Musundi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,583
- 2,600
Hivi hawa baadhi ya walimu wa shule za msingi wana matatizo gani hasa? Nimewaandikisha wanangu kuanza darasa la kwanza kwa miaka miwili tofauti. Wa kwanza nilipompeleka kumuandikisha mwalimu aliniomba nakala ya cheti chake cha kuzaliwa; nikampa. Miaka miwili baadaye nikampeleka kumwandikisha mwanangu wa pili; nikadaiwa pia nakala ya cheti cha kuzaliwa; nikampa.
Cha ajabu, yalipokuja kutoka matokeo ya mtihani wa Drs la 4 ya mwanangu wa kwanza, majina yalikuja yamekosewa. Sikuelewa.
Tatizo hilo hilo lilikuja kujitokeza tena kwa mwanangu wa pili, naye majina yalikosewa. Walimu wanajiandikia SPELLING wanazotaka bila kujali kinachosomeka kwenye Cheti cha kuzaliwa cha mtoto.
Hivi, tatizo la hawa viumbe ni nini? Wanaboa mno na kutuingiza wazazi na watoto katika matatizo hapo baadaye maana mpishano wa majina au spelling ni issue kubwa hasa zama hizi ambazo huduma nyingi hutolewa kwa kutumia mifumo ya computer.
Hivi nimemuandikisha wa tatu. Wakijichanganya tena, Wallah, naburuza jinga moja mahakamani!!