Can IPTL save us? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Can IPTL save us?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 22, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  IPTL kuwasha mitambo mwezi ujao

  Imeandikwa na Lucy Lyatuu;
  22nd October 2009

  Habari leo


  WAWEKEZAJI wa mitambo wa kuzalisha umeme wa IPTL wametii agizo la Rais Jakaya Kikwete, wameahidi kuiwasha mitambo hiyo ifikapo Novemba Mosi.

  Aidha, wamesema kwa sasa wanasubiri kukamilika kwa mazungumzo yatakayotoa mwelekeo wa gharama halisi za uendeshaji.

  Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Kaimu Meneja wa Operesheni wa IPTL, Gilbert Ndesamburo, wakati Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alipofanya ziara katika mitambo hiyo.

  Ndesamburo alisema, kwa sasa vikao vinaendelea baina ya msimamizi wa muda wa IPTL, Serikali na wahusika kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kujua gharama halisi za kuendesha mtambo huo pamoja na kupata mafuta mazito yanayotakiwa.

  “Hadi Novemba lazima mtambo huo uanze kufanya kazi kwa kuwa sasa mazungumzo yanayofanyika ni pamoja na kujua mafuta yatapatikana wapi,” alisema Ndesamburo.

  Kuhusu hali ya mtambo, alisema uzalishaji wake unahitaji kujua Tanesco wanahitaji kiasi gani cha umeme kwa saa ambapo wanatumia mashine za Wartsila zilizofungwa mwaka 1998.

  Alisema mashine moja ina uwezo wa kutoa megawati 10 na sasa ziko 10 na kwa uzalishaji wa kawaida wa mashine zote wanaweza kutumia tani 500 za mafuta ambazo ni sawa na lita 500,000.

  Aliongeza kuwa tangi moja lina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 500 na sasa mafuta hayo lita moja huuzwa kwa wastani wa Sh. 1,200.

  Kwa upande wake, Ngeleja alisema kinachofanyika sasa ni ufuatiliaji wa maelekezo ya Rais, ambapo vikao vinaendelea ili kujua uwashaji utachukua siku ngapi, jinsi ya kupata mafuta ili Waziri wa Fedha na Uchumi aweze kutoa fungu hilo na siku ambazo zinahitajika.

  “Pamoja na hayo yote hadi Novemba mosi mwaka huu mtambo huo utawashwa na utatoa megawati 100 zitakazoondoa kabisa mgawo wa umeme kwa kuwa kituo cha Tegeta cha megawati 45 nacho kitakamilika na Songas wenye uwezo wa megawati 20 utakamilika leo,” alisema Ngeleja.

  Alisema katika kikao hicho watafanya utaratibu wa mpito ambao hautaathiri haki na madai ya wahusika wa IPTL, kwa kuwa hawana uhakika kesi itakwisha lini na pia msimamizi wa muda wa mtambo huo aweze kusimamia kwa kuzingatia hali ya giza lililopo na Novemba tatizo litakwisha kabisa.

  Kuhusu mtambo wa Tegeta, Ngeleja alisema kila kitu kimeshakamilika na kilichobaki ni kukamilisha uunganishaji kwenye gridi ya Taifa.

  Alisema kituo hicho kinatakiwa kufanya kazi mchana na usiku ili kuhakikisha kuwa mtambo huo unakamilika ili kuiondoa nchi katika giza.

  “Tutazidi kufuatilia kwa karibu katika mitambo mingine ili kwamba dharura hii ya tatizo la umeme tuweze kuondokana nayo kabisa,” alisema Ngeleja.

  Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Kituo cha Tegeta, Norbert Ntimba, alisema awali walikuwa wanatarajia kukamilisha mtambo huo Oktoba 15, lakini kutokana na kucheleweshwa kutolewa kwa vifaa kutoka bandarini, ndiyo hali iliyosababisha.

  Hata hivyo alisema hadi sasa kila kitu kimekamilika na mafundi wanaendelea na kazi ambapo mwanzoni mwa Novemba utakamilika. Alisema mtambo huo unagharimu euro milioni 33 sawa na zaidi ya Sh bilioni 50 hadi kukamilika kwake na kwamba vifaa vyote vinatoka Finland.

   
 2. M

  Mong'oo Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good news
   
 3. M

  Mchili JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi Waziri hawezi kufanya kitu mpaka asubiri raisi aseme? Kweli ukimya wa JK unatunyima mengi.
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  lakini lita 500,000 za mafuta amazo ni 600,000,000/= kwa siku wajameni huu si ni msalaba mwingine kwa serikali ati??
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  This Day


  Independent Power Tanzania Limited (IPTL), which has long been tangled in a complex web of corruption and legal manoeuvring, has now been thrown back into the spotlight as the government desperately seeks a solution for the country’s latest and ongoing power crisis.

  The power plant based in Tegeta on the outskirts of Dar es Salaam has an installed capacity of 100 megawatts, and could immediately end the ongoing rolling blackouts if its thermal-powered turbines are switched on.

  Tanzania’s national grid currently has an 80-megawatt (MW) power shortfall, a situation that now appears to have forced the government to turn to the highly controversial IPTL project as a stop-gap measure to end the crippling load shedding.

  According to a statement issued by State House on Wednesday night, President Jakaya Kikwete has instructed government officials to work towards buying power from the privately-owned IPTL power plant, which is presently lying idle.

  This is notwithstanding the fact that IPTL, a joint venture project between Malaysian investors and a local company, is currently involved in protracted legal disputes on two different fronts - both externally and internally.

  On one hand, the company has unresolved legal issues with the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) regarding payment of capacity charges; and on the other hand, the firm is also embroiled in a long-running dispute between its shareholders.

  The High Court in Dar es Salaam recently put IPTL under receivership following a successful application by its local shareholder, VIP Engineering and Marketing of Tanzania (VIPEM), which owns a 30 per cent stake in the power company.

  VIP Engineering is owned by prominent Dar es Salaam-based businessman James Rugemalira.

  Mechmar Corporation of Malaysia, with a 70 per cent stake, is the majority shareholder in IPTL and is challenging the planned liquidation of the joint venture company.

  But despite being involved in a court case to wind up its operations, IPTL is still in a position to provide a short-term fix to the current national power crisis, according to State House.

  President Kikwete has already directed the ministries of energy and minerals, finance and economic affairs, and justice and constitutional affairs, to ensure that this plan is implemented immediately and IPTL power is injected into the national power grid as soon as possible.

  And according to Energy and Minerals Minister William Ngeleja who yesterday made an impromptu tour of the virtually-deserted IPTL Tegeta plant, this could be within a few weeks time - latest end-November.

  As the government now turns to IPTL as the anointed saviour of the nation’s power woes, here is a synopsis of how the dubious project was hatched, resisted, and eventually commissioned under a cloud of apparent corruption and major bribery:

  The origins of IPTL can be traced way back to 1992, when Tanzania started to experience extensive power rationing caused by a period of prolonged drought.

  In 1994, drought led to power shortages as TANESCO’s hydro catchment areas ran dry. The state power utility then invited private investor companies to provide emergency solutions.

  Seizing this opportunity, IPTL was formed in the same year (1994) as a joint venture project between Malaysian and Tanzanian investors.

  In May/June 1995, IPTL signed a 20-year power purchasing agreement (PPA) with the government to build and run a 100MW, slow-speed diesel (SSD) power plant at a cost of $163.5 million.

  The project, involving as it did Malaysian and Tanzanian investors working together, was initially hailed as a model for South-South cooperation. But widespread allegations of grand corruption and bribery soon surfaced over how the project was finally approved to go ahead.

  The founder president, Mwalimu Julius Nyerere, was once quoted as saying about IPTL: ”If this is ’South-South co-operation,’ then colonialism is preferable.”

  A damning report by the local chapter of Transparency International described the IPTL project as a ”Malaysian investment that may bleed Tanzania of hundreds of millions of dollars in bloated payments for electricity that the country neither needs nor can afford...”

  The widely-circulated Transparency International report gives explicit details on how bribes were allegedly paid to senior government officials to approve the IPTL project.

  The report says the then permanent secretary in the Ministry of Energy and Minerals, Patrick Rutabanzibwa, fiercely opposed the IPTL project for its obvious flaws, but was overruled by higher level government officials.

  Rutabanzibwa, a veteran senior civil servant, is now PS in the Ministry of Lands and Human Settlements Development.

  The Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) is said to have at one point launched an investigation into the corruption allegations surrounding the IPTL deal. But it remains unclear why no criminal charges were ever filed against known suspects.

  It emerged that between February 1995 and January 1996, IPTL negotiated with Watsila manufacturer of diesel and gas power turbines, to build and install a cheaper, medium-speed diesel (MSD) plant at the Tegeta site.

  In November 1998, TANESCO sought arbitration at the International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID), after IPTL failed to justify the project’s cost structure and payments, which were used to determine the monthly capacity charges and power tariffs.

  The London-based ICSID ruled in February 2001 that IPTL was overpriced by $23.5 million, but also that the contract still stands apparently because TANESCO was aware of the switch from SSD to MSD power turbines.

  TANESCO later discovered that IPTL’s equity in the multi-million dollar project had always been just 50,000/- (fifty thousand Tanzanian shillings only), and was never increased to $38.16 million (approx. 50bn/-) as agreed by the two parties.

  In the first four years of operation, TANESCO paid IPTL a staggering 159.5bn/- in capacity charges alone. On top of this, TANESCO also paid IPTL billions of shillings for its unusually high power tariffs.

  While TANESCO sells power to its customers for around 80/- per kilowatt hour (kw/h), the power utility paid IPTL 150.23/- per kw/h.

  There have been various attempts by the government to convert IPTL’s power turbines from diesel to natural gas, while moves for the state to buy the power plant outright have also been muted in the past.

  It remains to be seen how the government can get around the complex legal wrangles surrounding IPTL, and eventually put its currently-idle 100MW capacity to effective use in ending the latest power crisis to hit Tanzania as a whole.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  TANZANIA'S POWER CRISIS:  Corruption and bribery in public contracting and procurement, coupled with the systematic mismanagement of the nation's energy sector by senior government officials over a long period of time, are some of the main causes of the ongoing power crisis in Tanzania, THISDAY can reveal today.

  The country is currently in the midst of yet another series of rolling blackouts, just a few months after the government publicly declared that the nation will not face power rationing come what may.

  The Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, assured Tanzanians at a news conference in his office in Dar es Salaam on March 13 this year that there would be no power shedding this year.

  Ngeleja's assurance came in the wake of a wave of public outrage caused by a brazen announcement by Dr Idris Rashidi, managing director of the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), that the nation would be plunged into darkness because plans to buy second-hand power generators from the controversial Dowans Tanzania Limited company had been rejected.

  The TANESCO chief's 'threat' appeared to have come of age when the power utility abruptly announced the latest rolling blackouts earlier this month.

  And after appearing before the parliamentary energy and minerals committee in Dar es Salaam this week at the height of the ongoing power rationing, minister Ngeleja said he was now not even sure when the blackouts would end.

  That remark is in sharp contrast to his assertion in March that the country would not be hit by blackouts at all.

  The droning of generators on the streets and inside buildings are becoming a familiar sound in Dar es Salaam and elsewhere across the country.

  The lack of power has paralyzed a lot of normal activity, with dead traffic lights exacerbating traffic jams and services in hospitals, schools and various businesses grinding to a halt - just as the TANESCO boss 'predicted.'

  The owner of a five-star hotel in Dar es Salaam told THISDAY recently that the hotel spends more than $1,000 (approx. 1.3m/-) each day on diesel for emergency power generators during the ongoing power rationing.

  Thousands of small businesses, including secretarial bureaux and hair salons, are also suffering heavily from lost incomes.

  Looking at the bigger picture, Tanzania's national economic output is believed to be losing billions of shillings per day due to power outages.

  Government officials say the power crisis is far from over. TANESCO expects rolling blackouts to continue until it can increase its own power supply or buy more power from outside sources - independent power producers.

  There has been a lot of finger-pointing going on as to exactly who is responsible for this latest bout of 14-hour daily load shedding.

  Energy experts define a rolling blackout, also referred to as load shedding, as an intentionally-engineered electrical power outage. Such blackouts are a last-resort measure used by electric utility companies to avoid a total blackout of the power system.

  They are usually in response to situations where the demand for electricity exceeds the power supply capability of the network.

  Rolling blackouts have now become a staple in Tanzania. According to TANESCO, the latest power crisis was primary caused by two major factors - a prolonged drought that has depleted water levels at hydro-power stations, and more power plants than usual being out of service for a variety of reasons.

  Investigations by THISDAY show that the energy crisis now gripping the nation has been building up for years.

  TANESCO has suffered from systematic mismanagement over the years by successive Tanzanian management teams, NetGroup Solutions of South Africa, and political interferrence.

  As a result, the state-run power utility has entered into dubious power purchase agreements with several private companies, and has been paying billions of shillings in monthly capacity charges to them.

  They include Songas (6.8bn/-), Independent Power Tanzania Limited (3.67bn/-), Dowans ($3.644m), Alstom ($1.752m), and Aggreko ($1.485m).

  Some of these power purchase agreements, including the one with Dowans, recently expired but TANESCO still remains with massive liabilities, haemorrhaging money at an alarming rate.

  For example, the company's total turnover in 2003 was over 165bn/-, yet it incurred a loss before tax of a staggering 222bn/-.

  Similarly in 2004, TANESCO's total revenues amounted to more than 188bn/-, but the company posted a loss of over 62bn/-.

  The trend has repeated itself over the years to the point that the power utility is now one of the most heavily indebted state-owned companies.

  The staggering amounts paid each month as capacity charges and energy charges to Songas, IPTL, Dowans and others have left TANESCO virtually cash-strapped and unable to expand or even conduct proper maintenance of it's own hydro-power stations.

  At the same time, TANESCO has also apparently lacked the resources to develop new power generation sources in Tanzania from the amply available national energy resources.

  TOMORROW: An in-depth look at individual power purchase agreements in Tanzania and how they contributed to the current situation.

   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  The only problem is the fact they have oil machine instead of gas machine and oil machine cost more to run.
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  How can it save us when it was meant to stifle us!
   
 9. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mmnhhh mwizi anapogeuka kuwa mwokozi wako!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  ONLY FOUND IN TANZANIA !!!!!!!!
   
 10. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Maana yake ni kwamba Bei ya Umeme itaongezeka.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  It is obvious that solution to Tanzania's power blues is beyond IPTL. Hapa tunatapatapa tu
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Sasa ulitaka umeme ushuke kama chakula cha wana waIsrael wakitoka utumwani Misri?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  Date::10/22/2009Umeme wa IPTL kuigharimu serikali Sh 23 bilioni kwa mwezi


  [​IMG]
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye amewahakikishia watanzania kuwa sakata la mgao wa umeme litamalizika Novemba mwaka huu

  *KUWASHWA NOVEMBA MOSI, MKULO ASEMA FEDHA IKO

  Sadick Mtulya na Exuper Kachenje

  WAKATI mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) inatarajiwa kuwashwa Novemba mosi mwaka huu, uendeshaji wake utaigharimu serikali Sh23 bilioni kila mwezi.

  Juzi, Rais Jakaya Kikwete aliagiza kuwashwa mara moja kwa mitambo inayotumia mafuta baada ya nchi kuingia gizani kutokana na kuharibika kwa mitambo ya Songas na Kihansi na kufanya gridi ya taifa ipungukiwe megawati 80 za umeme.

  Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais iliziagiza Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Katiba na Sheria na Shirika la Umeme (Tanesco) kufanya kazi kila moja kwa nafasi yake kuhakikisha mitambo inawashwa.

  Kaimu Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Wartsila, Gilbert Ndesamburo aliwaambia waandishi akiwa pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa mitambo hiyo, ambayo ilizimwa miaka miwili iliyopita, ikiwashwa kwa saa 24 hutumia mafuta lita 625,000 yanayouzwa lita moja kwa Sh 1,200.

  Kiwango hicho kinaifanya serikali kulazimika kutumia zaidi ya Sh23 bilioni kuendesha mitambo hiyo hadi itakapofikia mwishoni mwa mwezi Novemba.

  Ndesamburo alisema kwa sasa Wartsila na Tanesco wapo katika kikao cha kujadili gharama za mafuta yatakayotumika kuzalishia umeme pamoja na siku zitakazotumika kuipasha mitambo hiyo kwa ajili ya kuiweka tayari.

  "Hii mitambo haiwashwi ovyo ovyo, inawashwa kwa kufuata taratibu maalumu na sasa tupo katika kikao na Tanesco kujadili gharama za mafuta yatakayohitajika kuendeshea mitambo hii pamoja na kujua tutumie siku ngapi kuipasha mitambo," alisema Ndesamburo.

  Ndesamburo alisema kituo hicho kina uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa wastani wa tani 15,000 sawa na zaidi ya lita milioni 15.

  Mitambo hiyo, ambayo ipo kumi na yenye uwezo wa kila mmoja kutoa megawati 10, ilifungwa nchini mwaka 1998. Alisema mitambo hiyo ipo tayari kwa ajili ya kutoa megawati 100.

  "Hii mitambo haina tatizo lolote, hapa unapoiona ipo salama na ukiweka mafuta inafanya kazi," alisema Ndesamburo.

  Ndesamburo alifafanua kuwa mitambo hiyo inayotumia mafuta mazito(HFO), ikiwashwa kwa ajili ya kutoa megawati 100 hutumia mafuta tani 500 sawa na lita 500,000.

  IPTL na Tanesco wako kwenye mgogoro wa kisheria na tayari kampuni hiyo binafsi ya kuzalisha umeme imefungua kesi jijini New York ikidai fidia kutokana na kutolipwa fedha zake za kuzalisha umeme uliouzwa kwa Tanesco.

  Serikali ilikuwa imeagiza mitambo hiyo ibadilishwe iwe inatumia gesi asilia kuiendesha, ili kupunguza gharama za uzalishaji, lakini Wizara ya Nishati na Madini ikasimamisha mchakato huo kusubiri kumalizika kwa kesi hiyo.

  Katikati ya mwaka huu Rais Kikwete aliagiza mchakato huo wa kubadili mitambo uendelee badala ya kusubiri kesi hiyo kumalizika.

  Naye Waziri Ngeleja alisema mgawo wa umeme unaolikabili taifa hivi sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Novemba mwaka huu.

  Alisema kuwa kuisha kwa mgawo huo kunatokana na kupatikana kwa megawati 100 kutoka katika mitambo ya IPTL, megawati 45 kutoka katika kituo cha Tegeta pamoja na megawati 40 kutokana mtambo wa Songas.

  Hata hivyo, alisema uendeshaji wa mitambo ya IPTL utaendeshwa na kampuni kandarasi ya Wartsila, ambayo iliingia mkataba wa miaka miwili na serikali, kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

  Alisema wakati Wartsila watakapokuwa wakiendesha mitambo hiyo, wamiliki wa IPTL hawatalipwa chochote na serikali.

  "Mitambo ya IPTL ya megawati 100 itawashwa Novemba mosi mwaka huu, sambamba na kuingizwa kwa megawati 45 za kituo cha Tegeta katika gridi ya taifa tarehe hiyo hiyo na kesho tunatarajia kupata megawati 20 kutoka Songas.

  Hivyo Tunatarajia mgawo huu wa umeme utamalizika mwishoni mwa Novemba mwaka huu," alisema Waziri Ngeleja.

  "Pia tumekubaliana kuwa mitambo hii itaendeshwa na kampuni kandarasi ya Wartsila na serikali haitawalipa chochote wamiliki wa hii mitambo ya IPTL bali itagharamia ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo hii."

  Waziri Ngeleja alisema pamoja na mambo mengine kuhusu matatizo ya umeme mkakati wa serikali ni kuendelea kuhakikisha na kufuatilia mitambo iliyoharibika inakarabatiwa na kurudi katika hali yake ya uzalishaji.

  Waziri huyo alifafanua kwamba pamoja na kufikiwa kwa makubaliano ya kuwashwa kwa mitambo hiyo serikali imedhamiria kuinunua au kugawana mali na IPTL.

  "Pamoja na yote hayo msimamo wa serikali ni kuinunua hii mitambo au kugawana mali na wamiliki wa IPTL," alisema Ngeleja.

  Mwaka 2006 nchi iliingia gizani wakati kulipotokea ukame mkubwa na kusababisha serikali kutafuta suluhisho la haraka ambalo lilisababisha ijikute ikiangukia kwenye kashfa ya Richmond.

  Tangu wakati huo serikali imekuwa ikihaha kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo ya umeme, lakini imejikuta ikilazimika tena kutafuta suluhisho la dharura baada ya mitambo ya Kihansi na Songas kuharibika.

  Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo amesema kuwa wizara yake iko tayari kutekeleza maagizo ya rais ya kutaka mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL iwashwe "mara moja" na wanachosubiri kwa sasa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tanesco ni kuwasilisha mchanganuo wa mahitaji.

  Waziri Mkulo alisema wizara yake imeshajipanga na kwamba wanachosubiri sasa ni mchanganuo wa mahitaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na William Ngeleja na Tanesco.

  Alisema wizara yake na nyingine zimeambiwa kutekeleza hilo na kwamba kimsingi mambo yote yanakwenda vizuri, ikiwemo uhakika wa fedha za kununulia mafuta yakiwa chini ya uangalizi.

  "Mawaziri tumeshaambiwa na kila mtu kakabidhiwa kazi yake, rais kaamua... na mimi kama Waziri wa Fedha nitatekeleza kama maagizo niliyopewa," alisema Mkulo.

  Alisema suala la fedha ni suala lake na wizara yake inaweza kutoa fedha au udhamini kwa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tanesco ili kununua mafuta na kuwezesha utekelezaji wa agizo la rais, ili kuwapunguzia wananchi adha ya mgawo wa umeme.

  "Tumeshaanza kutekeleza; 'no comment'... ni uamuzi tumeambiwa tuutekeleze. Fedha tunaweza kuwapa 'guarantee'(udhamini) au kukopa."

  Kuhusu mafuta Mkulo alisema kinachosubiriwa ni Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco kupeleka mchanganuo wa mahitaji ya fedha nao wahakikishe inapatikana.

  "Tumejadili kwa kina 'everything' (kila kitu)," alisema na kuongeza: "Tumewaachia Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco wachambue fedha inayotakiwa na walete kwetu, ili tuhakikishe fedha inapatikana."

  "Nitatekeleza maagizo ya rais; nakuhakikishia mipango yote kwangu ipo kamili na nitatekeleza ili kuhakikisha mitambo ya IPTL inawaka haraka iwezekanavyo." Hata hivyo Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe hakutaka kuzungumzia mikakati ya wizara yake kushughulikia agizo la rais.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Oct 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..huu uamuzi wa kuwasha mitambo ya IPTL umefanyika bila kujadiliana bei kwanza?

  ..usije ukakuta IPTL/Wartsila wanachukua bil 13, halafu bilioni 10 za kina JK,Ngeleja,Dr.Rashidi,...
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nipeni dili nipeni masela... nikamate mahela [maseela!!]
  Nipeni dili nipeni dili masela... nikamate mahela [maseela]

  Hebu cheki dowans na Richmond ili tupate mahelaa [maselaa]
  kisha cheli hapo dart na samaki wa pombe tupate mahela [maselaa]
  si kama sitamani zaidi lakini USAID wanabana mahela [maselaa]

  USAID wanabana mahela wakati sie tunachapisha helaa [maseela]
  EPA 230M wao wanabana 20M, hawa hawajui hela [maseela]

  habari ndio hiyo!!!!!!!:p;):p
   
 16. 911

  911 Platinum Member

  #16
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  In three months watakuwa wameraise enaf kununua mitambo brand nu from manufactures!
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ng'ombe wa maskini hazai!
  Hivi nchi yetu itaweza kujikwamua kutoka rindi la umaskini?
  2015 tulipaswa kupunguza umaskini by half ili by 2025 iwepo total eradication
  as per MKUKUTA, MDGs na Vision 2025.
  NACHOKA KABISA KILA NIKIFIKIRIA.
   
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hivi mitambo mipya ni sh.ngapi? hii mitambo wamekubaliana iwashwe kwa miezi mingapi? kipindi kile cha mwanzo tulikuwa tunalipa kiasi gani?

  Tunapaswa kujua kwamba hizo 23bil ni kwa ajili ya mafuta tu, bado gharama za kukodi mitambo yenyewe. Hapa lazima tukubali bao la kisigino.
   
 19. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hebu tujikumbushe enzi zile kwenye ma-calculation:

  Sh. 23 bilioni kuzalisha 100MW, kwa wastani nyumba moja ya kawaida inatumia umeme wa 1KW. kwa hiyo 100MW ni sawa na wateja 100,000.

  Kwa hiyo ukikokotoa vizuri ina maana sh. 230,000/= zitatumika kumhudumia mteja mmoja tu kwa mwezi. Maana yake kwa siku kumhudumia mteja mmoja anayetumia 1KW ni wastani wa karibu sh. 7,670/= kwa siku moja.

  Je, serikali imeyaangalia kwa makini mahesabu haya?
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,916
  Trophy Points: 280
  Mnashangazwa na mahesabu na wakati mmeshaliwa kisiasa,mlipofurahia mitambo kuwashwa hamkuangalia nyuma yake kuna nini?Mipango ilishapangwa zamani,habari ni mpya kwetu sisi lakini si kwa wanaojua mipango yote,habari zinatolewa kisiasa,yaani nusunusu na ndio maana maswali huwa mengi hapa JF,halafu nusu ya habari inapotolewa ki propaganda watu wanadandia bandwagon bila kujua wameingia mkenge.
   
Loading...