MASWALI KWA WAZIRI MKUU
Kabwe Zuberi Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Umma (Public Investments Accounts Committee).
24/07/2008
Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Mkataba wa Kulinda Makampuni ya Madini kutoka Kanada (FIPA) yaliyowekeza nchini Tanzania.
Mheshimiwa Spika, wa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Ripoti ya Kamati Kuhusu suala la Madini imewekwa wazi na itajadiliwa Bungeni.
Taarifa zilizochapwa katika Tovuti ya Idara ya Uwekezaji na Biashara ya Canada ambayo nimeipata kwa msaada wa Tovuti ya JamiiForums.com zinaoneshwa kuwa Tanzania ipo katika majadiliano na Serikali ya Canada ili kuingia Mkataba wa kulinda Makampuni ya Kanada yaliyowekeza Tanzania (Canada's Foreign Investment Promotion and Protection Agreements - FIPA). Tanzania imekubali kuharakisha mazungumzo hayo kabla Mapendekezo ya Taarifa ya Bomani hayajatungiwa sheria ili makampuni ya Kanada na hasa katika
sekta ya Madini na mengineyo yaendelee kufaidika na Utajiri wetu wa Madini. Serikali ya Tanzania haijatoa Taarifa kuhusu Mkataba huu kwa Umma ingawa majadiliano yanaendelea.
Kwa nini Serikali inakubali ku ‘undermine' Uhuru wa nchi yetu na kuingilia Mamlaka ya Bunge kwa kufanya majadiliano ya kulinda mikataba mibovu na wageni ilhali Ripoti ya Bomani ni suala la Bunge hivi sasa?
Mwisho.
Kuna NW mmoja wa serikali ya Kikwete aliwahi kwenda mbele ya Bunge akiwa na jibu la swali tofauti na lile aliloulizwa. Akalisoma almost lote kabla hajajua kwamba anajibu vitu tofauti na alivyoulizwa. Aliposhtuliwa ikamchukua mda mrefu sana akitafuta jibu la swali sahihi kwa aibu. Spika akaamua kumuokoa akamwambie akapumzike mpaka baadaye.
Kumbe ni tatizo la serikali nzima, kuanzia mtendaji mkuu wa serikali!
Kama hili ndilo swali, na kama Pinda alisema anaenda kupitia mitandao kwanza basi tuna matatizo makubwa kuliko nilivyodhani. Kwa sababu hata kama ni kupinda mambo kisiasa basi wangefanya kwa akili kidogo wakijua kwamba watanzania wa sasa ni tofauti na wale wa 1961.
Swali ni kwa nini serikali ina-undermine Uhuru wa nchi yetu...
Pinda ni mtendaji mkuu wa serikali. Anapaswa kujua (on top of his head) kama kuna mazungumzo yoyote au swala lolote linalo-undermine uhuru wa nchi na ajibu kwa kuwahakikishia watanzania kuwa hilo halipo au lipo na lina manufaa fulani ambalo hayako wazi na afafanue.
Lakini jibu la huyu Mheshimiwa ni kama vile aliulizwa je, serikali inachukua muda kupitia websites za FIPA na JF?
Majibu ya viongozi wetu yatueleza kitu kimoja tu: ni ya uongo. Uongo inabidi kila wakati upangwe. Uongo inabidi kila wakati utathminiwe ili msemaji asije akakutwa off-guard. Na uongo lazima kila wakati upimwe na uongo uliotangulia au utakaofuata kama vitaendana, ndio maana wanakuwa na tahadhari sana ya kujibu hata vitu ambavyo ni kama wimbo wa taifa.
Sio kweli hata kidogo kwamba serikali inaweza kuwa na makubaliano mazito kama hayo halafu Waziri Mkuu wa serikali hiyo hiyo hajui mpaka akasome website.