingine hata kwa Tanzania.. na hakuna online calculator kwa Tanzania kujua nahitaji kulipa kiasi gani.

Wakuu Capital Gain Tax ni nini?

Mbona ni kubwa kiasi hiki? Ni afadhali tusingenuza nyumba.. tuibakize iwe ya uridhi?
Capital gain tax ni mojawapo ya kodi ya zuio ambayo muuzaji wa asset anatakiwa kulipa. Faida ndio inayotozwa kodi. Kama ni raia wa Tanzania ni 10% na kama ni mgeni ni 20%. Hii inaaply kwenye asset kama nyumba na ardhi.
 
Hii kitu mie sio mtaalam ila mara nyingi nimeona inapotokea mauziano ya kitu na kikahusisha ubadili wa umiliki.

Mfano, ikiwa kuna kampuni inamilikiwa na watu na mmoja wapo akaamua kujitoa kwa kuuza hisa zake, kampuni itatakiwa kulipa pesa flani TRA ili mmiliki aliyejitoa aondolewe kisheria.

Ikiwa umeuza jengo, ukienda kubadili umiliki, TRA wanataka wapewe pato hapo. Shida ni kwenye kujua asilimia wanayokata. Ndio maana wengine wanaamua kuandika kiasi kidogo cha pesa kwente mauziano ili kupunguza asilimia ya pesa za hawa akina Zakayo.

Kimsingi ilitakiwa iwe ni 10% ya faida iliyopatikana kutokana na mauzo na sio asilimia kumi ya mauzo yote. Wajuvi watakuja kujazia jazia.

Ikiwa tayari nyaraka ulizopeleka zimeonyesha kuasi halisi cha pesa mlichouziana, hata usipoteze muda acha tu waendelee na walichoamua kuchukua.

Pole sana mkuu.

Narudia tena, mtanzania kuiona pepo sio kazi rahisi.
 
Baba yangu ameuza nyumba hapa Musoma mjini kwa sh mil 80. Nyumba ilikua na hati na vizuri na amenipa jukumu la kukamilisha zoezi la uuzaji na kuhakikisha mnunuzi anamaliza process zake vizuri.

Tuliyemuuzia akataka kufanya transfer kwenda kwenye jina lake.

Halmashauri wakatuomba kitu kinaitwa evaluation ambapo wakathaminisha nyumba na kusema ina thamani ya Mil 134.

Nyumba ina mwaka kama mmoja toka iishe.

Sasa baada ya kumalizana na hamashauri, wananiambia niliyemuuzia haweza kubadili jina kama sijalipa Capital Gain Tax.

Baada ya kupeleka docs TRA , wananiambia capital gain Tax ni 10% ya market value ambapo kwa mimi ni 10% ya mil 134 sawa na Mil 13.

Wakuu hapa nimechanganyikiwa naona kama naibiwa au wanajitisha nitoe rushwa.

Nimejaribu kugoogle napata maana nyingine hata kwa Tanzania na hakuna online calculator kwa Tanzania kujua nahitaji kulipa kiasi gani.

Wakuu Capital Gain Tax ni nini?

Mbona ni kubwa kiasi hiki? Ni afadhali tusingeuza nyumba. Tuibakize iwe ya urithi?
Chukua 80m toa gharama za kujengea hio nyumba, then 10% ya kile kinachosalia ndio capital gain tax, otherwise wanakuibia
 
Chukua 134m toa gharama za kujengea hio nyumba, then 10% ya kile kinachosalia ndio capital gain tax, otherwise wanakuibia
Hapana sio hivyo mkuu. Capital gain ni 10% ya net profit. Kwa mfano gharama halisi ya kununua nyumba ni 3,000,000 halafu ikauzwa kwa 4,000,000, faida yake ni 1,000,000. Capital gaini ni 1,000,000×10% = 100,000.
 
Ndio ipo hivyo Ndugu na hiyo haikwepeki, la sivyo hakuna transfer itafanyika...nimepita huko muda si mrefu.

Capital gain wao wanaitafsiri kama makato kutoka kwa ulichokipata (gain)....na ndio hiyo 10%.

Ninachokijua ni kuwa ukikaa nao chini wanaweza kupunguza ila si kihiivyo, wanaweza kukata hata hiyo tatu maana swala la valuation wakati mwingine halina uhalisia sana na linaweza kuathiriwa na utashi wa anayefanya hiyo valuation...na huwa ipo valuation ya TRA na ya Halmashauri/Manispaa.
 
Back
Top Bottom