Canada and Tanzania to begin negotiations on FIPA

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Background on the Canada-Tanzania FIPA Negotiations:

Canada and Tanzania have agreed to begin negotiations towards a Foreign Investment Promotion and Protection Agreement (FIPA). The parties have pledged to work together to conclude an agreement in a timely manner.

A bilateral FIPA will provide greater predictability and certainty for Canadian investors considering investment opportunities in Tanzania, and will underscore Tanzania’s reliability as an investment destination. Canada’s objective in entering these negotiations is to secure a comprehensive, high-quality agreement which will protect investors through the establishment of a framework of legally binding rights and obligations.



Jamani, hii taarifa nimekutana nayo huku Canada jana (tarehe 21/07/2008), wenzetu wako kwenye negotiations za Mkataba wa Investment Promotion and Protection Agreement with the Government of Tanzania.

Wenzetu wao wameamua kuliweka wazi kabisa na kulitangaza hadi kwenye website yao ya serikali, (http://www.international.gc.ca/trad...iaux/agr-acc/fipa-apie/tanzania-tanzanie.aspx) Lakini cha kushangaza ni kwamba sisi huko kwetu najua hakuna mtu yoyote anayejua chochote kuhusu mkataba huu muhimu sana. Sitashangaa tukiona tunaletewa tena mkataba mwingine wa ajabu manake kama ilivyo kawaida mikataba hii serikali yetu huifanya ikawa ya siri sana.

Kama wamediriki kufanya lobbying for the sake of their companies sitashangaa wakatubamiza kwenye mkataba huu, tusipokua makini tunaweza tukawauzia nchi yote kabisa.

Kwa wale wabunge ambao wapo humu ndani ya JF (Dr. Slaa na Zito na wengine) nawaomba mjaribu kulipigia kelele hili swala, tunaomba serikali watoe official statement kuhusu mkataba huu muhimu, wenzetu wao wametoa press statement na huu mkataba sio siri kwao, wananchi wao wametaarifiwa vizuri kabisaa.

Pia tunaomba kujua ni nani wanaoliwakilisha Taifa kwenye hizo negotiations za huu mkataba muhimu sana kwa Taifa. Tusije "tukadanganyika" kama ilivozoeleka.
[/SIZE][/COLOR]
 
Last edited by a moderator:
Mkuu muhafidhina mbona unachokonoa siri za serikali???????? LOL. Thanks for the info
 
Background on the Canada-Tanzania FIPA Negotiations:

Canada and Tanzania have agreed to begin negotiations towards a Foreign Investment Promotion and Protection Agreement (FIPA). The parties have pledged to work together to conclude an agreement in a timely manner.

A bilateral FIPA will provide greater predictability and certainty for Canadian investors considering investment opportunities in Tanzania, and will underscore Tanzania's reliability as an investment destination. Canada's objective in entering these negotiations is to secure a comprehensive, high-quality agreement which will protect investors through the establishment of a framework of legally binding rights and obligations.


Jamani, hii taarifa nimekutana nayo huku Canada jana (tarehe 21/07/200, wenzetu wako kwenye negotiations za Mkataba wa Investment Promotion and Protection Agreement with the Government of Tanzania.

Wenzetu wao wameamua kuliweka wazi kabisa na kulitangaza hadi kwenye website yao ya serikali, (http://www.international.gc.ca/trad...iaux/agr-acc/fipa-apie/tanzania-tanzanie.aspx) Lakini cha kushangaza ni kwamba sisi huko kwetu najua hakuna mtu yoyote anayejua chochote kuhusu mkataba huu muhimu sana. Sitashangaa tukiona tunaletewa tena mkataba mwingine wa ajabu manake kama ilivyo kawaida mikataba hii serikali yetu huifanya ikawa ya siri sana.

Kama wamediriki kufanya lobbying for the sake of their companies sitashangaa wakatubamiza kwenye mkataba huu, tusipokua makini tunaweza tukawauzia nchi yote kabisa.

Kwa wale wabunge ambao wapo humu ndani ya JF (Dr. Slaa na Zito na wengine) nawaomba mjaribu kulipigia kelele hili swala, tunaomba serikali watoe official statement kuhusu mkataba huu muhimu, wenzetu wao wametoa press statement na huu mkataba sio siri kwao, wananchi wao wametaarifiwa vizuri kabisaa.

Pia tunaomba kujua ni nani wanaoliwakilisha Taifa kwenye hizo negotiations za huu mkataba muhimu sana kwa Taifa. Tusije "tukadanganyika" kama ilivozoeleka.
[/size][/color]

Mhafidhina habari hii ni ya muhimu sana na haina budi kufuatiliwa!

Kwani huu mkataba mpya unaonekana ni wa kutufanya tushindwe kuvunja mikataba ya zamani.

KUWENI MAKINI WABONGO..!

Mkataba huo ukisainiwa basi HAKI HAITAKUWEPO NA DAMU ITANMWAGIKA.

Kwasababu hizi ni mbinu za kuilinda mikataba mibovu kwa kigezo cha sheria mpya ama mkataba mpya wa kulinda mikataba ya zamani isivunjwe na bunge letu.
Wacanada kuretreat kumbe ni kupanga mbinu ya kutumalizia mbali..Kwani mkataba huu ukisainiwa basi nguvu ya jeshi itatumika kutunyanyasa wananchi.
Yangu macho.
 
Canada's objective in entering these negotiations is to secure a comprehensive, high-quality agreement which will protect investors through the establishment of a framework of legally binding rights and obligations.

Tunataka legally binding obligations towards people's development.

Na hivyo mapendekezo ya kamati ya madini ndiyo ya kupewa kipaumbele.
 
Wana JF pamoja na watanzania kwa ujumla tunaomba mutumie contacts hizo hapo chini ili wa canada hao waulizwe kama mapendekezo ya kamati ya madini ya watanzania nayo yazingatiwe kwenye majadiliano hayo ya serikali za Canada na Tanzania yenye kuhusu kulinda mikataba ya wawekezaji kutoka Canada.Kwani kimtizamo inaonyesha wanataka kututingishia kiberiti ili kututisha na kutunyima haki zetu!




<H3>Contact Point
If you have questions or comments about this initiative, we would like to hear from you. Please contact:
Investment Trade Policy Division (TBI)
Department of Foreign Affairs and International Trade
Lester B. Pearson Building
125 promenade Sussex Drive
Ottawa, Ontario, K1A 0G2
Fax: 613-944-0757
E-mail: consultations@international.gc.ca
</H3>
 
Hakuna umuhimu wowote wa kusaini mkataba kama huu. Watanzania ni huru kama tunaona mkataba hauna maslahi kwa nchi yetu basi tuwe huru kuuvunja bila kumuogopa yoyote.
 
Jamani naomba huu mkataba ufuatiliwe kwa ukaribu, hii ndio ile mikataba tunayoingia kimya kimya halafu tunakuja kuweka mikono kichwani na kuishia kulalamika. Kama Kuna mtu yoyote anayeweza kufuatilia mkataba huu tafadhali naomba alifuatilie kwa manufaa ya watanzania wengine.

lasivyo hapo najua tu lazma tuingizwe mkenge tu, na tutaishia kuwauzia nchi sasa...!

Please naomba tulifiatilie kwa ukaribu sana JAMANI
 
Jamani naomba huu mkataba ufuatiliwe kwa ukaribu, hii ndio ile mikataba tunayoingia kimya kimya halafu tunakuja kuweka mikono kichwani na kuishia kulalamika. Kama Kuna mtu yoyote anayeweza kufuatilia mkataba huu tafadhali naomba alifuatilie kwa manufaa ya watanzania wengine.

lasivyo hapo najua tu lazma tuingizwe mkenge tu, na tutaishia kuwauzia nchi sasa...!

Please naomba tulifiatilie kwa ukaribu sana JAMANI

Unachosema ni kweli kabisa labda ndiyo maana yule Balozi wa Canada alikuwa Bungeni Dodoma hivi karibuni kuanza ufuatiliaji wa kuhakikisha mkataba huu unasainiwa na hivyo mkataba uliosainiwa na Barrick kuhusu uchimbaji wa dhahabu na madini mengine usiguswe tena. Watanzania kamwe tusikubali kusaini mkataba huu itakuwa ni kuuza haki yetu na kuwaachia wageni na mafisadi waendelee kutupora utajiri wetu wa mali asili tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu. Wakati wao wako tayari kulinda maslahi ya kampuni yao na shareholders wao, sisi hakuna yeyote sirikalini anayejali ili kuhakikisha maslahi ya Tanzania na Watanzania yanalindwa
 
Huo mkataba ni bomu jingine linatengenezwa tena kwa haraka. Chonde chonde wabunge makini (Zitto/Slaa et al) hakikisheni hii kitu haikatizi kwa kuitahadharisha na kuionya serikali kuacha hizi underground moves za kuliangamiza taifa letu.
 
duh! kweli nimeamini kuna siku mtu unaweza kulala na kuamka ukakuta nchi ishauzwa yote na wewe huna habari.

kwa nini serikali yetu inapenda kuficha ficha?

tunataka serikali ituambie mktaba huo una maudhui gani?
 
Tanzania na Canada zaanza mjadala wa kulinda Uwekezaji wa Wakanada
KLH News

Serikali ya Canada imeanza mchakato wa mazungumzo ya kuingia makubaliano na serikali ya Tanznia ili hatimaye serikali hizo mbili ziingie kwenye Mkataba wa Kupromoti na Kulinda Uwekezaji wa Kigeni ili wafanyabiashara na wawekezaji wa kigeni kutoka Canada waweze kuwa na utaratibu wa kisheria unaoongoza na kulinda mitaji na miradi yao nchini.

Mazungumzo hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa miezi kadhaa sasa haijulikani ni lini yatakamilika na kuanza kutekelezwa na ni kwa kiasi gani Bunge letu ambalo linajukumu la kutoa baraka zake kwenye mikataba ya serikali linahusika.

Mkataba huo wa Kupromoti na Kulinda Uwekezaji wa Kigeni ujulikanao kwa kiingereza kama "Foreign Investment Promotion and Protection Agreement" (FIPA) utakuwa ni mkataba wa pili kuingiwa na serikali ya Canada na nchi ya Kiafrika. Mkataba kama huo uliingiwa kati ya Canada na Afrika ya Kusini mwaka 1995, ingawa bado haujaanza kufanya kazi.

Kwa mujibu wa taarifa za Taasisi ya Mambo ya Nje na Biashara ya Canada, makubaliano ya FIPA yana malengo makubwa ya kumlinda mfanyabiashara au shirika la Kikanada linapofanya biashara katika nchi ya kigeni. Kwa mujibu wa taasisi hiyo "Makubaliano ya FIPA yanamhakikishia mwekezaji wa Kikanada kuwa atakuwa na nafasi sawa ya ushindani katika biashara sawa sawa na washindani wengine wa nje au wa ndani ya nchi husika".

Kwa maneno mengine endapo Mkataba kama huu utaingiwa basi wawekezaji wetu wazalendo watapaswa kushindana na Taifa kubwa na wafanyabiashara wakubwa wa Kikanada kana kwamba wako sawasawa kwa mitaji, uzoefu, raslimali na uwezo.

Zaidi ya yote makubaliano ya FIPA yanahakikisha kuwa unapotokea mzozo wa kibiashara mahakama za ndani zinawekwa pembeni na zaidi kukimbilia kwenye mahakama za kimataifa. Kwa uamuzi kama huo mahakama hizo nyingi za Kimataifa ziko tayari kwenye nchi za magharibi na mara nyingi zimekuwa zikitetea na kusimama upande wa nchi za Kibepari za Magharibi. Kwa kukwepa kutumia mahakama na sheria zetu, mkataba wa FIPA unaweza kabisa kutuingiza katika wavu wa kisheria kama uliotukuta wakati wa mkataba wa IPTL.

Endapo mkataba wa FIPA utaingiwa siyo tu utaifunga serikali kuu bali pia utafunga kwa masharti hayo hayo tawala za mikoa na serikali za mitaa.

Siku chache zilizopita tovuti hii na vyombo vingine vya habari kufunua habari za kushindwa kwa kampuni ya Barrick toka Canada kuwashawishi wabunge wa Muungano kutokukubali mapendekezo ya Kamati ya Bomani iliyoundwa kutoa ushauri kuhusu sekta ya madini.

Kampuni hiyo ikipigwa tafu na Balozi wa Kanada nchini ilijitahidi kwa karibu wiki nzima kuwashawishi wabunge mbalimbali kubadili misimamo yao ili hatimaye baadhi ya mapendekezo ambayo yanaigusa kampuni hiyo yasipokelewe. Hata hivyo baada ya kushindwa katika kujipigia debe, njia ambayo sasa inataka kutumiwa ni ile ambayo kimsingi itaifunga Tanzania katika makubalianao ambayo itakuwa ni vigumu sana kujitoa hapo baadaye.

Tunaendelea kufuatilia ili kujua kwa undani ni jinsi gani makubaliano haya yatakapoingiwa yataathiri uwekezaji wa kampuni za Kanada hasa katika sekta ya madini. Unaweza kusoma na kujifunza zaidi kuhusu FIPA kupitia hapa: http://www.international.gc.ca
 
kama kuuza nchi , nkapa kesha iuza, ndio maana alipewa degree ya heshima huko kanada, wanacho taka sasa ni kutufunga maisha na hiyo mikataba.
 
Nimejaribu kufuatilia kwa karibu na kubaini kwamba, wa-Canada wanaukimbiza haraka kweli huu mkataba usainiwe. Lengo lao hapo ni haya madini na tayari wameshafanya survey wakagundua kuna uwezekano wa kupata mafuta Tanzania, sasa wanachokifanya ni kuingia huu mkataba ili kuhakikisha watakapokuja kuwekeza hawapati tena mizengwe kama kwenye madini (dhahabu).

By the way, mkataba unaondoa nguvu ya sheria zetu kutumika endapo kutakua na mgogoro kati ya nchi hizi mbili kuhusiana na mkataba hu, kwa hio kitakachotumika ni vipengele vya mkataba huo mabavyo vimesukwa kitaalamu sana kuhakikisha Tanzania hatupati kitu.

Chonde chonde jamani bado nalipigia kelele hili swala, tusiliache likapita hivi hivi, naomba tulipigie makelele kila mahali, tunauza nchi hivi hivi...!
 
Namshangaa sana mtu anaesema kwamba hii ni siri ya serikali.

Huu mkataba utafuatiliwa na utajulikana na hata tuue ni wa muda gani kwani uzoefu wa kusoma habari unaonesha kwamba mikataba hii huwa ni ya miaka zaidi ya 30!

Yaani watu watakuwa wanaiba rasilimali za taifa kwa miaka hio 30!
 
manaowajua wabunge, please wasilianeni nao na waliongee hili Bungeni na kutahadharisha wabunge wengine na waulize nani anaiwakilisha Tanzania? na kwa nini mpaka sasahivi hatuambiwi chochote upande wa tanzania?.
 
Kwa mwanachama mtiifu nafurahi leo jamii forums imetinga bungeni kupitia swali la Zitto Kabwe kwa Waziri Mkuu Pinda. Kwa kuwa Pinda amehidi kwamba kabla ya kujibu swali hilo atapitia mitandao tajwa. Basi natarajia kwamba pamoja na kupitia mtandao wa Canada, atapitia pia Jamii Forums. Hivyo ni wakati wa kutoa maoni yetu ya kina kuhusu suala hilo ambalo lilishaanza kujadiliwa hapa tayari

JJ
 
Mnyika lakini hiyo post yako iko lose kidogo. Would you mind kama utatuhabarisha zaidi. Lakini pia kama una matarajio yoyote kutoka kwa PM sahau, huyu jamaa tulimtegemea sana kuwa ataleta discpline na heshima ya serikali lakini for some reasona inaonekana hakuna lolote analofanya zaidi ya kuzungumza.
 
Kwa mwanachama mtiifu nafurahi leo jamii forums imetinga bungeni kupitia swali la Zitto Kabwe kwa Waziri Mkuu Pinda. Kwa kuwa Pinda amehidi kwamba kabla ya kujibu swali hilo atapitia mitandao tajwa. Basi natarajia kwamba pamoja na kupitia mtandao wa Canada, atapitia pia Jamii Forums. Hivyo ni wakati wa kutoa maoni yetu ya kina kuhusu suala hilo ambalo lilishaanza kujadiliwa hapa tayari

JJ

John hebu kuwa muwazi kidogo mana si wote tunaweza kuangalia. Swali na msingi au nyongeza na lilikuwa linaulizwa kwa minajili ipi?

Asante
 
jAMAAA AMESHAKUWA MWANASIAASAA..BADALA KUWA MTENDAJI..............PINDA HANA JIPYA.....
 
We need to stop being TOTAL PESSAMIST.Lets give ourselves some hope of surviving in the ocean full of sharks (Mafisadi). JJ is only bring to the attention of those who are not able to watch live the Q & A session of the PM this morning from 9.00am to 9.30 am .
 
Back
Top Bottom