Camel Concrete: Wakandarasi Tutawaogopa kama Ukoma

Camel Concrete: Wakandarasi Tutawaogopa kama Ukoma

Mjomba M Mjomba

New Member
Joined
Sep 12, 2016
Posts
4
Reaction score
1
Hii ni tahadhari : Hii Kampuni yenye vinu Huku Mbagala na Eneo la Gereji Mandela Road Dar Es Salaam , inahusika na utengenezaji , uuzaji na usambazaji wa Zege kwa wateja ambao ni wakandarasi na watu binafsi kwa ajili ya ujenzi wa majengo makubwa na ya kati,

Nimegundua kuwa hawa Camel Concrete huwa na tabia ya kuwabambika ama kuwauzia wateja wao zege la kiwango cha chini sana tofauti na kiwango kinachokubaliwa kitaaluma , Mfano Grade ya zege inayotakiwa ni 25, wao kwa kufahamu na kuangalia mazingira kuwa mteja atawaamini na kutochukua sample wakati wa kumwaga zege kwa ajili ya kupeleka maabara hukuletea zege la kiwango cha chini mpaka grade 10.

Hili ni tofauti kabisa na makubaliano yao na wateja na hata bei halisi ya zege la grade mfano 25. Kuwaumiza zaidi wateja wao , kwenye delivery note huwaandikia kuwa wamewapelekea zege la Grade za juu zinazotakiwa ama walizokubaliana kitu ambacho sio kweli kwani ukweli halisi hufahamika baada ya kifanya vipimo vya kimaabara.

Ifahamike kuwa kufahamu kiwango cha uimara wa zege ni pale tu utakapochukua samples na kupeleka maabara ,ama vipimo hapo site, iwapo hukufanya hivyo ndio tayari watakuwa wamekuingiza mkenge, kwani tegemea lolote kwenye mapungufu ya uimara wa muundo (structure ) wa jengo lako kwa wao kukupa zege la kiwango cha chini sana.

Nimetumia muda wangu kufuatilia kadhia hii sehemu kadhaa ya kugundua kuwa ni tazizo ambalo limewakuta wateja wao kwani hutokea sehemu nyingine kwa zege kutokauka kabisa .

Natoa rai kwa Mamlaka zinazohusika , Tbs ( ambao hutoa viwago halisi elekezi vya zege) na kwa mamlaka nyingine husika kuchukua hatua kwa kufuatilia kadhia hii na kuimaliza kwa kuchukua hatua stahiki.

Pia kwa wakandarasi na wateia wa kawaida kuwa makini wanapopokea zege kwa kuchukua samples na sio kuamini wanachoandikiwa kwenye delivery note zao.
Sichoki kufuatilia kadhia hii na kuwaletea taarifa zaidi toka kwa wateja wao . Nawahakikishia hata picha nitawaletea.
Stay tuned............
 
mkuu; changanya mwenyewe kama vipi! sio lazima uwatumie hao!
agiza mwenyewe Lori cubic 20, agiza cement ya kutosha changanya mwenyewe!
kama utahitaji kinu (Plant ndogo) kwa ajili ya kuchanganyia zege ni pm mkuu nikuachie ufurahi na roho yako!!!!
Katika sehemu ambayo huwa simwamini mtu ni kwenye zege!
achana kabisa na hayo mazege ya issue! kwanza aggregate zenyewe wanachanganya size(mm) ndogo na (mm) kubwa!
 
Mtoa mada na mchangiaji wa kwanza inaonyesha ni mtu mmoja katumia ID mbili tofauti au ni watu wanaofanya kwenye kampuni ya concrete pamoja ambao wameamua kuwachafua CAMEL concrete baada ya kushindwa kiushindani katika soko la kuuza zege.Pia inawezekana ni mfanyakazi wa camel concrete ambaye ameliwa kichwa hivi karibuni kutokana na hali ya biashara kupungua kutoka na mtikisiko wa kiuchumi.
Mtoa mada watu Tuna akili nyingi kuliko wewe so wewe na waliokutuma pambaneni na hali zenu
 
Nimeshasema subiri evidence zinakuja zitasema kila kitu , hayo ya mchangiaji na mtoa mada ama aliyeliwa kichwa sio hoja ya kutatua tatizo . Badilikeni haraka.
Ama Stay tuned.......................
 
mkuu; changanya mwenyewe kama vipi! sio lazima uwatumie hao!
agiza mwenyewe Lori cubic 20, agiza cement ya kutosha changanya mwenyewe!
kama utahitaji kinu (Plant ndogo) kwa ajili ya kuchanganyia zege ni pm mkuu nikuachie ufurahi na roho yako!!!!
Katika sehemu ambayo huwa simwamini mtu ni kwenye zege!
achana kabisa na hayo mazege ya issue! kwanza aggregate zenyewe wanachanganya size(mm) ndogo na (mm) kubwa!

Mkuu afadhali hii mara elfu kuliko kumpelekea mteja zege lililo chini ya kiwango. Wateja wao wanapata kadhia kubwa sana. Fikiria zege lisilokauka. na upo sakafu (floor) ya tatu.
 
Shuka kidogo hapo dips nilipata zege la dili ongea Na madeleva, waka mwaga uani tope baasss tena
 
Hebu tuambie Kwanzaa zege zipo za aina ngapi?, michanganyo yake na sehemu zinapowekwa ndio tuanze mjadala huu WA kitaalam.
 
Acha chuki binafs na camel mimi nimefanya amsons group ambapo camel concrate ipo ndani tena audit dept hakuna kitu kama hicho wako very makini kwenye brand zao ni watu makini sana hasa bwana abdallah munif na edha abdallah
 
Mhuu kuharibiana biashara tuu huku. Pambana na hali yako mzee majungu siyo mtaji
 
Mtoa mada na mchangiaji wa kwanza inaonyesha ni mtu mmoja katumia ID mbili tofauti au ni watu wanaofanya kwenye kampuni ya concrete pamoja ambao wameamua kuwachafua CAMEL concrete baada ya kushindwa kiushindani katika soko la kuuza zege.Pia inawezekana ni mfanyakazi wa camel concrete ambaye ameliwa kichwa hivi karibuni kutokana na hali ya biashara kupungua kutoka na mtikisiko wa kiuchumi.
Mtoa mada watu Tuna akili nyingi kuliko wewe so wewe na waliokutuma pambaneni na hali zenu
N wewe inaonekana una maslahi na hao camel concrete
 
Mi nadhani ungeshauri kwa watu wafanyeje ili kupata concrete bora maana unapomtaja mfanyabiashara hivyo Mimi binafsi sikuelewi naona unatangaza biashara yako kwa kumchafulia huyo mwingine kiukweli haupo sawa muogope Mungu roho mbaya unalipwa ubaya hapa hapa...
 
Nyinyi mnaowatetea hao Camel ni wafanyakazi au wapambe wa Camel nimeona mmoja kamtaja sijui Munif na Abdalah Edha kwani hao ndio wapo ktk idara ya Zege?.km kuna makosa yarekebishwe mleta mada hajasema waende ktk kampuni yake ila ametoa malalamiko km mteja yaliyomkuta
 
Hebu tuambie Kwanzaa zege zipo za aina ngapi?, michanganyo yake na sehemu zinapowekwa ndio tuanze mjadala huu WA kitaalam.

Kutokana na matumizi yake zege inaweza ikawa
1: kawaida
2:Mkauko wa haraka
3: Nguvu na uimara wa haraka
4: kujengea kwenye kiwango kikubwa cha kemikali
 
Back
Top Bottom